The Deadly Treasure (Hazina ya Kifo)-61

KILA kukicha afadhali ya jana! Haya ndiyo aina ya maisha anayoishi Specioza kwani kila anapomaliza tatizo moja, ujue lingine lipo njiani linakuja. Licha ya kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kuhakikisha wanasheria wa kimataifa, James Mwang’amba na Hans Ludovick wanaanza kazi ya kutafuta utetezi wa kisheria ambao ungemweka huru Anointed na rafiki yake, Muddy, kikwazo kingine kinaibuka. Hans anaingiwa na tamaa ya kuvunja amri ya sita na Specioza.

Mumewe, Anointed na Muddy kwa pamoja walikuwa wakikabiliwa na kesi ngumu ya ujambazi na utekaji wa mtoto wa Waziri mkuu, Lucia ambapo kwa mujibu wa sheria za Tanzania, makosa hayo yangewafanya wahukumiwe kifungo cha miaka 30 au maisha jela. Kazi kubwa ya Mwang’amba na Hans ni kuhakikisha wanasimama mahakamani na kutoa utetezi ambao ungewarejesha uraiani Anointed na mwenzake.

Wakati taratibu za kisheria zikianza kukolea, tamaa ya Hans inazidi kuwaka na sasa anajiapiza kufanya kila linalowezekana ili kulifaidi penzi la Specioza. Kikwazo hicho kinakuja muda mfupi baada ya kile cha awali cha Specioza na mwanaye kunusurika kutekwa kupita.
Mambo yanazidi kuwa magumu kwa Anointed kwani akili na nguvu zote za Hans, aliyekuwa anategemea ataikamilisha kazi ya kumtoa gerezani haraka na mwenzake, inahamia kwenye penzi la Specioza. Mwang’amba anakuwa wa kwanza kushtukia na anamuonya mwenzake lakini haelewi.

Hans anaingia chumbani kwa Specioza na kufanikiwa kupanda kitandani wakati Specioza na mwanaye wakiwa wamelala fofofo. Anaanza kujiandaa kumuingilia kimwili Specioza ambaye haelewi chochote kinachoendelea.
 Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO...
 
Mapambano makali kati ya polisi na vijana waliokuwa wanataka kumtetea Ford yaliendelea kwa dakika zaidi ya ishirini, milio ya risasi ikawa inasikika huku na kule, hali iliyofanya raia wa kawaida kukimbiakimbia huku na kule kuokoa maisha yao. Polisi walizidi kuongezeka uwanjani pale, wakawa na kazi ya ziada kuhakikisha hakuna mhalifu hata mmoja anayekimbia.

Ford, licha ya kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote, alishindwa kujinasua kutoka kwenye mkono wa sheria, askari kadhaa wenye silaha nzito walimuandama kila alipokuwa anajaribu kutoroka, mwisho akakubali matokeo na kusalimu amri, akafungwa pingu na kutolewa mzobemzobe mpaka nje ya uwanja ambapo alipakizwa ndani ya karandinga la polisi. Vijana watatu kati ya wale waliokuwa wanapambana na polisi kwa lengo la kumuokoa, walipigwa risasi na kufa pale uwanjani, wengine wakafanikiwa kutoroka kwa kutumia Landrover nyeusi waliyokuja nayo.

Baada ya kukamatwa, Ford alipelekwa mpaka makao makuu ya polisi ambapo aliandikisha maelezo yake kwenye jalada maalum la kesi, kisha akapelekwa mpaka kwenye gereza kuu la ukonga chini ya ulinzi mkali. Aliingizwa na kwenda kufungiwa kwenye chumba cha peke yake, ndani kabisa ya gereza lile. Ile ndege iliyokuwa imebeba shehena kubwa ya madini ghali, ikabaki pale uwanja wa ndege huku askari wenye silaha nzito wakiilinda.

Baada ya kushindwa kumuokoa bosi wao kutoka kwenye mkono wa dola, genge la vijana wahuni waliokuwa nyuma ya Ford walianza kuandaa mkakati wa kwenda kuuteka uwanja wa ndege na kuondoka na ile shehena kubwa ya dhahabu iliyokuwa inashikiliwa baada ya Ford kukamatwa. Mipango kabambe iliandaliwa, magari matatu yakawekwa tayari kwa ajili ya kazi huku marubani wawili wa kampuni moja ya ndege wakiandaliwa kwa ajili ya kuitorosha ndege ile kutoka kwenye ule uwanja.

Mipango yote ilipokamilika, safari ya kuelekea uwanja wa ndege ikaanza. Vijana karibu ishirini, wakiwa na silaha nzito za kivita na mabomu ya kutupwa kwa mkono wakawa wanaelekea uwanja wa ndege huku wakiwa na lengo moja tu! Kutorosha hazina kubwa ya madini iliyokuwa kwenye ndege iliyozuiwa pale uwanja wa ndege baada ya Ford kukamatwa.

Dakika 30 zilitosha kuwafikisha uwanja wa ndege, wakasimamisha magari yao nje na kuanza kupanga namna ya kuingia kwa kishindo ndani ya uwanja ule bila kushtukiwa na mtu yeyote. Kila mmoja alianza kuikagua silaha yake kuhakikisha ipo tayari kwa kazi.        
***
Specioza akiwa kwenye usingizi mzito, alianza kuhisi hali ambayo haikuwa ya kawaida. Alianza kuota ndoto kama amelala na mumewe Annointed, akawa anafurahia joto la mwili wake, hali iliyomfanya azidi kujisogeza mwilini mwake na kumkumbatia kwa nguvu. Aliendelea kuuchapa usingizi huku ndoto yake ikiendelea kukolea.

Hans aliyekuwa na uchu wa penzi la Specioza kama fisi aliyeona mfupa, alishangaa Specioza akimkumbatia kwa nguvu, akawa anashangilia kimoyomoyo kwani aliamini muda mfupi baadaye atajilia vyake kiulaini. Alishangaa kwa nini Specioza amekubali kirahisi namna ile kumkumbatia. Kilichomshangaza zaidi, ni kuwa alimsikia akikoroma wakati akiwa amemkumbatia, jambo lililomfanya ahisi kuwa alikuwa ndotoni.

Aliamua kuitumia nafasi ile kikamilifu, taratibu akapitisha mkono wake mpaka mgongoni kwa Specioza, akaanza kufungua vishikizo vya ‘night dress’ aliyokuwa ameivaa. Taratibu akaendelea kuivua huku akijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote kutomshtua Specioza aliyekuwa anaendelea kukoroma. Alifanikiwa kuivua nguo ya juu, macho yake yakaganda kwenye kifua kizuri cha Specioza kilichokuwa kimenawiri vizuri na kupendezeshwa na vifuu viwili vya nazi vilivyokuwa vimejaa kisawasawa.

Hans alianza kubabaika, akawa haelewi nini cha kufanya. Kwa umakini mkubwa akakibusu kifua chake na kushika ncha za vifuu vya nazi, akamsikia Specioza akiguna usingizini na kuanza kujinyonganyonga mwili mzima. Hakuishia hapo, taratibu aliendelea kujaribu kuivua nguo iliyokuwa imebakia. Alipogusa pindo zake, Specioza alijinyoosha tena, safari hii kwa nguvu zaidi. Ilibidi Hans ajikaushe kama hakuna kilichotokea, akasubiri mpaka alipotulia kabisa, akaendelea.

Utundu wake ulisababisha mpaka akafanikiwa kuishusha nguo yake hadi magotini, akabakiza kazi moja tu... kuimalizia ya mwisho iliyokuwa imesalia maungoni mwa Specioza. Tamaa ya kula tunda la mti uliokatazwa ilizidi kuwaka ndani yake, akawa anatetemeka mwili mzima huku akianza kujihisi kama tayari yupo kwenye ulimwengu mwingine.

Specioza alishtuka kutoka usingizini na kitu cha kwanza ilikuwa ni kuangalia kama kisu alichokuwa amekificha chini ya mto aliolalia kipo mahali pake. Alipohakikisha kipo mahali pake, aliinua mkono kujaribu kuangalia kama mwanaye alikuwa amelala sehemu yake. Alipohakikisha yupo salama, alishusha pumzi ndefu na kupiga miayo mfululizo. Katika hali ambayo hakuitegemea, alipojinyoosha, alishangaa kujikuta akimgusa mtu pembeni yake, tena akiwa hana nguo hata moja mwilini. Mshtuko alioupata ulikuwa hauelezeki, mapigo yake ya moyo yakawa yanaenda kasi kama injini ya ndege.

Alitulia kwa sekunde chache huku mkono wake mmoja ukiwa tayari umeshakishika kisu kilichokuwa chini ya mto aliolalia. Hans akiwa amemezwa na tamaa ya kuvunja amri ya sita na Specioza, hakugundua kuwa tayari alikuwa amezinduka kutoka kwenye lindi la usingizi, akawa anaendelea na kazi yake aliyoianza muda mrefu uliopita. Alipitisha mikono yake kukizunguka kiuno cha Specioza, akashika pindo za kufuli lake na kujaribu kuivua.

Hilo ndiyo kosa kubwa lililomgharimu kuliko alivyotegemea kwani Specioza alitulia akitaka kujua yule aliyekuwa amelala kitandani kwao ni nani na alikuwa akitaka kufanya nini. Alijishangaa kushtuka na kukuta tayari nguo alizovaa wakati wa kulala zimevuliwa. Akahisi lazima kuna mbakaji amewaingilia. Alipomshika kiuno, akajua moja kwa moja kuwa alikuwa akitaka kumuingilia kimwili bila ridhaa yake, jambo ambalo hakutaka litokee kamwe maishani mwake. Kwa kasi ya ajabu aliinua juu mkono uliokuwa na kisu chenye makali pande zote mbili na kukizamisha kwenye mwili wa yule mtu, ambaye bado alikuwa hajamtambua ni nani.

Damu nyingi ziliruka juu mithili ya bomba la maji lililopasuka, zikatawanyika na kuchafua mashuka na nguo zote zilizokuwa jirani. Kwa kutumia nguvu za ziada, alikichomoa kile kisu mwilini mwa yule mtu, lakini akiwa anajiandaa kukizamisha kwa mara ya pili, alishtuka kupita kawaida baada ya kugundua kuwa mtu aliyekuwa eneo lile ni Hans.

“Dont kill me Specioza please... “ (usiniue Specioza tafadhali) alisema Hans kwa tabu huku akijaribu kuziba jeraha la kisu kwa kutumia mkono. Licha ya kujitahidi kuliziba, damu ziliendelea kumwagika mithili ya chemchemi, giza nene likaanza kutanda kwenye macho yake baada ya kuvuja kiasi kikubwa cha damu ndani ya muda mfupi.

Specioza aliinuka haraka na kumbemba mwanaye juujuu, akatoka mbio mpaka kwenye chumba cha Mwang’amba ambaye bado alikuwa akiendelea kupitia vitabu mbalimbali vya sheria kutafuta mbinu ya kumkomboa Anointed na mwenzake Muddy.

Mwang’amba alishangaa sana kuona Specioza akiingia chumbani kwake kwa kasi kubwa, akiwa amevaa nguo za kulalia na kujifunga kitenge, huku mwili mzima akiwa ametapakaa damu. Ilibidi amtulize kwanza na kuanza kuhoji nini kimetokea. Specioza huku akihema kwa nguvu, alieleza kila kitu kilivyokuwa. Kwa pamoja wakatoka na kukimbilia kwenye kile chumba alichokuwemo Hans.

Walipoingia walikuta akitapatapa kwa kurusha mikono na miguu kama mtu anayetaka kukata roho. ilibidi watoe taarifa kwa uongozi wa hoteli mara moja, gari la kubebea wagonjwa likawekwa tayari na dakika chache baadaye, Hans akatolewa chumbani na kwenda kupakizwa kwenye gari lile. Safari ya kuelekea kwenye Hospitali ya Aga Khan, ambayo ndiyo iliyokuwa jirani na pale walipo, ikaanza kwa kasi kubwa.
Je, nini kitafuatia? Usikose wikiijayo kwenye gazeti hili la Amani.

Views: 1535

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Mawazo Katota on February 25, 2012 at 12:01am

Kazi kubwa na mbichi

Comment by elias m slian on February 24, 2012 at 11:09am

khaaaaaaa hii kazi kwelikweli tamaa imezaa mauti

 

Comment by Emmanuel Mallewo on February 24, 2012 at 12:47am

Uliambiwa uache sasa umeona kinachokutokea

Comment by Van Lusiu on February 23, 2012 at 8:58pm
Katika mabwege ni pa1 na hansi. We uliona wapi mapenzi ya hivo.
Comment by DORAH FREDY on February 23, 2012 at 1:19pm
mmh pole sana Hans ulitaka mweyewe lakini
Comment by Nathanael michael on February 23, 2012 at 12:59pm
We umeona wap bwana kaz na mapenz vikashirikiana?!
Comment by FURAHA TAUSI on February 23, 2012 at 12:09pm

HANS ULIYATAKA MWENYEWE

Comment by faisalone on February 23, 2012 at 12:08pm
daa iyo kaleeeee
Comment by Daudi on February 23, 2012 at 12:08pm

Dah! Ni kweli tamaa mbele na mauti yanaf........???

Comment by william mhehe on February 23, 2012 at 12:07pm

Hii imekaa vizuri sana, tusubili vibaraka wake kule airport itakuaje?


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
12 minutes ago
GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
12 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website