SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA, LIYUMBA KITANZINI

Amatus Liyumba.

Morine Amatus.

Madawa ya kulevya waliyokutwa nayo akina Morine na wenzake.

Na Makongoro Oging’
LILE sakata la msichana Morine Amatus (22), anayetajwa kuwa ni mtoto wa Amatus Liyumba, aliyekamatwa na  Jeshi  la Polisi mkoani Lindi, akiwa na wenzake watatu, wakidaiwa kukutwa na madawa ya kulevya ya kilo 210 , yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.4 limeingia katika sura mpya baada ya baba yake (Morine) kutakiwa kukamatwa, hivyo kuingia kitanzini.
Habari za uchunguzi kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa Liyumba anaingia kitanzini kwa kuwa anatakiwa akamatwe na ahojiwe kuhusiana na madawa hayo kwa kuwa mtoto wake amedaiwa kuhusika na tayari katupwa gerezani akisubiri kesi yake kusikilizwa.
Chanzo chetu ndani ya jeshi la polisi kimesema kumekuwa na shinikizo kutoka serikalini kwa waziri mmoja (jina limehifadhiwa) kutaka Liyumba akamatwe na kutupwa rumande kwa kile kilichodaiwa kuwa, ili upelelezi uweze kufanyika kwa kina.
Alipoulizwa kwa njia ya simu na gazeti hili Jumapili iliyopita, Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa hakukiri wala kukataa kuhusu kukamatwa Liyumba ili uchunguzi ufanyike.
“Ninachoweza kusema ni kwamba uchunguzi juu ya tukio lile unaendelea. Kuhusu Liyumba ni kwamba mtoto wake ana miaka 22, hivyo ni mtu mzima kuna mambo anaweza kuyafanya bila baba yake kujua, lakini kama uchunguzi utatutaka baba yake akamatwe kuhojiwa, hatuwezi kushindwa kufanya hivyo,” alisema Kamanda Nzowa.
Alipododoswa zaidi, kamanda huyo alisema kwa kawaida polisi wanapofanya uchunguzi wao hawawezi kusema ni nani akamatwe na kuhojiwa na wala huwa hawasemi nani amewapa taarifa za mtu anayechunguzwa.
“Hizo ni kanuni zetu, hatuwezi kusema nani atakamatwa kwa jambo fulani au kumtaja mtu ambaye ametuletea taarifa za watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya na ndiyo maana tunafanya kazi vizuri sana, nawaomba wananchi wema wazidi kutupa ushirikiano,” alisema Nzowa.
Hata hivyo, Nzowa alifafanua kuwa kutokana na wingi wa madawa waliyokamatwa nayo, mtoto huyo wa Liyumba na wenzake, kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa itapelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Watuhumiwa wengine waliokamatwa pamoja na Morine katika Kijiji cha Mchinga Mbili, Lindi kwa mujibu wa Nzowa na kufikishwa mahakamani ni Pendo Mohamed Cheusi (67), mkazi na mkulima wa kijiji hicho na Hemedi Said (27), dereva na mkazi wa Mtoni, jijini Dar es Salaam ambaye pia ni mtoto wa mwenye nyumba hiyo.
Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni  Ismail Adamu, kwa jina lingine Athuman Mohamed Nyaubi (28), mfanyabiashara wa magari nchini Afrika Kusini na mkazi wa Morocco jijini Dar es Salaam.
Morine Amatus ni mkazi wa Mikocheni ‘B’ jijini Dar es Salaam na baba yake (Liyumba) alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)  na aliwahi kufungwa miaka miwili, Mei 24, 2010 kwa makosa ya kutumia vibaya ofisi ya umma.

NZOWA ATAHADHARISHA
“Niwatahadharishe wale wote wanaofanya au kufikiria kufanya biashara hii haramu ya dawa za kulevya, waache kwa sababu polisi kwa kushirikiana na raia wema tumejipanga. Maeneo yote siku hizi tunayalinda, watakaojiingiza ni lazima watakamatwa tu,” alionya.
Kamanda Nzowa amewashukuru  wote waliofanikisha kutoa taarifa ya kuwepo kwa madawa nchini na amewataka kuendelea kushirikiana na jeshi lake kwani alidai wote wanaokoa taifa na kuwa na watu mazezeta.

UCHUNGUZI WETU
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umegundua kuwa watuhumiwa hao wanahusishwa na askofu mmoja, Moris Charles ambaye inadaiwa amekimbilia nje ya nchi.
Tayari magari yake matatu yamedakwa na polisi wakati upelelezi ukiendelea huku kukiwa na taarifa kuwa familia yake ameitoroshea nje ya nchi.

Views: 4003

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Cosmasi Mitti on April 6, 2012 at 10:28pm

Mzee anaweza akawa ajahusika lakini mtoto mmmm siuna jua mitoto ya mjini ina jifanya inajua kilakitu

Comment by Mwafongo M on March 27, 2012 at 11:52am

siku ya kufa nyani miti yote huteleza,mtoto mdogo kama morine atapata wapi mtaji mkubwa kama huo na courage ya kufanya hayo bila baraka za mshua?hata hivyo ndio utafutaji unavyokuwa,asingekamatwa angewin,sasa amekamatwa akubali yaishe

Comment by Adam Raphael ndejembi on March 26, 2012 at 9:02pm

nawapongeza wafuatiliaji wa habari hizi na kwa moyo wao wa uzalendo.ni wakati muafaka kwa watanzania kupata habari zisizochakachuliwa.big up polisi wetu tz  ni wakati wenu muafaka kuwadhihirishia wananchi wenu kuwa mpo kazini.

Comment by Adam Raphael ndejembi on March 26, 2012 at 8:35pm

hongereni global publishers kwa uchunguzi wenu wa kina.kweli mnakwenda na wakati nina maana mnatambua wazi ni muda muafaka kwa watanzania kupata habari sahihi zisizochakachuliwa.

Comment by Beatus Nchemwa. on March 26, 2012 at 1:29pm

....Get Rich Or Die Tryn'......!

Comment by juma othman shaaban on March 24, 2012 at 3:45pm

Ama kweli mtoto wanyoka ni nyoka tuu, sheria ichukue mkondo wake. Hakuna liyumba wala baba yake 

liyumba sheri ni sheria tu.

Comment by Mamy Shaluathu on March 23, 2012 at 10:55am

Inawezekana Liumba ahusiki, kwani mtoto huyo ni kiukweli amefanya mambo makubwa tofauti na umri wake.  Madawa yameharibu nguvu kazi ya Taifa kubwa sana hapa inabidi sheria ichukue mkondo wake kwani watu hawa wamekamatwa na kidhibiti.

Comment by Mtanganyika Masalia on March 22, 2012 at 4:51pm

awe au asiwe mtoto wa liumba afikishwe mahakamani9 aeleze hayo madawa nani kaleta?

Comment by Devotha Meena on March 21, 2012 at 1:06am
Sheria isipindishwe tutashangaa kesho kesi inafutwa 7bu viongozi wa tanzania ndo wanacontrol mahakama
Comment by Mawazo Katota on March 20, 2012 at 11:42pm

Haya hawa ndio binadamu mabwingwa wa kutengeneza fitna

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ on Tuesday. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 22. 11 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 25. 29 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 22. 12 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 23. 36 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

Latest Activity

vanhelsing posted a status
9 seconds ago
vanhelsing posted a status
22 seconds ago
vanhelsing posted a status
33 seconds ago
vanhelsing posted a status
52 seconds ago
vanhelsing posted a status
1 minute ago
robinrubby posted a status
""
2 minutes ago
Profile IconGlobal Publishers via Facebook
Thumbnail

TAMASHA LA WAFALME KUWEKA HISTORIA SIKUKUU YA XMAS DAR LIVE

Facebook4 minutes ago · Reply
GLOBAL's 6 blog posts were featured
6 minutes ago
Profile IconGlobal Publishers via Facebook
Thumbnail

MICHEZO YA LEO NA KESHO KATIKA LIGI KUU YA ENGLAND

Facebook7 minutes ago · Reply
Nurislamtwo posted a status
8 minutes ago
Nurislamtwo posted a status
8 minutes ago
araf vai posted a status
10 minutes ago

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }