The Rotten Deal (Mpango Ulioharibika) - 75

TONY na Deusdedith Kahungo wanaendelea na kazi ya kuhakikisha wanapata namba nne za siri za kompyuta iliyokuwa na artwork ya fedha za Buzilayombo. Wanatumia kila mbinu kuhakikisha wanazipata namba hizo za siri ili kazi ya kuchapisha noti kwa kutumia mtambo walioununua kwenye Kampuni ya American Bill Currencies ianze.
Baada ya kufanikiwa kupata namba kutoka kwa bwana Masato, Msanifu wa Benki Kuu baada ya kumpa dola elfu kumi, Gavana wa Benki Kuu, Festo Chalo aliyekuwa na sifa ya kupenda totoz na kwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Peter Kizwalo, sasa wanahamia kwa Waziri wa Fedha, Andrea Kazinja.
Upelelezi wao wa awali unawafanya wagundue siri kubwa kuhusu maisha ya kigogo huyo wa serikali kuwa kumbe alikuwa akishiriki mchezo mchafu wa ushoga. Kijana Chisunga aliyekuwa akifanya kazi ya kutunza bustani nyumbani kwake, ndiye aliyekuwa akimuingilia kinyume na maumbile na uchafu huo ndiyo uliosababisha ndoa ya mheshimiwa huyo kuvunjika baada ya mkewe kugundua.
Tony na Deus wanasafiri mpaka kwenye kijiji alichokuwa anaishi kijana huyo, Isangu ambapo wanafanikiwa kumpata na kumdanganya kuwa wao ni maofisa wa Benki Kuu ya Buzilayombo. Wanatumia ushawishi wa fedha kutaka Chisunga awasaidie kuipata namba ya siri kutoka kwa Waziri Kazinja.
 Je, nini kitafuatia?
SONGA NAYO…

“NATAKA mnipe fedha za kuniwezesha kuishi maisha yangu vizuri baada ya kuacha kazi.”
“Kwa nini unataka kuacha kazi kwa waziri?”
“Nimechoshwa na kazi ya kutunza bustani.”
“Kwani wewe pale kwa Waziri Andrea Kazinja unafanya kazi ya kutunza bustani tu?”
“Ndiyo, kwani nani amewaambia ninafanya kazi nyingine?”
“Hapana tunakuuliza tu. Sasa kwa nini unataka kuacha kazi?” alihoji Tony huku wote wawili wakiwa wamemkazia macho Chisunga.
“Unajua… waziri Kazinja ni… ni…” alibabaika Chisunga kisha ghafla akabadilisha mada.
“Waziri Kazinja amefanya nini? Mbona humalizii kauli yako?”
“Ananifanyisha kazi ngumu lakini mshahara anaonilipa ni mdogo sana. Mi namfurahisha sana lakini wala hajali maslahi yangu.”
“Unamfurahishaje? Kazi gani ngumu unayomfanyia?” Deus na Tony walizidi kumuandama Chisunga kwa maswali wakitaka afunguke mwenyewe kilichokuwa ndani ya moyo wake.
Hata hivyo, Chisunga alikuwa hodari wa kubadilisha mada, kila alipokuwa akikaribia kufichua siri kubwa ya Waziri Kazinja, alikuwa akibadilisha mada haraka na kuanza kuzungumzia vitu vingine.
Tony na Deus walielewa haraka kuwa lazima Waziri Kazinja atakuwa amempa vitisho vikali kijana huyo juu ya kutotoa siri yake ya ushoga. Hata hivyo, kwa kuwa walikuwa wanajua kila kitu kuhusu tabia chafu ya waziri huyo kuingiliwa na Chisunga kinyume na maumbile, hawakutaka kuendelea kumdadisi.
“Kwa hiyo umesema tukikupa shilingi ngapi utatufanyia kazi yetu?”
“Si nimesema fedha zitakazonitosha kuishi kwa amani baada ya kuacha kazi?”
“Ok, sawa, tutakupa shilingi milioni hamsini. Zitakutosha?”
“Nyingi sana, nitafanyia nini zote hizo?”
“Tunataka ubadilishe maisha ya kwenu, uwajengee nyumba nzuri wazazi wako na nyingine utumie kwa matumizi yako binafsi.”
“Sawa nimekubali.”
“Tutakulipa nusu ya fedha hizo hapahapa na ukimaliza kazi tutakumalizia nusu nyingine. Usimwambie mtu yeyote kuhusu mpango huu, sawa?”
“Sawa,” aliitikia Chisunga huku akichekacheka kwa furaha. Fedha zilimtia ukichaa. Katika maisha yake, hakuwahi kuota kuwa anaweza kumiliki kiwango kikubwa cha fedha kama kile. Tony akafungua mlango wa gari na kuvuta briefcase iliyokuwa imejaa fedha, akatoa burungutu kubwa na kumpa Chisunga ahesabu mwenyewe.
“Mi sikusoma shule, nihesabieni wenyewe,” alisema Chisunga kwa aibu, Tony akamwambia kuwa zilikuwa shilingi milioni ishirini na tano taslimu. Chisunga alizichukua na kuzigawanya mafungu matatu, akaweka kwenye mifuko miwili ya mbele na mmoja wa nyuma.
“Kazi yetu itakamilika lini?”
“Kesho tu kila kitu kitakuwa tayari. Nipeni kabisa hicho kidonge.”
“Hiki hapa, utakisaga na kumchanganyia kwenye kinywaji chochote. Iwe pombe, maziwa, juisi au chochote lakini isiwe kwenye maji kwa sababu atashtuka.”
“Sawa, kesho mje muda kama huu nitakuwa nimeshamaliza kazi,” alisema Chisunga kwa kujiamini, akaaga na kuondoka kwa kasi kurudi nyumbani kwao.
“Lazima mpango wetu ufanikiwe, hizi fedha tunazotoa zitarudi tu, wala usiwe na wasiwasi,” alisema Tony huku akitabasamu.
“Unajua mimi bado najiuliza, yaani huyu kijana mchafumchafu kiasi hiki ndiyo anamfaidi Waziri Kazinja?”
“Ndiyo, mi si nilikwambia jamaa alianza tabia ya ushoga tangu akiwa sekondari? Yaani hata huyo mke wake unaambiwa siku aliyomfumania akishughulikiwa na mwanaume mwenzake, alizimia kwa mshtuko.”
“Daah! Kweli dunia imevaa taulo.”
“We acha tu, kibaya zaidi kumbe hata waheshimiwa kuna ambao si riziki,” Tony na Deus walikuwa wakipiga stori baada ya Chisunga kuondoka. Baada ya muda waliingia ndani ya gari lao na kuanza safari ya kurudi jijini Chato, kila mmoja akiwa na furaha ndani ya moyo wake kwani kazi ilikuwa ikielekea kukamilika.
***
“Bosi, leo utakuwepo nyumbani?”
“Ndiyo, vipi kuna tatizo?”
“Hapana bosi, nimekumbuka mambo yetu yale, usiku kucha leo sijalala.”
“Mh! Leo maajabu, yaani wewe ndiyo unanikumbuka wakati kila siku huwa nakulazimisha?”
“Nimeanza kunogewa na hako kamchezo, yaani kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele ndiyo ninavyozidi kukupenda bosi. Njoo unichukue basi ili usiku nikushughulikie.”
“Leo sitaweza kuja kwa sababu jioni kuna kikao cha bodi ya wizara, ila kama unaweza kodi taksi ukija nitalipa.”
“Nitakukuta wapi?”
“Nipitie kazini kwani nitachelewa kidogo kutoka leo.”
“Sawa bosi, I love you!”
“I love you too,” alisema Waziri Kazinja na kukata simu. Kama ungesikiliza mazungumzo yao, ungedhani Chisunga anazungumza na mpenzi wake wa kike na Waziri Kazinja anazungumza na mwanamke wake, lakini haikuwa hivyo, walikuwa wakizungumza wanaume tupu.
Baada ya mazungumzo yale, Chizunga alianza kujiandaa, akachukua noti moja ya shilingi elfu kumi na kuiweka mfukoni kisha zile nyingine akazichimbia kwenye shimo ndani ya chumba chake cha kulala na kuzifukia. Akaenda kuoga kisha akavaa nguo zake za sikukuu. Hakusahau kidonge cha Acetamine- D alichopewa na Tony.
Baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa, alitembea mpaka kwenye kituo cha magari, akapanda pick up iliyokuwa inaelekea jijini Chato. Baada ya mwendo wa takribani saa mbili, alishawasili mjini, akakodi taksi iliyompeleka mpaka ofisini kwa Waziri Andrea Kazinja.
“Nimeshafika bosi, nipo hapa nje na dereva taksi,” Chisunga alituma ujumbe mfupi kwenye simu ya Waziri Kazinja, muda mfupi baadaye akatoka mfanyakazi wa ofisi ile akiwa na fedha ya dereva taksi na funguo za nyumbani kwa Kazinja.
“Amesema mlipe kisha tangulia nyumbani kamwagilie bustani, yeye anaingia kwenye kikao,” alisema yule mfanyakazi wakati akimkabidhi Chisunga fedha na funguo.

Je, nini kitafuatia? Usikose kufuatilia Jumatano kwenye Championi Jumatano.

Views: 1067

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by abel john mwaka on January 2, 2013 at 5:06pm
Daaa we nomaaaaa
Comment by laida linga on January 2, 2013 at 9:41am

shigongo we una mambo duh!

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mayalilwa Mar 8. 26 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

Latest Activity

Tawanna Buck posted a status
5 minutes ago
GLOBAL's 8 blog posts were featured
11 minutes ago
GLOBAL posted blog posts
12 minutes ago
Felipa March posted a status
21 minutes ago
Leonida Nash posted a status
23 minutes ago
Shealtiely Urassa commented on GLOBAL's blog post BAHATI BUKUKU APATA MCHUMBA
"Bahat Dadangu pokeee! ila naomba usikilize vizur wimbo wako MAPITO…! naomba nikukumbushe…"
23 minutes ago
hope commented on GLOBAL's blog post VUGURU ZATOKEA MJINI IRINGA, POLISI WATUMIA MABOMU KUREJESHA AMANI
"bongo bana sijui tutafika lini"
23 minutes ago
hope commented on GLOBAL's blog post YANGA YAIGONGA SIMBA 2-0, YATWAA KOMBE LA VPL
"Unakosea unaposema Yanga leo imewaadhibu watani wao wa jadi, Simba SC ingewaadhibu kwa kurudisha…"
23 minutes ago
mvulaa mgalula commented on GLOBAL's blog post PAMBANO LA SIMBA, YANGA LAINGIZA MIL 500/-
"Makato kibaoo''timu zinanyonywa hata hivyo."
23 minutes ago
hope commented on GLOBAL's blog post DR. FERDINAND MASAU WA TANZANIA HEART INSTITUE AFARIKI DUNIA
"R.I.P"
23 minutes ago
hope commented on GLOBAL's blog post SISTA FEKI ANASWA
"Hii ni hatari kuliko huyo anatakiwa atoe maelezo yanayoeleweka vizuri"
25 minutes ago
RUKHAIYA ISSA commented on GLOBAL's blog post Queen of the Gorillas (Malkia wa Masokwe) - 111
"yaani simpendi linda kwa kulazimisha mapenzi hambapo hapendwi"
25 minutes ago

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service