SAKATA LA PICHA CHAFU, JIPU PWAA!

Na Mwandishi Wetu
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (MJJW) imeamua kupasua jipu, imeeleza kwa kinaga ubaga kuhusu sakata la picha za utupu na kutoa muongozo wa nini kifanyike kuhakikisha utamaduni wa Mtanzania unadumishwa.

Wizara hiyo, pia imejivua lawama kuhusu sakata hilo, baada ya kupigwa na ‘madongo’ kwa muda mrefu, ikishutumiwa kulikalia kimya wakati kizazi kinazidi kuharibika.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano katika wizara hiyo, Erasto Ching’oro, aliiambia gazeti hili wiki iliyopita kuwa MJJW inatupiwa mzigo wa lawama kwenye ‘ishu’ ya picha za utupu kimakosa.
Alisema, wizara yake haina sheria madhubuti ambazo inaweza kuzitumia kushusha rungu kwa wahusika, badala yake wanachobaki kufanya wao ni kutunga sera na mkakati wa utekelezaji kwa kuwashirikisha wadau.
Ching’oro alisema kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani, inaweza kuhusika moja kwa moja kwa sababu kupiga, kujipiga au kupigwa picha chafu kwa hiari ni kosa la jinai na mhusika anapaswa kuchukuliwa hatua kali.

Alieleza kuwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, nayo ina nafasi yake kwenye sakata hili kwa sababu inatakiwa kufanya kazi ya kulinda utamaduni wa Mtanzania.
“Kupiga picha za utupu ni kosa la jinai, pia ni kinyume cha utamaduni wa Mtanzania, kwahiyo utaona ni kiasi gani wizara hizo zinahusika,” alisema Chong’oro.

Msemaji huyo wa MJJW, alisema hayo, baada ya gazeti ndugu na hili, Ijumaa Wikienda kuripoti habari yenye kichwa “Sakata la picha za utupu, Waziri wa JK abanwa” kwenye toleo lake la Jumatatu iliyopita.
Katika habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilikariri maoni ya wadau ambao wengi wao waliituhumu MJJW kwa kushindwa kuonesha meno yake, hivyo kuwaacha mabinti ambao wengi wao ni wanafunzi, wakipotea.

“Tutaonesha meno yapi ikiwa hakuna sheria inayotupa nguvu? Wizara ina sheria moja tu nayo ni ya mwaka jana ambayo ni Sheria ya Mtoto 2009. Hapa tutasema kwamba kuanzia sasa, makosa yote ya ukatili dhidi ya mtoto tutayashughulikia ipasavyo,” alisema Chng’oro na kuongeza: “Si vibaya Watanzania kutoa maoni yao kuhusu mambo yanayohusu nchi, suala la picha za utupu ni zito kijamii, kwahiyo ni vizuri ijulikane kwamba sisi hatubebi mzigo wote.”

Picha za utupu ni ishu ambayo inachukua nafasi pana katika habari za kijamii, huku wanafunzi wa Sekondari na Vyuo, wakionekana ni wahusika wakuu wa mchezo huo.
Mnenguaji ‘bei mbaya’ Bongo, Aisha Mohamed Mbegu ‘Madinda’, aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Nsia Swai na wengineo wengi ni kati ya waathirika wa zahama la sakata hili.

Views: 17872

Tags: mchanganyiko11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Nyasae Chieng on May 14, 2010 at 11:36pm
Wote mpigaji na pigwaji picha wanahitaji kumwona mtaalamu wa magonjwa ya akili
Comment by Nyasae Chieng on May 14, 2010 at 11:32pm
Nilitarajia vifungu vya sheria vitajwe kwa uwazi ili kujua kama kweli mtu anaweza kuadhibiwa kwa ama kupiga,kupigwa,kupigana au kupigiwa picha za utupu na kuzitumia/kuzisambaza. Hii porojo haina uzito wowote!
Comment by Papaa on May 13, 2010 at 2:41pm
Duuu, aibu kweli kwa Taifa!!
Comment by mcmillan andrew laiza on May 13, 2010 at 12:54pm
na hao wanawake hawana akili,kwa sababu mwanamke anaye jieshimu hawezi kufanya upumbavu kama huo.mtu wa kwaza kulaumiwa ni muhusika anaye kubali kupiga picha hizo.na kwa upeo wangu mdogo sidhani kama kuna mtu anaweza kumpiga picha za aibu kiasi hicho bila makubaliano.kina dada jiheshimuni acheni mambo ya haibu,
Comment by Journey on May 13, 2010 at 11:59am
WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU MKO WAPI HEBU TUPENI MUONGOZO KUHUSU HILI,JE SERIKARI INA MAMLAKA YA KUMZUIA MTU ASIPIGE PICHA ZA UTUPU?? NA IKIFANYA HIVYO HAIFUNJI HAKI ZA BINADAM?? NINGEFURAHI KAMA NINGEPETA UFAFANUZ KUHUSU HILI
Comment by Pape on May 12, 2010 at 6:48pm
Oh aibu!
Comment by seiph juma luvena on May 12, 2010 at 5:11pm
ni upumbavu na kujidhalilisha kwa kiwango cha juu kiasi kwamba huna akili, hujithamini na umekata tamaa na maisha hadi kufikia hatua hiyo kupiga picha za uchi!!!!!!!! NONSENSE
Comment by mojaone on May 12, 2010 at 4:25pm
Roho mbaya ya nini wacheni tufaidi kuona picha za utupu kutoka nyumbani badala ya kukalia za Ulaya tu.
Comment by biliamson on May 12, 2010 at 3:58pm
Wandugu mimi nafikiri hayo tunayoyaona hatutaweza kuyakwepa hasa ukizingatia hali ya maisha ni ngumu. Nchini kwetu hapa hasa Dsm kuna akina dada, ule mlo wa siku moja tu unampa shida , akina dada hao hao wamezalishwa na kutekekezwa na wanume zao, wengine mimba zisizotarajiwa na bado yupo kwa wazazi wake,wengine wanaletwa mjini kama mahouse girls lakini vishawishi vinawafanya waingie mitaani kwenye mabar, na kundi jingine ni lile la wasomi, wasichana walio maliza vyuo lakini kupata kazi ni issue, wengine walioko vyuoni wanashawishika na maisha ya anasa na yale wanayo yaona ktk mitandao. Je wandugu mnategemea hawa akina dada kama akipewa shs 10,000/= apigwe picha za utupu atakataa ? wakati hana njia nyingine ya kupata pesa na mtoto anahitaji maziwa na yeye anahitaji kula na kvaa na kujiremba. Haya hatutaweza kuyakwepa hasa ukizingatia ongezeko la watu mijini linazidi kukuwa na nchi yetu ni maskini.
Comment by sparksheha on May 12, 2010 at 3:46pm
hata nyinyi wenye magazeti mnalishabikia hili suala na sio kulipigavita ili muuze magazeti zaidi, kwani mmegundua vijana wengi wanazipenda habari za aina hiyo.
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }