Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, jana ilifanya uzinduzi rasmi wa huduma yake mpya ya TIGO PESA Mkoani Mbeya katika uwanja wa Sokoine ambao ulifurika watu kibao. Huduma hiyo mpya, itawawezesha wateja wa Tigo kutuma pesa kwenda mitandao yote nchi nzima kwa gharama nafuu zaidi. Pichani: Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya jana.
Mmoja wa wakazi wa Mbeya, Timoth Mayunga (wa tatu kushoto) akitoa fedha shs 25,000/- kwa wakala wa Tigo Pesa mjini humo, Rehema Yona kwa ajili ya kufungua akaunti ya Tigo Pesa, wakati wa uzinduzi rasmi wa huma hiyo mjini Mbeya. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Tigo Pesa, Judah Semah.
Mwanamuziki nguli wa kikundi cha muziki wa kizazi kipya cha Tip Top Connection chenye maskani yake mitaa ya Manzese jijini Dar es Salaam, Madee, akiimba wakati wa uzinduzi wa huduma ya Tigo Pesa katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya jana
Wasanii wa kikundi cha muziki wa bongo flava cha Manzese Connection, Kassim Mganga na Richard Tunda ‘Tundaman’ (kushoto) wakitoa burudani wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya Tigo Pesa
Wasanii wa kikundi cha Sombe Sanaa Group wakionyesha umahiri wao
wakati uzinduzi wa huduma ya Tigo Pesa
Baadhi ya umati wa wakazi wa mji wa Mbeya na vitongoji vyake waliohudhuria uzinduzi rasmi wa huduma ya Tigo Pesa katika Uwanja wa Sokoine mjini humo
PICHA: Mpiga Picha Wetu
Comment
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
Dongonyo Juniour |
| 3 |
julius manning |
| 4 |
kadama J'z |
| 5 |
Ukweli100 |
| 6 |
Quality Centre |
| 7 |
kaka |
| 8 |
lumi mwandelile |
| 9 |
Mawazo Katota |
| 10 |
ANDERSON SOGOLE |
You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers