UANDISHI WA FILAMU NA MAIGIZO

JIFUNZE NAMNA YA KUANDIKA NA KUANDAA SCRIPTS

MUUNDO WA HADITH


SEHEMU YA NNE (4)

NGUZO KUU NNE ZA KUSIMULIA HADITHI NDANI YA SCRIPT

SUMULIZI NDANI YA UANDISHI WA SCRIPT

Ukiwa kama mwandishi wa script, ni hadithi ndani ya Script yako haswa itakayofanya utambulike. Hadithi yenye gumzo ndiyo itakayo watongoza mawakala na maproducer na kuwafanya kuisoma Script yako, wakati huo huo wahusika wakiikamilisha hadithi. Unaitaji hadithi yenye kumvuta mtu kwenye uhalisia ata kwa lazima, ili kumpa kibali Muhusika kukua na kuwafanya wasomaji (na haswa watazamaji) kuhusika kihisia.

Kusimulia hadithi ndani ya Script, ni mfumo ambao hautumii maneno tu, bali zipo njia ambazo hutumika ambazo katika Chuo cha sanaa hii, huitwa “NGUZO ZA SIMULIZI NDANI YA SCRIPT”

Na ili kuwafanya wasomaji au watazamaji kuipata hisia iliyotarajiwa ni lazima Nguzo kuu nne za kusimulia hadithi,kipindi ukiandika script zitumike, ukifanikiwa hapa utaweza kutengeneza Hadithi ya mfano wa kuigwa ndani ya script ambayo itakutambulisha kwa Wataalamu wengi wa Filamu ndani na nje ya nchi.

Zifuatazo ni nguzo kuu nne za Kusimulia Hadithi ndani ya Script

  1. Kumpa muhusika lengo

Kila mtu katika maisha analengo moja kuu. Sasa hivi, inawezekana lengo lako kuu ni kuwa Mwandishi m-bobezi wa Uandishi wa script na unajitahidi kutimiza hilo lengo kwa kuandika mara kwa mara, na pia kupitia darasa kama hili, lakini Lengo hili huwa ni tamu zaidi pale unapomtazama mtu akilifanikisha kupitia Filamu, kwa maana atakuwa na mwanzo, katikati na mwisho.Mpe Muhusika Lengo ambalo litamfanya kulitimiza kivitendo na kuhusisha maisha yake katika hilo. Ifanye iwe ngumu kulitimiza lengo na onesha namna wanavyo onekana pindi inavyo kuwa ngumu lengo lao kutimia.

LaziMa pawepo hatua katika hadithi ambapo itaonekana kwamba Muhusika hatoweza kamwe kufikia lengo, lakini hatimaye tengeneza suruhisho litakalo sababisha lengo kutimia.

  1. Mtengenezee changamoto Muhusika wako.

Tambua kwamba hadithi yako hutengenezwa zaidi katika kipindi ambacho Muhusika anapitia kipindi kigumu zaidi katika Maisha yake. Labda alikuwa analengo la kuja kuwa na ndoa na pia kuwa na watoto wa damu yake, lakini katika kupima anakutwa na VVU, onesha changamoto atakazo kutana nazo ili kufikia lengo, na umfanye aone kwamba haiwezekani kuolewa na umfanye aone kwamba ndoto za kujakuwa na Watoto wa damu yake zimekufa, Tambua kwamba changamoto hizo ndizo zitakazo badirisha Lengo lake. Tambua kwamba mtu anaweza kuolewa na kuoa au kuwa na watoto wasio na virsui ata kama atakuwa na VVU, kwahiyo utatafuta njia ya kumfanya ajikomboe, sikuzote katika script, Muhusika ndiye anayejikomboa, asitokee mtu na kumkomboa bali ajikomboe, yawezekana ni kwakumtumia mtu atakaye kumuelimisha na kisha yeye binafsi kupiga hatua dhidi ya changamoto zinazo mkabili,kihisia au kimwili.

Kunatatizo kubwa ambalo limekuwa likizikabili jamii nyingi, nalo ni kusubiri mtu aje akukomboe, au aseme badala yako, huu ni uvivu, na katika script hili ni tatizo,ni lazima itafutwe namna ya kumfanya huyu anaye subiri aache uvivu na kuamua kujikomboa mwenyewe, kimisuli, kielimu, kiroho(Maombi) au kihisia.

Katika Nguzo hii, siku zote Muhusika anapokuwa mvivu maana yake kila kitu kipo, hana haja ya kujikomboa maana haoni kama amefungwa, ili kumuamisha hapo Tumia Changamoto nzito.

Hata wale ambao wamefanikiwa na wanajituma kwa bidii ili kufikia lengo fulani kila wanapokaribia kufika katika lengo lao watupie Changamoto nzito haswa, na kumuweka katika Moto, kwa njia hii unampa nafasi Muhusika Kukua na kupanuka ndani yao mwishoni mwa hadithi

  1. Onesha namna Muhusika anavyo pambana na CHANGAMOTO

Maswali ya kujibu; Ni changamoto zipi ambazo Muhusika anazishughulikia vizuri?, zipi ambazo zinamsumbua? Anajifunza nini katika Vipingamizi hivi?

Tambua kwamba Mfumo wa kuandika Scene katika script yako, huwa katika Mlolongo wa safari ya kimaisha ya Muhusika wako,hii ni Pindi unapokuwa na Nusu nyama. Tambua kwamba Script ni lazima sikuzote ijihusishe zaidi na safari ya Muhusika wako, anapambanaje?, anakutana na nini?, bila mzunguko huu, script yako itajawa na ubababishaji. Na huu ndio msingi wa hadithi, kama ukidharahu huu msingi, Script yako haitoweza kutembea.

  1. Nguvu za Ndani na Nje

Hadithi siku zote husogea mbele kupitia Migogoro. Migogoro hutokea kwa kupitia Nguvu mbili,ambazo ni Nguvu ya ndani na ya Nje. Nguvu za Nje mara nyingi huwa ni “Waovu/watu wabaya/wenye nia mbaya n.k” na pia inaweza ikawa ni Matukio ya hatari ya hasiri “Natural disasters” au Mahusiano yasiyo eleweka “ complicated relationships” na mengineyo. Haya yote ni Vikwazo vya kimwili ambavyo vinamrudisha nyuma Muhusika wako Mkuu. Na huwa vinamfanya Msomaji atamani kuingia katika script ili kumsaidia Muhusika wako kupambana navyo.

Lakini kiukweli kabisa, ni Nguvu za ndani ambazo ndizo zinazo mrudisha nyuma Muhusika wako. Zile hisia zote za kuachilia na kufadhaika ndizo zinazo wasababisha kujiumiza wao wenyewe.Hivi vitabia vya ndani/Nguvu za ndani ndizo ambazo ni kizuizi cha Maisha ya Muhusika wako, na katika hadithi hizi ndizo zitakazo mkong’ota zaidi. Na kumuhumiza sana. Lakini kwa kuzipiga hizi nguvu za ndani ndipo Muhusika Mkuu hupata utukufu wa kweli. Labda atajifunza namna ya kujikubali au kushirikisha hisia zake kwa mke wake au watoto wake n.k. Pindi Muhusika wako atakapokuwa huru mbali na Uchafu wake wa kihisia ndipo atakapoweza kutembea kwa uwazi na kuwa sababisho la wengine kuwa na furaha, na kuanza safari ya kukamilisha lengo lake.

…Nimeamua kumalizia Vipengere vilivyo ndani ya “MUUNDO WA HADITHI” na zimebakia vipengere vifuatavyo

                  5. Uwazi wa Kipande cha Uigizaji  (Scene)

              6. Migogoro katika Uandishi wa Script

                  7. Kutengeneza Kipande cha Uigizaji chenye mvuto

                  8. Jenga Hadithi yako

                  9. Hadithi sambamba (Parallel Storylines)

                10. Kuheshimu Mipaka ya Muundo wa Hadithi

                11.Uandishi wa Aina Mbalimbali za Hadithi:Filamu za Vichekezo (Comedy)

                12. Uandishi wa Aina Mbalimbali za Hadithi:Filamu za vitu visivyo hasilia ( Sci-Fi)

                13. Uandishi wa Aina Mbalimbali za Hadithi:Filamu za Mapambano (Action)

Nitajitahidi kuanzia leo kwa Muda wa siku Tisa niweze kumalizia Vipengere hivyo vyote, kwa hiyo tukutane kesho…


Views: 466

Tags: , , BONGO MOVIE, BONGOWOOD, DAR-ES-SALAAM", DODOMA, FILAMU, HOLLYWOOD, KENYA MOVIE,, MAIGIZO, MOVIE, More…TANZANIA, UANDHISHI, UGANDA, UIGIZAJI

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by RIZOS on March 23, 2012 at 8:55pm

Safi sana kaka kwa uundaji na utengenezaji wa Film je ningependa sana tuwasiliana nawewe barua pepe yangu nii _:rbabingwa@yahoo.com

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }