UTAJIRI WA MWINGIRA WALIGAWA KANISA

Nabii Josephat Mwingira.

Na Mwandishi Wetu
MADAI na gumzo kwamba baadhi ya viongozi wa dini wanajilimbikizia mali yameibuka upya wiki iliyopita baada ya baadhi ya waumini wa Kanisa la Efatha jijini Dar es Salaam kugundua kuwa  Mtume na Nabii wao, Josephat Mwingira  ameiambia Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi kuwa  ‘amefyatua’ jumba la kifahari lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja katika kiwanja kilichopo Kawe Beach, wilayani Kinondoni.
Waumini hao wamekuja juu baada ya Mwingira (pichani) kudai mahakamani kuwa jumba hilo amelijenga kwa fedha zaidi ya shilingi bilioni moja lipo kwenye eneo lake ambalo ni kiwanja namba 548 (b)  Kawe na alipewa na Wakili Evarist Hubert Mbuya aliyeibuka mahakamani hapo na kudai kuwa eneo hilo ni lake kihalali.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya waumini walioomba majina yao kuhifadhiwa walidai kuwa Mwingira amejilimbikizia mali kwa sababu jumba lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja ni la kifahari mno ukilinganisha na hali ya uchumi ya waumini wake wengi.
“Sadaka zingetumika kufanya shughuli za kijamii zaidi. Hatuoni sababu ya kiongozi wetu kujenga jengo la kifahari kiasi hicho wakati kuna mipango mingi ya maendeleo ya kanisa inahitaji fedha,” alisema muumini mmoja wa kike ambaye alionesha waziwazi kuwa upande mwingine wa imani baada ya kudai kuwa waumini wananyonywa.
Hata hivyo, muumini mwingine wa kiume alisema alishtushwa sana aliposoma kwenye gazeti kuwa Mwingira aliiambia mahakama kuwa ana jengo lenye thamani ya zaidi ya shilingi 1,000,000,000.
“Hayo ni mambo ya kidunia, anatufundisha tusiwe na tamaa ya kuwa na vitu kama hivyo na badala yake tuwekeze mbinguni, iweje anakuwa na jengo lenye thamani kubwa kiasi hicho?” alihoji muumini huyo.
Mwandishi wetu alimpigia simu Mwingira ili aweze kufafanua kuhusu madai ya waumini wake, awali mtu aliyepokea alisikiliza kile alichoulizwa na mwana habari huyo, akajibu kuwa yeye siyo kisha akakata simu.
Hoja ya kiongozi huyo kujenga jumba kubwa la kifahari aliibua mwenyewe wakati wa kesi yake na Wakili Mbuya ambapo kupitia kampuni ya uwakili ya Ligal Link Attorney, amedai kujenga jengo hilo la thamani kwenye kiwanja hicho hali iliyofanya waandishi wetu kwenda na kuliona (Angalia picha ukurasa wa mbele).
Mwingira kupitia kampuni hiyo  ya Mawakili ya Ligal Link Attorneys alifungua kesi namba 226 /2010, Agosti 23, mwaka jana katika Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi akitaka itoe amri ya utekelezaji wa kile alichokiita mkataba wa ugawaji wa eneo.
Katika madai hayo, Mwingira anaomba Mbuya alipe gharama  ya kesi na mambo yote ambayo mahakama itaona inafaa.
Hata hivyo, Mbuya naye kupitia kwa wakili wake, Michael Ngalo ameiambia mahakama hiyo kuwa eneo hilo alilojenga Mwingira ni lake na alishaghairi kulipa kanisa.
Ameiomba mahakama iamuru ‘mjengo’ huo ubomolewe kwa kuwa haukujengwa kihalali na imuondoe na Mwingira aamuriwe kulipa gharama zote za zoezi hilo.
Mbuya amekwenda mbali zaidi kwa kuiambia mahakama kuwa gharama za kubomoa mjengo huo ni shilingi za Kitanzania milioni 56.
Alisisitiza hoja yake kuwa eneo hilo ni lake kwa kutoa nakala za nyaraka za serikali kutoka Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi yenye kumbukumbu namba LD/184624/17 ya Juni 17, 2010  na nyingine ya Machi 11, 2011 yenye kumbukumbu namba LD/184624/24.

Views: 5590

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by kaka on February 26, 2012 at 9:01am

TAFUNA SADAKA KAKA WAKIAMBIWA DINI NI MOJA WANAKUWA WAKALI KAMA PILIPILI MBUZI

 

Comment by Ludovick Peters on February 19, 2012 at 2:40pm

kanisa la ukweli ni moja tu. Hayo mengine yote ni ya kitapeli tu

Comment by baraka ndesamburo on February 19, 2012 at 10:51am

wonders shall never end haya makanisa mapya nayo mhhhh kweli dalili za siku za mwisho zimenza kuonekana

Comment by Abihudi Kissai on February 16, 2012 at 1:02pm

too bad,not interesting kwa watumishi ka hawa

Comment by Ukweli100 on February 16, 2012 at 3:54am

mwisho wa watu kama hawa ni aibu yao!

kuliko kuchoma sh mil 56 nyingine, ni suala boara kama nyumba inaweza kutaifishwa au kufanyiwa shuguli nyine za kibiashara na maendeleo

Comment by saidi on February 15, 2012 at 8:02pm
Mtolee mwanaa saadaka
Comment by Bacron Lyimo on February 15, 2012 at 4:38pm

hamkujua mlipo jiunga

Comment by issa m moshi on February 15, 2012 at 8:06am

mkiambiwa hizi dini zingine nibiashara mnakuwa mbogo,iko siku mtaujuwa ukweli sasa hivi bado kwanza.

Comment by Beatus Nchemwa. on February 14, 2012 at 8:30pm

acheni kulalamika, biblia imeandikwa kuwa wataibuka manabii wa uongo! ndo hao wanaotafuta utajiri kupitia imani za watu! wajinga ndo waliwao!

Comment by bongo on February 14, 2012 at 7:08pm

Vyoote hivo vizuri mtaviacha duniani na mtalala ktk masanduku na kufukiwa chini ya ardhi na wala hakuna kutoa hewa.Na hatimae kazi itaanza kaburini kusikilizwa mashitaka yote kama vilipatikana kwa uhalali au kidhulma.Na mwisho wa dunia ndio uamuzi wa mwenyezimungu ndio utakaoweza kujijua ubaya ulioufanya duniani kama ni peponi au motoni kwani mwenyezi mungu hapendi dhuluma huwa anajali haki tu.

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

andi posted a status
1 minute ago
vitalia posted a status
1 minute ago
GLOBAL's 10 blog posts were featured
2 minutes ago
andi posted a status
2 minutes ago
misu babu posted a status
3 minutes ago
andi posted a status
3 minutes ago
misu babu posted a status
4 minutes ago
misu babu posted a status
4 minutes ago
andi posted a status
5 minutes ago
misu babu posted a status
6 minutes ago
tahmina sultana posted a status
6 minutes ago
tahmina sultana posted a status
6 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }