True Memories Of My Life [Kumbukumbu za Kweli za Maisha Ya Shigongo] - 5

ERIC SHIGONGO, mwandishi mahiri wa vitabu barani Afrika, Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers, mjasiriamali wa kimataifa na mhamasishaji, ameamua kuyaweka wazi maisha yake ya zamani kupitia gazeti hili.
Alianza kueleza kuanzia jinsi alivyoanza darasa la kwanza, maisha ya tabu waliyoishi na wazazi wake, jinsi baba yake, marehemu mzee James Bukumbi alivyokuwa akiihangaikia familia yake mpaka walipohamia jijini Mwanza, wakiishi kwenye kibanda kidogo cha matope. Anaendelea kusimulia matukio mbalimbali aliyokutana nayo katika safari yake ya maisha.
UNGANA NAYE…
MIEZI michache baadaye baba aliamua kutuandikisha ili tuendelee na masomo ya shule ya msingi kwenye Shule ya Msingi Gedeli, iliyoko eneo liitwalo National kama kilometa tano hivi kutoka nyumbani kwetu, ilikuwa ni shule nzuri, mwalimu mkuu akiwa Mwalimu Maega.
Siku ya kwanza tu darasani nilimwona Ally Saleh (mtoto wa familia tajiri  ambaye yeye na kundi lake walinipiga na kuyanywa maziwa niliyotumwa na mama), nikakumbuka kila kitu alichonitendea na hasira ikanipanda.
Sikuwa na la kufanya sababu yeye alikuwa na marafiki wengi na mimi nilikuwa mgeni, nikaamua kubaki kimya,  nikaapa ndani ya moyo wangu sitaongea naye maisha yangu yote, hiyo ilikuwa mwaka 1979.
Huwezi kuamini nikikuambia nilichokisema ndicho kilichotokea, sikuongea na Ally Saleh mpaka tukamaliza darasa la saba, hali iliendelea hivyo hivyo, nikiwa na chuki naye mpaka mwaka 2005 baadaye, kaka yangu alipofariki dunia na tukakutana kwenye msiba Mwanza, ndipo tukakaa na kuzungumza tukiwa watu wazima, yote yakaisha.
Siipendi sana tabia yangu hii ya kushikilia jambo, lakini ambacho huwa nataka ni mtu aliyenikosea kuketi chini na mimi na kuyazungumzia, kama hatujazungumza na  kueleweshwa au kuambiwa neno moja tu “samahani” ambalo hakika hunivunja nguvu, chuki yangu haitaisha. Napenda sana kuzungumzia matatizo hata kama ni magumu, ili kuyatafutia ufumbuzi na tukishamaliza tumemaliza, hutasikia tena.
Sikumbuki vizuri  kama kuna mtoto  mwingine alikuwa akienda shuleni akiwa hana viatu isipokuwa mimi na dada yangu Joyce,  tulisoma katika mazingira magumu sana tukibezwa na wanafunzi wengi,wakati mwingine hata walimu. Umasikini ni kitu kibaya ndiyo maana naupiga vita kwa nguvu zangu zote, masikini haheshimiwi hata kama ana mawazo mazuri kiasi gani, hicho ndicho kilichonipata mimi na familia yangu nikiwa mdogo.
Rafiki pekee niliyekuwa naye shuleni alikuwa ni Daudi Kanizio, sababu yeye pia alitoka katika familia masikini, baba yake akiwa fundi wa ujenzi, masikini kwa masikini walitengeneza urafiki. Sijui hapo nilitegemea kupata nini? Hili ndilo tatizo la watu wengi duniani, kutafuta watu wanaofanana nao na kuanzisha nao urafiki.
Sisemi kwamba kuwa na rafiki masikini ni vibaya, ubaya ninaouona mimi ni  mazungumzo ambayo watu wawili masikini hufanya, mara nyingi yamekuwa  ni ya umasikini na kulalamika badala ya kuchukua hatua ya kujikomboa.
Ninachojaribu kuonesha hapa ni kwamba mara nyingi mazungumzo ya watu wanaofanana huwa ni yaleyale, inakuwa si rahisi sana kupiga hatua kama mnazungumza mambo yaleyale kila siku, matokeo yake mtaendelea kubaki watu walewale kila siku. Hakuna ubaya kubaki na rafiki yako masikini lakini ukajaribu kutafuta rafiki mwingine mwenye nafasi tofauti kiuchumi, ukajaribu kujifunza kwake kila siku.
Maongezi yangu  na Daudi  kila siku yalikuwa ni malalamiko na kujitesa na chuki iliyotujaa vifuani dhidi ya watu waliofanikiwa na kuwaona kama wao ndiyo chanzo cha matatizo yetu. Tulitupa lawama nyingi kwa watu wengine kwamba ndiyo waliohusika  na matatizo yetu, mfano  tulisema: “Hawa matajiri wanatunyonya ndiyo maana sisi tunateseka.”  
Katika mazungumzo kama hayo kweli ulitegemea tutoke? Haiwezekani, matokeo yake tuliendelea kubaki watu walewale, wenye chuki dhidi ya watu waliofanikiwa tukiwa tumejitenga na watu wengine ambao yawezekana wangeweza  kutupatia  mawazo ya kutuondoa mahali tulipokuwa.
Shuleni palikuwa ni kama  kilometa mbili hivi,  ambazo ilikuwa ni lazima nitembee kwenda na kurudi nikipita katikati ya milima iliyopo kati ya Mecco na National, ambako hivi sasa kumeenea nyumba nyingi za kifahari. Nilipenda sana kumpitia Daudi nyumbani kwao, sehemu iliyoitwa Majanini,  sababu nyumba nyingi eneo hilo zilikuwa zimeezekwa kwa nyasi.
Watoto wengine ambao nawakumbuka mimi na dada yangu tulioongozana nao kwenda shule walikuwa ni  Deogratius Manumbu (ambaye hivi sasa yupo Chuo Kikuu cha SAUT),  Mary Ambrose (ambaye hivi sasa ni marehemu)  na Paul Malale (huyu pia  alifariki dunia miaka mingi iliyopita).
Sikuwa na marafiki wengi sana shuleni, mara nyingi nilijitenga na  sikuwa muongeaji sana, kwa sababu niliamini kile ambacho ningekisema kingekuwa kimekosewa! Sikuwa najiamini kabisa, hivyo ndivyo jamii ilivyonijenga, nilifanywa nijipuuze kwa jinsi watu walivyoniita na kunichukulia nami nikakubaliana nao na kuona walikuwa sahihi.
Hata mwalimu alipouliza swali darasani sikunyanyua mkono wangu kujibu, nikiamini jibu langu lisingekuwa sahihi! Mfano, mwalimu alipouliza swali kama; watoto mbili mara mbili ni ngapi? Nilijua kabisa moyoni mwangu kwamba jibu ni nne, lakini sikunyoosha mkono, mwalimu aliponinyanyua na kutaka nijibu nilisema sijui, nikiwa sina uhakika kama kweli nne lilikuwa jibu sahihi.
“Wee mjinga sana,  hata mbili mara mbili hujui?” mwalimu alisema.
“Haa!Haaa!Haaa!” wanafunzi wote darasani walicheka, nami nikaketi kwa aibu.
“Ntambo, hebu jibu mbili mara mbili ni ngapi?”
“Ni nne mwalimu!”
“Mh! Kumbe na mimi ningejibu ningepatia,” niliwaza baada ya jibu kutolewa.
Hata siku moja sitaisahau siku nilipopigana na kijana mmoja aitwaye Cosmas, jina la baba yake silikumbuki maana imekuwa muda mrefu na kwa sasa yeye ni marehemu.  Yeye alijifanya mbabe na vijana wote walimuogopa, hiyo ilimfanya apende sana kunizomea na kuniita madaso kila nilipopita, siku moja nilipita mbele ya nyumba yao nikiwa na mpira wangu wa matambara, akauchukua kwa nguvu.
“Cosmas nipe mpira wangu.”
“Hakuna mpira hapa, nitakubonda.”
“Huwezi! Nipe mpira wangu.”
“Kwenda zao kule, madaso wee.”
Kilichotokea hapo ilikuwa ni vumbi, wote tukiwa chini, silaha zote za mwili zikitumika kuanzia mikono, miguu, meno nk. Watu wakajaa na kutuzunguka, badala ya ‘kutuamlia’ tulikuwa tukishangiliwa, watoto wakisema: “Tunataka tujue nani gangwe!”
Tulipigana karibu saa nzima, wote tukawa tumechoka, damu zikitutoka. Katika kuserereka, kumbe bila kujua tulikuwa tumefika kwenye shimo la maji machafu lililokuwa likichimbwa, tukadumbukia ndani yake! Tukiwa humo hatukuacha,watoto wakiwa wamejaa juu wakichungulia na kushuhudia.
Itaendelea wiki ijayo,

Views: 1469

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by penina mwailunda on November 20, 2012 at 12:31pm

mh!!! haya lete vionjo ili tupate nasi msisimko wa maisha tuweze jikwamua na maisha

Comment by DORAH FREDY on November 20, 2012 at 11:51am

Maisha ya umaskini duhhh acha tuuuu

Comment by FRANK CASTORY on November 20, 2012 at 2:48am

mmmmmmmmmmmh kweli binadamu tunatoka mbali sana

Comment by godwin julius leo on November 19, 2012 at 12:59pm

inahuzunisha na kufurahisha,ila ni kweli mawazo ya maskini hayadhaminiwi

Comment by ADON H FALETH on November 19, 2012 at 12:23pm

hahahahaha

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mayalilwa Mar 8. 26 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service