Utajiri wa Babu Loliondo kufilisiwa

Mojawapo ya magari anayomiliki babu Ambilikile Masapile.

Na Mwandishi Wetu
MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’ (pichani), anaendelea kusakamwa na wagonjwa wanaodai hawakuponyeshwa na dawa yake, wapo walioweka nia ya kumburuza mahakamani lakini mpya ni pendekezo la kumfilisi.


...nyumba yake mpya.


Wanaharakati wameeleza kuwa miongoni mwa mashtaka ambayo wanamfungulia Babu Ambi, mojawapo ni kumfilisi mali zote alizochuma endapo atakutwa na hatia ya ulaghai, wakati wa kutangaza maono aliyopewa na Mungu kuhusu tiba ya kikombe.


Wanadai kuwa Babu Ambi, mkazi wa Kijiji cha Samunge, Loliondo, alitumia matatizo ya Watanzania  ya kuugua maradhi sugu ili kujinufaisha, hivyo akatengeneza ulaghai wa tiba ya kikombe kwa maelezo kwamba ni ufunuo aliopewa na Mungu.

Madai hayo yanakuja wakati ambao Babu Ambi ameukata, ameshakamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kisasa kijijini Samunge, pia anamiliki magari mawili ya bei mbaya, Toyota Land Cruiser (pick-up) na Isuzu (pick-up).

Babu Ambi, ameshahama nyumba chakavu aliyokuwa anaishi zamani na sasa anaendesha maisha yake kwenye mpya ya kisasa ambayo kwa Samunge, inaonekana ni kama Ikulu kwa jinsi inavyomeremeta.


...sola anayotumia nyumbani kwake.


Wakati Babu alizoea kukanyaga vumbi kwenye nyumba yake ya awali ya udongo, yenye chumba kimoja cha kulala, hivi sasa anatembea juu ya sakafu iliyotandikwa vigae (tiles) kila eneo.

Nyumba ya Babu, pia ina kila kitu ambacho hustahili kuwemo kwenye nyumba ya kisasa yenye hadhi ya mtu mwenye fedha, vile vile ina umeme wa mionzi ya jua na maji ya uhakika.
Mali zote hizo, wanaharakati wanataka zifilisiwe kwa sababu zimepatikana kwa njia ya udanganyifu.

Muungano wa Vyama vya Watu  Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (Tanopha) ni wanaharakati wa kwanza kutoa tamko la kumburuza mahakamani.

Tanopha wanasema, miongoni mwao, walitumia kikombe cha Babu Ambi lakini hakuna hata mmoja aliyepona.
Wanasema, kila walipokwenda kupima ili waone matokeo ya tiba ya kikombe, majibu yalikuwa ni yaleyale kwamba hakuna mabadiliko.


...babu akiwa amepozi nyumbani kwake.


“Hatuwezi kupoteza muda na fedha zetu kwa kwenda kunywa dawa  ambayo haitibu, hii ni kuwarubuni  wananchi, wengi wameuza mali zao, wengine  kutumia akiba ya fedha walizokuwanazo kwenda Loliondo wakijua wangepona lakini cha kushangaza ni kwamba baadhi yetu wanakufa.

“Wengine wako mahututi baada ya  kupewa kikombe, tulikuwa na matumaini ya kupona hadi tuliacha kutumia vidonge vya kurefusha maisha vya ARV, hatuna mengi zaidi ila tunaomba umtafute mwenyekiti wetu akueleza zaidi,” alisema mmoja wa wanachama wa Tanopha.

Mwenyekiti wa Tanopha, Julius Kaaya, aliliambia Uwazi kwa njia ya simu kuwa taasisi yake ilipeleka watu 14 kunywa dawa Loliondo lakini hakuna hata mmoja aliyepona.

“Nakumbuka kwamba kipindi  tunaenda huko Loliondo Machi 19, mwaka huu, tulifanya mkutano na waandishi wa habari, tulifika Samunge Machi 22, ambapo Machi 24 walikunywa dawa hiyo kila mmoja  akiwa na matumaini ya kupona.

“Baada ya siku 20 tangu wanywe dawa hiyo walienda hospitali kuangalia  kama wamepona, daktari aliwaambia  hakuna hata mmoja aliyepona, siku 90 baadaye majibu yakawa yaleyale,“ alisema Kaaya.

MCHUNGAJI MTIKILA
Naye Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation, Christopher Mtikila kwa upande wake amesema kwamba dawa hiyo haitibu na analishughulikia suala hilo ili kumfikisha mahakamani pamoja na mawaziri, wabunge na viongozi wa  juu waliokunywa kikombe.


...mjengo wake mpya.


“Mawaziri hao wamewahamasisha wananchi kwenda Loliondo kunywa dawa, lazima tuwashitaki pamoja na viongozi wa dini waliopiga debe,” alisema Mtikila. Viongozi wa dini waliohamasisha ni Askofu Thomas Laizer na Martine Shayo.

Baadhi ya Mawaziri waliopata kikombe ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli. Wengine ni wabunge Augustino Mrema, Edward Lowassa na wakuu wa mikoa Yohana Balele na Abbas Kandoro.

TAMKO LA WIZARA
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda, alisema hivi karibuni kuwa kikombe cha Babu siyo tiba na kwamba wote waliokwenda Loliondo, walipoteza muda.

Kauli ya waziri, ilifuatia ripoti ya uchunguzi wa madaktari bingwa kwamba kikombe cha Babu wa Loliondo, hakitibu.

WABUNGE NAO
Katika Mkutano wa Tano wa Bunge la 10, baadhi ya wabunge walitaka Babu wa Loliondo achukuliwe hatua kwa sababu dawa yake haitibu.

Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, alikwenda mbali zaidi kwa kutaka mawaziri waliokwenda Loliondo, wahojiwe na waseme kama wamepona, kwani wao kwa kiwango kikubwa walihusika kupotosha umma.


...babu Ambi akiwa amepozi, pembeni ni bafu la kisasa analotumia kwa sasa.


UTETEZI WA BABU
Kwa upande wa Babu Ambi, ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa dawa yake imeponyesha wengi.

“Kama hawajapona siyo makosa yetu. Tuliwaambia kabla kuwa katika tiba hii kigezo cha kwanza ni kuwa na imani na hapa tuna uthibitisho wa kutosha wa watu walioponywa na maajabu ya dawa hii wakiwemo wagonjwa wenye Ukimwi,” alisema Babu Ambi na kuongeza kuwa anapigwa vita na wengi kwa sababu ya wivu.

Kuhusu utajiri wake, alisema kuwa yeye hana mamilioni ya fedha kama inavyodaiwa ila akakiri kumiliki nyumba ya kisasa pamoja na magari mawili ambayo amesema yanamsaidia kubeba dawa pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Loliondo.

KUHUSU KIKOMBE
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa KKKT Arusha, Thomas Laizer, zaidi ya watu milioni tatu wameshatibiwa Loliondo.

Kila mgonjwa alikuwa analipa shilingi 500, hivyo kwa hesabu ya watu milioni tatu, maana yake kikombe kimeshaingiza zaidi ya shilingi bilioni 1.5.

Views: 8791

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Paul Freddo on December 13, 2011 at 6:21am

Wangapi wamekufa Muhimbili?

Wangapi walienda kutibiwa ulaya wakafariki (akiwemo baba wa Taifa)?

Wangapi wamepona kwa babu?

Ndege ngapi zimeua watu kwa matatizo ya kiufundi?

 

Nyumba ya babu ya kisasa?

Tuache utani jamani. Mlishaona mabafu na nyumba za mafisadi.

 Mafisadi wanachukua ma-BILION US$ serikalini tunawaogopa.

Babu tumempa pesa wenyewe, tunantaka tumfirisi.

 Someni Biblia Yohana Sura ya NANE;

“Hebu Yeye asiye na dhambi atupe jiwe la kwanza”

Comment by Kim Matola on December 7, 2011 at 11:01pm

Babuuu!

Comment by Kim Matola on December 7, 2011 at 11:01pm

Babu alishasema toka awali imani yako ndo itakuponya. Hili swala la kiroho zaidi kumpeleka mahakamani ni kupoteza mda ...

Comment by pjoan audes on December 7, 2011 at 5:43pm

Wamwache Babu wa watu, mbona hata Hospitali kuna wanaopona na wasiopona pia?!

Comment by ROSE on December 7, 2011 at 2:34pm

Akili kichwani hamna mtu aliye lazimishwa kwenda kwa Babu kupata kikombe kila mtu alikwenda kwa hiari yake mwenyewe, Babu asisumbuliwe na mali zake.

Comment by Kakytee The Director on December 6, 2011 at 3:56pm

duh kawapata kweli mia 5 mia5 nyingi sana kwa kweli na msuruuru wa wajinga waliokuwa wakenda si mchezo

Comment by kokwenda shumbusho on December 6, 2011 at 11:34am

Sasa mnalalamika nini kuna m2 aliwafunga kamba na kuwavuta muende kupata kikombe si mlitaka wenyewe sasa masuala ya kumfilisi babu na kutaka kumfikisha mahakamani yametoka wapi tena muachani Babu wa watu ale vinono afaidi matunda yake

Comment by JOSEPH G MALEKO on December 5, 2011 at 8:02pm

DAH ACHENI UJINGA HIVI KUNA M2 ALIEMLAZIMISHA KWENDA LOLIONDO!KAMA SIO SHIDE ZENU NANI ANGEFATA KUMBUKENI MWENYE SHIDA NDIO MFUATA HUDUMA

Comment by Lillian Kitunga on December 5, 2011 at 10:20am

jamani acheni ujinga kwani kuna mtu alilazimishwa kwenda kunywa kikombe?? Je kila dawa unayotumia inatibu?? hta malaria hukataa dawa lo

Comment by kadama J'z on December 4, 2011 at 8:58pm

teh teh teh aaah nyie acheni mambo ya ajabu bwana kumbukeni kwanza babu alisema tanguliza imani yako kwanza ndio utapona sasa kama wewe ulienda kwa kujaribu ngoja nione kama tapona maana yake hukua na imani na kikombe chake so kama vipi nyie pigeni kimya muacheni babu wa watu apumzike bwana.


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
8 minutes ago
GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
8 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website