Raymond and Stephanie Raymond na Stephanie - 108

HAKUNA marefu yasiyo na ncha na wahenga walisema ukiona giza linazidi kuongezeka ujue mapambazuko yamekaribia. Msemo huu unadhihirika kwa Stephanie, msichana mrembo kutoka nchini Marekani ambaye anatokea kumpenda sana kijana wa Kitanzania, Raymond aliyekuwa akifanya biashara ya kuuza vinyago.

Kwa bahati mbaya, Raymond ambaye naye alitokea kumpenda Stephanie lakini akakosa ujasiri wa kumtamkia, anapata ajali mbaya huku Stephanie akishuhudia ambapo anajeruhiwa vibaya kichwani na kwenye uti wa mgongo.
Kwa kuwa alikuwa na mapenzi ya dhati kwa Raymond, Stephanie anajitolea kwa hali na mali kuhakikisha anayaokoa maisha ya kijana huyo. Kwa gharama zake anamsafirisha mpaka nchini Afrika Kusini ambapo anapatiwa matibabu ya nguvu mpaka anaporejewa na fahamu zake.

Baada ya kupata ahueni kubwa, wanaruhusiwa kurudi Tanzania ambapo mapenzi yao yanazidi kushamiri huku kila mmoja akijiwekea nadhiri ya kuishi na mwenzake kwa siku zote za maisha yao mpaka kifo kitakapowatenganisha.
Kwa mara ya kwanza, Stephanie anaenda na Raymond mpaka nyumbani kwake ambapo anamsaidia kufanya kazi zote za ndani kuanzia usafi mpaka mapishi. Penzi linazidi kushamiri na sasa wanafikiria jambo moja tu, ndoa.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

Baada ya kufika nyumbani kwake, Stephanie hakutaka kufanya kazi yoyote, akaenda chumbani kwake kubadilisha mashuka kisha akaenda kuoga na kurudi chumbani, akajitupa kitandani huku hisia tamu juu ya penzi la Raymond zikimsisimua mwili wote.
Hakupata usingizi mapema, bado aliendelea kumfikia Raymond huku kumbukumbu za yote waliyoyafanya pamoja zikizidi kujirudiarudia ndani ya kichwa chake kama filamu ya kusisimua.
“Hivi kumbe nampenda kiasi hiki? Yaani aliponikumbatia nilihisi kama nimepigwa na shoti ya umeme, nampenda sana Raymond jamani mpaka najishangaa, lazima niyabadilishe maisha yake,” alisema Stephanie huku akigalagala kitandani, akiwa ameukumbatia mto wake.
Aliendelea kumuwaza kijana huyo huku uso wake ukiwa umejawa na tabasamu pana mpaka usingizi ulipomchukua. Akiwa usingizini aliendelea kuota ndoto nyingi za mapenzi mpaka alipokuja kuzinduliwa asubuhi na mzee Chambo.
Akaamka na kwenda kumfungulia mlango kwani tangu aanze kushughulikia matatizo ya Raymond, alijikuta akiwa mbali na mzee huyo ambaye kimsingi ndiyo alikuwa mwenyeji wake jijini Dar es Salaam.
Kwa kuwa siku nyingi zilikuwa zimepita bila wawili hao kuonana, walikumbatiana kwa furaha huku mzee Chambo akimpa pole kwa matatizo yote na safari ndefu ya kwenda na kurudi Afrika Kusini. Stephanie alimshukuru sana na kumkaribisha ndani, wakakaa na kuanza kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu mgonjwa wake.
“Una roho ya huruma sana Stephanie, nilishangaa sana niliposikia umeamua kugharamia safari ya kumpeleka Raymond nchini Afrika Kusini, Mungu akubariki sana,” alisema mzee Chambo, Stephanie akaachia tabasamu pana.
“Nashukuru sana mzee, ilikuwa ni lazima nifanye hivyo kwa sababu nampenda sana Raymond.”
“Ni vizuri kupendana kwa sababu tuliagizwa upendo. Natamani binadamu wote wangekuwa kama wewe,” aliendelea kuongea mzee huyo huku akitumia mbinu zake za kiutu uzima kutaka kubaini kama wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kawaida au tayari walishazama kwenye dimbwi la mapenzi.
Stephanie hakuwa na kificho, alimueleza mzee huyo ambaye alizoea kumuita babu kwamba ukiachilia mbali upendo wa kawaida, hisia zake zilikuwa zimemuangukia Raymond tangu siku ya kwanza alipomuona na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya awe tayari kufanya chochote ilimradi aokoe maisha yake.
“Nilishaligundua hilo, tangu siku ya kwanza mlipokutana nilikuona ukiwa umebadilika na kuwa na hali ya tofauti ingawa hukutaka kuwa muwazi kwa hisia zilizokuwa ndani yako.
Pole sana kwa sababu mimi ni shahidi wa jinsi ulivyokuwa ukihangaika kufikisha ujumbe uliokuwa ndani ya moyo wako kwa Raymond,” alisema mzee Chambo, wakaendelea na mazungumzo yao.
Katika mazungumzo hayo, Stephanie alimueleza mzee huyo kwamba anafikiria kuhamia nyumbani kwa Raymond au kumshawishi kijana huyo ahamie kwake kwa sababu anapenda kuwa karibu naye muda wote.
“Unaonaje kila mmoja akiendelea kukaa kwake kwanza mpaka mtakapofunga ndoa ya halali na kuwa mume na mke?”
“Nahisi wanawake wengine wanaweza kunizidi ujanja, sitaki kumpoteza Raymond,” alisema Stephanie huku akionekana kumaanisha alichokuwa anakisema.
Hata hivyo, mzee Chambo aliendelea kumsisitiza kuwa vijana wengi wanafanya makosa kama hayo ya kuishi na watu wawapendao kabla ya kufunga ndoa, matokeo yake wanazoeana baada ya kukutana kimwili mara kwa mara na mwisho suala la ndoa linakuwa gumu kwao.
“Kama kweli unampenda, wataarifu wazazi wako na yeye akawataarifu wa kwake kisha mfanye taratibu za kufunga ndoa ili muishi kama mume na mke halali.
Kwa sasa unaweza kuwa unaenda kushinda naye lakini usihamie moja kwa moja nyumbani kwake,” alisema mzee huyo, maneno yaliyoonesha kumuingia Stephanie.
“Ila yeye amesema wazazi wake wote wawili walishatangulia mbele za haki,” alisema Stephanie kwa huzuni, mzee Chambo akamwambia hata yeye anaweza kumsimamia kama mzazi wake hivyo asiwe na shaka.
Stephanie alifurahi sana kusikia hivyo kwani zile ndoto zake za siku nyingi za kuishi na Raymond zilikuwa zinaelekea kutimia. Alimshukuru sana mzee huyo kwa ushauri mzuri aliompa, wakaagana na kukubaliana kuwa wakutane tena siku inayofuata kwa ajili ya kujulishana walipofikia.
Kwa kuwa Stephanie alikuwa amekaa siku nyingi bila kwenda kuripoti kazini kwake, alijiandaa asubuhi hiyohiyo na safari ya kuelekea kazini ikaanza. Baada ya muda, tayari alishamaliza kujiandaa, akatoka na kwenda moja kwa moja mpaka kazini kwake.
“Waooo Stephanie! Vipi mgonjwa wako anaendeleaje?” mfanyakazi wa mapokezi ambaye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumuona Stephanie alisema kwa sauti ya juu na kwenda kumkumbatia binti huyo wa Kizungu. Muda mfupi baadaye, Stephanie alikuwa amezungukwa na karibu wafanyakazi wote ambao walimpa pole kwa matatizo yaliyotokea na kumpongeza kwa moyo wa kipekee aliouonesha.
Kwa mara ya kwanza akagundua kuwa kumbe kuna watu wengi ambao walikuwa wakimpenda sana kutokana na mapokezi waliyompa. Aliwaeleza kila kitu kilivyokuwa mpaka matibabu ya Raymond yalipokamilika. Kila mtu alifurahi sana kusikia kuwa hatimaye kijana huyo alikuwa amerejea nchini akiwa mzima.
“Inabidi akuoe uwe shemeji yetu kwani umefanya kazi kubwa ya kuokoa maisha yake, tunasubiri kula pilau,” alisema mfanyakazi mmoja kwa masihara na kushangiliwa kwa nguvu na wenzake. Baada ya kuripoti kazini, Stephanie alipewa wiki moja ya mapumziko ili apate muda wa kuendelea kuwa jirani na mgonjwa wake, jambo ambalo lilimfurahisha sana.
Baada ya kumaliza taratibu za kiofisi, Stephanie aliondoka na kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Raymond huku akiwa na shauku kubwa ya kuonana naye. Alipofika, alifungua mlango na kuingia moja kwa moja ndani kama mwenyeji, akamkuta Raymond amekaa sebuleni akisoma kitabu.
Wakakumbatiana kwa furaha huku wakiangushiana mvua ya mabusu. Wakakokotana mpaka chumbani ambapo Stephanie ndiyo alikuwa wa kwanza kupanda, akamsaidia Raymond kisha wakagusanisha ndimi zao na kuanza kuelea kwenye ulimwengu tofauti uliojaa huba.

***
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu, maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana yanapita kama maua, wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unaendelea kupumua, ni vyema basi ukafikiria maisha baada ya kifo, kila siku ujiulize: “Hivi nikifa leo nitakwenda jehanamu au peponi?” kila mmoja wetu analo jibu lake.
Bila shaka sote tungependa kwenda peponi, kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu. Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia Jumamosi katika Gazeti la Risasi Jumamosi.

Views: 2889

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by LJH_3 on August 14, 2013 at 3:41pm
Raymond utaweza kula mate tu bila mambo. .mwenzako Martin yalikuwa ni majaribu kwake kila siku lkn aliyashinda mpaka anakufa...haya tuone hayo mabusu yataishia wapi..
Comment by Baltazary Theobald Zary on August 14, 2013 at 12:35pm
Sigongo unaweza... that is so good story
Comment by neema erasto on August 14, 2013 at 12:21pm

lovely

Comment by DORAH FREDY on August 14, 2013 at 11:01am

Woooh mpaka mimi mwenyewe nimefurahi sana

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }