Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Flora Mvungi ameangua kilio ukumbini katika sherehe yake ya kufundwa maarufu kama ‘Kicheni Pati’ baada ya kupewa maneno mazito na msanii mwenzake Wastara Juma, Risasi Mchanganyiko lilikuwepo.

Flora Mvungi akilia.

Sherehe hiyo ambayo ni king’ora cha kuelekea kwenye ndoa yake, ilifanyika wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Livingstone, Kinondoni, Dar na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na Flora.

MACHOZI
Wastara alikuwa mmoja wa waliopangwa kutoa nasaha kwa bibi harusi mtarajiwa, ingawa  walitangulia wengine na kumshauri, ilipofika zamu ya Wastara ndipo Flora alipomwaga machozi.

Wastara akitoa nasaha zake.

Katika nasaha zake, pamoja na mambo mengine Wastara alimshauri Flora kuwa na uvumilivu ndani ya ndoa yake, maneno ambayo yalionekana kumchoma na kuangua kilio.
Kazi kubwa ilikuwa kwa shoga yake Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye alikuwa mpambe wake kumtuliza  huku akimfuta machozi.

MASTAA WAMSUSIA
Tofauti na ilivyo kwa sherehe za wasanii wengine kuhudhuriwa na mastaa kibao, katika hafla ya Flora walionekana kumsusa kwani walihudhuria kiduchu.
Ukiwaondoa Wastara na Nisha wengine ni Jacqueline Wolper, Isabela Mpanda, Suzan Lewis ‘Natasha’ na Yvonne Cherry ‘Monalisa’.

Flora na mpambe wake, Salma Jabu ‘Nisha’.

KALAMA AVAMIA SHEREHE
Katika hali ya kushangaza msanii wa Bongo Fleva,  Luteni Kalama alivamia sherehe hiyo ambapo aliongozana na mpenzi wake Isabela Mpanda hali iliyowaacha watu midomo wazi.
“Dume zima linavamiaje shughuli ya wanawake? Ni ushamba au wivu? Hata kama ni wivu ni wa aina gani? Huyu wa ajabu kweli,” alisikika mdau mmoja aliyekuwepo ukumbini humo.

Burudani.

VIKOROMBWEZO
Ukiachilia mbali waalikwa kupendeza sana kwa mavazi, vyakula na vinywaji vya kumwaga, mshereheshaji wa sherehe hiyo aliye mwanamuziki wa Injili, Sarah Mvungi aliendesha vizuri sana.
Flora alibadilisha nguo mara mbili hivyo kuzidi kuinogesha sherehe hiyo.

Wasanii waliohudhuria wakiwa kwenye picha ya pamoja na Flora.

KIFUATACHO
Kwa sasa Flora anatarajia kufunga ndoa na msanii wa Bongo Fleva, Hamisi Baba ‘H – Baba’ Juni 8, mwaka huu ikiwa ni baada ya kukaa kwenye uchumba kwa muda mrefu.

Views: 12708

Tags: mchanganyiko11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by nasoro mkangwa on June 12, 2013 at 7:40pm

Hongera sana  Tulia na mumu wako

Comment by Rashid Mtotela on June 9, 2013 at 8:07pm

huyo dume aliyevamia sherehe ya wakina mama, du kali kweli

Comment by hope on June 7, 2013 at 10:30am

Kila la kheri

Comment by penina mwailunda on June 6, 2013 at 8:44am

Hongera mdada, Itakuwa umepata ujauzito kabisa au umenenepa?  

Comment by mayalilwa on June 6, 2013 at 6:28am

Angalia usiishie kweny kitchen party tu.

Comment by steven emmanuel on June 5, 2013 at 8:15pm
H BAba nakutarajia utabadilika zile tabia za kihuni!!!
Comment by lumi mwandelile on June 5, 2013 at 5:06pm

NDOA IDUMU HIYO, OLE WAKO TUSIKIE UMEACHIKA, HONGERA SANA

Comment by lumi mwandelile on June 5, 2013 at 5:05pm

HONGERA DADA KAITUNZE NYUMBA NA MUMEO NDOA IDUMU

Comment by tatu said on June 5, 2013 at 4:10pm

Kila la kheri mamy.

Comment by Edna Mugini on June 5, 2013 at 3:50pm

HONGERA MDADA

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ on Tuesday. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 22. 11 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 25. 29 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 22. 12 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 23. 36 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

Loading… Loading feed

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }