Brighton Masalu na Imelda Mtema
SEXY girl, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunua kinywa juu ya skendo zake ambazo ni funga kazi kwa mwaka 2011, The Udaku Master, Ijumaa limembana kwa saa moja na kumpa aya kadhaa ili afunguke, shuka nazo.

KWANZA TUJIKUMBUSHE SKENDO FUNGA KAZI ZA LULU
Miongoni mwa skendo za Lulu zilizotikisa mwaka huu ni pamoja na ile ya usagaji, masuala ya utoaji mimba na kutoka kimapenzi na mapedeshee na waume za watu.

Nyingine ni matumizi ya kinga au kondomu wakati wa tendo la ndoa, kuwa mcharuko na kubwia ulabu kama hana akili nzuri hadi kuzimika kwa nyakati tofauti kwenye klabu za starehe za usiku na hadharani huku suala la kutembea au kukaa nusu utupu nalo likitajwa kumponza.

Katika mfululizo wa skendo hizo, pia Lulu aliwahi kudaiwa kuonesha utovu wa nidhamu kwa mzazi wake (mama) kwa kumtoroka na kwenda kujirusha bila kujali kuwa yeye ni kioo cha jamii na nyuma yake kuna rundo la wasichana wadogo wanaomuiga.

Akizungumza na mapaparazi wa Ijumaa ndani ya ofisi ya gazeti hili, Bamaga-Mwenge, Dar es Salaam, Jumatano wiki hii, Lulu ambaye ni muigizaji bei mbaya kwa sasa Bongo, alichambua skendo hizo moja baada ya nyingine hadi akatokwa na kijasho chembamba.

USAGAJI
Lulu mwenye miaka 18 aliwahi kudaiwa kuwekwa kinyumba na mwanamke mwenzake aliyetajwa kwa jina la Waukweli akihusishwa na masuala ya usagaji.

Kuhusu tabia hiyo mbaya isiyovumilika, alisema: “Nilifahamiana na Waukweli kwa sababu ya mdogo wake tuliyekuwa tunasoma wote. Nilishangaa kusikia naishi na msagaji eti kisa Waukweli ambaye alikuwa na skendo hiyo alikuwa karibu na mimi. Naomba jamii ijue ukweli kwamba sijawahi na sitajaribu uchafu huo.”

UTOAJI MIMBA OVYO
Kuna madai kuwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo, Lulu akiwa miongoni mwao, ni hodari wa kuchoropoa mimba ovyo.
 Kwa upande wa staa huyo alifafanua: “Mnapo-dili na mastaa wenye tabia hiyo, naomba jina langu lisitajwe hata siku moja kwa sababu sijawahi kubeba ujauzito na sina mpango huo kwa sasa kwani nahitaji kutengeneza maisha ili hata siku nikipata mtoto awe na maisha bora.”

KUTOKA KIMAPENZI NA MAPEDESHEE
Lulu aliwahi kukumbwa na skendo ya kuhongwa nyumba na mbunge mwenye kitambi kutoka mikoa ya Kusini mwa Tanzania (jina tunalo) na baadaye ilidaiwa kuwa ukarabati wa nyumba hiyo ulifanywa na pedeshee maarufu jijini Dar (naye jina tunalo).
Kuhusu hilo, msanii huyo hot alifunguka:

“Baada ya stori ile kujaa tele kwenye gazeti lenu la Ijumaa Wikienda, mheshimiwa (huku akimtaja jina) alinipigia simu na kuniuliza juu ya suala hilo. Nilishtuka sana kwani nafahamiana naye tu ila nyumba nilijenga mwenyewe. Nilimweleza ukweli na nikamwambia mimi sijui chochote.

“Jamani! Jamani! Naomba mashabiki wangu wanielewe, sijawahi ‘kutoka’ na pedeshee yeyote pamoja na kwamba wananitongoza kila kukicha, tena wengine ni watu ninaowaheshimu sana. Siwezi kufanya kitu ka’ hicho.”

VIPI LULU ANATUMIA KINGA KWENYE TENDO LA NDOA?
Kwenye makabrasha ya Ijumaa kuna listi ya mastaa wa kike waliowahi kukiri kutotumia kondomu wakati wa tendo la ndoa bila kujali gonjwa la Ukimwi na matokeo yake waliambulia mimba wasizotarajia, kuhusu hilo, Lulu alisema:
“Nawaonea huruma sana. Haiwezi kutokea kwangu, hakuna kitu ambacho huwa niko makini nacho kama hicho kwani najali afya yangu.”

LULU MCHARUKO
Staa huyo mwenye jina kubwa ndani na nje ya Bongo kupitia filamu na video za wasanii wa Bongo Fleva, aliwahi kutamba kuwa miongoni mwa mastaa wa kike nchini yeye ni mcharuko namba moja.

Katika hilo aliweka mambo sawa: “Kwa sasa nimebadilika sana, mimi siyo yule Lulu wa zamani. Kwanza nimekua na ndiyo maana sitaki kuitwa Lulu tena, natamani niitwe Lizzy ili kuonesha kuwa mimi siyo mcharuko tena.”

UCHAPOMBE
Mara kadhaa Lulu aliwahi kuripotiwa kulewa tilalila na kufanya mambo ya aibu (hayafai kufafanuliwa kwa watoto chini ya miaka 18), alipopewa nafasi na Ijumaa kufafanua juu ya hilo, alisema:
“Nilishawaomba Watanzania wanisamehe katika hilo na nazidi kuwaahidi kuwa hali hiyo haitajirudia kwani ule ulikuwa utoto tu.”

WAUME ZA WATU
Msanii huyo kinda aliwahi kukumbwa na skendo ya kupora mume wa mtu na adhabu yake ilikuwa ni kuchanwa viwembe usoni na mwanamke ‘mwenye mali’ hivyo kumharibu vibaya sehemu ya paji la uso wake.

Akifafanua juu ya skendo hiyo, Lulu alifunguka: “(huku akipapasa kovu la viwembe usoni) sina tabia hiyo. Kilichotokea ni kwamba yule mwanamke alihisi natembea na mumewe, lakini ukweli ni kwamba jamaa alikuwa ni rafiki yangu wa kawaida tu na hata mkewe huyo alikuwa anajua kwa hiyo si kweli kwamba mimi ni hodari wa waume za watu.”

KUTEMBEA/KUKAA UCHI
Kwa kumuona tu, huwezi kuuliza kama Lulu anapenda kutembea au kukaa uchi kutokana na mavazi yake. Vilevile aliwahi kuponyokwa na maneno kinywani mwake kuwa akivaa nguo ndefu huwa anawashwa.

Katika hilo, alisema: “Napenda sana miguu yangu kwani ni mizuri ndiyo maana huwa naiacha wazi. Si kweli kwamba napenda kukaa uchi. Kuna watu wangapi mitaani wanatembea utupu lakini hawaonekani? Najua ni kwa sababu mimi ni staa ndiyo maana ni rahisi kwa watu kusema.”

MPENZI WAKE NI NANI?
Lulu: “Kwa sasa sina mpenzi. Nilikuwa naye lakini tumeachana kwa kuwa nahitaji kuwa peke yangu.”

ANATAKA KUOLEWA NA MWANAUME GANI?
Alisema: “Mwanaume yeyote atakayenipenda kwa dhati, awe staa, asiwe staa, tajiri au maskini.”

NENO LA IJUMAA
Kwetu sisi Lulu ni miongoni mwa vijana watafutaji wanaopaswa kuigwa. Ameahidi kwa kinywa chake kuwa amebadilika hivyo ni matumaini yetu kuwa atatunza maneno aliyoyatamka ili kujiwekea hazina ya heshima mbele ya jamii.


SKENDO ZA LULU…

 

Brighton Masalu na Imelda Mtema

 

Sexy girl, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunua kinywa juu ya skendo zake ambazo ni funga kazi kwa mwaka 2011, The Udaku
Master, Ijumaa limembana kwa saa moja na kumpa aya kadhaa ili
afunguke, shuka nazo.

 

KWANZA TUJIKUMBUSHE SKENDO FUNGA KAZI ZA LULU

Miongoni mwa skendo za Lulu zilizotikisa mwaka huu ni pamoja na ile ya usagaji, masuala ya utoaji mimba na kutoka kimapenzi na mapedeshee na waume za watu.

Nyingine ni matumizi ya kinga au kondomu wakati wa tendo la ndoa, kuwa mcharuko na kubwia ulabu kama hana akili nzuri hadi kuzimika kwa nyakati tofauti kwenye klabu za starehe za usiku na
hadharani huku suala la kutembea au kukaa nusu utupu nalo likitajwa kumponza.

Katika mfululizo wa skendo hizo, pia Lulu aliwahi kudaiwa kuonesha utovu wa nidhamu kwa mzazi wake (mama) kwa kumtoroka na kwenda kujirusha bila kujali kuwa yeye ni kioo cha jamii na nyuma
yake kuna rundo la wasichana wadogo wanaomuiga.

Akizungumza na mapaparazi waIjumaa ndani ya ofisi ya gazeti hili, Bamaga-Mwenge, Dar es Salaam, Jumatano wiki hii, Lulu ambaye ni muigizaji bei mbaya kwa sasa Bongo,
alichambua skendo hizo moja baada ya nyingine hadi akatokwa na kijasho
chembamba.

 

USAGAJI

Lulu mwenye miaka 18 aliwahi kudaiwa kuwekwa kinyumba na mwanamke mwenzake aliyetajwa kwa jina la Waukweli akihusishwa na masuala ya usagaji.

Kuhusu tabia hiyo mbaya isiyovumilika, alisema: “Nilifahamiana na Waukweli kwa sababu ya mdogo wake tuliyekuwa tunasoma wote. Nilishangaa kusikia naishi na msagaji eti kisa Waukweli ambaye
alikuwa na skendo hiyo alikuwa karibu na mimi. Naomba jamii ijue ukweli kwamba
sijawahi na sitajaribu uchafu huo.”

 

UTOAJI MIMBA OVYO

Kuna madai kuwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo, Lulu akiwa miongoni mwao, ni hodari wa kuchoropoa mimba ovyo.

 Kwa upande wa staa huyo alifafanua: “Mnapo-dili na mastaa wenye tabia hiyo, naomba jina langu lisitajwe hata siku moja kwa sababu sijawahi kubeba ujauzito na sina mpango huo kwa sasa kwani
nahitaji kutengeneza maisha ili hata siku nikipata mtoto awe na maisha bora.”

 

KUTOKA KIMAPENZI NA MAPEDESHEE

Lulu aliwahi kukumbwa na skendo ya kuhongwa nyumba na mbunge mwenye kitambi kutoka mikoa ya Kusini mwa Tanzania (jina tunalo) na baadaye ilidaiwa kuwa ukarabati wa nyumba hiyo ulifanywa na
pedeshee maarufu jijini Dar (naye jina tunalo).

Kuhusu hilo, msanii huyo hot alifunguka:

“Baada ya stori ile kujaa tele kwenye gazeti lenu la Ijumaa Wikienda, mheshimiwa (huku akimtaja jina) alinipigia simu na kuniuliza juu ya suala hilo. Nilishtuka sana kwani
nafahamiana naye tu ila nyumba nilijenga mwenyewe. Nilimweleza ukweli na
nikamwambia mimi sijui chochote.

“Jamani! Jamani! Naomba mashabiki wangu wanielewe, sijawahi ‘kutoka’ na pedeshee yeyote pamoja na kwamba wananitongoza kila kukicha, tena wengine ni watu ninaowaheshimu sana. Siwezi kufanya kitu ka’
hicho.”

 

VIPI LULU ANATUMIA KINGA

KWENYE TENDO LA NDOA?

Kwenye makabrasha ya Ijumaa kuna listi ya mastaa wa kike waliowahi kukiri kutotumia kondomu wakati wa tendo la ndoa bila kujali gonjwa la Ukimwi na matokeo yake waliambulia mimba
wasizotarajia, kuhusu hilo, Lulu alisema:

“Nawaonea huruma sana. Haiwezi kutokea kwangu, hakuna kitu ambacho huwa niko makini nacho kama hicho kwani najali afya yangu.”

 

LULU MCHARUKO

Staa huyo mwenye jina kubwa ndani na nje ya Bongo kupitia filamu na video za wasanii wa Bongo Fleva, aliwahi kutamba kuwa miongoni mwa mastaa wa kike nchini yeye ni mcharuko namba moja.

Katika hilo aliweka mambo sawa: “Kwa sasa nimebadilika sana, mimi siyo yule Lulu wa zamani. Kwanza nimekua na ndiyo maana sitaki kuitwa Lulu tena, natamani niitwe Lizzy ili kuonesha kuwa mimi
siyo mcharuko tena.”

 

UCHAPOMBE

Mara kadhaa Lulu aliwahi kuripotiwa kulewa tilalila na kufanya mambo ya aibu (hayafai kufafanuliwa kwa watoto chini ya miaka 18), alipopewa nafasi na Ijumaa kufafanua juu ya hilo,
alisema:

“Nilishawaomba Watanzania wanisamehe katika hilo na nazidi kuwaahidi kuwa hali hiyo haitajirudia kwani ule ulikuwa utoto tu.”

 

WAUME ZA WATU

Msanii huyo kinda aliwahi kukumbwa na skendo ya kupora mume wa mtu na adhabu yake ilikuwa ni kuchanwa viwembe usoni na mwanamke ‘mwenye mali’ hivyo kumharibu vibaya sehemu ya paji la uso wake.

Akifafanua juu ya skendo hiyo, Lulu alifunguka: “(huku akipapasa kovu la viwembe usoni) sina tabia hiyo. Kilichotokea ni kwamba yule mwanamke alihisi natembea na mumewe, lakini ukweli
ni kwamba jamaa alikuwa ni rafiki yangu wa kawaida tu na hata mkewe huyo
alikuwa anajua kwa hiyo si kweli kwamba mimi ni hodari wa waume za watu.”

 

KUTEMBEA/KUKAA UCHI

Kwa kumuona tu, huwezi kuuliza kama Lulu anapenda kutembea au kukaa uchi kutokana na mavazi yake. Vilevile aliwahi kuponyokwa na maneno kinywani mwake kuwa akivaa nguo ndefu huwa anawashwa.

Katika hilo, alisema: “Napenda sana miguu yangu kwani ni mizuri ndiyo maana huwa naiacha wazi. Si kweli kwamba napenda kukaa uchi. Kuna watu wangapi mitaani wanatembea utupu lakini
hawaonekani? Najua ni kwa sababu mimi ni staa ndiyo maana ni rahisi kwa watu
kusema.”

 

MPENZI WAKE NI NANI?

Lulu: “Kwa sasa sina mpenzi. Nilikuwa naye lakini tumeachana kwa kuwa nahitaji kuwa peke yangu.”

 

ANATAKA KUOLEWA NA MWANAUME GANI?

Alisema: “Mwanaume yeyote atakayenipenda kwa dhati, awe staa, asiwe staa, tajiri au maskini.”

 

NENO LA IJUMAA

Kwetu sisi Lulu ni miongoni mwa vijana watafutaji wanaopaswa kuigwa. Ameahidi kwa kinywa chake kuwa amebadilika hivyo ni matumaini yetu kuwa atatunza maneno aliyoyatamka ili kujiwekea hazina ya
heshima mbele ya jamii.

 

 

MONALISA kugombea urais

 

Na Gladness Mallya

 

MWANADADA mwenye heshima katika kiwanda cha filamu Bongo, Yvone-Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ amechukua fomu ya kuwania nafasi
ya urais wa Shirikisho la filamu Tanzania (TAFF).

Katibu wa shirikisho hilo, Wilson Makubi aliliambia Ijumaa juzi kuwa, katika nafasi hiyo ya urais waliochukua fomu za kuwania ni wanne akiwemo aliyekuwa rais wa muda, Saimon
Mwakifwamba.

“Katika uchaguzi huu utakaofanyika Desemba 22, mwaka huu wamejitokeza wasanii wa kike wawili na wa kiume wawili kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo akiwemo Maria Salungi, Emmanuel Pemba,
Saimon Mwakifwamba na Monalisa,” alisema Makubi.

Akaongeza kuwa, uchaguzi huo utakuwa chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Bodi ya Filamu, Afisa Utamaduni Manispaa ya Kinondoni pamoja na wawakilishi kutoka taasisi zisizokuwa za
kiserikali.

 

Rehema Fabian apata pigo

Na Shakoor Jongo

 

Mshiriki wa Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian ‘Video Queen’ amepata pigo baada ya kufiwa na baba yake mzazi mzee Fabian Salao asubuhi ya Novemba 23, mwaka huu huko Dodoma alikokuwa amekwenda kikazi.

Akiongea na Ijumaa huku akionekana kuchanganyikiwa, Rehema alisema ameumia sana kumkosa mzazi wake huyo ambaye alikuwa akimtegemea kwa ushauri na mambo mengine.

Alisema awali alipata taarifa kuwa baba yake huyo anaumwa lakini hakupita muda mrefu akapigiwa tena simu na kuelezwa kuwa mzazi wake huyo amefariki dunia.

“Kwa kweli taarifa za kifo cha baba yangu zimenishtua na nimesikitika sana, hapa nilipo nimechanganyikiwa kwani nimepoteza mtu muhimu katika maisha yangu,” alisema Rehema.

Enzi za uhai wake mzee Fabian alikuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari Unga Limited iliyoko jijini Arusha.

Gazeti hili linampa pole Rehema na linamuombea kwa Mungu ampe nguvu katika kipindi hiki kigumu.

 

Harufu ya ndoa yambadilisha Mainda

 

Na Erick Evarist

 

SIKU chache baada ya kuvalishwa pete ya uchumba, muigizaji wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amebadilika na kuonekana kuwa na uchu wa kuitwa mke wa flani.

Chanzo chetu ambacho ni rafiki wa Mainda kilichoomba hifadhi ya jina lake kilisema, msanii huyo amekuwa hajichanganyi kama ilivyokuwa huko nyuma na kwamba mara nyingi amekuwa akipatikana
nyumbani kama siyo ‘lokesheni’.

“Mwenzangu anaonekana kuwa na uchu sana na hiyo ndoa, yaani sasa hivi si mtu wa kujichanganya viwanja kama ilivyokuwa nyuma, ni Mainda mwingine kabisa,” kilisema chanzo hicho.

Katika kuthibitisha hilo, juzikati msanii huyo akiwa ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar, alionekana akiwa ametulia huku wenzake wakichetuka ile mbaya.

Alipoulizwa aliishia kusema: “Sasa hivi mimi siyo yule uliyekuwa ukimjua zamani.”

 

Joyce anaswa akinunua ‘makufuli’

Richard Bukos

 

Huku tabia ya kutovaa makufuli ikishamiri kwa mastaa wengi, Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live kupitia Televisheni ya EATV, Joyce Kiria ameonekana tofauti
baada ya hivi karibuni kunaswa akichagua nguo hizo za ndani.

Joyce a.k.a Mrs Kilewo alinaswa akifanya ‘shopping’ hiyo hivi karibuni ndani ya duka moja lililopo kwenye Jengo la Biashara la Quality Centre jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika harakati za kuchagua ‘makufuli’ yanayomtosha ili asije akachagua ambayo ni ‘over size’, mwanadada huyo alikutana uso kwa uso na paparazi wetu ambaye alimpiga picha kabla ya
kufanya naye mazungumzo.

Katika maelezo yake Joyce alisema: “Si unajua tena Krismasi inakaribia kwa hiyo nafanya maandalizi.”

 

RECHO:

 

Piga, ua siwezi kuzaa

kabla ya kuolewa

Na Gladness Mallya

 

KUFUATIA baadhi ya mastaa wa Bongo kuanzisha tabia ya kuzaa kabla ya kuolewa, mwanadada anayeuza sura kwenye filamu Bongo, Rachel Haule ‘Recho’ amesema piga ua, yeye
hatazaa nje ya ndoa.

Akichezesha taya na paparazi wetu, Recho alisema ndoa ni jambo la heshima hivyo atapambana kuhakikisha anaolewa akiwa hajaenda kinyume cha utamaduni wa kabila lao.

 “Wazazi wangu walinizaa ndani ya ndoa na mimi nitafuata nyendo zao, siwezi kuzaa kabla ya ndoa… unajua kuna raha yake mtu ukizaa ukiwa ndani ya ndoa na jamii inakuheshimu tofauti na kuzaa kabla,”
alisema Recho.

Akaongeza kuwa, kwa sasa ana ‘sweet heart’ aliyemkabidhi moyo na anaamini atamvumilia kwa msimamo wake huo hadi watakapofikia hatua ya  kuwa mke na mume.

 

 

 

KABULA: Nami kalio n’nalo jamani!

 

Na Shakoor Jongo

 

MUIGIZAJI asiyekaukiwa na vituko, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ hivi karibuni amefunguka na kusema kuwa licha ya kuonekana ni mwembamba lakini anamshukuru Mungu kwa
kumjaalia kuwa na kalio.

Akizungumza na Ijumaa juzikati, Jini Kabula alisema kwa mwanamke sehemu hiyo ya mwili ni muhimu na ndiyo maana wapo wanaofikia hatua ya kutumia dawa za Kichina kuikuza.

“Sikatai mimi ni mwembamba lakini ukiniacha nikakutangulia, utadata mwenyewe na kijungu changu, kwa hilo namshukuru Mungu,” alisema Kabula.

 

Dokii:

 Nafurahi sana

mtu anaponiteta

 

LEOkatika safu hii tunaye msanii ambaye amekuwa akifanya vizuri kwenye tasnia ya muziki pamoja na filamu hapa Bongo kwa muda mrefu. Anaitwa Ummy Wenslaus lakini
kisanii anajulikana kwa jina la Dokii.

Naye juzikati alikutana uso kwa macho na TQ kisha akamwagiwa mvua ya maswali lakini kutokana na nafasi yetu kuwa finyu, leo utapata kujua mawili matatu kuhusu yeye kupitia majibu ya maswali 10
niliyomuuliza.

 

TQ: Katika maisha yako ni siku gani ambayo ulifurahi sana?

Dokii: Ni siku niliyopata fursa ya kuimba mbele ya Rais Jakaya Kikwete, alifurahia sana nyimbo zangu.

 

TQ: Umewahi kuchezea kichapo?

Dokii: Kila nikipigana huwa nashinda tu kwa hiyo sijawahi kupokea kipigo.

 

TQ:Unaweza kukumbuka ni filamu gani ya kwanza ambayo ulicheza?

Dokii: Naikumbuka, inaitwa Nakuhitaji.

 

TQ:Katika matumizi yako kwa siku unaweza kutumia kiasi gani cha fedha?

Dokii: Nina matumizi mengi sana hivyo kuna siku natumia hadi zaidi ya shilingi 150,000.

 

 

TQ:Nasikia wasanii mkiwa kambini huwa mnafanya vitendo vya ajabu, hii ikoje?

Dokii: Ni kweli wasanii wengi wawapo kambini hufanya mambo ya ajabu kama, kulewa chakari na kufanya ngono ovyo.

 

TQ:Ni nguo gani huwezi kukutwa ukiwa umezivaa mbele za watu?

Dokii: Huwezi kunikuta nimevaa pensi au kitop kifupi kwa kuwa maadili ya kazi zangu na dini pia hairuhusu.

 

TQ: Ni maeneo gani ambayo unapendelea kwenda kustarehe hasa ziku za wikiendi?

Dokii: Napenda sana sehemu za beach hasa zenye hoteli zilizotulia.

 

TQ: Ukiwa chumbani na mpenzi wako, ni vitu gani unapenda avifanye mwilini mwako?

Dokii: (Huku akikunja ndita) sipendi kuweka hadharani maisha yangu ya kimapenzi kwa sababu hayo ni mambo yangu binafsi.

 

TQ: Unajisikiaje pale mtu anapokuteta vibaya mbele za watu?

Dokii: Napenda mtu aniongelee mabaya kwa watu kwani katika kufanya hivyo, napata baraka zaidi kwa  Mwenyezi Mungu.

 

TQ: Ni filamu gani ambayo ilikupa wakati mgumu sana wakati wa kuiandaa?

 

Dokii: Filamu ya Scandle ilinipa wakati mgumu sana hadi ikafika wakati nikahisi nisingeikamilisha kwa wakati lakini nashukuru lengo lilitimia.

 

Views: 12961

Tags: ijumaa11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Dodoma Isaq Kifaluka on February 1, 2012 at 10:13am

    ,,nani kakudanganya kuwa una miguu mizur???!     ,look very,..,,!

Comment by Jimmy Sammy on December 6, 2011 at 12:03pm

Mbona umeanza kuzeek kabla ya wakati? Ukiolewa je?

Comment by kokwenda shumbusho on December 6, 2011 at 11:36am

hongera sana kwa uamuzi mzuri wa kubadilika lulu

Comment by Edwin Tesha on December 5, 2011 at 2:55pm

ok fine

Comment by Edwin Tesha on December 5, 2011 at 2:54pm

tanguliza maombi ddangu kubadilika c mchezo.

Comment by nancy george on December 5, 2011 at 1:37pm

yaani huyu mtoto natamani ningekuwa dada wa hiyari kwake niwe namchaapaaaaaaa coz anawehuka sana na ustaa alonao....... Cpendi tabia yake hata kidogo na huwezi ukajitangaza umebadirika twahitaji matendo toto tunduuuuuuu....

Comment by Ngassa Jr on December 4, 2011 at 11:57am

Hata mshtakiwa mahakamin analia hatorudia kosa... ukimwachilia tu... yale yale... haya yangu macho

Comment by Mamy Shaluathu on December 2, 2011 at 12:29pm

Mungu atamsaidia, kwani hakuna anaezaliwa na tabia za kishenzi.

Comment by Ponsian Samagwa on December 2, 2011 at 11:50am

tabia haina dawa ila mwisho wake atauona wakatiakiomba hata wakumsogezea kikombe cha maji ya kunywa hatomuona kwani KIVUMACHO................................................... dah mla huliwa.

Comment by yusuph marijani on December 2, 2011 at 10:32am

dah! lulu katt kadogo ila kanamambo? she is suppose to change.

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }