Irene Uwoya.
Wema Sepetu.
Kajala Masanja.
Na Mwandishi Wetu
NYUMA ya kuporomoka kwa afya ya Irene Uwoya, kuna siri nzito ambayo imefichuka, ikidaiwa kuwa pamoja na yeye, mastaa wengine wa kike Bongo akitajwa Wema Sepetu na Kajala Masanja, wanatumia dozi maalumu ya wanawake ya kupunguza unene.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa ambacho kimeweka kambi kwenye tasnia ya muvi Bongo, warembo hao wamekuwa ‘bize’ kwa wiki kadhaa wakijitahidi kuweka miili yao miepesi kwa kutumia dozi hiyo.
“Kuna baadhi ya mastaa ukiwaona utahisi wanaumwa au wana matatizo yanayowakondesha, lakini ukweli ni kwamba wanatumia dozi ya kujikondesha,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Nyie wenyewe ni mashahidi, juzikati kuna baadhi ya mastaa walikuwa wakilalamikia unene, lakini sasa malalamiko hayasikiki tena kwa sababu mkombozi amepatikana.”
KWANI UWOYA ALISEMAJE?
Hivi karibuni Uwoya alinaswa akiwa amedhoofu afya yake kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Taifa, Dar ambapo alipoulizwa kulikoni kukondeana kiasi hicho alijitetea: “Ni mabadiliko tu ya kawaida, hata mimi najishangaa.”
NI DAWA GANI?
Chanzo hicho kiliendelea kutambaa na mistari kuwa, kuna dawa ambayo inatolewa na mwigizaji mmoja maarufu ambayo inaitwa Slimming Tea kutoka Afrika Kusini.
NI STAA GANI?
Ijumaa lilipombana mtoa habari huyo kuhusu staa anayetoa dozi hiyo, alikubali kumtaja kuwa ni Ummy Wenslaus ‘Dokii’ na kwamba amekuwa akiwapa dozi hiyo mastaa wengi pamoja na wanawake wengine.
DOKII ATOBOA SIRI
Baada ya kumegewa mchongo huo, Ijumaa lilizungumza na Dokii ambaye alitoa siri kutoa dozi hiyo kwa mastaa mbalimbali ambayo imewasaidia kuweka sawa maumbile yao.
“Kusema kweli nimetoa dozi kwa wanawake wengi na wanashukuru. Hata mastaa nimewapa wengi tu,” alisema Dokii.
Juzi Jumatano mwandishi wetu alifanya jitihada za kuwapata Wema na Kajala kuzungumzia juu ya matumizi ya dozi hiyo lakini hakufanikiwa kuwapata kufuatia simu zao za mkononi kutokuwa hewani.
Comment
Comment by pjoan audes on February 16, 2012 at 6:44pm
Comment by Medaice Ice on February 16, 2012 at 12:12am
Comment by Fauzia Maundi on February 13, 2012 at 8:56am DOKII TUNAOMBA UWEKE NAMBA YAKO YA SIMU ILI IWE RAHISI KUWASILIANA NA WEWE KWANI TUKO WENGI TUNAO ITAKA HIYO DAWA YA KUPUNGUZA UNENE SLIMMING TEA YA KUTOKA AFRIKA KUSINI
MIMI NAMBA YANGU NI 0715025723 NAOMBA UNIPIGIE ILI NIWEZE KUPATA HUDUMA HIYO
Comment by isabella godfrey on February 13, 2012 at 8:41am kweli kazi mnayo kila kitu mkisikia mmo subilini shuguli yake maana mmekalia kumkosoa mungu alivyowaumba.
Comment by DR .ALLY MOHAMED MAKWATILA on February 11, 2012 at 7:23pm dawa za namna hiyo zina madhara makubwa kwa baadaye
Comment by samora rajab albert on February 11, 2012 at 7:08pm izo dawa hazina madhara lkn?
Comment by marimar ethan on February 11, 2012 at 11:46am ila irene ahapendza kbsaa alvyopungua sijpendaa ametshaaa mhmm
Comment by marimar ethan on February 11, 2012 at 11:46am AAGRIIIIIIIIIIIIIIIIIIII MI NIKAJUA SIJUI KITU GN DUH
Comment by Bryso Wilson on February 11, 2012 at 11:25am
Comment by Edna Venant on February 11, 2012 at 8:42am | 1 |
GLOBAL |
| 2 |
julius manning |
| 3 |
Man KKK |
| 4 |
Sili Silali |
| 5 |
IL-YA |
| 6 |
chama baby |
| 7 |
msichoke mlugu |
| 8 |
kaka |
| 9 |
Maji Marefu |
| 10 |
Kelvin Luhala Eto'o |
othman Ochu posted a status
mrembo commented on Sili Silali's photo

You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers