Steven Kanumba enzi za uhai wake.

Mwili wa Marehemu Steven Kanumba ukiwa mochwari.

Pichani juu ni waombolezaji wakiwa na simanzi kubwa iliyopelekea wengine kuzimia kwenye msiba wa Steven Kanumba.

Elizabeth Michael ‘Lulu' anayedaiwa kuwa na Kanumba kabla ya mauti kumfika.

Na Waandishi Wetu
NYOTA ya msanii maarufu wa sinema za Tanzania, Steven Charles Kusekwa Kanumba imezimika ghafla kufuatia kuanguka chumbani kwake na kufariki dunia katika tukio linalohusishwa na ugomvi baina yake na msanii mwenzake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na hii ndiyo ripoti kamili.
CHANZO
Tukio hilo la kusikitisha na lililoacha machozi nyuma yake, lilijiri usiku wa Aprili 7, mwaka huu maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza Kijiweni, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu aitwaye Sethi Bosco, staa huyo alikuwa chumbani kwake na Lulu, baadaye alisikia kelele za mzozo kutokea huko.
Akasema, kilichofuata baada ya mzozo huo, Lulu aliondoka ghafla, yeye akaenda chumbani na kumkuta Kanumba yuko chini, bila kujua kilichomsibu.
Kijana huyo ambaye alikiri kwamba Kanumba alikuwa amekunywa pombe usiku huo, aliendelea kusema:
“Nilipofika chumbani nilimkuta (Kanumba) amekaa chini huku ameegemea ukuta. Baada ya kumchunguza nikaona anatokwa na povu na damu kinywani.
“Niliampigia simu daktari wake na kumweleza hali hiyo, naye alifika haraka na kuanza kumfanyia uchunguzi.”

AKIMBIZWA MUHIMBILI
Sethi alisema daktari alipomchunguza alishauri akimbizwe Muhimbili. “Tulipofika alifanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa, alishafariki dunia muda mrefu,” alisema kwa uchungu kijana huyo.

MASTAA WAFURIKA MUHIMBILI
Habari zaidi zinasema kuwa, katika hali isiyotegemewa, mastaa mbalimbali, wakiwemo wa sinema, wacheza mpira na wanamuziki, walianza kumiminika katika hospitali hiyo ya taifa ili kujiridhisha na habari za kifo cha Kanumba.
Wengi wakiwa bado hawaamini, walipofika na kuhakikishiwa waliangua vilio, wengine kupoteza fahamu na kupewa huduma ya kwanza.

ASKARI WACHARUKA
Saa 10 alfajiri huku mastaa wakizidi kuwasili, askari wa Muhimbili walilazimika kuwaondoa waombolezaji hao kwa madai kuwa vilio vyao vilikuwa vikivuruga utaratibu mwingine wa hospitali hiyo.
Ndipo Mwenyekiti wa Bongo Movie Club, Jacob Steven ‘JB’ alipoanza kutumia nguvu ya ziada kuwataka wasanii hao kuondoka eneo hilo na kwenda nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya maombolezo na taratibu nyingine.
Hata hivyo, mpaka saa nne asubuhi bado kulikuwa na wasanii wengine wa filamu katika hospitali ya Muhimbili wakiwa hawaamini kifo cha mwenzao.

NYUMBANI KWA  KANUMBA
Watu walianza kumiminika nyumbani kwa Kanumba, vilio vilitawala huku wengine wakiwajulisha waliowaacha majumbani kuhusu kifo hicho, hali iliyosababisha eneo hilo kuonekana la simanzi.
Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda, Waziri  wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samuel Sitta, Katibu wa Itakadi na Uenezi wa NEC, CCM, Nape Nnauye, Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan, Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo, bosi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba walikuwa ni sehemu ya watu waliofika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kuomboleza.

ALIKUWA NA MIPANGO YA KWENDA MAREKANI
Kwa upande wake, mama mzazi wa marehemu akiongea tokea Bukoba alikokwenda, alisema mwanaye huyo alimpigia simu hivi karibuni na kumuomba arudi Dar ili waagane kwa vile alikuwa kwenye mipango ya kwenda Marekani.

KWA NINI LULU?
Msanii wa filamu, Lulu alidakwa na maafande wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar akidaiwa kuisadia polisi kufuatia kifo cha Kanumba.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema Lulu alikamatwa kwa sababu ni mshukiwa wa kwanza wa kifo hicho kwa vile alikuwa mtu wa mwisho kuwa na marehemu usiku wa tukio.

JE, NI KWELI WALIKUWA WAPENZI KITAMBO?
Madai yaliyotua juu ya meza ya gazeti hili yanasema kuwa, Lulu na Kanumba wamekuwa wapenzi kwa muda mrefu huku wakikutana kwa siri, hali iliyozua maswali kutoka kwa watu waliokuwepo msibani hapo.
“Jamani, kwani ni kweli Lulu alikuwa mpenzi wa Kanumba? Mbona haiwezekani? Kama  ni kweli basi walikuwa na siri kubwa,” alisikika akisema mwombolezaji mmoja.
Mama mwenye nyumba wa marehemu Kanumba (jina lake halikupatikana mara moja) alisema ameshamuona Lulu mara kadhaa akiwa na Kanumba nyumbani hapo.

KILICHOMUUA CHAJULIKANA
Kwa mujibu wa daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, kinachoonekana marehemu alijigonga kichwa mahali pagumu, akapata tatizo la kuvuja damu kwa ndani (internal bleeding).
Akasema kwa mtu anayepata tatizo hilo ni rahisi kufariki dunia au akipona anaweza kupatwa na ugonjwa wa kurukwa na akili.
“Kuna uwezekano mkubwa (Kanumba) angepona angeweza kuwa na tatizo la akili,” alisema daktari huyo.

MAISHA YAKE KUELEKEA KIFO
Majirani wa marehemu walisema kuwa, saa mbili usiku wa tukio, Kanumba alitoka nje akionekana mwenye hasira, baadhi ya watu wake wa karibu walimchukua na kumrudisha ndani.
Mpaka tunakwenda mitamboni, habari zinadai marehemu Kanumba anatarajiwa kuzikwa kesho jijini Dar es Salaam.
Mungu ailaze pema peponi, roho ya marehemu Steven Kanumba. Amina.

Imeandikwa na Imelda Mtema, Erick Evarist, Gladness Mallya, Issa Mnally, Richard Bukos, Shakoor Jongo na George Kayala.

Views: 12089

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Focus Kunambi on April 10, 2012 at 5:23pm

R.I.P KAMANDA

Comment by Dancan mkenya on April 10, 2012 at 1:12pm

kifo hutafuta sababu tofauti tofauti...siku ikifika haijalishi nilipi litakuondowa Duniani...ila tu pole kwa washukiwa na wahusika... na Mungu ailaze roho yake kanumba pema mahali...tuliobaki tuwaombee jamaa na ndugu zake waliobaki katika wakati huu mgumu, kwani sirahisi kuamini tukio hilo....maskini LULU pole sana kwa yaliyo kupata...inasikitisha sana unajuwa( R.I.P) Honarable STEVO i will remember you always.

Comment by Aminael FF on April 10, 2012 at 12:22pm

inauma na inasikitisha sana, sote safari yetu inaendeelea hapa duniani ketu ni mbinguni cha msingi tujiandae ili kifo kikifika uwe mikononi mwa YESU!!!!!!!!!!!

Comment by Real De' Dear on April 10, 2012 at 9:31am

duh! inasikitisha sana RIP Kanumba.

Comment by Mia andy on April 10, 2012 at 6:03am

RIP Kanumba.

Na nyie watu wa magazeti mnatuchanganya. mnatoa maelezo yanayopingana. mara mseme lulu alimwambia Seth kuwa brother ameanguka mara mseme lulu alitoweka then Seth akamkuta brother kadondoka. mara mseme Kanumba alimfuata lulu akikimbia na kumkamata na kumpeleka chumbani.mnachanganya.

Katika kipindi hiki kigumu kwa wafiwa na hata kwa lulu mnatakiwa muwe makini mnavyoandika habari zenu.

Comment by kaka kajuga on April 10, 2012 at 5:30am

Najua watu wana masikitiko kwas sasa baada ya kupoteza kijana ambaye alikuwa mdogo na maisha marefu mbele yake, lakini tusianze kumhukumu Lulu kabla ya kupelekwa mbele ya sheria. Sheria ya nchi lazima izingatiwe still Lulu is innocent until proven otherwise under the law, lulu hakuwa amepanga kumuua steven na inawezekana steven alianguka akimkimbiza Lulu kwa hiyo kwa sasa ngoja wote tusubiri uchunguzi ifanyike na facts zipatikane na baadaye tuache sheria ichukue mkondo wake

Comment by kysimkok Tall on April 10, 2012 at 1:12am

Duh kweli kifo hakina mwenyewe..Kanukmba ni kijana sana,ila tu yanisikitisha aina ya kifo kwani amekufa akiwa ameshautwika ulabu,halafu yaelekea alikua ametoka kupasha na dogodogo,wewe dada na wewe kaka nini tuna jifunza kwa hili,tujue vyovyote tunavyo ishi tujue ipo siku tutaondoka tena ghafla,wangapi waliugua muda mrefu waka teseka kitandani lkn hawakufa na ugojwa ule,na wangapi kama Kanumba wameondoka ghafla pasi na kuugua.tujireke bishe,tumrejee muumba,wakati wowote twaweza kuyeyuka.Poleni wafiwa kwa kuondokewa na muwapendao.

Comment by amos sute on April 9, 2012 at 10:29pm

LULU MDOGO WANGU  POLE NA POLE  SANA  SASA KILICHO BAKI KWAKO  NA KAMA  UTASOMA  UJUMBE HUU  KIMBILIA KWA YESU  NA UMPOKEE SASA HIVI HAPO ULIPO ,  YALIYO TOKEA  KWAKO YAMETOKEA [ LAKUVUNDA HALINA UBANI ] MTETEZI WAKO  SASA NI YESU TUUUUUU  HATA KAMA UTAHUKUMIWA KUNYONGWA  USIJALI  UNA NAFASI  YA KUTETEWA NA MUNGU  VILIVYO  KAMA UTAJIKABIDHI MIKONONI MWAKE  ZINGATIA HAYA  KULIKO YOTE.KANUMBA AMEKWENDA NA HESABU ZAKE KAMA  ZILIVYO  MBOVU AU NJEMA .LAKINI WEWE UNAYO  NAFASI TENA KUBWA KULIKO HATA SISI TUNAO SIKITIKA NA KULIA NA KUSEMA NA KULAUMU  NA KUJISAHAU KWAMBA SIKU YAJA  UPESI SANA  ZINGATIA MWANA NGU LULU UJUMBE HUU  NAWE UTAKUWA SALAMA  MUNGU ANAKUSUBILI UCHUKUE HATUA  YA KUFUATA YESU  NJOOO KWAKE HARAKA  ILIUPONE  NA YOTE

    AMINA AMINA 

Comment by haji shehe (ustadh on April 9, 2012 at 9:15pm

Ndio mwisho wetu binaadamu yaliyobakia tutakamatana tu kumbe wakati ukifika hakuna yeyote atakae weza kuzui HII NI KAZI YA MUUMBA MBINGU,ARDHI NA VILIVYOKUAMO AKISEMA KUA JAMBO LINAKUA (KUN-FAYAKUN) mola amfanyie wepesio safari yake hii ambao na ss inatukabili pia na ss atufanyie wepesi pindi itakapo wadia kwa upande wetu AMIN!

Comment by Ukweli100 on April 9, 2012 at 9:02pm

MANY THINGS INVOLVED HAPA

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

K Nagr posted a status
13 seconds ago
aslam uddin posted a status
1 minute ago
md Razib posted a status
1 minute ago
skysports24 posted a status
1 minute ago
skysports24 posted a status
2 minutes ago
mdsohel173 posted a status
2 minutes ago
mehrablokki lokki posted a status
2 minutes ago
skysports24 posted a status
2 minutes ago
mdsohel173 posted a status
3 minutes ago
dardedil posted a status
3 minutes ago
mdtyuiop posted a status
3 minutes ago
misu babu posted a status
4 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }