Eric James Shigongo (kulia) akiwa na mama yake mzazi.
ERIC Shigongo ameamua kuelezea historia ya maisha yake yote, alikotoka mpaka alipo sasa bila kuficha umasikini ulioikumba familia yao, manyanyaso na mateso mengi kutoka kwa watoto wenzake mitaani huku akiitwa majina mengi ya kukarahisha.
Ni majina haya ndiyo yaliyomfanya aamue kubadilika, aliufahamu umasikini na katika maisha yake hakuutaka na kuamua kubadilika. Mara kadhaa akikumbuka maneno ya baba yake kwamba hawakuwa mahali sahihi akiwaeleza kama yeye alishindwa, basi wao walitakiwa kufanya kitu fulani maishani mwao.
Ni maneno hayo ndiyo yalimfanya kuukataa umaskini na kuupinga kwa nguvu zake zote. Hakika hakuupenda. Marehemu baba yake, hakuishia hapo, aliwapa elimu ya ujasiriamali kwani alielewa hicho ndicho kitakachowakomboa katika maisha yao.
Hata darasani, uwezo wake ulikuwa wa chini kabisa lakini alijaliwa kipaji kikubwa ambacho hakuna mwingine aliyekuwa nacho, kusimulia hadithi. Anaendelea kusimulia historia ya maisha yake...
KWA sababu nilifeli Hesabu, Historia, Jiografia, Siasa, Kiswahili na masomo mengine, basi nilionekana sina kitu chochote ndani yangu, hakuna aliyefahamu kwamba kule kusimulia hadithi, kilikuwa ndicho kitu ambacho Mungu alikiweka ndani yangu ili kinikomboe kutoka kwenye umasikini na hatimaye kusaidia Watanzania wenzangu na hata kukutana na watu ambao hakika nisingekutana nao kama nisingekigundua kipaji changu.
Hivi ningekutana wapi na kuwa rafiki wa mtu kama Dk. Reginald Mengi, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Dk. Emmanuel Nchimbi, Richard Branson, Donald Trump kama ningeendelea kukubaliana na jina la ujinga nililoitwa kwa sababu sikufanya vizuri darasani? Ndugu zangu nataka kusema wazi leo kuwa maisha ambayo watu wengi wanaishi si maisha yao, walichaguliwa na watu wengine na wao wakakubali.
Kataa jina hilo, simama na uanze kupeleleza ndani yako Mungu ameweka nini. Ndiyo maana wakati ule Magreth Sitta akiwa Waziri wa Elimu niliwahi kumwandikia barua na kulalamika kwamba mfumo wa elimu uliopo hapa nchini unawafanya watoto wanaofeli masomo, waitwe wajinga! Wajione hawafai na wasio na faida bali wale wanaofaulu na kuitwa wenye akili ndiyo wajione bora.
Lakini mwisho kinachotokea ni kwamba, aliyekuwa na akili nyingi darasani, akasoma hadi chuo kikuu na kukuta ajira hakuna na aliyebaki kijijini baada ya kufeli darasa la saba akaamua kujiingiza kwenye ujasiriamali kama njia pekee aliyobaki nayo, lakini wakati msomi anarejea kutoka chuo kikuu atamkuta mjinga ana maduka mawili, mashamba ya kahawa na malori ya kubebea mizigo! Hii huwafanya wasomi mwisho wajione wajinga.
Siongei haya kupuuza wasomi au kupuuza elimu kwa sababu mimi sikusoma, ninachosema hapa ni kwamba, hata watoto wangu nawapeleka kwenye shule nzuri ili wapate elimu bora, lakini mwisho wakirejea nyumbani nawafundisha ujasiriamali, hicho ndicho nilichotaka Wizara ya Elimu ifanye, ifundishe ujasiriamali kwenye shule zetu si kufanya kama ambavyo huko nyuma ilifanyika; kuondoa masomo ya biashara, kilimo kwenye mitaala ya kufundishia. Hivi tulikuwa tunajenga taifa la aina gani?
Sikumbuki kama nilijibu hata swali moja kwenye mtihani wangu wa darasa la saba, karibu kila kitu nilikiona ni ‘Kichina’ kwenye karatasi ya mtihani. Ninachofahamu ni kwamba matokeo yalipotoka nilikuwa nimefeli, jina la mjinga likathibitika kabisa. Na nikawa na uhakika asilimia mia moja kwamba kweli nilikuwa mjinga sababu hata serikali ilikuwa imeona hivyo. Mimi na dada yangu wote tulifeli.
Dada yangu alilia sana, lakini mimi niliona ni sawa na nilimshangaa kwa nini alilia, tushinde vipi wakati tulikuwa wajinga? Kilichofanyika baada ya hapo ni kukubaliana na matokeo, kama sikosei walifaulu wanafunzi wawili tu darasa zima, majina yao siwakumbuki maana sikuwa na mawasiliano na mtu yeyote baada ya pale.
Nikajiunga rasmi na baba yangu sokoni Buzuruga, kufanya kazi aliyonifundisha; kuchuuza. Kazi yangu ikawa ni kumsaidia kuwafungia wateja bidhaa, lakini jioni nilifanya kazi ya kurusha (kulangua) sigara ambazo wakati huo zilikuwa ni bidhaa adimu, ndani ya muda mfupi tu nikawa nimeshakuza mtaji wangu mpaka shilingi mia saba, nikamkabidhi baba anitunzie! Nikaendelea tena, wakati huo nikawa nimekwishaanza biashara ya kuuza mafuta ya taa mitaani na karanga za kukaanga, wakati mwingine mayai ya kuchemsha.
Nikifanya yote hayo niliwaona watoto wa matajiri na watu wenye uwezo wakienda shule, wakati huo Mwanza kulikuwa na shule mbili tu maarufu, Mwanza Sekondari ambayo iliitwa kwa kifupi Mwanza Seco, wanafunzi wake wa kike walivalia sketi za kijani zenye mistari miwili ya rangi nyeupe inayoshuka chini! Msichana aliyevaa sketi ya aina hiyo alijiona malkia mtaani na aliheshimika kweli, acheni siku hizi watu wadharau elimu ya sekondari kwa sababu kuna sekondari za kata, wakati ule mtoto wa sekondari si mchezo, aliheshimiwa na kila alikopita watu walisema, “Kanasoma seko” na walijidai.
Shule nyingine ilikuwa ni Lake Sekondari, ambako watoto wa matajiri tu walisoma kwa sababu ilikuwa ni ya kulipia, wasichana walivalia sketi za rangi ya kahawia, nazo zikiwa na mistari miwili ya kushuka chini kama Mwanza Sekondari, wavulana walivaa suruali za kahawia na wote mashati meupe! Kwa hakika walivutia na nilitamani kuwa miongoni mwao, lakini ujinga wangu ndiyo ulikuwa umeniweka sokoni kushirikiana na baba. Walipopita wakienda shule niliwaonea wivu.
Yombo Paul ambaye hivi sasa kama sikosei anafanya kazi na shirika linaloitwa FINCA ambalo hutoa mikopo kwa wajasiriamali na Fidelis au Vedastus ambaye hivi sasa anafanya kazi Tanesco Mwanza, walikuwa ni miongoni mwa vijana waliokuwa wakisoma sekondari wakati ule, Fide pia alisoma kwa tabu sana lakini alikuwa na akili nyingi, alijulikana kama mchawi wa hesabu na wakati wa likizo alifanya kazi ya ufundi uashi.
Sitaisahau siku ambayo Yombo na Fide walipita sokoni Buzuruga na kukuta njaa imenishika kuliko kawaida, nataka niende nyumbani kula lakini baba amekataa akinitaka nisubiri mpaka jioni kwa sababu hakuwa na mtu wa kumsaidia, alikuwa akiniambia, “ikazage duhu ngosha” (jikaze tu mwanaume), siku za hivi karibuni Yombo alinitembelea ofisini kwangu na nilishangaa sana aliponikumbusha maneno hayo ya baba yangu, kumbe aliyasikia, tulicheka na kusema, “ya kale yamepita, tazama sisi ni watu wapya.”
Je, nini kitaendelea? Usikose wiki iijayo.
Comment
Comment by sabbo sabbo on January 2, 2013 at 4:20pm Mie hukukubali sana Erick!ulikuwa huna lakini ukipata mbona sawa tu na aliyekuwanavyo!nakuombea kwa MUNGU!uzima ndo wa maana!nilianza kusoma magazeti yenye hadithi zako toka kuanza!nikawa nasisimka na kutetemeka mno!kama vile miaka ile nikiwa shule ya msingi nilisoma vitabu vya hadithi vya mtu mmoja aitwa PATRICK MUSIBA' ivi 'sina hakika na jina lake' nilikuwa kijana mdogo!akiwatumia wahusika kina Veronika Ammando!kweli yale ni ya kale!ila nilitetemeka na kusisimka mwili hivyo hivyo!ila sikuacha kusoma hadithi zile!ndo maana I do value you a lot!!
Comment by sarah rolick on December 31, 2012 at 3:36pm una nii inspire real..............nitakutafuta kaka nikuone live..Mungu akulinde.
Comment by DORAH FREDY on December 31, 2012 at 12:36pm ha ha ha ha ha ha ha ha ha kweli maisha ni mapito duhh Erick ulipitia mapito ndiyo hivyo lakini
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
NDAUKA the GREAT |
| 3 |
julius manning |
| 4 |
LJH_3 |
| 5 |
hope |
| 6 |
Tatu Majaliwa |
| 7 |
mayalilwa |
| 8 |
steven emmanuel |
| 9 |
Mishy chunga |
| 10 |
shabani abdallah nguluko |
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies 0 Likes
JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies 8 Likes
Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies 3 Likes
Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…
Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mayalilwa Mar 8. 26 Replies 5 Likes
HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies 4 Likes
Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…
Tags: SOKA
Started by GLOBAL in Habari. Last reply by Billy Frank Irungu Apr 26. 118 Replies 21 Likes
Tags: NCHINI, HAPA, UNAFURAHIA, HUDUMA, ZAKE?
Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies 4 Likes
hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?
Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies 9 Likes
Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…
© 2013 Created by Global Publishers.




You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers