The Girl In My Dreams (Msichana Ndotoni Mwangu) -93

“TUNAKUBALIANA na yote yaliyoandikwa humo na tuko tayari kumtunza na kumlea mtoto tutakayemchukua hapa kwa nguvu na juhudi zetu zote tukihakikisha anapata  maisha yanayostahili.”
“Basi ni wakati wa ninyi kula kiapo mbele ya mwanasheria wetu.”
“Sawa sista,” walijibu kwa pamoja wakala kiapo  na zoezi hilo lilipokamilika sista mkuu akauliza swali  akiwataka wataje  walihitaji mtoto wa jinsi gani na umri wake.
“Kuanzia miezi mitatu na awe wa jinsi ya kike.”

Hakujibu tena kitu akawataka wamfuate naye akaongoza moja kwa moja mpaka kwenye  moja ya vyumba vilivyokuwa karibu kabisa na ofisi yake akawakaribisha na kuwaingiza ndani. Wakaingia na kukuta watoto wadogo wakiwa wamelala kwenye vitanda na wafanyakazi wachache wakiwa hapo kuwaangalia.
Hapo walitaka kuchagua mtoto mmoja tu ambaye ndiye wangemchukua na kwenda kumtunza mpaka mwisho wa uhai wake, wakafumbua macho yao yote kuwaangalia watoto hao kwa kweli walikuwa wazuri mno.
“Mnachagua mmoja tu,” sista mkuu aliongea akitabasamu.

“Mh! Watoto wote wazuri sijui tumchukue yupi kati yao?” Lina alimuuliza Phillip.
“Huyu hapa anafanana na sisi.”
“Sawa…sista huyu ndiye tuliyemchagua.”
Aliongea Phillip akimnyanyua mtoto mzuri aliyekuwa amelala kitandani, alikuwa ni mdogo lakini uzuri wake ulionekana wazi.


Upande wa pili wa hadithi hii tunamwona tajiri Fedorov akiwa hospitali ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi na tayari mtoto mmoja ameshaanza kuonyesha dalili ya kurejewa na fahamu zake kwa kupiga chafya, madaktari na wauguzi wanafurahia hilo na  kuwekeza tumaini kwa mtoto mwingine wakiamini kwamba baada ya muda si mrefu  naye ataamka.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

MAMBO hayakuwa kama walivyotarajia  kwamba baada ya saa kadhaa mtoto huyo angeamka na kuungana na mwenzake, saa ya kwanza ikapita na sasa ilikuwa ikielekea ya pili, Victor Fedorov uvumilivu ukaanza kumshinda akajikuta akimwaga machozi kama mtoto mdogo, kazi ya wauguzi ndani ya chumba ikawa ni kumtuliza wakimtaka awe mvumilivu.
“Lakini ni muda mrefu sana mbona mwenzake amesharejewa na fahamu?” aliuliza akisogea karibu kabisa na kitanda cha pacha ambaye  hakuonyesha dalili yoyote ya kuamka.
“Ataamka, kuwa mvumilivu.”

“Mbona kama ni upasuaji umefanyika kwa saa sawa iweje yule aamke na huyu bado?” bado aliendelea kuuliza maswali mfululizo.
“Tafadhali tunaomba sasa mzee utupishe tuendelee na matibabu yetu tutakuwa tukikujulisha kila kitu kadiri muda unavyokwenda tunaomba uende nje,” aliongea daktari mmoja,  muuguzi aliyekuwa karibu na Fedorov akamshika mkono na kumwongoza kutoka nje naye pia akijaribu kuongea maneno ya kumpa faraja.

Mzee huyo akatoka akilia, mawazo na akili zake zote zilikuwa juu ya mtoto wake huyo ambaye hakuonyesha matumaini, akatembea hatua ya kwanza na ya pili kisha akageuka nyuma kuangalia mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi.
“Sitakwenda popote nitakaa hapahapa mpaka mwisho nataka kujua nini kinaendelea,” aliongea Fedorov akiketi chini, akiwa hapo haikupita hata sekunde tatu mlinzi wake naye akaungana naye, pia akijaribu kumfariji mzee huyo lakini zoezi hilo lilionekana kuwa gumu.

“Naumia, moyo wangu una wasiwasi mkubwa sana juu ya  mtoto wangu…sijui kama ataamka…lakini kama kuna kitu kibaya kwa nini wanifiche?  Nataka wanieleze ukweli ili nijiandae kwa tatizo linalokuja,” aliongea akibubujikwa machozi.
“Hapana bosi hawezi kufa, Mungu mkubwa  anatenda.”
“Najua hilo lakini kwa sasa nimekata…….”
“Hutakiwi kukata tamaa unachotakiwa kufanya hivi sasa ni kuamini kwamba naye pia ataamka, mimi ninaamini kwamba yuko katika mikono ya madaktari bingwa atapona tu.”
“Mh! Labda hebu tuone,”aliongea  Fedorov akijifuta machozi.

***
“Mnachagua mmoja tu,” sista mkuu aliongea akitabasamu.
“Mh! Watoto wote wazuri sijui tuchukue yupi kati yao,” Lina alimuuliza Phillip.
“Huyu hapa anafanana na sisi.”
“Sawa…sista huyu ndiye tuliyemchagua.”

Mabusu mfululizo yakatua kwenye paji la mtoto waliyemchukua, alikuwa ni mtoto wa jinsi ya kike,  pamoja na kuwa mtoto mdogo uzuri wake ulionekana wazi, rangi ya ngozi yake ilifanana kabisa na ya Phillip, furaha ya ajabu ikatawala, hakuwepo hata mtu mmoja kati yao aliyeamini kwamba sasa wangekuwa wakiitwa baba na mama wa mtoto waliyemuasili kutoka katika Kituo cha Msimbazi.
“Tutamlea na kumtunza mpaka mwisho wa uhai wetu tukimpatia kila aina ya mahitaji,” Phillip aliongea akimwangalia sista mkuu.
“Ombi letu kwenu ninyi  ni hili hapa,” sista aliongea.
“Ndiyo sista tunakusiliza.”

“Tutakuwa tukihitaji kumtembelea mtoto huyu kila baada ya mwezi mmoja kujua na kufahamu anaendeleaje, hiyo ni moja ya sheria zetu mpaka atakapofikisha umri wa miaka kumi na nane ambapo tutakuwa huru kumwacha aendelee na maisha yake kwani atakuwa ni mtu mzima.”
“Hilo halina shaka sista na kama inawezekana tunaweza tu kuongozana mpaka nyumbani.”
“Nitawapa  mtu ambaye mtaongozana naye  mpaka huko kwa ajili ya kupafahamu na kama kutatokea mabadiliko yoyote yawe ya kuhama nyumba au kwenda nje ya nchi ni vyema mkatujulisha mapema, sawa?” sista mkuu aliuliza.

“Tumesikia,” Phillip na Lina walijibu kwa pamoja na kuanza kutoka nje ya chumba kuelekea ofisini kwa sista mkuu ambako wangekamilisha taratibu zote kisha kuondoka na mtoto waliyekuwa naye.
Taratibu maalum zikafanyika ikiwa ni pamoja na kupigwa picha na kutia saini kwenye makubaliano yote yaliyofanyika ofisini kisha wakakabidhiwa mtoto na sista mmoja ambaye wangeongozana naye mpaka mahali wanapoishi. Wakatoka na kumshukuru sista kisha kutembea kuelekea sehemu waliyokuwa wameegesha gari, Phillip ndiye alikuwa dereva na Lina aliketi kiti cha nyuma akiwa amempakata mtoto.

Gari liliendeshwa na kwa muda wa saa moja tu walifika nyumbani kwa Phillip na Lina wakamkaribisha sista waliyeongozana naye wakimweleza wazi kwamba hapo ndipo palikuwa nyumbani kwao ambako mtoto waliyekuwa wamemwasili angeishi maisha yake yote akitunzwa na kulelewa  vyema.
“Karibu sana sista hapa ndipo nyumbani kwetu ambako mtoto huyu atalelewa na kuishi, akitunzwa kwa hali na mali.”
“Mh! Ahsanteni sana nafurahi kupafahamu tutakuwa tukija kila mwezi kumtembelea ili kujua maendeleo yake.”
“Karibuni sana.”

Dakika kumi na tano baadaye sista aliyeongozana na Phillip na Lina aliaga na kuondoka akiahidi kurejea tena baada ya mwezi mmoja kujua hali ya mtoto huyo. Wakamsindikiza kisha akaondoka.
Kwa siku nzima walishinda ndani ya nyumba wakipanga  mipango  yote na jinsi ya kumlea na kumtunza mtoto huyo.  Lina akatoa wazo kwamba ni vyema wangemtafuta mfanyakazi wa ndani ambaye angekuwa tayari kumlea mtoto huyo na wao wangemlipa mshahara ambao angeutaka.

“Ni lazima atafutwe mtu wa kumlea mtoto huyu kwa upendo wote,” Lina aliongea.
“Kabisa, lakini nashauri awe mtu mzima kidogo.”
“Jinsi ya kumpata sasa ndiyo tatizo, sijui tuanzie wapi?”
“Hebu subiri kidogo,” Phillip aliongea akinyanyuka kitini kuelekea chumbani.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia siku ya Jumatatu katika Gazeti la Ijumaa Wikienda.

Views: 1980

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Mawazo Katota on February 11, 2012 at 12:26am

Good story

Comment by HAPPINESS MARCEL MASSAWE on February 10, 2012 at 9:31pm

Mh. kazi ipo hapo kwenye kumlea huyo mtoto

mnatakiwa kutafunta mtu anayependa watoto la sivyo mtaumbuka

Comment by Daudi on February 10, 2012 at 9:09pm

Huyo yaya asijekuwa ndio mama wamtoto alimtelekeza kwa sbb ya ugumu wa maisha.

Comment by Van Lusiu on February 10, 2012 at 8:15pm
its nice!
Comment by kaka on February 10, 2012 at 2:24pm

MMMMMMMMEEEE TEEEEEEE

Comment by laurenciamsunga on February 10, 2012 at 1:14pm
Nyie Lina na Philip muwe makini na huyo yaya wa mtoto wenu asije akaibiwa
Comment by FURAHA TAUSI on February 10, 2012 at 11:01am

EHE


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
8 minutes ago
GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
8 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website