Na Mwandishi Wetu
MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako ametamba kwamba yeye ni tajiri tishio kuliko watumishi wenzake kwani anamiliki magari sita ya kifahari na nyumba ambayo ina kiyoyozi (AC).

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako'.

Akihubiria waumini wake kanisani hapo juzikati, Ubungo- Kibangu, jijini Dar es Salaam na kuoneshwa na Kituo cha Runinga cha C2C na Channel Ten hivi karibuni, Mzee wa Upako alisema magari yake hayo ya kifahari yote yana viyoyozi na si ya kutoka Japan, akimaanisha ya gharama kubwa zaidi.
“Mimi ndiye Mzee wa Upako, nikitoka nje nakuta magari yote sita yapo, nachagua leo niendeshe hili au lile. Najiambia hapana hili nililiendesha jana, nachukua lingine,” alitamba kiongozi huyo.

Mercedes Benz.

Aliyataja magari hayo kuwa ni Mercedes Benz, Land Rover Discovery, Range Rover Sport, BMW X5, Ford Escape na Range Rover Vogue ambayo Uwazi linatafiti bei zake na kuwapelekea wasomaji siku zijazo.
Aidha, mtumishi huyo wa Mungu aliendelea kutamba kuwa nyumbani mwake mna viyoyozi ‘vikali vya kufa mtu’ na kubainisha kwamba huwa akitoka kwenye gari lenye kiyoyozi anaingia katika nyumba yenye kiyoyozi.
“Mimi nasema hayo kwa sababu ni mlipaji mzuri wa kodi za serikali, sioni sababu ya kuficha mali zangu, kwa nini nifiche?” alihoji na kuongeza:

Land Rover Discovery.

“Magari yote nimeandika kwa jina langu ili niyalipie kodi, situmii mwamvuli wa kanisa kwa kukwepa kodi.”
Aliwaambia waumini wake kuwa kazi yake ni kugawa upako wa baraka za utajiri na kwamba kupitia kanisa lake watu wengi wameneemeka kimaisha.
“Nasisitiza kuwa kila mtu anatakiwa kuwa tajiri lakini utajiri wa halali siyo ule wa kudhulumu, ndiyo maana nasimama hapa kutaja mali zangu, magari hayo si mali ya kanisa ni yangu,” alisema.

BMW X5.

Pia aliyachambua makanisa kwa kusema: “Makanisa yetu haya ya kiroho ni hovyo, wameingia matapeli na ninayasema haya kwa kuwa ninayajua, nipo ndani, ndiyo maana najua kitu ninachokisema na mtu akitaka tubishane kwa hoja hii hawezi kunishinda.
“Najua hili ninalozungumza ni jambo zito na sasa ninaposema haya maneno ni sauti ya Mungu mwenyewe inatoka kupitia kinywa changu.”
Mzee wa Upako aliwahi kusema kwamba amekuwa akitumia zaidi ya shilingi 300,000,000 kwa mwaka kwa ajili ya kuendesha vipindi vyake katika runinga na fedha hizo huchangisha kupitia akaunti zake, akasisitiza vipindi vya runingani ni mali yake na si kanisa.

Ford Escape.

Wachambuzi wa mambo wameichambua hesabu hiyo na kugundua kwamba mchunga kondoo huyo hutumia zaidi ya shilingi 25,000,000 kwa mwezi kulipia vipindi hivyo.
Kiongozi huyo ana kanisa kubwa la ghorofa Ubungo Kibangu na mabasi makubwa  kadhaa ambayo hutumika kuwasomba waumini bure kutoka Barabara ya Mandela hadi kanisani kwake.
Hivi karibuni Mzee wa Upako amewahi kuwakemea wachungaji wenzake wa makanisa ya kiroho kwa kujitajirisha kwa kujiita manabii na mitume akidai kwamba kufanya hivyo ni kuwatapeli waumini.

Range Rover Vogue.

“Inawezekana vipi mabomu yapigwe madhabahuni halafu wewe kama mtume na nabii usifanye jambo lolote la Kimungu dhidi ya waliofanya kitendo kile madhabahuni?” alihoji Mchungaji Lusekelo.
Alidai kuwa kuna mitume hapa nchini kazi yao ni kugombania ardhi. “Kama kweli wewe ni mtume na nabii halafu unagombania ardhi ya mashamba na Wazaramo, huo ndiyo utume tulioitiwa? Ndiyo maana hata serikali haitutambui,” alisema Mzee wa Upako huku akishangiliwa na waumini wake.
* MAGARI YANAYOONEKANA PICHANI JUU NI MIFANO YA MAGARI ANAYOMILIKI MZEE WA UPAKO.

Views: 7265

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by richardngeze on January 11, 2013 at 6:20pm

Dah! waumini wake wajinga wajinga wanatembea hadi ndala zinachanika lakini yeye magari kibao! kweli freemanson imemtoa.

Comment by Edson Robhinson on January 8, 2013 at 11:39pm
wezi wakubwa nyie UTAJIRI UMEPEWA NA FREEMASON WENZAKO hafu ujifanye unahubiri? kwanini wewe tuuu na sio yule mama mzee? hv unafikiri utazikwa nazo? hebu tubadilike tuubiri kuhusu wokovu kuliko mali
Comment by lumi mwandelile on January 4, 2013 at 9:45am

WIZI MTUPU

Comment by mayalilwa on December 24, 2012 at 5:23pm

du! mbona Yesu alikuwa masikini? na alisema ni vigumu kwa tajiri kuurithi ufalme wa Mbingu, itakuwaje kwa lusekelo atauona ufalme wa mbinguni kweli!

Comment by Majoto baridi on December 24, 2012 at 3:45pm

ANATISHA NINI?? ATAISHI NAYO MILELE HAYO MAGARI NA VIYOYOZI? ULIMBUKENI TU.  KAMA UMEPATA MSHUKURU MUNGU THEN PIGA KIMYA TUMIA TARATIBU USUBIRI SIKU YAKO YA KUFA NA KUVIACHA VYOOTE! UNGETAMBA KAMA UNGEHAKIKISHIWA NA MUNGU KUISHI MILELE.

Comment by pjoan audes on December 22, 2012 at 3:30pm

Saafi sana mjasiriamali lusekelo, amesema kweli kwakuwa utajili anapewa na hao wanaomchangia kile kinachoitwa sadaka, na bado kama hiyo haitoshi akiwa anahubiri huwa wanamtunza kama wafanyavyo kwa wanamziki wa dansi! na hao akina mwingila anaowasema wanagombania ardhi ya wazaramo na kupigwa mabomu madhabauni kwa makanisa yao, yuko sahii kabisa kwasababu wanakosa mbinu ya kula kiulaini mpaka wanapora hata mali za masikini!

Comment by DORAH FREDY on December 22, 2012 at 10:18am

Duh inatisha halafu kwa sasa mnaumbuka sana

Comment by Focus Kunambi on December 15, 2012 at 9:42pm

wajinga ndio waliwao, wakikuletea sadaka wewe bamba tu, wao waendelee kushindia miogo na maji ya kisimani, wewe ni mahambager na mahanjuhanju kila siku

Comment by Domino Bagambisa on December 14, 2012 at 9:07pm

kuibuka kwa kasi haya makanisa kunatia shaka bila shaka wanasukumwa na maslahi binafsi zaidi ya kuhubiri neno la mungu. Hii ni njia ya kupitia kwa kuuaminisha umma kuwa ni nguvu za Mungu sasa wanaanza kulumbana wenyewe kwa wenyewe.

Comment by ronald musiba on December 13, 2012 at 1:44pm

dah! kweli mbuz anakula kulingana na urefu w kamba yake meeeeeeeeeeeeeeeen

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE on Monday. 27 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service