Vyakula vya kuepukwa na wajawazito

Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe bora na mlo sahihi. Mwenye jukumu la kutoa lishe bora na sahihi kwa kiumbe kilichomo tumboni ni mama. Anatakiwa kujua aina ya vyakula anavyopaswa kula. Vivyo hivyo, anatakiwa kujua aina ya vyakula vya kuviepuka.


Katika makala ya leo, tunaangalia orodha ya vyakula vilivyokatazwa. Mama mja mzito haruhusiwi kuvila vyakula vifuatavyo kwa faida ya kiumbe kilichomo tumboni na kwa faida yake mwenyewe:

NYAMA MBICHI
Epuka kula samaki au nyama mbichi au iliyopikwa lakini haikuiva vizuri. Utajiepusha na uwezekano wa kula bakteria na vijidudu vingine hatari kwa afya ya mtoto tumboni. Mjamzito anapokula nyama, anatakiwa kuhakikisha imeiva sawasawa.

‘SOSEJI’ NA ‘SANDWICHI’
Mjamzito haruhusiwi kula ‘soseji’, ‘sandwichi’ za nyama na vyakula vingine vilivyotengenezwa kwa nyama. Inaaminika kuwa nyama zinazoandaliwa kwa ajili ya kutengenezea vyakula kama hivyo, huwa vimewekewa vihifadhi vyakula (preservatives) ambavyo vinaweza visiwe vizuri kwa afya ya mtoto.

SAMAKI WENYE ZEBAKI (MERCURY)
Wajawazito wamekatazwa kula samaki wenye kiasi kingi cha madini ya zebaki. Ulaji wa zebaji kwa wajawazito umehusishwa na uzaaji wa watoto taahira. Mfano wa samaki hao ni pamoja na Papa, Chuchunge na dagaa wakubwa.

MAYAI MABICHI
Ulaji wa mayai mabichi au vyakula vilivyochanganywa na mayai mabichi, mjamzito haruhusiwi kuvila. Kuna baadhi ya ‘Ice Cream’ na ‘mayonaizi’ hutengenezwa kwa kuchanganywa na mayai mabichi. Mjamzito amekatazwa kuvila vyakula hivyo.


MAINI
Maini yana kiwango kikubwa cha madini aina ya chuma. Hata hivyo, yana kiasi kikubwa cha Vitamin A ambacho huweza kuwa na madhara kwa mtoto kikizidi.

MAZIWA MABICHI
Maziwa mabichi huweza kuwa na bakteria ajulikanae kama ‘Listeria’, ambaye huweza kusababisha kuharibika kwa mimba. Unapokunywa maziwa, hakikisha yamechemshwa au kama ni ya paketi hakikisha ni yale yaliyoandikwa ‘Pasteurized’ na siyo ‘Unpasteurized’.

KAFEINI (CAFFEINE)
Ingawa baadhi ya utafiti unaonesha kuwa unywaji wa kiasi kidogo cha kafeini hauna madhara, lakini kuna utafiti mwingine unaonesha kuwa unywaji wa kafeini una uhusiano na kuharibika kwa mimba. Kafeini ni aina ya kirutubisho kinachopatikana ndani ya kahawa.


Iwapo mjamzito atakunywa kahawa, basi anywe kiasi kidogo sana kisichozidi kikombe kimoja kwa siku. Kwa kawaida kahawa hukausha maji mwilini, hivyo unywaji wake husaidia kukauka maji mwilini ambayo ni muhimu sana kwa mjamzito.


Utafiti mwingine unaonesha kuwa kafeini inahusishwa pia na uharibikaji wa mimba, uzaaji wa watoto ‘njiti’ na watoto wenye uzito mdogo. Ni vizuri kunywa maji ya kutosha, maziwa na juisi na kuepuka kunywa vinywaji vyenye kahawa.

POMBE
Hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa unywaji wa pombe kiasi kidogo wakati wa ujauzito hauna madhara, kwa maana hiyo matumizi ya pombe hayaruhusiwi kabisa wakati wa ujauzito, hata kama ni kidogo.
Unywaji wa pombe wakati wa ujauzito huweza kuathiri ukuaji mzuri wa mtoto. Kutegemeana na kiasi atakachokunywa mjamzito, pombe inaweza kumsababishia mtoto ugonjwa hatari utokanao na pombe (Fetal Alcohol Syndrome).

Views: 31602

Tags: ARE, EAT_Vyakula, WHAT, YOU, kuepukwa, na, vya, wajawazito

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by raji juma issavi on June 5, 2015 at 3:47pm

sawa wa mama wawe waangalifu kwa vyakula hivi ambavyo haviwafai wakiwa katika hali ya ujauzito.

Comment by Didas Ngowi on November 23, 2012 at 1:09pm
Ni wakati mzuri sasa kwa akina mama kujua ni aina gani ya vyakula unatakiwa ule wakati ukiwa mjamzito, kweli maini ni matamu ni vyema mkafuata ushauri wa madaktari.
Comment by naomi (naenae) on January 30, 2011 at 7:30am
hahaha wengine tumenywewa pombe sana tuu
Comment by Mohamed Hajis mohamed on January 27, 2011 at 8:25am
Jamani kina Mama zingatieni kwa makini kuhusu hili somo kwani elimu kuhusu afya ya uzazi ni pana sana GPL endeleeni kutoa somo ili mtu apate kujilewa kwani kuna hatari kubwa ya Mama mjamzito kupoteza maisha au  kumpoteza mtoto kwa mambo kuntofahamu mambo kama haya
Comment by Mohamed Hajis mohamed on January 27, 2011 at 8:23am
Jamani kina Mama zingatieni kwa makini kuhusu hili somo kwani elimu kuhusu afya ya uzazi ni pana  sana GPL endeleeni kutoa somo ili mtu apate kujilewa kwani kuna hatari kubwa ya Mama mjamzito kupoteza maisha au  kumpoteza mtoto kwa mambo kuntofahamu mambo kama haya.
Comment by Chebe Boy on January 26, 2011 at 10:09am
Dah inabidi wajawazito wajifunze kutotamani ila unaweza kuta mtu mwingine anatamani kitu hadi anaisi roho inataka kutoka sijui mtu wa aina iyo ata epukaje vitu kama vilivyotajwa hapo juu asanteni kwa somo zuri
Comment by Sili Silali on January 26, 2011 at 9:56am

Makala nzuri, inaelimisha!

Upungufu wa hii makala:

1. Hii ni kazi ya "copy and paste" kutoka mitandaoni bila kuzingatia mazingira halisi ya Tanzania hasa vijijini. Nilitegemea ndugu mwandishi ungezungumzia  vitu vinavyoliwa sana na kina mama wajazito kama vile udongo na madhara yake.

2. Maini ni chakula bora kwa mama wajawazito, si sahihi kusema maini hayafai, ungesema kwa matumizi ya maini kwa kiasi kikubwa, maini yana madini ya chuma na virutubisho vingine kwa wingi ambavyo ni muhimu.

3. Kiasi kidogo cha pombe husaidia mwili kuweza kunyonya vizuri virutubisho kutoka tumboni, Tatizo la pombe ni kama itatumika kwa wingi. Wine ni nzuri zaidi, isizidi robo glass ya kawaida (ml 50) na inywewe baada ya mlo

4.Nchi zetu za kiafrika hasa vijijini bado tuna tatizo la uhifadhi bora wa nafaka. Mara nyingi nafaka zilizohifadhiwa sehemu nyevu hupata kuvu(fungi). Kuvu hawa huwa na sumu (Aflatoxin) inayoweza kumdhuru mtoto kirahisi. Ni vyema wajawazito wakaepuka kutumia nafaka ambazo hazikuhifadhiwa vyema.

Makala yako ni nzuri sana, pamoja na mapungufu hayo machache

Comment by besta msumange on January 26, 2011 at 9:54am
asanteni kwa elimu yenu nzuri
Comment by Maggy on January 26, 2011 at 9:49am
Somo zuri sana jamani, endeleeni kutujuza na mngine yahusuyo afya.
Comment by Sarah Anuary on January 25, 2011 at 8:35pm
Haya tena watarajiwa mambo mazuri haya........
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

TOP NEWS WEEK HII

Loading… Loading feed

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }