HALI inazidi kuwa tete ndani ya Gereza la Segerea. Wakati matukio ya kutisha ya mauaji ya wafungwa wawili wa kike ndani ya gereza hilo yaliyotokea katika mazingira ya kutatanisha yakiwa bado hayajasahaulika, kunatokea songombingo la aina yake.
Muuaji hatari aliyekuwa anashikiliwa kwa makosa ya kuwaua watu wengi na kuwakata vidoa vya urembo, Nsia, anatoroka katika mazingira ya kutatanisha baada ya kuwazidi ujanja askari magereza waliokuwa lindo usiku wa tukio.
Anaanza kwa kujifanyisha kuwa anaumwa sana, ambapo askari magereza mmoja anapomsogelea, anamuonea huruma na kuamua kufungua mlango ili ampeleke kwenye Hospitali ya Magereza, kosa linalosababisha maafa makubwa.
Nsia anamgeuka askari huyo na kumkaba kwa nguvu mpaka anapoteza fahamu, anakimbia mpaka kwenye lango kuu ambapo napo anamkaba askari aliyemkuta na kufanikiwa kutoroka hadi nje. Muda mfupi baadaye, askari wengine wanagundua juu yakutoroka kwake na kengele ya hatari inagongwa haraka.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO...
“Kuna mfungwa ametoroka muda mfupi uliopita, amefanikiwa kuwazidi ujanja askari magereza wote na kutoroka. Askari wawili wapo hoi baada ya kukabwa kwa nguvu na mfungwa huyo.”
“Afande huyo mfungwa ni mwanaume au mwanamke?”
“Maswali gani ya kipuuzi unayouliza, kwani upande huu wanakaa wafungwa gani? Sitaki maswali, nataka kila mmoja akachukue silaha na kuanza kazi ya kumsaka kwa udi na uvumba. Asipopatikana wote mliokuwa lindo leo mtaingia kwenye matatizo makubwa, tawanyika!”
Askari magereza walianza kukimbia huku na kule, wengine wakaelekea kwenye bohari kuu ya silaha ambapo walipewa bunduki na risasi, wengine wakaelekea mahali walipokuwa wanahifadhiwa mbwa wa kijeshi, kazi ya kumsaka Nsia ikaanza mara moja.
“Afande, huyo mfungwa mwenyewe si ndiyo yule aliyekuwa na kesi nzito ya mauaji ya watu kibao na kuwakata vidoa vya urembo?”
“Nasikia ndiyo huyo, yaani hapa natetemeka kweli, inaonekana anaongozwa na nguvu za giza yule, tukijifanya kimbelembele anaweza kutuua hata sisi.”
“Mh! Ila kweli, unajua yale mauaji yaliyotokea hivi karibuni humu gerezani ni yeye ndiyo aliyasababisha?”
“Ndiyo, yaani hatari tupu,” askari magereza wawili waliokuwa wamebeba bunduki, walikuwa wakijadiliana huku wakikimbilia nyuma ya gereza lile pamoja na wenzao kumsaka Nsia.
Tochi nyingi zikawa zinamulikwa kwenye vichaka vilivyokuwa nyuma ya gereza lile huku milio ya mbwa wa kijeshi nayo ikizidi kuongezeka. Msako mkali uliendelea eneo lote la kuzunguka gereza mpaka mitaani wanakoishi raia lakini hakukuwa na dalili zozote za Nsia kupatikana.
Mpaka kunaanza kupambazuka, hakukuwa na matumaini yoyote ya Nsia kupatikana. Vyombo vya habari zikiwemo redio na runinga vikawa vinatangaza juu ya habari za mfungwa wa kike kutoroka gerezani katika mazingira ya kutatanisha. Picha zake zikawa zinaoneshwa kwenye runinga huku zawadi nono ikitangazwa kwa yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwake.
“Mimi nimemuona kwa macho yangu alfajiri ya leo, ni yeye kabisa.”
“Umemuona wapi?”
“Asubuhi wakati natoka kwenye kazi yangu ya ulinzi nimepishana naye kule kwenye bonde la Mto Msimbazi akiwa anakimbia.”
“Alivaaje?”
“Alivaa nguo kama za askari magereza, kichwani alivaa kofia iliyomziba usoni,” msamaria mwema mmoja alikuwa akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Gereza la Segerea. Harakaharaka taarifa zile zilianza kufanyiwa kazi, askari wengi wakaelekezwa kuelekea kwenye Bonde la Mto Msimbazi.
Polisi wenye silaha waliongezwa kusaidia kazi ile, nao wakaungana na wenzao wa magereza kulizingira bonde la Mto Msimbazi. Kila walipokuwa wakipita na kuulizia kama kuna mtu aliyevaa nguo za askari magereza au za kifungwa ameonekana, baadhi ya watu walikiri kumuona alfajiri na mapema akikimbia kwa kasi.
“Mimi pia nilimuona alfajiri wakati nikifanya mazoezi ya viungo, nikadhani ni askari yupo mazoezini.”
“Alikuwa anaelekea upande gani?”
“Upande wa Jangwani, alikuwa akikimbia pembezoni mwa bonde la Mto Msimbazi, mkimuwahi mtamkuta, naamini bado hajafika mbali,” msamaria mwema mwingine alitoa taarifa baada ya kuona habari ile ikirushwa kwenye runinga.
Taarifa zile zilizidi kuwapa moyo askari kuwa muuaji hakuwa amefika mbali, magari ya kijeshi yenye askari wengi yakawa yanarandaranda pembezoni mwa bonde la Mto Msimbazi. Askari walipofika Jangwani, tayari kulikuwa kumepambazuka kabisa huku kijua cha asubuhi kikiwa kimeanza kuchomoza.
Eneo lote la Jangwani lilipekuliwa bila mafanikio, watu waliokuwa wanahisiwa kumficha mtuhumiwa wakawa wanapewa misukosuko ya hapa na pale lakini bado haikusaidia kitu.
“Inawezekana amevuka barabara na kuendelea kukimbia kwenye majani marefu pembeni ya Mto Msimbazi. Hebu waamrishe askari nao wavuke barabara,” alisema mmoja wa makamanda waliokuwa wanaongoza msako ule. Amri ikatolewa kuwa askari waendelee kufanya msako kwenye bonde la Mto Msimbazi, wakavuka barabara eneo la Jangwani na kuhamia upande wa pili, nyuma ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Kuna mtu nimemuona muda si mrefu akikimbia pembezoni mwa Mto Msimbazi, alikuwa amevaa nguo kama za askari magereza.”
“Sasa kwa nini usimkamate?”
“Nitamkamata askari? Kwani kosa lake nini?”
“Kwani wewe hujui kilichotokea? Huna redio au runinga?”
“Nitavipata wapi wakati nipo kazini?” mlinzi wa Hospitali ya Muhimbili alikuwa akihojiwa kwa ukali baada ya kueleza kuwa alimuona Nsia akikimbia. Kila mmoja alimuona mzembe kwani taarifa zilishazagaa karibu kila kona ya Jiji la Dar es Salaam juu ya kutoroka kwa mfungwa huyo.
Hata hivyo, bado aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa hakuwa akielewa kinachoendelea, ikabidi askari waachane naye na kuendelea na msako mkali, wakielekea kule alikowaelekeza kuwa ndiyo alikimbilia.
“Hebu simameni, hiki kitu gani?”
“Ni nguo za askari magereza.”
“Mungu wangu, atakuwa ameshabadilisha mavazi, kazi inazidi kuwa ngumu,” alisema askari mmoja baada ya kukuta nguo zilizosadikiwa kuwa ndiyo alizotoroka nazo Nsia zikiwa zimetelekezwa kwenye msitu wa mikoko, jirani na Daraja la Salenda. Mbele kidogo walikuta nguo nyingine wavaazo wafungwa nazo zikiwa zimetelekezwa.
“Mh! Kwa hiyo amebaki uchi au?”
“Hata mimi sijui, mi nadhani lazima atakuwa jirani na hapahapa, hawezi kukimbia bila nguo.”
Wakati askari wale wakiwa bado wanaulizana, walishtuka kusikia purukushani kwenye kichaka, jirani na pale walipokuwa wamesimama. Wakapeana ishara haraka na kuanza kusogea kwa tahadhari kubwa kwenye kile kichaka, jirani kabisa na Daraja la Salenda.
Baada ya muda, wote walipigwa na butwaa baada ya kubaini kuna mtu alikuwa amefungwa kamba na kuzibwa mdomo na matambara, akiwa uchi wa mnyama. Wakazidi kusogea wakidhani ni Nsia lakini haikuwa hivyo. Waligundua kuwa mtu huyo alikuwa ni mwanaume. Wakamtoa matambara mdomoni na kuanza kumhoji.
“Kuna mwanamke ameniteka na kunifunga kamba kisha akanivua nguo zote na kuzivaa yeye. Alitaka kuniua, ni Mungu tu,” alisema mwanaume yule huku akitetemeka kuliko kawaida.
“Ameelekea wapi?”
“Amepanda juu ya daraja na kusimamisha gari, atakuwa ameshafika mbali sana muda huu.”
“Kwani wewe ulikuwa umevaa nguo gani?”
“T-shirt na jinzi, kichwani nilivaa kofia aina ya pama.”
“Amesimamisha magari ya kuelekea wapi?”
“Daladala ya kuelekea Mwenge.”
Je, nini kitafuatia? Usikose Jumanne ijayo kwenye Gazeti la Uwazi.
Comment
nsia ni balaa
Comment by Ainess Willy on January 3, 2013 at 11:36am nitazidi kusema hana kosa huuniutumwa ulioachwa na wazazi wake kwa kuabudu mizimwi mungu wangu msaidie apunguze makali yakuuwa tu basi
Comment by raphael Joram on January 2, 2013 at 9:47pm
Comment by DORAH FREDY on January 2, 2013 at 10:05am Mungu hyuyu Nsia ni balaa
HAYA SASA NSIA AMEINGIA KAZINI TENA
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
NDAUKA the GREAT |
| 3 |
julius manning |
| 4 |
LJH_3 |
| 5 |
Tatu Majaliwa |
| 6 |
hope |
| 7 |
mayalilwa |
| 8 |
steven emmanuel |
| 9 |
Matilanga Lukingita |
| 10 |
tina babi |
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies 0 Likes
JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies 8 Likes
Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies 3 Likes
Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…
Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE on Monday. 27 Replies 5 Likes
HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies 4 Likes
Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…
Tags: SOKA
Started by GLOBAL in Habari. Last reply by Billy Frank Irungu Apr 26. 118 Replies 21 Likes
Tags: NCHINI, HAPA, UNAFURAHIA, HUDUMA, ZAKE?
Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies 4 Likes
hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?
Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies 9 Likes
Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…
© 2013 Created by Global Publishers.





You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers