Manka anashindwa kuitumia vyema bahati ya kipekee aliyoipata ya kuchaguliwa kuwa mshiriki mkuu wa filamu ya Sweet Pain baada ya kushinda usaili na kupata mkataba mnono wa dola za Kimarekani milioni mia moja kutoka kwenye Kampuni ya Centurion Films ya Hollywood, Marekani. Anabadilika kwa kila kitu baada ya kufika huko.

Hakumbuki tena maisha ya dhiki aliyokuwa akiishi kijijini Shokoni na anamsahau kabisa hata mpenzi wake waliyetoka naye mbali, Martin na kujikuta akiangukia mikononi mwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Centurion, Jon Curtis.

Baada ya kufikia kiwango cha juu cha mafanikio, Manka anaporomoka kwa kasi baada ya kuingizwa kwenye dimbwi la matumizi ya madawa ya kulevya na Jon ambaye anamhadaa kwa penzi la kisaliti na kufanikiwa kumteka kiakili. Baada ya kutopea kwenye matumizi ya dawa za kulevya, Jon anamtapeli kila kitu.

 Baada ya kufanikisha azma yake, anaenda kumtelekeza Manka kwenye kituo cha mateja cha LDARE, Los Angeles akiwa mjamzito. Baada ya kumfikisha huko, Jon anakata mawasiliano kabisa na haendi tena kumjulia hali.

 Mabadiliko ya hali ya Manka yanakuwa gumzo Hollywood, Marekani na dunia nzima kwa ujumla. Vyombo vya habari vinambeza na kumuona kama limbukeni aliyevamia Hollywood kwa pupa. Magazeti yanaandika sana habari zake na kila mtu anamuona kama kituko.

Hatimaye baada ya miezi saba kupita, Manka anajifungua mtoto wa kike ‘njiti’ ambaye anawekwa kwenye chumba cha joto hospitalini ili amalizie sehemu ya ukuaji wake kwani alizaliwa kabla ya muda.

Upande wa pili, Martin anapata mafanikio makubwa na tayari amejiunga na Chuo Kikuu cha Muhimbili kusomea shahada ya utabibu. Kasi anayoingia nayo chuoni inamfanya kila mtu amzungumzie na kuwa kipenzi cha wahadhiri na wanafunzi wenzake, hususan wasichana ambao wanaonekana kuchanganywa naye kimapenzi.
Je, nini kitaendelea?
SONGA NAYO…

Manka alitaka kujaribu kuinuka lakini maumivu makali ya tumbo na sehemu ya chini ya kitovu yalimrudisha kitandani, manesi waliokuwa wamezunguka kitanda chake wakimpa huduma wakamueleza kuwa alikuwa amejifungua mtoto wa kike.

Naomba nimuone tafadhali,” aliongea Manka huku akiwa bado anatokwa na udenda mwingi mdomoni. Manesi wakamtazama kisha wakanong’onezana kitu kwa sauti ya chini ambayo mwenyewe hakusikia. Kitendo cha kutokwa na udenda mwingi mdomoni kiliwashangaza wengi.
“Whats wrong with her?” (Ana tatizo gani?)

“She is an addict from LDARE.” (Ni mraibu wa dawa za kulevya kutoka Kituo cha LDARE.)
“Can we show her baby? Im worry that she can harm it, addicted people do not think proper.” (Tunaweza kumuonesha mtoto wake? Nina mashaka anaweza kumdhuru, mateja huwa hawafikiri vizuri.)

“She can’t! We will be guiding her in each and everything,” (Hawezi, tutampa mwongozo wa kila kitu) aliongea mkunga mkuu wakati akijadiliana na wauguzi wenzake juu ya hali ya Manka.

Baada ya muda manesi wawili waliondoka na kuelekea kwenye chumba maalum ambacho watoto waliozaliwa kabla ya miezi tisa kukamilika huhifadhiwa. Dakika chache baadaye walirejea wakiwa wamembeba mtoto mchanga kwa umakini mkubwa.

“Mwanao huyu hapa,” aliongea yule nesi aliyekuwa amembeba mtoto, wakamsaidia kukaa kwa kuegamia kitanda kisha wakamuweka mtoto mikononi mwake.

“It is very cute, its name will be Theresia,” (Ni mzuri sana, jina lake ataitwa Theresia,” aliongea Manka huku uso wake uliokuwa umepoteza matumaini ukichanua kwa tabasamu pana.

Licha ya kuwa alikuwa kwenye maumivu makali, ujio wa mtoto yule ulimfariji kwa kiasi kikubwa. Aliendelea kumtazama mtoto usoni kwa makini huku akitabasamu. Alikuwa amefanana kwa kila kitu na Jon. Aliamua mwanaye aitwe Theresia kwa sababu ambazo alizijua mwenyewe.

Kadi ya mtoto ikaandikwa jina la Theresia Jon Curtis. Licha ya kuwa hakuwahi kumuona tena Jon tangu alipompeleka kwenye kituo cha mateja cha LDARE, Manka alikuwa na matumaini makubwa kuwa atarejea na akimkuta amejifungua mtoto mzuri, penzi lao litachanua upya. Madawa ya kulevya yalikuwa yameathiri ubongo wake kwa kiasi kikubwa hadi kushindwa kuukubali ukweli kuwa Jon alikuwa amemuacha kwenye mataa.

Baada ya kukaa naye kwa muda, manesi walimchukua mtoto na kumrejesha kwenye chumba maalum. Manka akabaki akitabasamu huku udenda ukizidi kumtoka kwa wingi mdomoni. Licha ya kuwa alikuwa akipewa tiba maalum ya kumfanya aondokane na matumizi ya dawa za kulevya, bado athari zake zilikuwa hazijaisha mwilini mwake.

Daktari wake aliyekuwa akimhudumia tangu mwanzo, Dk Reynold alipofika hospitalini pale kumjulia hali yake, alipewa taarifa na manesi kuwa mgonjwa wake alikuwa amepoteza damu nyingi wakati wa kujifungua hivyo alitakiwa kuongezewa nyingine lakini tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya lilifanya kazi iwe ngumu.

“She is running a severe shortage of blood, she bleeds excessively during labor,”
(Anakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa damu, alitokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua) aliongea mkunga mkuu wakati akiwasilisha ripoti ya maendeleo kwa Dk. Reynold.

“Worse enough, transfusion is impossible to her, she may run blood incompatibility due to drug use,” (mbaya zaidi zoezi la kumuongezea damu haliwezekani, anaweza kupata tatizo la damu kutochangamana kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.)
“What can we do then?” (Tutafanya nini sasa?)

“Let’s try to inject her with iron syrup to compensate the loss then she should undergo through special diet.”
(Tujaribu kumchoma sindano za madini chuma kufidia upungufu uliopo, kisha ataanzishiwa mlo maalum).

Baada ya mkunga mkuu na Dk Reynold kukubaliana, utekelezaji ulianza mara moja ambapo Manka alichomwa sindano za madini chuma kisha akaanzishiwa mlo maalum ambao sehemu kubwa ilikua ni mboga za majani na matunda.

Taratibu hali yake inaaza kuimarika, tatizo la upungufu wa damu likapatiwa ufumbuzi na mtoto wake akawa anaendelea kukua vizuri bila matatizo. Baada ya kukamilisha miezi tisa, mtoto wake alitolewa kwenye chumba maalum na kupelekwa wodini alikokuwa amelazwa Manka. Wakakaa pamoja kwa siku kadhaa kabla ya kuruhusiwa kurejea kwenye kituo cha mateja cha LDARE.

Sharti kubwa alilokuwa amepewa ni kutomnyonyesha mwanaye kwani kwa kufanya hivyo kungemaanisha kuingiza madawa ya kulevya kwenye mwili wa mtoto, jambo ambalo lilikuwa ni la hatari zaidi.

Kwa kipindi chote hicho, licha ya taarifa kutumwa mara kwa mara kwa Jon kuwa Manka amejifungua, bado hakwenda hata mara moja. Haja yake ilikuwa imetimia na hakuona sababu ya kuendelea kuwa na uhusiano naye wa aina yoyote.

Licha ya ufyele wa Manka, bado aliendelea kutumia tiba ya kumaliza tatizo la matumizi ya dawa za kulevya kwa kutumia unga maalum wa healing powder na kwa kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele, alionesha mabadiliko makubwa. Taratibu tatizo la kushindwa kuyazuia mate na kusinzia ovyo likaanza kupungua, hali ambayo ilileta matumaini makubwa kwa Dk. Reynold na wataalamu wengine waliokuwa wakimhudumia.
***
Martin ambaye sasa alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili (MUCHS) akisomea shahada ya utabibu, alizidi kukomalia masomo na hakutaka kitu chochote kimchanganye. Nyumbani nako alizidi kujitumana kuwa mtiifu kwa wazazi wake wa hiyari, wakili Akaro na mkewe ambao aliwaona kama watu muhimu waliochangia kwa kiasi kikubwa mafanikio yake

Baada ya kufanya vizuri katika mtihani wa kumaliza muhula (Semister) wa kwanza na jina lake kuanza kuwa maarufu miongoni mwa wahadhiri na wanachuo wenzake kutokana na alama za juu alizopata, Martin alianza kupata usumbufu kutoka kwa wasichana waliokua wakimtaka kimapenzi. Japokuwa haikuwa utamaduni wa wanawake wa Kitanzania kuwatamkia wanaume kuwa wanawapenda, Martin kila siku alikuwa akitamkiwa neno hilo.

“Kaka Martin naomba leo nikutoe lunch,” aliongea Munira Gramston au Munny kama alivyozoeleka chuoni pale, binti mrembo aliyekuwa na mchanganyiko mzuri wa mama Msambaa na baba Mhispania (chotara) aliyekuwa akisoma kitivo kimoja na Martin.
“Hamna shida Munny, ngoja nimalizie assignment tuliyopewa then tutakwenda,” alijibu Martin huku akiendelea kufanya shughuli zake. Munny alibaki kumtazama Martin huku akionesha wazi kuwa alikuwa na jambo alilotaka kumweleza.

Martin alishatambua kilichokuwa moyoni mwake, lakini kila alipokumbuka maumivu aliyosababishiwa na Manka, hakutaka kabisa kujihusisha na mapenzi. Baada ya kumaliza kazi zake, Martin na Munny waliongozana hadi kwenye canteen ya chuo ambapo waliagiza chakula na kuomba wafungiwe (takeaway).

Wakaenda kukaa kwenye moja kati ya bustani nzuri za maua zilizokuwa chuoni pale. Wakiwa wanakula, Munny aliamua kufunguka juu ya hisia alizokuwa nazo kwa Martin. Alimweleza kuwa ameshindwa kuvumilia na kuendelea kukaa na hisia moyoni.

“Ahsante kwa kunipenda, lakini nasikitika kukwambia sitakuwa tayari kwa hilo kwa sababu kilichonileta hapa ni masomo na si vinginevyo,” alijibu Martin kwa msisitizo huku akionesha kumaanisha kile alichokisema.

“Jamani Martin, hata mimi nimekuja kusoma na huwezi amini kuwa sijawahi kumpa mwanaume yeyote mwili wangu, ukinikubali wewe ndiyo utakuwa wa kwanza.” 
Licha ya maelezo yale aliyoyatoa Munny huku akimuangalia Martin kwa jicho la mahaba, hakukubaliana naye. Akashikilia msimamo wake, hali iliyomtoa machozi Munny.

“Ok, hata kama hunitaki basi naomba angalau unikiss tu roho yangu itulie,” aliongea Munny huku akijifuta machozi. Macho yao yakagongana, wakaangaliana kwa muda. Licha ya kujifanya ana msimamo mkali, uzuri wa Munny ulimfanya Martin afikirie mara mbili mbili.

Hakutaka kuchanganya mambo mawili kwa wakati mmoja lakini moto wa mapenzi ulionekana kutaka kuanza kumzidi.
“Kiss me please!” (nibusu tafadhali) aliongea Munny huku akisogeza uso wake kwa Martin.

Je, nini kitaendelea?  Fuatilia kwenye Gazeti la Risasi Jumatano.

Views: 1157

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by seamanmoo hussein on July 26, 2011 at 10:16pm
oya starehe hazishi babu na bibi wamezikuta na wameondoka wameziacha,tafuta elimu kwanza umsaidie mzazi wako na familia ya akina kyaro.starehe na masomo ni vitu viwili tofauti kama vile mbingu na ardhi.soma baba kaza buti nitakuajiri katika hospital yangu bro
Comment by Abdul Kilange on July 26, 2011 at 12:17pm
haya bwana martin zamu yako ya kutesa ndo hii, jidai bro!
Comment by JOSEPH G MALEKO on July 25, 2011 at 7:29pm
sawa sawa
Comment by Lightness Alex Kweka on July 25, 2011 at 11:53am
nimeamini sio kila cku maumivu bwana ona leo jamaa ana zali la kubusiwa hadi raha munirah kazana mama
Comment by Glady-Cathy on July 25, 2011 at 11:24am
mmmmmh
Comment by CHARLES HAMZA on July 25, 2011 at 1:43am
mambo yameiva,,,,,,,,,
Comment by Paul masonda on July 23, 2011 at 11:39pm
Mambo matamu hayo dah
Comment by Kadri Yahaya on July 23, 2011 at 8:46pm
Martin zali hilo

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

skysports24 posted a status
1 minute ago
zia12 posted a status
2 minutes ago
GLOBAL's blog post was featured
2 minutes ago
nazmulhasan posted a status
2 minutes ago
sona mona posted a status
2 minutes ago
Vortis posted a status
2 minutes ago
zia12 posted a status
2 minutes ago
zia12 posted a status
2 minutes ago
GLOBAL posted a blog post
2 minutes ago
Vortis posted a status
2 minutes ago
kemeya posted a status
2 minutes ago
Vortis posted a status
3 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }