Shakoor Jongo na Musa Mateja
USIKU uliobatizwa jina la Diamonds Are Forever ulikuwa wa majuto kwa nyota wa sinema za Bongo, Wema Isaac Sepetu kwa kuangua kilio kufuatia kitendo cha aliyekuwa mchumba wake, msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ kumdhalilisha ukumbini, Ijumaa Wikienda lina kitu cha kueleza.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mapaparazi wetu lilijiri usiku wa kuamkia Machi 31, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City ambapo Diamond alikuwa akiangusha shoo kwa ajili ya kumshukuru mama yake na mashabiki wake kwa kusababisha afike alipo sasa.
CHANZO CHA KILIO
Ilikuwa pale Diamond alipopanda jukwaani na kuimba kibao chake cha Mawazo na mashabiki kuchenguka licha ya kwamba msanii huyo alichelewa kufika ukumbini hapo.
Baada ya mambo kukolea, kama kawaida, baadhi ya mashabiki walikwenda mbele kumtunza msanii huyo mwenye mvuto wa kipekee Bongo.
Kila shabiki aliyenyoosha mkono kumpa fedha, Diamond alipokea huku akizidi kumwaga mashairi ya wimbo huo kitendo kilichoufanya ukumbi kulipuka kwa shangwe na vifijo achilia mbali vigelegele.
Ndipo Wema naye alipotoka kwenye kiti chake na kwenda mbele peke yake kwa lengo la kumtunza nyota huyo huku mkononi akiwa ameshika fedha zinazokadiriwa kuwa shilingi laki mbili.

WEMA ASHINDWA KUAMINI MACHO YAKE
Staa huyo alipofika jukwaani alinyoosha mkono kumpa fedha Diamond, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwana Bongo Fleva huyo hakuzipokea na hivyo kumsababishia mwenzake kuganda kwa dakika karibu nne akisubiria.
Diamond akiwa ameshika ‘maiki’ kwa mikogo, alimkodolea macho Wema huku akitamba jukwaani kwa kwenda kulia na kushoto, wakati mwingine kuganda katikati bila kupokea fedha hizo.
Hali hiyo iliwafanya baadhi ya mashabiki wamzomee Wema na wengine wakimtaka aondoke jukwaani kwa kile walichodai anajipendekeza kwa mtu asiyempenda.
“Wewe toka hapo mbele, mtu hakutaki unajipendekeza nini? Angalia sasa unavyodhalilishwa, huyo keshagoma kupokea fedha zako, rudi kwenye kiti chako,” alisikika shabiki mmoja aliyekuwa amesimama karibu na mapaparazi wa Ijumaa Wikienda.
WEMA AKUBALI MATOKEO
Wema alipokubali matokeo, alizibwaga fedha hizo jukwaani na kugeuza zake huku mayowe yasiyokuwa na tafsiri kutoka kwa watu yakimsindikiza hadi kwenye meza aliyokaa.
Mashostito wake walimzunguka wakimfariji kwa pole za hapa na pale, wengine wakitaka kujua kwa undani kilichotokea jukwaani hali iliyomfanya mwanadada huyo kuanza kulia.

WACHEZA SHOO WASHUKA
Huku ukumbi ukiwa bado haujatulia kwa udhalilishaji huo, watu wakijadili tukio hilo kulingana na ukaribu wa meza zao, wacheza shoo wa Diamond walishuka na kwenda kumnyanyua ‘zilipendwa’ huyo wa bosi wao na kuanza kucheza naye kitendo kilichoonesha kumkera Diamond kwani ghafla aliukatisha wimbo huo.
Baada ya hapo, gumzo ukumbini humo likawa ni Diamond ‘kamdhalilisha’ Wema, Diamond ‘kamdhalilisha’ Wema.
WEMA AGOMA KUONDOKA UKUMBINI
Hata hivyo, Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006 aliendelea kuwemo ukumbini humo akiwa amekaa kwenye kiti kwa muda wote huku makundi mawili ya watu yakimzunguka.
Kundi moja likimtaka achukue fursa hiyo kumwomba radhi Diamond, lingine likisema jamaa ndiye aombe msamaha kwa kitendo cha kumdhalilisha mnyange huyo.
MANENO YA DIAMOND
Katika hali iliyowashangaza wengi, Diamond alipoamua kuzungumza na wadau wake, badala ya kuomba radhi, alikuwa na haya ya kusema:
“Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru mama yangu pamoja na nyinyi mashabiki wangu kwani kwa namna moja au nyingine mmenifanya nifikie mafanikio makubwa katika maisha yangu.
“Kwa kweli sina la kuwalipa ila Mungu ndiye anayeweza kuwalipa nyinyi.”
MATUKIO YA AWALI
Kitendo cha Diamond kuchelewa kuingia ukumbini nusura kitibue shoo kufuatia baadhi ya mashabiki kudai wamepigwa changa la macho kwa vile waliambiwa shoo ingeanza saa 3:00 usiku lakini badala yake ilifika saa 6:00.

Views: 14160

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Mr Bwire on April 14, 2012 at 12:18pm

Du!!!!!!!!!jamaa anajua kusoma alama za nyakat kwel angepokea tu wema angejitapa sana

Comment by Stella Kunambi on April 11, 2012 at 12:26pm

Pole sana wema.

Comment by Godwill Akilimali on April 4, 2012 at 12:42am

ushamba huo!

Comment by MARANDE MOHAMED on April 3, 2012 at 6:26pm

kk diamond huu ni ushamba!!!!!!!!!!!!

Comment by DORAH FREDY on April 3, 2012 at 3:07pm
Diamond mtoto wa mjini nimefurahi sana ulivyofanya hivyo safi sana wema na wewe duhhhhhhhhh
Comment by Kabakia on April 3, 2012 at 2:39pm

Asante sana kaka KILOS kwa ujumbe wako maana nilikuwa sikufikiria jambo hilo hapo kabla kutokana na amzingira ambayo niliomo huku. Kwa hiyo kaka usijali jambo hilo nalifanyia kazi mara moja. MUNGU akulipe kheri kaka maama hatukuitwa binaadamu ila kwa kutokana na wingi wa kughafilika.

Asante sana kaka.

Comment by TZ on April 3, 2012 at 10:33am

Mimi huyu Diamond sioni kama ni mwanamume kamili na haya ni mawazo yangu tu na ndio akina Wema wanachukuwa Advantage hiyo mbona mzee wa Ikulu hakumfanyia upuuzi huu?

Comment by Edwina Edwin on April 3, 2012 at 10:12am

wema alitaka kuiba umaharufu toka kwa diamond.. na diamond mtoto wa mjini akaiona hiyo na akamuumbua..  wenzake ambao walikuwa mamiss wanafanya mambo ya maana ndani na nje ya nchi..yeye anajidhalilisha.. move on na maisha yako mtoto wa kike.. husijipatie umaharufu toka kwa diamond.. mwenzio ana kipaji cha mziki na anafanya vitu vya maana.. unajitia aibu kweli na hata uzuri umekuisha kwa jinsi unavyojiaribu na mambo yako..sijui ulikulia wapi?

Comment by king kiss on April 3, 2012 at 9:52am

HILI WEMA KWELI JINGA HALAFU LINAONEKANA LIMBUKENI WA MAPENZI HANA HATA HAYA!

Comment by Paul Madatta on April 3, 2012 at 8:35am

kuachana sio ugonvi, angepokea tu hiyo pesa akaendelea na shoo yake, au alihofia mambo flan ya ndumba? Haaaaa, pole wema

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ on Tuesday. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson 3 hours ago. 12 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by maleka sakeha 3 hours ago. 30 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 22. 12 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 23. 36 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }