Gladness Mallya na Hamida Hassan
MENGI yamesemwa na yanaendelea kusemwa kwamba, mpaka kifo chake, Marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ alikuwa mwanachama wa imani ya Freemason (wajenzi huru) ambayo inashika kasi katika nchi za Kiafrika, lakini mama wa marehemu, Flora Mtegoa ametoa tamko juu ya tuhuma hizo za mwanaye.

Akizungumza na waandishi wetu hivi karibuni nyumbani kwa marehemu Kanumba, maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza jijini Dar, mama Kanumba alisema amesikia kuwa mwanaye alikuwa muumini wa imani hiyo yenye utata duniani.

Lakini akasema: “Namjua Kanumba, alikuwa mwanangu, mambo yake mengi nilikuwa nayajua maana tulikuwa tunaishi kama marafiki, habari hizo si za kweli.

“Watu wanasema sana, sijui wanatumia vigezo gani? Mwanangu alikuwa muumini mzuri sana wa Kanisa la African Inland Church (AIC), sasa huo u-Freemason aliuchukulia wapi?”

 Akizidi kumimina maneno kwenye kalamu za waandishi wetu, mama Kanumba alisema kuwa kama ni suala la picha ambazo watu wanasema alipiga akiwa na mapozi ya imani hiyo, ni kwa kutokujua lakini si kweli kwamba alikuwa muumini wa jamii hiyo.
“Huo ni uzushi uliopitiliza,” alisema mama Kanumba.
VIGEZO VYA WATU MITAANI
Wengi mitaani wamekuwa wakisema baadhi ya picha za marehemu Kanumba zilionesha viashiria vya kuwa mfuasi wa imani hiyo ambayo mpaka sasa Watanzania wengi hawaijui vizuri.
KIGEZO CHA PICHA
Zipo baadhi ya picha ambazo marehemu Kanumba anaonekana akiashiria alama za Freemason. Mfano, kuna picha ambayo mkono wake wa kulia ameweka vidole mfano wa pembe za mbuzi.

 Aidha, kuna picha marehemu amevaa tisheti nyeusi yenye picha kubwa ya fuvu la binadamu linalodaiwa kuwa miongoni mwa nembo za Freemason. Picha nyingine marehemu amevaa cheni yenye kidani ambacho kinasadikiwa ni utambulisho wa u-Freemason.
SUTI YA MAZISHI
Miongoni mwa magumzo yaliyotikisa siku ya kuuaga mwili wake ni suti nyeusi aliyovalishwa ambapo upande wa kushoto wa koti kuna nembo inayotafsiriwa ni ya Freemason.
Waandishi wetu waliwasiliana na mama wa marehemu na kumuuliza nani aliyemvisha koti hilo, yeye alijibu kwa kifupi:
“Sijui ni nani?”
KASI YA MAFANIKIO
Kigezo kingine ambacho baadhi ya watu wamekuwa wakikiamini kwamba marehemu alikuwa muumini wa dini hiyo ni kasi ya mafanikio yake.

 Wengi wanasema kuwa marehemu Kanumba alikuwa mcheza filamu kama wengine, wakiwatolea mfano akina JB, Rich, Frank, Pastor Muyamba, Claud, Dk. Cheni na wengineo, lakini yeye kasi ya maendeleo ilikuwa kubwa zaidi ukilinganisha nao.
Kwa sababu hiyo, baadhi ya watu wakasema kuwa wamesikia mtu anapokuwa Freemason anawezeshwa kwenye shughuli zake kwa kuwa na bahati ya kutajirika.
MVUTO NAO WATAJWA
Baadhi ya watu wamekuwa wakitaja mvuto aliokuwa nao marehemu kwamba nao ni dalili tosha kuwa alikuwa kwenye imani hiyo.

 Wengi waliodai wana elimu kuhusu Freemason walisema kuwa, mara nyingi mwanachama wao hupoteza maisha wakati nyota yake ikiwa inawaka sana.
Walitoa mfano wa marehemu Pepe Kalle, kwamba alipotoa albamu ya Cocktail aliwika sana na ndipo alipoaga dunia ghafla.
KANUMBA NA MASTAA WENGINE
Bado wengi wanazidi kuamini kifo cha ghafla cha Kanumba kinafanana na cha maarufu wengine duniani, marehemu Michael Jackson ‘The Jacko’, Whitney Houston na Madilu System ambao pia walihusishwa na u-Freemason.
RAMSEY NOAH ANYOOSHEWA KIDOLE
Watu hao wanaopepeta huko mitaani kuwa marehemu Kanumba alikuwa muumini wa imani hiyo walizidi kuibua mapya ambapo wanaamini nyota wa filamu za Nollywood (Nigeria), Ramsey Noah naye ni mwanachama wa dini hiyo.
Wakadai mcheza filamu huyo alikuja Bongo na kucheza na Kanumba Filamu ya Devil’s Kingdom ambayo sehemu kubwa ya stori ni maisha ya imani ya Freemason.

 “Mimi nina wasiwasi na Noah (Ramsey), yule jamaa nasikiasikia naye ni muumini, sasa alikuja hapa kwetu (Tanzania) akacheza na marehemu filamu ya Devil’s Kingdom, huenda alimuingiza mwenzake kwenye imani hii,” alisema Rukia, mkazi wa Ubungo Kibangu jijini Dar.
Ili kunogesha habari hizo, ilidaiwa kuwa baadhi ya waigizaji wa filamu hiyo akiwemo Ramsey mwenyewe walipatwa na masahibu ambapo ukiacha Kanumba aliyefariki, staa huyo wa Nigeria alipata ajali huku Kajala Masanja akisota Segerea hivyo inawezekana walibumburua siri za Freemason kupitia Devil’s Kingdom, jambo ambalo waumini wa imani hiyo hawakulipenda.

KUTOKA KWA MHARIRI

Hakuna muda maalumu ambao mtu amepangiwa kupata utajiri, umaarufu au ushawishi hivyo sisi tumejaribu kuwasilisha kile kinachosemwa mitaani ambapo tunaamini mama mzazi wa marehemu Kanumba amemaliza utata hivyo mjadala huo umefungwa rasmi.

Views: 22598

Tags: risasi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by eric samuel on May 3, 2012 at 12:01pm

UZUSHI TUPU

Comment by yemima mushi on April 27, 2012 at 5:35pm

INATISHA, EE YESU UCNIACHE NISHIKE MKONO BABA

Comment by lumi mwandelile on April 23, 2012 at 1:54pm

umbea tu

Comment by Mamy Shaluathu on April 23, 2012 at 12:09pm

Na bora muufunge kwani tumechoka kusikia habari za Kanumba.

Comment by manka on April 22, 2012 at 1:57pm

Free masson n i muungano wa wa watu matajiri duniani huyu Kanumba ambaye hata nyumba hajaacha mjini mnatumia vigezo gani kumweka katiaka kundi la watu matajiri duniani? au akili zenu zimeganda hamwezi kutafuta maana ya mantikiya vitu mnabaki kudakia dakia tu vitu na kuanza kutafsiri mpendavyo nyie? au hii company ya GPL ni ya undugu ndiyo maana hakuna mtu wa kutafakari mambo ya maana ya kuleta mbele ya jamii, ilio mtujuze na kutupa elimu?

Comment by manka on April 22, 2012 at 1:51pm

awe mason awe mlokole, ameshakufa, na kila mtu atakufa sasa nyie GPl mnavyochokonoa chokonoa marehemu ndiyo atafufuka? naona sasa mnakaa tu ofisini nakuanza kutunga story za walio kufa, au na nyie ni wafu? acheni kutubore na habari ambazo hazina mantiki.

Comment by Boazstev on April 22, 2012 at 11:53am

Iwekweli au si kweli Hatupaswi kuwafuatilia nimaisha ya mtu na tabia zake mwenyewe.

Comment by Boazstev on April 22, 2012 at 11:51am

Kama mama yake amesema alikuwa muumini kanisani Muacheni Mama yake kanumba na Maisha ya mwanae aliekwisha kufa waandishi si vyema sana kumgasi mwana mama huyo muacheni apumzike.

Comment by john bosco on April 22, 2012 at 3:07am

kuhusu ile nembo wanayosema eti ya u-freemasson. ningependekeza mama ke kanumba afunguwe kesi > aliyemvisha atafutwe na atowe sababu kamvisha ile nembo. sababbu aliyemvisha yupo na wanamfahamu. kanumba hanakosa lolote. ukisha kufa utafanyiwa chochote hautabishi. watu wengina wanapenda kudhalilisha watu hata kwenye vifo vyao!!!!!

Comment by nellicy maluli on April 22, 2012 at 12:30am

Mengi yatajitokeza zaidi siku hata siku, mwacheni mtoto wa watu apumzike kwa amani, kuna habari nyingi za kuandika na si yeye tu kila siku, kazi alioijia duniani ameimaliza nasi tusubili muda wetu ufike. Tumieni ustaarabu jamani mkae mkijua kuwa siku moja mtasafiri kwenda kujiunga naye kwenye makao ya milele.

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

kemeya posted a status
44 seconds ago
Tipu Sultan posted a status
54 seconds ago
misu babu posted a status
1 minute ago
sabuj posted a status
1 minute ago
kemeya posted a status
1 minute ago
kemeya posted a status
1 minute ago
misu babu posted a status
1 minute ago
suny suriyan posted a status
2 minutes ago
bdsantarani posted a status
2 minutes ago
vanhelsing posted a status
2 minutes ago
bdsantarani posted a status
2 minutes ago
bdsantarani posted a status
2 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }