WAOMBAJI KAZI WAMETAKIWA KUJIANDAA WANAPOENDA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira, Bw. Xavier Daudi (kushoto) akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) na kulia ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira, Bw. Bakari Mahiza.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi amesema ofisi yake hivi sasa itakuwa ikitoa ratiba ya usaili mapema kila mara ili kuwawezesha wasailiwa kuwa na muda wa kutosha kujiandaa kabla ya kwenda kwenye usaili husika.
Amesema hayo leo wakati akiongea na mwandishi wa habari ofisini kwake alipokuwa  akitoa ratiba ya usaili kwa mwezi Septemba, 2012 pamoja na tangazo la kuita kazini waombaji waliofaulu usaili uliopita. Aliongeza kuwa ili msailiwa aweze kufanya vizuri katika usaili pamoja na vigezo vya kitaaluma alivyonavyo bado anatakiwa kujiandaa vyema na kujiamini anapojibu maswali wakati anapokuwa kwenye usaili.
Daudi amesema hivi sasa dunia imekuwa ya utandawazi na fursa za ajira ni za ushindani zaidi, maana wahitimu hivi sasa ni wengi na hawana ajira hivyo ni vyema kwa wahitimu wanapoomba nafasi za kazi na kuitwa kwenye usaili wawe wamejiandaa vya kutosha ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata ajira.
Katibu amesema usaili kwa mwezi Septemba,  utaanza tarehe 18 Septemba  hadi 5 Oktoba, 2012 kwa taasisi zifuatazo; Wakala wa Barabara (TANROADS), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), TEMESA, ADEM, CARMATECH, NEEC (UWEZESHAJI), Chuo cha Utalii, Chuo cha Diplomasia, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Wizara ya Fedha (PFMRP) EPZA, na Maafisa Tarafa.
Amesema kwa maelezo zaidi ya nafasi hizo na wapi usaili utafanyika ni vyema waombaji wakaperuzi tovuti ya Sekretarieti ya Ajira pamoja na tovuti za Taasisi husika na kufungua tangazo la kuitwa kwenye usaili  ili kuiona ratiba nzima ya tarehe ya mchujo na usaili kama zinavyoonekana katika tangazo lenye orodha ya majina ya kuitwa kwenye usaili.
Aidha, amesisitiza ni muhimu kwa waombaji kuzingatia masharti ya tangazo pindi wanapoenda kwenye usaili kwani ni njia mojawapo ya kujua msailiwa amejiandaa kwa kiasi gani.
Wakati huohuo, Katibu amewataka waombaji wa nafasi za kazi waliofanya usaili kuanzia tarehe 7 hadi 31, Agosti, 2012 katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Biashara  (CBE), Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Chuo cha Maji (WDMI), Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP), Chuo cha Serikali za Mitaa- Hombolo, COASCO, Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Tume ya Mionzi (TAEC), Taasisi ya Utafiti wa Samaki (TAFIRI), Wakala wa Mbegu (TOSCI), Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA)  kuangalia majina yao katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira pamoja na taasisi husika ili kujua waliofaulu.
Amesema kwa waliofaulu usaili wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Aidha, barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao za posta.
Alimalizia kwa kusema kuwa, kwa wale ambao hawataona majina yao  katika tangazo husika  watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuendelea kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.

Views: 1181

Tags: ajira

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by David Wagwene on September 17, 2012 at 11:01pm

Taarifa nzuri lakini maana unaweza kuwa na CV nzuri ukakuta bado unakosa kazi kumbe kwa sababu ya makosa madogomadogo

Comment by julius manning on September 15, 2012 at 9:36am

nimekubali

Comment by steven emmanuel on September 15, 2012 at 8:50am

hii nzuri maana watu weng wanaenda kwnye usaili bila maandaliz yoyote mwisho wa siku hakikosa lawama bora wametoa taarifa mapema

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ on Tuesday. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 22. 11 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 25. 29 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 22. 12 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 23. 36 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

Loading… Loading feed

Latest Activity

kitong posted a status
32 seconds ago
vanhelsing posted a status
40 seconds ago
sakalvela posted a status
41 seconds ago
ketrina1liono posted a status
""
41 seconds ago
sakalvela posted a status
53 seconds ago
Polat Salla posted a status
55 seconds ago
dtsi100 posted a status
""
1 minute ago
nazmulhasan posted a status
1 minute ago
aniket posted a status
1 minute ago
bujangan posted a status
1 minute ago
bujangan posted a status
1 minute ago
Herum posted a status
1 minute ago

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }