Kwa mara nyingine tena, kile kinachoelezwa kama 'wananchi wenye hasira, kimefanya kazi yake tena baada ya kumchoma moto wa tairi kijana aliyedhaniwa kuwa kibaka. Jamaa anaonekana kijana mmoja akimsaidia Israel kutoa roho ya kibaka huyo aliyedaiwa kutaka kuiba baiskeli kwenye nyumba ya mkazi mmoja maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam leo alfajiri. Jina la kijana huyo halikuweza kufahamika mara moja.


Kijana aliyedaiwa kuwa kibaka akiteketea kwa moto na kipigo huku akiwa amevishwa tairi.


….Kibaka akiteketea! .Dah!


PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

Views: 75

Tags: CHA, KIBAKA, KIFO, KINATISHA

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Akram on June 15, 2011 at 9:36pm
Duh huu ni unyama sana wa kumchoma mtu moto jamani serikali inafanya kazi gani?
Comment by jero mkali on February 20, 2011 at 2:20pm
Sheria mkonon sio vizur.
Comment by Tajiel Warucha on July 16, 2010 at 8:51am
wote mliohusika kumuua huyo mtu mkatubu,je ninyi ni wakamilifu!! kati yenu hamna wazinzi,wasioheshimu wazazi,hata wasiotunza amri za Mungu? Je Mungu angewaua ingekuwaje?

Mkatubu mara moja!!!
Comment by Nyasae Chieng on July 15, 2010 at 9:58pm
Pamoja na kwamba si haki kuua inapobidi nafikiri ni haki yao hawa vibaka. Hebu fikiria pale kibaka anapokukaba kwa ubao wenye misumali na kuchukua simu yako wakati wewe utaugulia hospitali+gharama za matibabu+umepoteza namba zote za simu ambazo ni muhimu kwako. Kibaka yuko tayari kuvunja ukuta wa nyumba yako ili aibe sufuria, atavunja dirisha la nyumba ili aibe suruali. Atavunja kioo cha gari ili aibe hata doli la mtoto. Fikiria hasara unayopata. Ukisema apelekwe mahakamani fikiria muda uataopoteza kufuatilia kesi kama hiyo. Ukisema akatwe mikono, bado ataweza kuwaeleza wenzie ambao watakuja kukufanyizia ili kulipa kisasi. Bora kumfutilia mbali tu angalua idadi yao itapungua, wahenga walisema bandubandu humaliza gogo!
Comment by kibabaa on July 15, 2010 at 6:31pm
Nafikiri hii ni Tanzania ya leo, watu wamechoshwa, fisadi anatanua na kibaka anauwawa, lakini pia wakati mwengine inatia uchungu hasa hawa vobaka wakikutaiti utakoma ubishi, mimi nafikiri reaction ya hawa watu inatokana na experience yao, kama hujakutana na vibaka utatoa blaaa blaa nyingi za kisheria, wewe chukua simu yako nzuri na tembelea maeneo ya Tandika au Manzese, ukipigiwa poke na tanua. kama utadumu nayo muda wa dk 5 basi wewe mwanaume. hii adabu ni fundisho na sio kusema huyo jamaa akamatwe hebu muulize mwana familia wa Pro. Mwakyusa (mungu ailaze pema peponi roho yake) atafanya nini kama wauwaji wakikamatwa mbele yake? jibu unalo. usipayuke tu bila kuangalia kwanini watu wanafanya hivi.?
Comment by shawn junior on July 15, 2010 at 6:01pm
Kama kuna mtu alishawahi kuibiwa au kukabwa na hao watu sidhani kama utasema huyo aliyemchoma moto akamatwe siku yakikuta ndo utajua
Comment by Bengal Sanke on July 15, 2010 at 4:20pm
Nadhani hapo polisi ushaidi wa picha upo, serikali ilishaweka wazi hakuna mtu mwenye haki ya kuchukua sheria mkononi kutoa uhai wa mwingine labda kama ni mazingira ya kujitetea ama kujiokoa na hatari mbaya inayoweza kusababisha mvamiwa kudhurika . Huyo jamaa anayemchoma huyo kibaka anaoneka vyema kabisa, akamatwe atataja na wenziwe ili wote wakamatwe. Ni rahisi kuua ukiwa katika kundi kubwa lakini ukiambiwa uue peke yako huwezi.
Comment by nayla on July 15, 2010 at 4:14pm
wezi wa baiskeli wanachomwa,mafisadi wanatembea kwa matanuzi na jeuri,kama mahakama imeshindwa kazi iwakabidhi mafisadi kwa wananchi tuwashughulikie
Comment by chapombe on July 15, 2010 at 3:39pm
jamani vijana wenzangu,msiwaibie hawa watu,wamepagawa hawa,mnaona wanaua bila huruma.
wenyewe wana hasira na maisha yao na wala hawazijui sheria,bora muuze tu mitumba mkimbizane na askari wa jiji,kuliko wananchi hawa wa uswahilini
Comment by BENJA on July 15, 2010 at 3:15pm
Hii inatokana na wananchi kukosa imani na jeshi la polisi, zamani wizi ulikuwepo na watu walikuwa wanaimani na jeshi la polisi na mtu akiwa chini ya polisi hatua za kisheria zitakuchukuliwa dhidi yake kwa misingi ya haki MAHAKAMANI. lakini siku hizi polisi na mahakama wanafanya kazi ya rushwa tu na haki hakuna tena. HAKI HUJENGA TAIFA NA KUKOSEKANA KWA HAKI HUSABABISHA TAIFA KUANGAMIA.


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
8 minutes ago
GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
8 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website