uhohehahe unasababisha wasanii kuukwepa muziki wa asili, adai pamoja na kutesa na albamu ya ‘Chambua Kama Karanga’ hakufanikiwa kununua hata baiskeli


Na George Kayala
KILA inapoitwa leo wasanii wa Bongo Flava wanaibuka kama uyoga uotavyo kipindi cha msimu wa mvua hasa kwenye mikoa yenye rutuba nzuri. Jiji la Dar es Salaam naweza kulifananisha na mikoa yenye ardhi nzuri ambayo nyakati za masika suala la kurudi na uyoga nyumbani ukienda msituni ni jambo la kawaida.

Kuibuka kwa wasanii hao kunatokana na baadhi yao kuona kuwa huko ndiko sehemu ya kuchomokea kimaisha. Utakuta kijana analala akiota anaimba na akiamka asubuhi anaanza kutafuta studio kwa ajili ya kuingiza ‘voko’.

Kutokana na haraka ya kutaka kutoka kimaisha kwa kutumia njia ya muziki ndiyo maana hujikuta wanarekodi nyimbo ambazo huwa na utamu kama wa ‘jojo’ ukianza kuitafuna lakini kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo inavyozidi kubadili ladha yake. Nyimbo za wasanii wa namna hii huvuma kwa miezi kadhaa ama nusu mwaka kisha hutoweka sokoni kimya kimya na kuwaacha wahusika wakiwa hawana nyuma wala mbele.

Msanii wa muziki wa asili ya Kihaya, Saida Karoli, hivi karibuni nilimtupia swali la kwa nini waimbaji hasa wa muziki wa Bongo Flava huvuma ghafla kisha kutoweka. Saida, bila hiyana alisema kuwa kinachofanya wasanii wengi na si wa muziki wa kizazi kipya pekee bali hata miondoko mingine nyimbo zao zichuje haraka, ni kutokana na kuwa na mtaji mdogo wa kurekodi vibao vyao.

Saida alisema kuwa, inawezekana msanii akawa na mashairi mazuri na yenye kueleweka katika jamii, lakini tatizo hutokea ukosekanaji wa vionjo katika miziki yao ambayo huwa haiwashawishi wasikilizaji.

Mwanadada huyo ambaye kwa sasa ameibuka na albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Wakati ndiyo huu’ aliongeza kuwa, wapenzi wa muziki wamegawanyika katika makundi matatu.

Kundi la kwanza ni watu wanaopenda kusikiliza ujumbe unaoimbwa, la pili ni la wale wanaopenda vionjo vya vyombo vya muziki na la tatu hupenda vyote. Hivyo, ili kuufanya wimbo wako udumu sokoni unatakiwa kila eneo ukamilike.

Saida aliyefanikiwa kujizolea umarufu mwaka 2002 kutokana na albamu yake ya ‘Chambua Kama Karanga’ alisema kuwa, mbali na kuwa na wimbo uliokamilika kila idara, wakati wa kuurekodi kwenye video kunahitajika ubunifu wa hali ya juu ili kila atakayeiangalia asichoke.

“Muziki ni ubunifu, unaweza kurekodi kibao chako safi kikawa na kila kionjo lakini wakati wa kutengeneza video yake unavurunda kutokana na kulipua wakati wa kufanya kazi hiyo. Unatakiwa kutulia na kutumia muda mwingi wa kuandaa kitu kilicho bora zaidi ili kisichuje sokoni,” alisema Saida.

Saida aliongeza kuwa, ili kudhihirisha anachokiongea ni cha kweli, mfano mzuri upo kwake kwani alilitambua hilo na kukubali kutumia muda mrefu kurekodi wimbo mmoja kwa gharama kubwa na ulipotoka kila mtu akaukubali.

Mwanamama huyo aliyeonekana kivutio kwa watu wengi hasa wakazi wa Dar kutokana muonekano wake ‘wa kishamba’, miaka ya 2002 alidai kuwa kinachofanya wasanii warekodi chini ya kiwango ni kutokana na uhohehahe walio nao.

Nilipomtaka aeleze kwa nini ameg’ang’ania muziki wa asili badala ya kugeukia miondoko mingine, Saida alisema kuwa, tangu utoto alikuwa anacheza ngoma za kabila lake (Kihaya) na alipopata wazo la kuzibadili ngoma hizo kwenda kwenye midundo ya kisasa, akaona faida yake na kwa sasa hana mpango wa kuacha asili yake.

“Muziki huu wa asili umefanikiwa kunitangaza kimataifa kwani naonyesha vitu vya asili ya Tanzania. ”Mbali na hilo tangu nikiwa mtoto nilikuwa nacheza sana ngoma za Kihaya na nilipofanikiwa kupata wazo la kuzipiga katika muziki wa kisasa, hakika nimeona faida yake na wala sitarajii kuacha,” alisema Saida. Aliongeza kuwa wasanii wengi wanakwepa kupiga muziki wa asili kutokana na uhohe hahe wao kwani muziki huo unahitaji gharama kwa kuingiza kila chombo kimoja baada ya kiingine.

Saida alihitimisha kwa kusema kuwa, pamoja na kutesa na albamu zake za ‘Chambua Kama Karanga’, na ‘Mpenzi Nakupenda’ ‘Neli’, hakufanikiwa kununua hata baiskeli bali aliambulia kupata umaarufu pekee na kipindi hicho alikuwa chini ya meneja wake, Felician Muta.

Aliongeza kuwa baada ya kuachana na Muta alimpata mfadhili mwingine aliyekwenda kwa jina la Madaraka Tivol mwenye maskani yake Mwanza ambaye anamiliki Tivol Studio na akiwa na jamaa huyo amefanikiwa kufyatua albamu mbili ambazo ni ‘Diana Akatanyukwile na ‘Wakati ni huu ‘Kalibatano’. Albamu hizo alidai zimefanikiwa kumpa angalau pesa ya kubadilisha mboga.

Views: 797

Tags: risasi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Carrie Hudson on October 3, 2010 at 1:10am
She was busy bleaching her skin and forgot to save money for the rain days and now here we go again always have to come with excuses after screwing up everything. Go to school and educate yourself you ignorant woman nobody want to hear your stupid excuses put yourself together and start from the scratch again. Who are you trying to fool here you cant fool anybody but yourself so dumb and what do you want us to do feel sorry for you?? or what I mean seriously get lost dummie!!!
Comment by Maiza on October 2, 2010 at 4:38pm
Pole, wenzio walikufanya mtaji, na kwa kuwa kuhujua mjini shule, ndo maana ukaambulia umaarufu. Da pole sana
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

War Tune posted a status
1 minute ago
livestream posted a status
2 minutes ago
livestream posted a status
2 minutes ago
livestream posted a status
2 minutes ago
livestream posted a status
2 minutes ago
livestream posted a status
3 minutes ago
livestream posted a status
3 minutes ago
livestream posted a status
4 minutes ago
livestream posted a status
4 minutes ago
livestream posted a status
4 minutes ago
livestream posted a status
4 minutes ago
livestream posted a status
4 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }