Raymond and Stephanie Raymond na Stephanie -43

Raymond wala hakuwahi kufikiria katika maisha yake kwamba ipo siku angekutana na machungu, aliamini jambo moja tu katika maisha yake, kwamba  maisha ni kusoma kwa bidii na kuikomboa familia yake, aliufahamu umasikini uliokuwa umewagubika.
Nyuma ya hatua zake, wazazi wake walimpa moyo na kumhimiza kuhusu elimu huku wakimsaidia kwa kila kitu pamoja na kwamba kipato chao kilikuwa kidogo,  walihakikisha anapata kila alichokihitaji ili asome.
Amefanikiwa kuingia kidato cha tatu baada ya kufaulu vizuri mtihani wa kidato cha pili, jambo hilo ndilo linalompelekea mkuu wa shule pamoja na walimu wengine wamwite ili wamfahamu zaidi kutokana na sifa aliyokuwa ameipelekea shule yao.
Ni hapo Raymond anapopatiwa barua na kuelezwa kwamba ahakikishe inawafikia wazazi wake ambao walitakiwa kufika shuleni hapo mara tu watakapoipata  barua hiyo. Anaipokea na kuipekekea barua hiyo kwa baba yake ambaye anaisoma na kuufurahia mwaliko huo.
Si Raymond wala wazazi wake waliofahamu kitakachojiri mbele ya safari, wote walifurahi kupata mwaliko huo. Siku inayofuata asubuhi, Raymond anadamka na kuelekea shuleni kama kawaida yake huku akiwahimiza wazazi wake kufika kama barua ilivyowaelekeza.
Akiwa shuleni anawasubiri wazazi wake kwa muda mrefu bila ya mafanikio, hatimaye wakati wa kuondoka shuleni unapowadia Raymond anakuwa na huzuni kutokana na kutowaona wazazi wake.
Anatembea taratibu akiongozana na wanafunzi wenzake kurejea nyumbani, kichwani mwake akiwa na swali moja tu ni kwa nini wazazi wake hawakufika shuleni siku hiyo.
Wakiwa barabarani wanakutana na kundi kubwa la watu huku damu nyingi zikiwa zimetapakaa barabarani, wanasogea ili kupata habari, ni hapo ndipo Raymond anapokiona kiatu cha baba yake, mtandio na kiatu  kingine cha mama yake, anapigwa na butwaa, anapojaribu kumweleza rafiki yake  kuhusiana na vitu hivyo anapigwa kwa kuambiwa kuwa amevifananisha tu lakini Raymond anakataa, anatoka mbio bila kusema chochote.
Anapofika dukani anakuta limefungwa, anaanguka chini na kuzimia.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

Hakika yalikuwa ni maumivu yasiyovumilika wala kuelezeka, kufiwa na wazazi wake wote wawili tena kwa mpigo, lilikuwa ni pigo kubwa kwake.
Alihisi tukio hilo ni kama ndoto lakini kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo ndoto hiyo Ilivyozidi kuyoyoma akilini mwake.
Kila macho yake yalipoziangalia vizuri maiti zilizokuwa ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, yalikataa kuamini kwamba tukio lile lilikuwa ni ndoto.
Ndugu zake, marafiki zake, watu pekee aliokuwa nao duniani walikuwa wamemwacha.
Hapo akaamini kwamba duniani alikuwa amebaki peke yake baada ya kuondokewe na ndugu pekee aliowafahamu, moyo wake ukajaa uchungu, akaiona dunia ni sawa na kitu kisichikuwa na maana tena, akatupa lawama kwa Mungu akimlaumu kwa kutoinusuru ajali hiyo.
Ni machungu hayo ndiyo yaliyopelekea Raymond kuzimia kwa mara nyingine tena huku mwili wake ukichuruzika jasho jingi.
Watu waliokuwepo karibu yake walimshuhudia akilegea na kuanguka chini kama mzigo,  wakajaribu kumwita ili aamke lakini ilikuwa ni kazi bure.
 Walijaribu kusikiliza mapigo yake ya moyo lakini hayakusikika, hofu kubwa ikawatawala.
“Hii ni hatari sasa.”
“Mimi mwenyewe naiona.”
“Sasa tunafanyaje?”
“Ni vizuri hali hii imetokea tukiwa tupo hospitali, madaktari watatusaidia.”
Haraka wakambeba Raymond juujuu na kumkimbiza mapokezi ambako waliomba msaada.
“Amepatwa na nini?”
“Amezimia.”
“Sababu?”
“Tulikuja hapa kuangalia maiti ambazo zililetwa mchana na kati hizo tumewakuta baba na mama yake wote wamefariki, hiyo ndiyo sababu.”
“Hizi zilizokuja hapa muda mfupi uliopita?”
“Mh!”
“Mungu wangu ni ajali mbaya sana ile hata majeruhi nao wapo katika hali mbaya, ni kuomba Mungu tu,” aliongea muuguzi waliyemkuta mapokezi. Hakika ajali hiyo ilikuwa imemshtua kila mtu.
Haraka wakampokea na kumuandikisha jina, kisha akapakiwa katika kiti maalum kilichosukumwa na kuingizwa kwa daktari ambako alipatiwa huduma zote muhimu.
Daktari aliwataka wamuache kwanza ili aweze kumwangalia hali yake kwa ukaribu. Raymond akapatiwa kitanda na kulazwa huku akiwa katika hali ya kutojitambua.
Baada ya kupatiwa huduma hiyo, mtihani ukawa kwa vijana wawili waliokuwa wamemsindikiza hospitalini hapo, hawakujua ni wapi wangeweza kupata msaada wowote wa kuwatambua ndugu wa Raymond, si hilo tu msiba ungefanyika wapi? Yalikuwa ni maswali ambayo hakika hayakuwa na majibu ndani ya vichwa vyao.
“Itabidi wewe ubaki hapa kumwangalia mimi nirudi dukani nikajaribu kuongea na watu ili tuone tutafanya nini.”
“Sawa.”
Kwa muda wa saa moja na nusu Raymond bado alikuwa amelala akiwa kimya kitandani bila hata kujitingisha hali iliyozidisha wasiwasi kwa daktari aliyekuwa  akimhudumia.
“Alitakiwa awe ameshazinduka muda mrefu,” aliongea akikisogelea kitanda huku akiwa amekodoa macho yake kumwangalia mgonjwa wake. Akasogea karibu zaidi na kujaribu kumshika bega ili kuona kama hisia zake zilikuwa tayari zimerejea.
“Raymond,” aliita daktari na ghafla akayashuhudia macho ya Raymond yakifunguka kwa tabu.
“Unajisikiaje?”
“Mh!”
“Hebu nieleze hali yako kwa sasa.”
Raymond hakujibu kitu alionekana kama mtu aliyekuwa akivuta kumbukumbu zake ili kufahamu ni kitu gani kilikuwa kimemtokea, akazungusha shingo yake huku na kule ndani ya wadi huku akijaribu kunyanyuka kitandani kwa tabu, akaketi.
“Niko wapi hapa?”
“Hospitali.”
“Hospitali?”
“Mh.”
“Kwani ninaumwa?”
“Umepatwa na mshtuko kidogo, lakini hivi sasa tunaona unaendelea vizuri.”
“Mshtuko wa nini?”
Badala ya kujibu daktari  akageuza shingo yake kumwangalia kijana aliyekuwa pembeni.
“Daktari nakuuliza mshtuko wa nini?”
“Mh! Unajua…ah, nimesha…lakini unaumwa kijana, naomba utulie,”  daktari alishikwa na kigugumizi kwa kuwa hakujua jibu la kumpa Raymond kwani kumweleza kwamba alikuwa amepoteza wazazi wake wote wawili ingezua tatizo kubwa zaidi.
Lakini ilikuwa ni lazima aelezwe ukweli ili kukubaliana na hali iliyokuwa imejitokeza, kabla hajafungua mdomo kumweleza, tayari Raymond alishakumbuka kila kitu,  picha ya tukio zima ilipita ndani ya ubongo wake kama sinema huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
“Baba, mama hatimaye mmekwenda, mmeniacha, ninaumia kwa kuwa sikuweza kutumiza ndoto yangu ili nanyi muonje matunda yangu, jambo moja tu ninaloweza kusema kwenu ni kwamba kamwe sita…” Raymond alishindwa kumalizia kauli yake, kwikwi za kilio zikamkaba.
“Raymond tafadhali jikaze.”
“Siwezi hakika inaniuma mno.”
“Lakini hayo ndiyo maisha yetu.”
Badala ya kujibu Raymond aliendelea kulia bila kunyamaza, machungu aliyokuwa nayo hakika yalikuwa hayaelezeki hata kidogo, kwake kila kitu kilikuwa kimeharibika, kuanzia elimu yake mpaka maisha yake hakujua mwelekeo.
Kibaya zaidi hakumfahamu ndugu hata mmoja kutoka upande wa mama  wala baba yake, aliowafahamu  walikuwa wameshalala usingizi wa milele.
“Baba wako wapi ndugu zangu?” lilikuwa ni swali kutoka kwa Raymond.
“Mama wako wapi ndugu zangu?” akauliza tena safari hii akinyanyuka kitandani.
Si daktari wala kijana aliyekuwa ndani ya wadi aliyeweza kumpatia Raymond jibu la maswali yote aliyouliza, wao pia mioyo yao iliwauma.
Kwa takribani nusu saa nzima walimwacha Raymond alie na kisha wakamuomba ajikaze ili waelekee nyumbani ambako wangepanga ni kitu gani cha kufanya.
“Nyumbani? Kufanya nini? Mimi sina ndugu, niliokuwa nao ndiyo hawapo tena, hivi ninyi mnanichekesha eeh?” aliongea huku machozi yakimbubujika mashavuni mwake.
“La hasha, sisi tupo kukusaidia, siye ndiyo tutakuwa ndugu zako, tafadhali jikaze tunaahidi ushirikiano mpaka mwisho.”
“Halafu kitafuata nini baada ya hapo?”
Hawakuwa na jibu, wao nao  wakashikwa na vigugumizi.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia siku ya Jumatano katika Gazeti la Risasi Mchanganyiko.

Views: 1631

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by FURAHA TAUSI on December 31, 2012 at 9:03am

huzuni kubwa

Comment by Saleh Gilla on December 29, 2012 at 7:23pm
inasikitisha mno...dah!!
Comment by HAPPINESS MARCEL MASSAWE on December 29, 2012 at 1:20pm

inaumiza sana jamani

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mayalilwa Mar 8. 26 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service