TAMKO RASMI LA CHADEMA UK KUHUSU MLIPUKO WA BOMU ARUSHA

Ndugu zangu Watanzania wenzangu,
Sisi Watanzania wapigania maendeleo - CHADEMA UK tumelazimika kuwasilisha majonzi yetu kwenu kwa njia hii, ikiwa ni katika kuonyesha mshikamano wa kitaifa kwa kujifariji na pia kuwafariji ninyi waTanzania wenzetu kutokana na tukio kubwa la kuhuzunisha sana ambalo limetokea hivi majuzi nchini mwetu huko mkoani Arusha.

Pamoja na kwamba pamekuwa na matukio kadhaa yaliyoikabili nchi yetu hili la Arusha tumeonelea tulisemee kwa njia ya kipekee, kwa sababu licha ya kwamba ni tukio la kigaidi, lisilokuwa na mantiki yeyote ile zaidi ya umwagaji damu wa raia wasio kuwa na hatia, bali pia utekelezwaji wake unaweza kutuachia athari kubwa sana kisaikolojia na kimahusiano kama tusipojaribu kulitathmini na kulitafakari kwa upekee wake.

Wakati ambapo sala na maombi yetu kwa sasa yawaeendee wafiwa na wale ambao wamedhurika moja kwa moja kimwili ama kisaikolojia kutokana na tukio hili, tunapenda pia kupongeza juhudi zilizofanywa na kila mmoja wetu aliyeweza kuwafikia na kutoa msaada wa aina moja ama nyingine kwa wahanga wa janga hili bila kujali tofauti ya vyama, itikadi, kabila, dini ama falsafa. Hiyo ndiyo Tanzania tunayoijua sisi. Pamoja na tofauti zetu nyingi ki hali,afya ama kipato, lakini kamwe hatubaguani katika misingi ya rangi, kabila ama dini. Na hili ndio haswa linalotusukuma sisi kuwasilisha huu waraka wa rambirambi kwenu ninyi wenzetu leo hii.

Tuna imani kwamba vyombo vyetu vya usalama vitafanya utafiti wa kina kuchimbua na kutujuza chanzo cha ufedhuli huu, ni lazima sisi wenyewe pia tufarijiane kwa maombi, michango na tafakuri mbalimbali zenye kutiana moyo katika kipindi hiki kigumu kwetu sote. Tuna imani kwamba yeyote aliyehusika katika mkakati huu atapatikana na kupewa adhabu inayostahili.

Kwetu sote Watanzania, huu ni wakati muafaka kuonyesha mshikamano wetu kuwatumia ujumbe hao wachache wenye nia mbaya kwamba Watanzania tumeundwa kutoka jumuiya ya makabila zaidi ya mia moja, wenye asili, rangi, dini na madhehebu mbalimbali na wasioamini. Na kati yetu wote sisi ni marafiki na ndugu, wengine ni ndugu wa damu kabisa, kupitia ndoa, wazazi n.k. Hivyo sisi hatuwezi kubaguana wala kuwa na chuki miongoni mwetu kwani hiyo si asili yetu. Na yeyote yule atakayejaribu kupandikiza mbegu hii chafu miongoni mwetu tumkatae na kumchukilia hatua stahiki kumtokomeza yeye na kundi lake.

Ujumbe wetu kwa Watanzania ni huu:
HII NI VITA DHIDI YA UMOJA WETU WA KITAIFA NA SIYO KUNDI AU IMANI FULANI.

Asanteni sana, Mungu awabariki nyote. Mungu alibariki taifa letu Tanzania.
Kwa niaba ya CHADEMA UK    
G Mboya
Katibu

Views: 562

Tags: CHADEMA, UK

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by julius manning on May 9, 2013 at 12:36pm

nimekubali

Comment by mayalilwa on May 8, 2013 at 2:39pm

Mungu hamfichi mnafiki, ukweli utajulikana tu.

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }