NI matumaini yangu kuwa wadau wa kolamu hii ya ujasiriamali ni wazima wa afya, karibuni tena kwenye mada mpya ya soko la hisa. Kabla ya kuendelea mbele, tukumbushane kwa kifupi yale tuliyojadili kwenye mada iliyomalizika wiki iliyopita.
Tuliianza mada yetu kwa kuangalia maana ya ujasiriamali na mbinu zinazoweza kukufanya upate utajiri wa kudumu.
Pia tuliangalia vitu vya msingi ambavyo wewe kama mjasiriamali unatakiwa kuvizingatia unapotaka kuanzisha biashara mpya, kuendeleza biashara uliyonayo au mambo ya kufanya inapotokea biashara yako imetetereka.
Ni matumaini yangu kwamba umejifunza mambo mengi ambayo yamekuongezea hali ya kujiamini na kukupa nguvu ya kusonga mbele, kuelekea kwenye mafanikio ya kweli.
Leo nakuja na mada mpya inayohusu soko la hisa. Nadhani wengi bado hawaelewi hisa ni nini na zina faida gani kwa wajasiriamali. Twende pamoja hatua kwa hatua ili tujifunze.
HISA NI NINI?
Hisa ni mgao (share) ya umiliki wa kampuni au biashara yoyote kubwa. Unaponunua hisa maana yake umetoa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa kampuni au biashara husika kwa hiyo na wewe ni miongoni mwa wamiliki na nguvu au umuhimu wako unatokana na mgao ulionao.
Kama kampuni ina mtaji wa shilingi laki moja na wewe umenunua hisa za shilingi elfu hamsini, maana yake utakuwa na nguvu ya kushiriki hata kwenye maamuzi nyeti yahusuyo kampuni au biashara husika, tofauti na mtu mwenye hisa za kwa mfano shilini elfu kumi.
Soko la hisa (stock exchange) ni mfumo wa kibiashara ambapo wajasiriamali na wafanyabiashara, hununua vipande (stock) za kampuni au biashara na kuwekeza fedha zao kwenye mtaji kwa lengo la kuisaidia biashara husika kuendelea kukua. Soko kubwa zaidi duniani lipo jijini New York, Marekani likiwa na jina la New York Stock Exchange (NYSE).
Kwa mujibu wa shirika la fedha duniani, soko la hisa ndiyo linaloongoza kwa kuingiza fedha nyingi kwenye mzunguko kuliko biashara nyingine zozote, takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2008, mtaji katika soko la hisa dunia nzima ulikuwa ni dola za Kimarekani, trilioni 36.6 na mpaka mwezi Juni mwaka huu, mtaji ulikuwa umepaa na kufikia dola za Kimarekani trilioni 791, ikiwa ni mara kumi na moja zaidi ya uchumi wa dunia.
Huu ni uthibitisho kuwa soko la hisa linakua kwa kasi kubwa na ndiyo lililoushikilia uchumi wa dunia. Kwa msingi huo, ni lazima kila mjasiriamali ajifunze juu ya soko la hisa ili kuyafikia mafanikio ya kweli.
Wiki ijayo tutaendelea kufafanua juu ya faida za soko la hisa na jinsi wajasiriamali wanavyoweza kunufaika nalo.
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
NDAUKA the GREAT |
| 3 |
julius manning |
| 4 |
LJH_3 |
| 5 |
hope |
| 6 |
Tatu Majaliwa |
| 7 |
mayalilwa |
| 8 |
steven emmanuel |
| 9 |
Matilanga Lukingita |
| 10 |
Mishy chunga |
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies 0 Likes
JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies 8 Likes
Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies 3 Likes
Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…
Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE yesterday. 27 Replies 5 Likes
HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies 4 Likes
Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…
Tags: SOKA
Started by GLOBAL in Habari. Last reply by Billy Frank Irungu Apr 26. 118 Replies 21 Likes
Tags: NCHINI, HAPA, UNAFURAHIA, HUDUMA, ZAKE?
Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies 4 Likes
hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?
Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies 9 Likes
Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…
tina babi left a comment for JOHN KAZUNGU© 2013 Created by Global Publishers.




You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers