TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU VURUGU ZA ARUSHA

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda Paul Chagonja akizungumza na Waandishi wa habari katika Makao makuu ya Jeshi hilo leo.

   Video ikionesha jinsi polisi walipokuwa wakituliza ghasia katika vurugu hizo.

Baadhi ya Makamanda wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, wakiangalia sehemu ya video iliyokuwa ikionesha jinsi Polisi walivyokuwa wakituliza ghasia huko Arusha.

PICHA NA HARUNI SANCHAWA / GPL

Views: 25

Tags: ARUSHA, JESHI, KUHUSU, LA, POLISI, TAARIFA, VURUGU, YA, ZA

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by nzagamba on January 17, 2011 at 5:12pm
ushuhuda ulio tiliwa ukarabati.hiyo video clip walio onyeshwa waandishi wa habari ilikuwa na lengo mahksusi ya kuupotosha uhalisia wa tukio lenyewe. ina wezekana kuna mambo fulani ndani ya taarifa hiyo yana ukweli. kama mawasiliano ya awali baina ya pande hizo mbili.nk. lakini polisi ili taarifa hiyo iwe na mashiko,ilbidi wawe na timing nzuri ya wakati wa kuitoa.kosa walilo lifanya ni kuchelewa kuitoa wakati vyombo vingine vya habari, vilitangulia kuitoa. na sisi sote tusio na vijiboriti kwenye macho yetu tulijionea sawia virungu vilivyo shushwa katika maungo ya binadamu. hivi hiyo "scenario "ya kuwa walitaka kuteka kituo cha polisi,kuufuta mji wa arusha katika ramani ya dunia!! hee. huyo nduli alie kuwa na jeshi nyuma yake alishindwa. sembuse wadudi hawa wa kawaida. ambao silaha yao kubwa ilikuwa vidole viwili vilivyo chanua,mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusiana na umeya ulio chakachuliwa.ndio intelijensia tunayo taka kuaminishwa kuwa ndio ilitumiwa kuwa dhibiti. tafadhalini banaa. hata kama umekataa kufikiri, au unajilazimisha unayo taka kuya amini kwa vile tu ndo imezoeleka hivyo. basi utazame ukweli ulio mbele ya macho yako. hebu tazama picha ya askari mwenye tabasamu nene baada ya kumdunga rungu mchumba wa dkt slaa.eti kwa kosa la kuwa mwanachama wa chama usichokipenda. hebu tazama kitambaa cheupe alicho jifunga begani halafu unipe tafsiri yake. lkn bado intelijensia inatushawishi ya kuwa mama huyo alikuwa ana tu gruneti kadhaa mfukoni. amaa!! unashangaa nini. si wewe ulie jishebedua, na kujitia boriti macho yako. ukijiaminisha yakuwa ulio yaona kwenye runinga ni ze komedi. TBC,ITV tumeshuhudia kwa macho yetu. na huko TBC na shaka alie sahau ku-edit hiyo clip nae wanaweza waka MTIDO. jeshi la polisi la sasa naamini wasomi wapo wa kutosha kudhibiti mihemko ya hawa wanao subiri kupewa amri tu. huo mpango kazi ndio taratibu za kisayansi za kutekeleza majukumu ya professionals kama polisi. so what kama wanataka kutumia njia zaidi ya moja. jukumu lenu ku-adapt accordingly. nasio kutumia sababu dhaifu za kupambana na wananchi. bila confrotation ya polisi, hakuna uvunjifu wa amani. sana sana vibaka wa kawaida ambao kwao mkusanyiko wowote ni neema kwao. hawa wana dhibitika hata na waandamanaji halisi wenyewe. POLISI mmeteleza. jifunzeni , muimarike kutokana nakuliona kosa lenu. sio kujificha nyuma ya " spin masters". mtaendelea kupambana mpaka lini na waandamanaji? na hasa wale ambao serikali haitaki kupokea malalamiko yao. mkiwa sababisha wakaenda underground. nadhani hiyo itakuwa mbaya zaidi. na mtakuwa mmetengeneza tatizo kubwa zaidi. Arusha ni mji ambao unasifa ya siku nyingi kama kimbilio la watalii,na pia makao makuu ya taasisi nyingi za kimataifa. ikiwemo mahakama ya kimataifa ya mauaji ya rwanda. itakuwa aibu kubwa kama na sisi itafunguliwa mahakama kutazama kesi za ukatili wa polisi kwa raia ndani ya nchi. hebu tazameni kisa kilivyo anza. ni uchu tu wa madaraka ya kisiasa ya chama tawala.kumpata meya kutoka chama hicho. kwani wana fahamu fika kuwa bila kufanyika madudu yaliyo fanyika. hakika meya wa jiji la arusha kutokana na wingi wa madiwani kupitia chama cha chadema arusha, angetoka miongoni mwao. kifanyike nini? ahaa!! tuwakoroge hawa itisha uchaguzi bila kuwashirikisha chama chenye madiwani wengi. hivi swala hili linge fanyika mathalan manispaa ya ilala ambako madiwani walio wengi ni kutoka ccm. linge vumilika.?  la hasha. polisi kuweni impartial ktk kutekeleza majukumu yenu. wananchi wanaona treatment chama tawala inavyo pata toka jeshi la polisi. mara zote wanapokuwa na shughuli zao na kinyume chake wapinzani wanapo taka kufanya shughuli zao. kama ni lawama. ielekezwe kwa hawa viongozi wetu ambao kwao maslahi yao binafsi, kikundi cha watu wachache ndani ya chama ndio yanayo pewa kipaumbele. hata dhidi ya maslahi ya wananchi walio wengi. Hongera mzee lowasa kwa kuiona hatari inayo tukabiri sio kwa wana arusha pekee na hata sehemu nyingine. kama hatuta jenga tabia ya kukaa meza moja tunapo tofautiana na kutetea mustakbali wa taifa kwanza. halafu mambo mengine ya vyama yaka fuata. hongera viongozi wote ambao mnalisemea na kukemea haka katabia ka kulazimisha mambo hata kama ridhaa ya wananchi haipo. na wale viongozi ambao kwa masikitiko makubwa vichwa vyao wamevichimbia shimoni wakiamini wamejificha mithili ya mbuni.basi wajue amani itakapo toweka na wao itawakumba tu.   
Comment by Elisha Elias on January 15, 2011 at 11:12pm
VIONGOZI CHADEMA WANA DAMU ZA WANANCHI MIKONONI MWAO-ARUSHA

Kwa ninavyoona mauwaji na vurugu za arusha wengi wamelaumiwa, na shutuma nyingi kwa CCM, Polisi, Serikali Nk. Na hata kuna ma punguani wachache ambao hata wanalaumu watu wasiohusika, na kuna watu wamefanywa waonekane kuwa “Watakatifu” sana hali wana damu za wananchi mikononi.... Najua hatupendi kusikia hili tulio wengi ila liwalo na liwe “Bora Kumfunga Paka Kengele” kwani nani anafurahia wananchi wanapoumia kwa maslahi ya kisiasa ya wanasiasa wachache, Ukiangalia kwa undani pande zote mbili kwa mtazamo wa Polisi na nafasi waliyokuwa nayo na kama ungejiweka nafasi yao ungekuwa wewe ni Polisi na kama ukiangalia taarifa zote mbili ya Polisi na CHADEMA.
Viongozi wa CHADEMA ni wakulaumiwa sana tu kwa vurugu, maumivu na vifo vilivyojitokeza Arusha na tena nao wana damu za wananchi mikononi mwao na wanapaswa kulaumiwa bila kuficha. Wa kwanza kumlaumu ni viongozi wa CHADEMA wote waliohusika kuwachochea na kuwaamuru wananchi kwenda kuwatoa viongozi wao wa chama waliokuwa wanashikiliwa na Polisi, tumewalaumu Polisi vya kutosha na tunaweza kuendelea tu kama kawa, ila ukweli viongozi wa chama cha CHADEMA kila moja kwa nafasi yake waliokuwako siku ile ni chanzo cha yote yaliyotokea kwa kuwa walikuwa na nafasi ya kutumia njia mbadala ambazo zisingepelekea vurugu na mauwaji ila hawakuzitumia, na kwa kuwachochea wananchi kufanya wanayotaka wao,
Polisi wana matatizo yao, wana mapungufu yao, si Malaika,....hayo sote tunayaelewa ila hata kama wewe ungalikuwa moja wa wale Polisi kituoni, usingekubali wananchi waje wavunje kituo,na wafanye wanavyotaka au wawatoe watuhumiwa na wahalifu wote,pamoja na watuhumiwa wanaowahitaji, pale kuna vithibiti vya kesi mbali mbali zingine zote wanazofanyia kazi, waingie ofisi wanazotaka na pale kuna silaha pia, je watu hao wanaofanya wanachotaka wakiwa na mawe tu, na hawaongozeki, hawazuiliki wakiwa na silaha za moto kama bunduki na mabomu itakuwaje??
Lile halikuwa swala la polisi na waandamanaji tu, lilikuwa swala la polisi na watu waliotumwa, na waliopokea utume huo toka kwa mtu mwenye ushawishi mkubwa na aliye kiongozi wa muda mrefu na mtu Aliyekuwa Baba wa kiroho wa watu wengi kabla hajaingia kwenye siasa, na walipokea maneno yake kama injili namaanisha… (Bila swali bila kubisha, na kwa moyo wao wote hata ikibidi kupoteza maisha yao). Nasikitishwa kwa vifo vya wanachi wasio na hatia waliojitolea kwa moyo wakitetea kufa na kupona hadi kupoteza maisha. Naumia kwa viongozi waliowatuma hali wakijua yangetokea na wakijua kuwa polisi waslikuwa wanawashikilia viongozi tu na kuna dhamana, wangetoka, na polisi wasinge wadhuru.
Damu ya watanzania iliyomwagika ipo mikononi mwenu wazee wangu viongozi wa CHADEMA, nasema haya kwa masikitiko,ya kuwa tujifunze kuchukua maamuzi tukiangalia maslahi ya wananchi tunaowawakilisha, na next time you want to use a human shield, try to be in the front line from the beginning to the end, or send your fiancée, wife, son, daughter and other close people so you can also feel the same these innocent faithful civilians felt near to the Police station in Arusha.

una lolote limekugusa mpaka hapo tuma sms kwenye namba yangu 0763737372 "Elisha Elias"
Comment by Joeli Simion on January 14, 2011 at 7:24pm
Kama ndivyo ilivyo kamataarifa isomekavyo', basi jeshi la Polisi halina makosa. Kwani hatuko tayari kuona silaha zamoto zikizagaa ovyo mitaani. Kwani unafikiria nini kingetokea iwapo wangefanikiwa kukiteka kituo cha Polisi?
Comment by sherry shebe on January 14, 2011 at 10:50am

hawa chadema sasa wanafikia azma yao ya kumwagisha damu kwa sababu hiki ni kitu wamekuwa wakijiapiza ila kwa bahati mbaya wanamwagisha baki labda wengine hawakuwa hata sehemu ya chadema jamani hata kama mabadliko tunataka mabadiliko ya amani na sio ya kumwaga damu kamani hivyo bora tubaki na serikali hii mnayosema ya mafisadi kuliko watu wasiojali maslahi yetu

Comment by besta msumange on January 14, 2011 at 10:09am
hii taarifa hainiingii akilini ,naomba kuuliza mkutano uliruhusiwa je hao wanachama na wapenzi wa chadema wangefikaje huko kwenye viwanja vya NMC ? wangepaa,maana hapa nashindwa kuelewa kabisa,kwa sababu kikao kilikuwa na muda maalum kwahiyo kila mtu amepanga /amekadiria muda wake wa kufika mkutanoni hilo halikwepeki lazima watakutana na wafuasi wengine wakielekea eneo la tukio na kuongozana ,na pia nashindwa kuelewa kuandamana nini maana yake ,kwa ufahamu wangu watu wakiwa watano wanatembea waweza sema wanaandamana,na je nawauliza hao polisi hicho kituo cha polisi  kilivamiwa na waandamanaji baada ya kutembea km 2,au ilikuwaje ,pia kama wenyewe na full video tunaomba watuonyeshe mwanzo mwisho wa tukio lenyewe ili watanzania wajiridhishe, na je ni haki kupigana na watu wasio na risasi ,kirungu wala baruti,au kama walivyosema wao kuwa waandamanaji walikuwa na mapanga na visu,hii ni uongo uliokomaa ,hii ilitokea pemba mwaka 2000 defender za polisi zilikuwa zinatembea na mapanga kwenye gari ,wakikamata vijana wanawalazimisha wakamate yale mapanga then wanawapiga picha kumbe huku kukawa na wajanja ambao wanarekodi tukio nzima. kwa hayo yote polisi naomba tutumie busara na hekima kubwa katika kazi zenu ,la sivyo jeshi litapoteza ushirikiano na wananchi.
Comment by Nicholaus sanga on January 14, 2011 at 9:57am
Kwa kweli inasikitisha sana, Police kutumia nguvu nyingi sana kwa kuua inzi, kwani walikuwa na uwezo wa kutumia maji ya kuwasha tuu ingetosha. police wanambinu nyingi sana za kuweza kutawanya umati mkubwa bila madhara yeyote. kwa kweli hii itawaghalimu sana maana kutoa roho kwa kweli ni Dhambi kubwa kwa watu wasio na hatia. Fikilia familia zao, watoto,mke,na jamaa kwa ujumla watawaonaje police wakiwa Barabarani?.!!!!.
Comment by Mrs Tina allen on January 14, 2011 at 9:40am
ha ha ha kweli mfa maji haachi kutapatapa .kweli serikali hii imelala fo fo fo.Wanafikiri kuwa wananchi wote ni wajinga na hawaoni.Hio Taarifa yenu ya kutunga sijui mmetungiwa na nani. hivi uhuru wa kuandamana uko kwa CCM tu??????.Wengine wakiandamana kunakuwa nataarifa za kiinteligensia?? Kwa nn hizo Mbinu za kujua taarifa za kiinteligensia msitumie kwa Dowans,Richmomd,Kagoda na mafisadi wengi walioko seriakalini???? Jeshi sasa limekuwa la kisiasa zaidi. Mjue ya kuwa Chadema ni chama halali na kimesajiliwa na kina uhalali wa kufanya mikutano yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi.KATIBA SI YA CCM peke yake ni ya wananchi wotee .Hakika DAMU YA WANA WA ARUSHA ITAWALILIA NA HAKIKA MTALIPWA. Acheni usaniii Hatudanganyikiiiiiiiiiiii
Comment by baraka ndesamburo on January 14, 2011 at 9:04am
mheshimiwa uliyeandika hiii taarifa unaonekana una kipaji kikubwa sana cha siasa maana nimeshindwa kuelewa hii ni taarifa ya polisi au siasa ushauri wangu tu usikilazie damu kipaji chako 2015 ugombee uraisi nahakika utashinda na hata kura yangu utapata hongera kwa kukomaa kisiasa
Comment by helen ahaz ntahena on January 14, 2011 at 9:01am
kwakweli mmejalibu kutudanganya
Comment by MSEMI MGONZA KIRUNGI on January 14, 2011 at 12:59am

polisi mmezoea kutumia nguvu kwa wananchi sasa watu wameshachoka tunasema huu huwe ndio mwisho wenu wa kuwanyanyasa raia kwani nani hafahamu kuwa huyo igp wenu kafanya hivyo kwa kumlidhisha huyo wake mary chatanda ili liwe fundisho la kudai uchaguzi wa umeya urudiwe na wake chatanda asishiriki kuanzia sasa atujari kama kuna mwema au makamba tutapambana nanyi mpaka mwisho.


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
8 minutes ago
GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
8 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website