http://en.hummer-cars-club.com/graphics/classifieds/45/full/hummer-08er-h2-6-2l-t1-bremrhvn-1.jpg

Usafiri wa Mchungaji.

Usafiri wa Muumini.

Nyumba ya Mchungaji.

Nyumba ya Muumini.

Na Makongoro Oging' na Haruni Sanchawa
RIPOTI nzito inayohusu utajiri wa kutisha kwa baadhi ya viongozi wa dini  wakiwemo  wachungaji na maaskofu  na kuweka  utofauti mkubwa wa maisha baina ya waumini, umezua gumzo kubwa katika makanisa  mbalimbali  nchini.
Waumini wengi waliozungumza na gazeti hili  wamewashitukia baadhi ya viongozi hao  wa dini  kutokana na kile walichodai kuwa wamezidi kujilimbikizia mali huku wakiwahimiza (waumini) kutoa sadaka na michango mbalimbali ya mara kwa mara.
Kutokana na  hali hiyo,  baadhi ya waumini wamekuwa wakihama kutoka kanisa moja kwenda lingine huku wakiamini kuwa Mungu atawasaidia wabadilike kimaisha  au kumaliza matatizo yao.
Kutokana  na mgongano huo baina ya viongozi wa makanisa na waumini, baadhi ya wachungaji na maaskofu waliozungumza na gazeti hili walikuwa  na michango yao juu ya hali hiyo na walizungumza kama ifuatavyo:
Askofu Mokiwa
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Dk. Valentino  Mokiwa  akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hilo la viongozi wa dini kujitajirisha  alishauri kwamba  makanisa ya watu binafsi ambayo viongozi wao wamejipatia mali  nyingi  zenye utata wachunguzwe kwa karibu.
“Viongozi wa dini au muumini  kuwa tajiri  siyo jambo baya kwani hata sisi katika makanisa yetu ya Anglikana kuna maaskofu  matajiri na maskini na hakuna sheria  inayomkataza kiongozi wa dini kuwa tajiri  bali inategemea  jinsi alivyoupata, ambao haijulikani utajiri wao umetoka wapi, wachunguzwe,” alisema Askofu Mokiwa.
Aliongeza kuwa utajiri huo wa viongozi wa dini inabidi uwe ameupata kihalali, vinginevyo itakuwa ni dhambi kwa Mungu.
Alisema kwamba utajiri wa viongozi unaweza kutokana utafutaji kwa njia ya halali alitolea mfano wakati anasomea uchungaji nchini Marekani, kwamba   walikuwa wakifundishwa ujasiriamali wa kupata fedha kwa njia ya kilimo.
Mch. Mtikila
Naye Mchungaji Christopher Mtikila alisema kwamba viongozi wa dini kujitajirisha na kuwasahau waumini wao au kutumia fedha za waumini maskini  kujineemesha hao hawana wito wa Mungu.
Askofu Kakobe
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe alisema viongozi wa dini na hata wasio viongozi wanapaswa kujiwekea utajiri mbinguni na si duniani.
Askofu Kakobe ambaye amesifiwa na watu wengi kwa kuonesha kwenye televisheni nyumba na hata chumba chake cha kulala na kutajwa kuwa ni mfano, alisema kwake yeye anachokifanya ni kufundisha watu kuwekeza mbinguni.
“Siwezi kuacha kukemea watu wanaovaa vimini, wigi, kusuka nywele bandia, kuvuta sigara eti kwa sababu tutakosa sadaka,…kipaumbele ni Mungu,” alisema Askofu Kakobe.
Nabii Flora
Nabii Flora wa Kanisa la Maombezi lililoko Mbezi Beach kwa upande wake alisema  mtumishi wa Mungu aliye wa kweli hawezi kutajirika huku waumini wake wanalia na shida.
“Kanisa ni sehemu ya jamii ambayo inasaidia watu mbalimbali kupata Neno la Mungu pamoja na kusaidia shida za kijamii, si sehemu ya kiongozi kujitajirisha,” alisema.

Mch. Mtemela
Naye Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste jijini,  Alphonce Mtemela amesema kwamba katika Kitabu cha  Biblia Yohana 3.1 Mungu amesema utakuwa mbunifu kuwasaidia watu wako  unawaongoza ili wafurahie  wokovu wa Mungu.
“Kutokana na kifungu hicho ni wazi Mungu hataki mtu aishi  maisha ya majuto au masikitiko baada ya kumjua yeye.”
Akaongeza kwamba wokovu siyo mzigo ni furaha na kiongozi hapaswi kufurahi kuona watu anaowaongoza maisha yao yakiwa ni ya majuto wakati yeye anaishi  maisha mazuri.
Alisema watumishi wa Mungu waangalie jinsi ya kuwasaidia watu wenye shida na siyo waishie kubadili suti na kujitajirisha kila siku wakati waumini wanateseka  na kuishi maisha ya shida.
Mch. Rwakatare
Hata hivyo, Mchungaji Getruda Rwakatale kwa upande wake alipohojiwa hakupenda  kuchangia  lolote  kuhusiana na suala hilo.


Francis.

Mary.

Waumini wanasemaje
Uwazi liliongea na baadhi ya waumini wa madhehebu kadhaa kwa nyakati tofauti walisema mtumishi wa Mungu wa kweli ni yule anayejali maisha ya waumini wake  na siyo yule anayejilimbikizia mali  huku ‘kondoo’ wake wakitaabika.
Mmoja wa waumini hao alisema anapeleka sadaka kanisani ambayo inamzidi uwezo, kitu ambacho si sahihi hata kwa Mungu.
Furaha Josephat ambaye amewahi kuwa muumini wa Kanisa la Efatha na sasa anasali Kanisa la Romani Katoliki, Mwenge amesema kwamba wachungaji  wanakosea wanapokuwa  matajiri.
“Haiwasaidii, ni bora mali zikiwa nyingi  zitolewe kwa wasiojiweza pamoja na yatima kama sadaka,” alishauri Josephat.
 Aliongeza kwamba  viongozi wengi wa dini wanapenda kujilimbikizia mali  bila kutoa  msaada, akawashauri waangalie  maeneo mbalimbali ya kutoa msaada kama vile kujenga hospitali, shule na visima vya maji.
 Naye Mary Andemile ambaye alijitambulisha kuwa huwa anasali Kanisa la Gwajima alisema kuwa viongozi wa dini wanapaswa wawasaidie  watu wenye hali duni badala ya kujitajirisha.
Alitoa mfano kuwa Mchungaji  Gwajima  
ni kiongozi ambaye siyo tajiri lakini amekuwa akiwasaidia waumini  wake jinsi ya kujikwamua na maisha magumu.
Muumini mwingine, Francis Mbena  kwa upande wake aliwashauri viongozi wa dini wasiwafanye waumini wao kuwa  vyanzo vyao vya mapato ili wawe matajiri.
“Ni vema mtu akatoa sadaka kulingana na uwezo wake, wasitumie imani kuwalazimisha waumini kutoa michango mingi huku wakijua hali zao ni duni, huko ni kuwanyonya,” alisema.
 Daudi Antony kwa upande wake amesema kuwa ukweli ni kwamba kutokana na utajiri wa viongozi kuwa mkubwa, wakiwemo wanasiasa, taifa linaelekea kugawanyika.
“Makanisani, serikalini sasa hakuna huduma, baadhi ya wachungaji wamegeuza makanisa kama miradi yao vivyo hivyo kwa viongozi wa serikali, ofisi zao ni miradi ya kuchumia fedha au ni biashara,” alisema Anthony.
Naye Gerad Philipo amesema viongozi wengi wa dini wameshindwa kuwa na huruma kwa watu wanaowaongoza kwani huwakamua na hasa ile kanuni ya fungu la kumi, alidai inaumiza wale wasiokuwanacho.

Views: 5490

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Abass Hamad on March 5, 2012 at 9:45pm
mnahitaji pia uchunguzi na ikibidi maombezi km mnavyoombea wenzenu,
Comment by HAPPINESS MARCEL on February 25, 2012 at 4:51pm

Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhh Mungu ndo anajuwa wa kweli ni yupi na asiye wa kweli ni yupi

Comment by pjoan audes on February 24, 2012 at 4:47pm

Wajinga ndio waliwao kama unapeleka sadaka kwa ahadi ya kuwa tajili lakini mchungaji akatajirika yeye huoni kuwa uliyataka mwenyewe? wokovu u kwa bwana na wala si kwa wachungaji kwakuwa nao wanachumia matumbo yao.

Comment by Mtanganyika Masalia on February 23, 2012 at 10:55pm

carl marx once argued religion is an instrument of exploitation

Comment by adam safari yusuph on February 23, 2012 at 2:31pm

ifike wakati waumini tuwe tunahoji matumizi ya sadaka zetu tusifaidishe mafisadi wakati hali zetu ngumu.

 

Comment by adam safari yusuph on February 23, 2012 at 2:29pm

makanisa mengi yamekua ya kibiashara, matapeli wanafungua makanisa kwa lengo la kujipatia mali wanafiki tu.

Comment by Geofrey Andrew Sanga on February 22, 2012 at 8:20pm

Jamani tuwe wawazi utajiri sio dhambi kwani hata ktk biblia watu kama AYUBU,IBRAHIM,DAUDI NA SULEMANI Walikuwa matajiri tena utajiri wa kutisha fikiria ayubu alikuwa na farasi zaidi ya 50 @600000 ng'ombe zaidi 300@500000 je huo sio utajiri? tatizo liwe umepataje? huo utajiri huo na unautumiaje? tena hata wewe masikini jiulize hizo shilingi 2 na makochi yako hayo uliyapata wapi je hukumdanganya mtu yeyote.

Comment by ANDERSON SOGOLE on February 22, 2012 at 7:43pm
wa madhabahuni atakula vya madhabahuni
Comment by elizabeth edward manko on February 22, 2012 at 3:22pm

Hao wote wezi tu, hakuna mchungaji, hao wachungaji wa pesa za watu mifukoni wanaamishia kwao

Comment by moudy on February 22, 2012 at 1:27am

hii inasikitisha kwa kweli,kwa sababu mitume karibia wote hawakuwa matajiri,na walitangaza maneno ya mungu kidhati sasa hwa wamepata wapi kama ukiwa muhubiri lazima uwaibie waumini mali zao maana huo ni wizi kabisa,tuwe makini ndugu zangu na viongozi kama hawa hii ni hatari sana jamani

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

sohag posted a status
1 minute ago
mlon1988 posted a status
1 minute ago
mlon1988 posted a status
2 minutes ago
mlon1988 posted a status
2 minutes ago
mlon1988 posted a status
2 minutes ago
mlon1988 posted a status
2 minutes ago
mlon1988 posted a status
2 minutes ago
mlon1988 posted a status
2 minutes ago
mlon1988 posted a status
2 minutes ago
mlon1988 posted a status
3 minutes ago
mlon1988 posted a status
3 minutes ago
mlon1988 posted a status
3 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }