RAYMOND AND STEPHANIE (Raymond na Stephanie) - 31

Ni urafiki wa Stephanie na Martin uliosababishwa na kufanana kwa masweta yao walipokutana shuleni ndiyo uliozaa mambo yote haya.
Hatimaye, urafiki huo unawafikia wazazi wao, nao wanaufurahia na kuamua kukutana ili kufahamiana zaidi.
Uamuzi huo unakubaliwa, wazazi wanatafuta siku ambayo wataitumia kwa ajili ya kufahamiana kwa undani zaidi, ni hapo ndipo baba wa Martin anapotoa wazo la kukutana kwenye hoteli yenye hadhi kubwa iliyoko ndani ya Jiji la Chicago, Hilton Chicago.
Wote wanakubaliana na hilo huku kila upande ukiwa na hamu ya kuufahamu vyema upande mwingine.
Familia ya Martin inatoka Maywood kuelekea Oak Park, wanamchukua Stephanie na wazazi wake kuelekea Hilton Chicago. Njia nzima wote wanaonekana kutawaliwa na furaha.
Uzuri wa Jiji la Chicago unaonekana waziwazi, mataa ya jiji hilo yanalifanya kuonekana kuwa la kisasa na kuvutia zaidi.
Stephanie na Martin wanasimama na kutupa macho yao nje kuushangaa uzuri  wa jiji hilo.
Baada ya mwendo wa saa moja zima, wanawasili kwenye hoteli hiyo na kutafuta sehemu maalum ya kuegeshea gari lao.
Wanaelekea ndani ya hoteli hiyo huku Stephanie na Martin wametangulia mbele wakiwa wameshikana mikono.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

Walipoingia, mlangoni walipishana na walinzi walionekana kuvalia nguo rasmi za kazi zao, mbele kidogo wakapokelewa na mhudumu aliyekuwa maalum kwa ajili ya wageni.
Hewa na mandhari ya eneo hilo yalikuwa ya kuvutia zaidi, walizungusha macho yao na kuangalia huku na kule kuonekana kupendezwa na eneo hilo.
Mhudumu aliwaongoza moja kwa moja hadi ndani ambako walichagua moja ya meza ilizokuwepo pembezoni kabisa na bwawa la kuogelea na kuketi hapo.
Hapo ndipo walipochagua kwa ajili ya kula, kunywa na kufurahia maisha pamoja huku kila upande ukitaka kuufahamu upande mwingine kwa ufasaha zaidi.
Ndani ya hoteli hiyo walikuwepo watu wengi maarufu, nao pia walikuwa hapo kufurahia maisha.
“Duh!” baba yake Stephanie aliguna baada ya kumshuhudia mtu akiruka juu na kudumbukia ndani ya bwawa, hakika ilikuwa ni siku ambayo ingeweka kumbukumbu nyingine katika familia hizo, sababu kubwa ikiwa ni urafiki wa watoto wao Stephanie na Martin.
Hao ndiyo waliozikutanisha familia hizo mbili chanzo kikiwa ni kufanana kwa masweta yao.
Wahudumu waliovalia sare maalum walikuwa wakipita huku na kule ili kuhakikisha wateja wao wanapata huduma zote muhimu zilizokuwa ndani ya hoteli hiyo.
“Habari?” ilikuwa ni sauti nyororo ya msichana mrembo aliyesogea karibu kabisa na meza yao.
Alikuwa hapo kwa ajili ya kuwasikiliza walichohitaji kwani hiyo ndiyo ilikuwa desturi ndani ya hoteli hiyo.
Mkononimwake alionekana kushika kitu kama kitabu hivi, akanyoosha mkono wake na kukiweka juu ya meza.
“Ahsante,” sauti zilisikika zikijibu kwa pamoja huku walioesema hivyo wakimtaka mhudumu huyo kuwapa muda kidogo ili wafanye uamuzi.
“Hakuna shida, nitasimama pale pembeni kidogo,” alijibu akitembea kuondoka eneo hilo.
Kwa takribani dakika tano nzima familia zile ziliendelea kutafakari huku wakijiridhisha kwa kusoma vyema kitabu hicho.
“Leo ni siku ya kufurahi pamoja ndugu zangu, huku tukifahamiana vyema, hakika ningependa urafiki uliojengwa na watoto wetu tuukuze na kuuimarisha vilivyo.”
“Hivyo ndivyo itakavyokuwa.”
Mhudumu akaitwa na kusogea karibu, kila mtu akaonekana kuagiza kitu alichokitaka huku nyuso zao zikitawaliwa na furaha.
Dakika tatu tu baadaye meza ilikuwa imechafuka kwa vinywaji na vyakula mbalimbali, wote wakifurahia maisha na kuongea mambo mengi kuhusu maisha na malengo ya watoto wao.
“Stephanie? Martin?” ilikuwa ni sauti ya mama Martin akiwaita watoto hao ili nao wajumuike mezani.
“Ndiyo mama,” Martin aliitika.
“Ni vyema mkapata kwanza chakula halafu mtaendelea na michezo baadaye.”
“Ahaa! Sisi tutakula baadaye acha kwanza tucheze.”
“Hapana hebu njooni haraka sana.”
Watoto wale baada ya kusogea karibu, ndiyo kwanza wakazidi kutokomea mbali kabisa huku wakicheza na kufurahia pamoja.
“Michezo imewanogea sana leo, hebu waache wakisikia njaa watakuja kula.”
“Sawa kabisa.”
Hivyo ndivyo mambo yalivyoendelea ndani ya Hoteli ya Hilton, wazazi wa pande zote mbili wakila na kunywa huku wakifurahia kukutana kwao.
Dalili za kuujenga umoja wao zilikuwa zikionekana kuanzia siku hiyo waliyokutana.
Kwani walizungumza mambo mengi huku wakionekana kuwa na furaha, hali iliyozidisha upendo miongoni mwao.
“Nafasi hii niliitafuta siku nyingi sana, ni kutokana na sifa nyingi za Martin alipokuwa akimzungumzia Stephanie, alinipa hamu ya kutaka kumfahamu vyema mtoto huyo.
“Ahsante, sisi pia tulitamani iwe hivyo, kwani haikupita dakika bila Stephanie kulitaja jina la Martin.”
“Ndiyo maana leo tupo hapa kufurahi, nasi tunahitaji kuwa kitu kimoja kama ilivyo kwa watoto wetu.”
Hivyo ndivyo ilivyotokea, wazazi wa pande zote mbili nao wakawa kitu kimoja, kama ilivyokuwa kwa watoto wao.
Ni wakati wakiwa katika maongezi hayo, mara kadhaa Stephanie na Martin waliisogelea meza na kula kidogo kisha kutokomea kwenda pembezoni kabisa mwa hoteli.
Siku hiyo ndiyo pekee ambayo Stephanie na Martin waliitumia kucheza na kufurahi tofauti na ilivyokuwa kwa nyingine wanapokuwa  shuleni muda mwingi waliutumia katika masomo. Waliketi pembezoni kabisa mwa hoteli hiyo wakiwa wawili tu.
Hata wazazi wao walipowafuatilia kutaka kujua ni kitu walichokuwa wakifanya walipigwa na butwaa  kuwakuta wakiwa wamekaa pamoja wa muda mrefu.
Lakini hawakuhisi kitu kingine chochote, waliuchukulia uhusiano wa watoto wao kuwa ni wa kawaida.
Ingawa walikuwa watoto lakini mapenzi yao hayakufichika, yalionekana dhahiri na kudhihirisha kama walikuwa wakipendana kwa dhati.
***
Maisha ya familia ya David yalikuwa yakiendelea vizuri, mabadiliko makubwa yalishaonekana kuanzia mavazi, chakula mpaka malazi.
Raymond alikuwa akiendelea na shule na pale alipotoka shule  na kurejea nyumbani alimsaidia mama yake kazi zote zilizomhusu kisha kujisomea kidogo.
Siku za wikiendi mara nyingi alipenda kuongozana na baba yake kwenda dukani huko alikuwa akifunza kuhusu biashara pamoja na uchongaji wa vinyago.
Ndani ya moyo wake alionesha wazi kuipenda kazi hiyo.
“Baba siku moja nasi tutakuwa matajiri wakubwa,” hayo ndiyo yalikuwa maneno yake kila mara, Raymond alikuwa mdogo lakini aliifahamu vyema shida iliyokuwa katika familia yao.
Alitamani akikua ayabadili maisha yaliyokuwepo na kuwa bora zaidi.
“Ukisoma kwa bidii mwanangu yote yanawezekana.”
“Nakuhakikishia nitasoma ili siku moja nije kuikomboa familia yangu, najua hili linawezekana.”
Hivyo ndivyo David alivyoongea na mwanaye siku zote.
Alipenda kumtia moyo kwa kumtaka kusoma kwa bidii ili aje kuikomboa familia yao, alimhakikishia kuwa hilo litawezekana kama atajituma na kufanya bidii katika masomo yake.
Mpaka wakati huo Raymond alikuwa darasa la tatu, uwezo aliokuwa nao ulianza kuonekana, alikuwa akijitahidi katika masomo yake yote, jambo ambalo  liliwapa heshima wazazi wake.
“Huyu mtoto ana akili nyingi sana, sijui amerithi za nani? Tangu aanze shule amekuwa akishika namba moja, akiendelea hivi…” ilikuwa ni sauti ya mama yake Raymond usiku mmoja alipokuwa akiongea na mumewe.
“Mimi pia ninafurahi, tuzidi kumwombea, ila nisingependa ajue hili, kwani sifa zinaweza kumlewesha akajikuta akiboronga, endelea kumsisitiza kuhusu masomo, huku ukimwambia nini maana ya maisha, sawa mke wangu?”
“Hiyo ndiyo kazi yangu siku zote. Kwa uwezo wa Mungu nitahakikisha mtoto wetu anakuwa katika njia sahihi huku nikimsihi kuhusu elimu, nina uhakika atakuwa tunavyotaka.”
“Na iwe hivyo mke wangu,” aliongea David kwa sauti ya upole kama ilivyo kawaida yake siku zote.
Tabia hiyo ya upole wa kupindukia ilikuwa ni hulka ya David kipindi chote alichoishi na mkewe Catherine.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia Jumatano katika Gazeti la Risasi Mchanganyiko.

Views: 2219

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by FURAHA TAUSI on November 19, 2012 at 10:34am
inanichanganya kiasi
Comment by penina mwailunda on November 19, 2012 at 9:40am

Huyu mtunzi ana akili sana, nasubiria nione ataiunganisha vipi hii hadithi na maisha ya Stephinie hadi kilichompata akaolewa na David na kuishi kimasikini sana

Comment by kwangaya hamisi on November 19, 2012 at 12:00am

OK NZURII

Comment by Sylvester Francis on November 18, 2012 at 1:38pm

stehanieeeeeeeee????????????????

Comment by Fotidas rwazo on November 17, 2012 at 11:14am
Dah martin na huyo stephanie vp tena mbona........mh
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }