MBUYU: MTI WENYE FAIDA LUKUKI KIAFYA

Mungu ameumba miti na mimia kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

UBUYU WENYEWE
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una Vitamin C nyingi kuliko hata machungwa na ina kiwango kingi cha madini ya kashiamu (Calcium) kuliko hata maziwa ya ng’ombe.
Aidha, unga wa ubuyu ni chanzo kikubwa cha madini mengine aina ya chuma (iron), Potasiamu (Pottasium) na manganizi (magnesium). Inaelezwa kuwa kiwangao cha Potasiamu kilichomo kwenye unga wa ubuyu ni mara sita zaidi ya kile kinachopatikana kwenye ndizi. Ubuyu ni muhimu sana kwa watu wenye matatizo ya figo.
Vile vile unga wa ubuyu una uwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili  (antioxidant) kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vya kuongeza kinga mwilini dhidi ya magonjwa nyemelezi. Kiwango chake kinazidi hata kile kinachotolewa na matunda mengine kama vile Krenberi, bluberi na blakberi. Ili upate faida za unga wa ubuyu zinazoelezwa hapa, lazima ule ubuyu halisi usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha.

MAFUTA YA UBUYU
Mafuta ya ubuyu, ambayo hutengenezwa kutokana na mbegu zake, ni mazuri kwa kulainisha ngozi na kukarabati au kuponya ngozi iliyoathiriwa na magonjwa ya ngozi mbalimbali, ikiwemo fangasi, vipele na chunusi.
Mafuta ya ubuyu yana uwezo wa kuifanya ngozi kuwa nyororo na laini kutokana na kuwa na kiasi kingi cha mafuta aina ya Omega 3 na Omega 6 na ina kiasi kingi cha Vitamin A, D na E ambazo zote ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa ngozi ya binadamu.
Mafuta ya ubuyu yanaelezwa kuwa na virutubisho vinavyoweza kuondoa mikunjo ya ngozi, mabaka, michirizi na hata makunyazi na kuicha ngozi kuwa mpya. Hutoa kinga dhidi ya uharibifu wowote wa ngozi unaoweza kujitokeza baadaye.

JINSI YA KUTUMIA MAFUTA
Mafuta ya ubuyu unaweza kuyatumia kwa kupaka usoni au mwili mzima moja kwa moja. Unaweza kuyatumia mafuta haya kwa kupaka sehemu tu iliyoathiriwa kama dawa. Unaweza pia kuchanganya na mafuta au losheni unayotumia.
Ili kupata matokeo unayotarajia, hakikisha unatumia mafuta halisi ya ubuyu ambayo hayajachanganywa na kitu kingine wakati wa kutengeneza.

UPATIKANAJI WAKE
Bidhaa za ubuyu zimeanza kujipatia umaarufu nchini Tanzania na hivi sasa kuna makampuni na wajasiriamali binafsi wanaojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na ubuyu, hivyo upatikanaji wake ni rahisi iwapo utaulizia maeneo unayoishi.
Bidhaa zingine zinazoweza kutengenezwa kutokana na mti huu ni pamoja na majani yake ambayo hutumika kama dawa, mizizi na magamba yake pia. Kwa ujumla mti wote wa ubuyu una faida na hakuna kitu kinachotupwa kwenye mti huu ambao ni miongoni mwa miti yenye matunda bora yaliyopewa jina la ‘superfruit’.

Views: 11999

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by kabebiiiii on May 15, 2012 at 11:06am

Ni kweli ubuyu ni dawa kubwa sana hasa mafuta, lakini wapi tunayapata? kwa bei gani kwani ushauri wangu waweke katika paki ndogo ndogo ili kila mtu anunue yale ambayo anauwezo.

 

 

Comment by OMAR INT: (NO FLY ZONE) on May 6, 2012 at 3:20pm

jiti kubwa tu lakini pia lina hasara yake!hata kibao cha kukalia hupati kazi kufuga majini tu!

Comment by Ndegesha on May 2, 2012 at 11:56pm

faida tumeisha pata asante

Comment by julius manning on May 1, 2012 at 5:25pm

nimekubali yamejaa sana shambani mwangu nataka niyakatilie mbali yananiharibia mavuno

Comment by lety. on May 1, 2012 at 3:07pm

ahsanteni kwa somo zuri.

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ Dec 16. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson 13 hours ago. 13 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by maleka sakeha yesterday. 30 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson 12 hours ago. 13 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson 14 hours ago. 38 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }