Na Musa Mateja
Inawezekana isimshtue Mtanzania kutokana na jinsi walivyozoeleka lakini ni sahihi kumuweka wazi kwamba tabaka la warembo mastaa ni kundi la pili kwa utoaji wa mimba, likitanguliwa na wanafunzi wa sekondari na vyuo.

Ijumaa Wikienda a.k.a The Biggest IQ Paper, linaandika kile kilichofanyiwa utafiti wa kina ambapo imebainika kuwa warembo wengi wenye majina makubwa nchini wamefuzu kwa kupata alama ‘A’ katika mpango mzima wa kunyonga vitoto vichanga tumboni.

Aisha Mohamed Mbegu ‘Madinda’
Katika utafiti wetu ambao ulifanywa kwenye vituo vya kutoa mimba, imeonekana kuwa licha ya tabaka la mastaa kuwa na memba wachache lakini namba ya ‘waumini’ wa mchezo wa kunyonga vichanga tumboni inatisha.
Hata hivyo, utafiti huo umebaini kuwa bado idadi yao haiwezi kufika hata nusu ya wanafunzi wa kike ambao kila siku iendayo kwa Mungu, wanahudhuria vituo mbalimbali vinavyotoa huduma hiyo haramu.

Ijumaa Wikienda limebaini kuwa tofauti na wanafunzi ambao huhudhuria vituo vyovyote, iwe uswahilini, uchochoroni kwa wataalamu wenye majina makubwa, mastaa wao hukimbilia kwa madaktari wanaowajua ili kutunza siri.

Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’
Aidha, imebainika kuwa mastaa wengine hupelekwa kuchoropoa mimba kwa kushikwa mkono na wenzao kwa mtindo wa: “Dokta fulani yeye ni fasta, hakawizi na hakuna atakayejua.”
Daktari mmoja (jina tunalo) alisema na gazeti hili kuwa warembo mastaa wengi wanajikuta wanatoa mimba kwa sababu ya kusumbuliwa na hofu ya kuchoka mapema na kuoneka ni wazee.

“Mimi sitoi mimba ila nimewahi kufuatwa na warembo wengi wakiamini natoa mimba, nilipowahoji wakaniambia hawataki kuzeeka pia wakanifichulia mengi,” alisema daktari huyo ambaye ana hospitali yake binafsi wilaya ya Kino, Dar.

Aliendelea kusema kuwa sababu nyingine inayowafanya warembo mastaa kutoa mimba ni mtindo wa kufanya ngono isiyo na matarajio ya kesho, huku wakitumia msemo wa “kumegana kisela”.
Alisema kuwa warembo wengi mastaa hufanya mapenzi yasiyo salama na wanaume ambao hawana makubaliano nao na ndiyo maana baada ya kupata mimba hukimbilia kuchoropoa.

“Unakuta mrembo anaamua kufanya mapenzi kama game, wala haoni kama kuna tatizo, huyo mwanaume ambaye anaingia naye kwenye tendo anakuwa hampendi toka moyoni, kwahiyo akipata mimba huwa anatoa.
“Hii kasi ya warembo kutoa mimba inaweza kupungua ikiwa wataamua kubadilika, wafanye mapenzi na wapenzi wao au wawe na utaratibu wa kutumia kinga,” alisema daktari huyo na kuongeza:

“Hata hivyo hao mastaa hawawezi kufikia idadi ya wanafunzi. Kwa sasa mastaa wanashika nafasi ya pili, halafu kundi la tatu ni wake za watu na wanawake wengine wanaofanya kazi maofisini ambao hawajapata wachumba rasmi.”
Kutokana na hayo, gazeti hili lilizungumza na baadhi ya warembo mastaa ili nao wazungumzie skendo hiyo ya utoaji mimba lakini hakuna hata mmoja aliyeonyesha ushirikiano huku wengine wakithubutu kutoa lugha chafu.

Mastaa waliohojiwa na gazeti ni Blandina Chagula ‘Johari’, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’, Jacqueline Wolper na Aisha Mohamed Mbegu ‘Madinda’.
Johari alisema kuwa hawezi kuzungumzia masuala binafsi, akaongeza: “Hivi wewe ukiulizwa swali kama hilo unaweza kujibu nini? Halafu hivi sasa nipo ‘bize’ na kazi zangu.
Aunt alisema: “Mbona nyie hamuwaandiki mademu zenu waliowahi kutoa mimba? Tena kwa ufupi sihitaji kusikia mambo hayo wala kuzungumzia, hayawahusu.”

Jacqueline alisema kuwa kwa upande wake yeye hahitaji kuzungumzia chochote na kusisitiza: “Sitaki magazeti, tafadhali sipendi.”
Aisha Madinda yeye alimjia juu paparazi wetu na kudai yanayohusu maisha yake ni yake mwenyewe: “Endelea na mambo yanayokuhusu wewe mwenyewe, mimi sipendi.”

Views: 316

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by bill p on May 10, 2010 at 8:07pm
Yaaani psycholigacalyy kwa response ya hao walioojiwa lazima wote wamewahi kutoa. Kutoa sio tatizo lakini kama dhamira zao zinawashtaki ndo maana wanakuwa wakali.
Comment by asmaa on May 10, 2010 at 1:53pm
MIMBA MTATOA UKIMWI JE?????...Isitoshe tusiwahukumu tuna ushahidi gani kuwa wanafanya ngono isiyo salama au wametoa mimba?....kabla hujatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio.....tupunguze unafiki na uzandiki teh teh nimenukuu.
Comment by issa m moshi on May 10, 2010 at 1:34pm
nyinyi wanafunzi pamoja na mastaa wetu chonde chonde jamani mnajifanya mmesahau kifo juweni kifo hakiwasahau kina wakumbuka kila dakika na siku zote mtu akihadaika sana na hii dunia basi mauti humshukia kama mwewe
Comment by kokusima on May 10, 2010 at 12:55pm
Ukimwi utawaumbua endeleeni na kamchezo kenu, kwani nidhahili hamtumii kinga. Mungu avirehemu vichanga hivyo amen.
Comment by lui handsome on May 10, 2010 at 11:15am
yeye atoaye huai ni yeye tu ndio anachukua na wala si mwingine......sasa wewe unaye ua vichanga tukuweke wapi? unatoa huai wewe?
Comment by Mackairre Rockeatouh on May 10, 2010 at 11:00am
Huyo Wolper sina hakika. lakine hao wengine mh...tutemee mate chini...shauri yenu ipo siku hizo mimba zitachomoka na roho zenu pia na nyie mnngefanyiwa hivyo na mama zenu leo mngekua mnakula bata kihasarahasara?
Comment by Mackairre Rockeatouh on May 10, 2010 at 10:57am
Tatizo la mastaa wetu virus vinawatafuna hivyo wanaogopa mimba zitawaumbua...virus na mimba noma ona majibu yao yalivyo mawenge
Comment by anisa a.salim on May 10, 2010 at 9:58am
Jamani kila siku mnaandika wasichana hivi,wasichana vile.Mbona wapo wanaume wenye kubadilisha wanawake kama nguo?tena wengine ni vioo vya jamii.hao hamuwasemi,au akifanya mwanaume ni sawa tu na kwa mwanamke ni malaya?ukienda kwenye web site ya harusi yangu,vilio vingi vya wanawake wanaotendwa na wanaume.Kama kusema mseme kote kote sio kwa upande mmoja tu.mkelenga upande mmoja na nyie mnatoa mfano tosha kuwa akifanya mwanamume ni sawa tu,kwa mwanamke si sawa.
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }