The Rotten Deal (Mpango Ulioharibika) - 58

TONY anasafiri na Barbara mpaka nyumbani kwao, Ichenjezya nchini Buzilayombo anakoenda kumtambulisha mchumba wake huyo kwa walezi wake. Wanapokelewa kifalme na mjomba wake na mkewe waliowafuata mpaka kwenye Uwanja wa Ndege wa Chato. Wanawapeleka mpaka nyumbani kwao kwa kutumia gari la familia.
Barbara anashangazwa na kila anachokiona kiasi cha kumfanya ajihisi yupo ndotoni. Kwanza haamini kama kweli Tony ameamua kumtambulisha kwa wazazi wake lakini pia anashangazwa na mazingira ya Bara la Afrika na mapokezi aliyopewa ukweni.
Walezi wake na watu wote waliokuja kuwasalimia Tony na Barbara, wanashangazwa na uzuri wa kipekee alionao binti huyo Mmarekani mweusi, wanampongeza Tony kwa kujua kuchagua na wanawaombea kila la heri kwenye maandalizi yao ya kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Je, nini kitafuatia?
SONGA NAYO…
TONY na Barbara walikaa kwa muda wa wiki mbili ukweni. Kwa siku zote hizo watu mbalimbali wakawa wanaenda kuwatembelea pale nyumbani na kuwatakia kila la heri kwenye maisha ya ndoa waliyokuwa wameyakaribia. Pia bado watu wengi waliendelea kumshauri Tony kuwa agombee ubunge au urais kwenye uchaguzi mkuu uliokuwa unafuata.
“Tazama mbunge wetu tumemchagua lakini tangu aingie madarakani hajafanya lolote, hata huku jimboni haonekani tena. Kila siku anashinda Chato na mara utamsikia kapanda ndege sijui kaenda nchi gani, yaani laana tupu,” alisema mzee mmoja wa makamo, akaendelea kumsisitiza Tony kuwa wanamtegemea awakomboe.
Baada ya wiki mbili kuisha, Tony na Barbara walijiandaa kwa safari ya kurejea jijini New York. Waliagwa kama mfalme na malkia kwani ilibidi kufanyike sherehe ndogo ya kijadi, watu wakala na kunywa. Shughuli zote zilipomalizika, msafara wa magari matatu uliwasindikiza kutoka Ichenjezya mpaka Chato, wakapelekwa moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege.
Kwa kuwa tiketi walizokatiwa awali na wazazi wa Barbara zilikuwa ni za kwenda na kurudi (go and return), hawakupata shida, wakaenda moja kwa moja kwenye ofisi za American Airways na kutoa taarifa zao, wakaelekezwa kusubiri kidogo.
Muda mfupi baadaye, waliingia uwanjani kwa kupitia mlango wa VIP kama tiketi zao zilivyokuwa zinaeleza, wakaenda na safari ya New York ikaanza.
“Tony, kweli nimeamini wewe ndiyo mume wangu mtarajiwa, unajua kila kinachotokea najihisi nipo kwenye ndoto.”
“Usijali Barbara, nilikuahidi kuwa nitakuoa na hilo lazima litimie, umehangaikia penzi langu kwa kipindi kirefu sana, huu ni muda wako wa kujidai.”
“Unasema kweli Tony? Ooh! Ahsante Mungu kwa kusikia kilio changu cha muda mrefu, naahidi kuwa mke mwema, daima nitakulinda baba,” alisema Barbara huku akijilaza kwenye kifua cha Tony. Ndege iliendelea kupasua mawimbi na baada ya muda, usingizi ukawapitia wote wawili.
Hatimaye waliwasili jijini New York, wakateremka kwenye ndege na kupitiliza moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Tony.
“Karibu nyumbani mpenzi wangu.”
“Ahsante baba, nimeshakaribia,” alijibu Barbara, wakasogeleana na Tony na kukumbatiana, wakasimama kwa takribani dakika mbili nzima huku kila mmoja akionekana kuzama kwenye hisia nzito za mahaba.
“Ukinioa utataka nikuzalie watoto wangapi?”
“Mmoja tu anatosha, nataka tujenge familia bora.”
“Kweli?”
“Kweli kipenzi changu, maisha yangu yote nayakabidhi mikononi mwako,” alisema Tony kwa sauti nzito, wakasogezeana vinywa vyao na kugusanisha ndimi, wakabebana juujuu mpaka kwenye chumba cha kulala, wakaanza kuelea kwenye ulimwengu tofauti.
Siku ile walilala pamoja mpaka asubuhi, kulipopambazuka Barbara akajiandaa na kurudi nyumbani kwao kwa makubaliano kuwa siku ileile Tony atatuma mshenga kupeleka barua ya posa. Barbara alipoondoka, Tony alijiandaa na kwenda nyumbani kwa mzee Gikonyo, Mkenya aliyekuwa anaishi naye mtaa mmoja.
Alipanga mzee huyo wa makamo ndiyo awe mshenga wake. Alipofika nyumbani kwake, alipokelewa na mkewe, baada ya muda wakawa wamekaa kwenye chumba cha maongezi na mzee huyo ambaye bila hiyana alikubaliana naye. Akamuelekeza namna ya kuandika barua ya posa na taratibu nyingine muhimu.
Taratibu zote zilipokamilika, Tony alimchukua mzee Gikonyo kwenye gari lake na kwenda naye mpaka jirani na nyumbani kwa akina Barbara, akamuelekeza nyumba kisha yeye akarudi nyumbani kwake. Mzee Gikonyo akashuka garini akiwa na bahasha yake, akawa anatembea taratibu kuelekea kwenye kasri la akina Barbara.
“Kijana anaoa kwenye familia nzuri sana huyu, natamani ningekuwa mimi enzi za ujana wangu,” alijisemea mzee Gikonyo wakati akikaribia kufika kwa akina Barbara. Uzuri wa jumba walilokuwa wanaishi Barbara na wazazi wake, ulimchanganya kila mtu.
Baada ya kufika getini, Mzee Gikonyo alijitambulisha na kwa sababu Barbara alishawapa taarifa za ugeni huo wazazi wake, alipokelewa kiheshima na kupelekwa mpaka ndani. Akakutanishwa na baba mzazi wa Barbara, mzee Washington. Walizungumza kiutu uzima na Gikonyo akaikabidhi barua ile, akaambiwa arudi kufuata majibu baada ya siku tatu.
***
“Tony, yule mzee uliyemtuma kuleta posa amepokelewa vizuri na baba hadi nimefurahi. Wamezungumza kwa muda mrefu, naamini wamefikia muafaka mzuri maana nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana, si unawajua wazazi wangu?”
“Kama amepokelewa vizuri nashukuru sana kipenzi changu, naamini kila kitu kitaenda sawa.”
“Yaani nimefurahi sana Tony, unajua nilishakataa barua kibao za posa, leo wazazi wangu wamefurahi sana, naamini watatoa mchango mkubwa sana kwenye harusi yetu.”
“Nakumbuka kuna siku baba yako aliniambia kuwa unakataa kuolewa kwa sababu yangu, akaniambia nikiendelea kukufuatilia atanipiga risasi, nahisi alidhani nataka kukuchezea na kukuharibia maisha tu.”
“Ndiyo, awali walidhani hata mimi nimechanganyikiwa lakini naona kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo wanavyozidi kunielewa, namshukuru sana Mungu wangu,” alisema Barbara wakati akizungumza na Tony kwa simu. Walizungumza mambo mengi kisha simu ikakatwa.
Muda mfupi baadaye, Mzee Gikonyo alipiga simu na kumtaarifu Tony juu ya muafaka waliofikia na wazazi wa Barbara. Wakakubaliana kusubiri hizo siku tatu walizopewa ziishe.
Jumamosi asubuhi, siku tatu tangu mzee Gikonyo alipopeleka barua ya posa, alijiandaa kufuatilia majibu. Alipofika, alipokelewa kwa uchangamfu kuliko hata awali, Mzee Washington akamwambia binti yao ameridhia kwa moyo mkunjufu kuolewa na Tony, wakapangiana mahari na kukubaliana kuwa watawasikiliza wahusika juu ya siku wanayotaka kufunga ndoa.
Mzee Gikonyo aliaga na kuondoka, akiwa na furaha tele na kumrudishia Tony majibu, ikiwa ni pamoja na mahari ndogo waliyokuwa wanaitaka wazazi wa Barbara. Miongoni mwa siku ambazo Tony alikuwa na furaha maishani mwake, ilikuwa ni siku hiyo. Alirukaruka kwa furaha kama mwendawazimu, akamkumbatia mzee Gikonyo kwa nguvu na kumshukuru kwa kazi kubwa aliyoifanya.
Tony aliwapigia simu ndugu zake wa Buzilayombo na kuwaeleza hatua aliyokuwa amefikia, nao wakaonyesha kufurahishwa sana.
“Tunataka harusi uje kufungia huku, tunataka kukushuhudia ukioa,” alisema mjomba wake Tony, wazo lililoungwa mkono na Tony, akamwambia harusi itafungwa jijini New York lakini sherehe za ndoa zitafanyikia Buzilayombo.
Mchakato wa maandalizi ya harusi ukaanza, Tony akawapa taarifa wafanyakazi wenzake juu ya mipango yake ya kuoa, kila mmoja akawa anampongeza kwa hatua aliyofikia. Japokuwa hakuomba kuchangiwa ili kufanikisha shughuli ile, kwa jinsi alivyokuwa anaishi vizuri na wenzake, wengi walitoa michango mikubwa.
Upande wa familia ya akina Barbara nako mambo yalipamba moto. Mzee Washington aliyekuwa anafanya kazi ikulu ya Marekani aliwapa taarifa wazee wenzake, marafiki, ndugu na jamaa kuhusu kuolewa kwa binti yake. Kwa kuwa alikuwa na uwezo mkubwa kifedha, wenzake walimshauri kuifanya sherehe hiyo kuwa ya kihistoria.
Wakawa wanamchangia fedha nyingi huku wengine wakiahidi kufanya mambo mbalimbali ili kufanikisha sherehe hiyo.
“Mimi nitatoa boti kubwa itakayowasafirisha maharusi mpaka katikati ya bahari na kufungia ndoa huko, kisha sherehe itaendelea hukohuko. Boti yangu ni ya kisasa na ina kila kitu. Inaweza kubeba watu zaidi ya mia tatu, ina kumbi nzuri za starehe na kila kitu, naamini watafurahi sana,” Norris Lincoln, tajiri maarufu jijini New York alikuwa akizungumza na mzee Washington na kutoa ahadi hiyo kubwa.
Siku zikawa zinasonga mbele kasi huku maandalizi yakiendelea, hatimaye zikasalia siku chache kabla ya kufanyika kwa sherehe hiyo.
Je, nini kitafuatia? Usikose kufuatilia kwenye Gazeti la Championi Jumatano.

Views: 1579

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by raphael Joram on November 19, 2012 at 9:06pm
hata barbara aamue kumlinda tony kumbe.kahangaika hivyo kumpata.
Comment by mammy on November 19, 2012 at 3:22pm

mambo sasa tayari

Comment by de ginnethon jr on November 19, 2012 at 2:58pm

utamuuuuuu huoooooo dahhhhhh

Comment by Sylvester Francis on November 19, 2012 at 11:43am

 dah! inavutiaa!! inapendeza sana!!! inasisimua ile mbaya!!!!!!

Comment by FURAHA TAUSI on November 19, 2012 at 9:57am
mambo yamenoga

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

livestream posted a status
24 seconds ago
livestream posted a status
33 seconds ago
livestream posted a status
45 seconds ago
livestream replied to livestream's discussion http://livevsstream.com/houston-texans-vs-new-orleans-saints-live/
50 seconds ago
livestream liked livestream's discussion http://livevsstream.com/houston-texans-vs-new-orleans-saints-live/
1 minute ago
livestream replied to livestream's discussion http://livevsstream.com/houston-texans-vs-new-orleans-saints-live/
1 minute ago
livestream posted a status
1 minute ago
livestream posted a status
1 minute ago
livestream posted a status
2 minutes ago
livestream posted a status
2 minutes ago
online2pcgame posted a status
2 minutes ago
online2pcgame posted a status
2 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }