Queen of the Gorillas (Malkia wa Masokwe) - 89

JITIHADA za dhati alizozionesha Harrison katika kupigania penzi la malkia wa masokwe, zimeanza kuzaa matunda baada ya kufanikiwa kutoroka na msichana huyo kutoka kwenye msitu mkubwa wa Tongass, uliokuwa kwenye mpaka wa Marekani na Canada.
Anatembea naye kwa siku kadhaa porini mpaka wanapokuja kutokezea upande wa pili wa msitu huo, kwenye mji mdogo wa wafugaji wa Petersburg nchini Canada. Wakiwa kwenye mji huo, Harrison anajaribu kuulizia mahali penye benki, kijana mmoja mdogo anamuelekeza kuwa inabidi asafiri kwa treni mpaka mji wa pili uitwao Abbotsford.
Harrison akiwa amemshika mkono malkia wa masokwe aliyekuwa na mwonekano uliomshangaza kila mtu aliyemuona, anafanikiwa kwenda mpaka stesheni ya treni na kwa bahati nzuri, ananunua tiketi mbili kwa kutumia kadi yake ya benki, muda mfupi baadaye safari ya kuelekea Abbotsford inaanza.
Baada ya kusafiri kwa saa kadhaa, wanawasili kwenye mji huo uliopo nchini Canada ambapo Harrison anakwenda moja kwa moja benki, kwa bahati nzuri, baada ya kuingiza kadi yake kwenye mashine ya ATM, anagundua kuwa bado fedha zake zote zilikuwa salama kwenye akaunti yake.
Akatoa kiasi ambacho kilitosha kununulia mavazi mapya, kupanga chumba kwenye hoteli, kula na nyingine ya akiba kwa ajili ya matumizi madogomadogo. Harrison na malkia wa masokwe wakayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu.
Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida, anaanza kufuatilia kwa kina kutaka kuujua ukweli. Anawaomba wazazi wake apelekwe upya shuleni kusomea masomo ya upelelezi na ujasusi.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

BAADA ya kutoa fedha benki na kununua mavazi mapya, Harrison alienda kupangisha chumba na kulipia kwa muda wa wiki nzima. Akaongozana na malkia wa masokwe mpaka ndani ya chumba chao, ndani ya hoteli ya kifahari ya Glaciers Peak Motel.
“Nakupenda sana mpenzi wangu, sitaki kukupoteza, nitafanya chochote ilimradi niishi na wewe,” alisema Harrison lakini malkia wa masokwe hakuwa anaelewa chochote. Alikuwa ametulia kimya kwenye kiti, akiendelea kushangaa kila kitu alichokiona ndani ya chumba kile.
Kutokana na jinsi mwili wake ulivyokuwa mchafu, Harrison aliamua kuanza kwa kumsafisha, akamshika mkono na kumpeleka bafuni, akamvua nguo na kumkalisha chini, akafungulia bomba la maji, akaanza kumsugua sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimpaka sabuni iliyokuwa inanukia vizuri.
Kazi haikuwa nyepesi lakini alijitahidi kutumia nguvu zake zote. Alipomaliza kumsafisha mwili mzima, alianza kumsugua meno ambayo yalikuwa yamebadilika rangi kutokana na kula mizizi na matunda ya porini kwa kipindi chote cha maisha yake. Pia kazi haikuwa nyepesi kwani malkia wa masokwe alikuwa akiutafuna mswaki na fizi zake zilikuwa zikitoa damu.
Alipomaliza, alimpunguza nywele ambazo zilikuwa zinamfanya aonekane kama mnyama wa porini. Akamsugua na miguu yake iliyokuwa imepasukapasuka kutokana na kutembea bila viatu kwa kipindi kirefu. Alipomaliza alimrudisha chumbani na kumlaza kitandani, akachukua mafuta mazuri yanayonukia, aliyoyanunua maalum kwa ajili ya malkia wa masokwe.
Akaanza kumpaka mwili mzima, mwanzoni malkia wa masokwe alikuwa akileta upinzani lakini baadaye akatulia, Harrison akaendelea kumpaka mwili mzima. Alipomaliza alimbadilisha nguo na kumvalisha nyingine ambazo nazo zilikuwa mpya. Wakapumzika kitandani.
***
Mzee Ford aliamua kumtimizia mwanaye alichokuwa anakitaka, akaenda kumuandikisha katika chuo cha upelelezi cha Scotland College of Crime Scene Investigation (SCCSI) kilichokuwa jijini London, Uingereza. Kila kitu kilikamilishwa haraka, Linda akapanda ndege na kuelekea jijini London.
Siku tatu baadaye, alianza masomo huku akijiapiza kufanya juhudi ili aelewe kwa kina namna ya kufanya uchunguzi kitaalamu. Siku zilizidi kusonga mbele, Linda akawa anaendelea na masomo huku akijitahidi kuyazoea mazingira mapya ya nchini Uingereza.
Kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, Linda alizidi kuwa mahiri kwenye masomo, hali iliyomfanya aanze kupata marafiki wengi. Hata hivyo, bado akili yake ilikuwa ikimuwaza Harrison, uchungu ukawa unazidi kumshika ndani ya moyo wake, akawa anajiapiza kuhakikisha anaujua ukweli juu ya kifo chake.
Miezi mitatu baadaye, Linda alirudi nyumbani kwao nchini Marekani baada ya chuo chao kufungwa. Akiwa nyumbani kwao, muda mwingi alikuwa akipenda kukaa peke yake huku akionekana kuwa na mawazo mengi.
 Mara kwa mara wazazi wake hasa baba yake alikuwa akimfariji na kumtaka akubaliane na hali halisi. Hata hivyo, haikusaidia kitu kwani mara nyingi alikuwa anashinda ndani akikataa kuonana na marafiki zake.
Baada ya likizo kuisha, Linda alirudi chuoni kuendelea na masomo, ikawa kila baada ya miezi mitatu kuisha anarudi nyumbani kwao na kupumzika kwa siku kadhaa kisha kurudi tena chuoni. Alifanya hivyo kwa sababu alikuwa hajazoea kukaa mbali na wazazi wake. Suala la nauli halikuwa tatizo kwao kwani baba yake alikuwa na uwezo mkubwa kiuchumi.
***    
Siku ya kwanza iliisha, Harrison na malkia wa masokwe wakiwa hotelini, huku msichana huyo akizidi kumzoea Harrison taratibu. Japokuwa hakuwa amevizoea vyakula vya kawaida malkia wa masokwe alilazimika kuanza kula mikate na vyakula vingine alivyofundishwa na Harrison. Mara mojamoja alikuwa akienda kumnunulia matunda kwenye ‘supermarket’ iliyokuwa jirani na hoteli ile.
“Inabidi nimtafutie mwalimu wa kumfundisha lugha, tutaendelea kukaa kama mabubu mpaka lini?” aliwaza Harrison huku akipitia kitabu cha namba za mawasiliano (yellow pages) kilichokuwa ndani ya chumba kile. Akapata jina la mwalimu anayeweza kumsaidia kufanya kazi ile.
Alimpigia simu na kuomba kukutana naye siku inayofuatia. Kesho yake asubuhi, mwanaume wa makamo aliyekuwa na kichwa chenye mvi nyingi, alifika kwenye Hoteli ya Glaciers Peak Motel na kuomba kuonana na Harrison.
“Naomba unisaidie kumfundisha mpenzi wangu kusoma, kuandika na kuzungumza kama watu wengine.”
“Kwani ana matatizo gani? Ana mtindio wa ubongo?”
“Hapana, ameishi sehemu ambayo haina watu, amekaa porini kwa muda mrefu.”
“Utanilipa shilingi ngapi?” alisema yule mzee huku akijaribu kuwasiliana na malkia wa masokwe kwa lugha ya ishara.”
 “Nitakupa kiasi chochote utakachohitaji,” alisema Harrison huku akimtazama mzee yule alivyokuwa anawasiliana na malkia wa masokwe. Baada ya kufikia makubaliano, Harrison aliongozana na yule mzee mpaka benki iliyokuwa jirani na hoteli ile, akatoa fedha kiasi benki na kumlipa kama malipo ya awali kwa ajili ya kazi ile.
Kesho yake asubuhi, mzee yule wa makamo ambaye baadaye alijitambulisha kwamba anaitwa mwalimu Gallagher, aliwasili akiwa na vifaa vyake vya kufundishia. Kwa kuwa ilikuwa vigumu kwa malkia wa masokwe kukaa peke yake na mtu ambaye hajamzoea, ilibidi Harrison akae naye, mwalimu akaanza kumfundisha kusoma na kuandika.
Mwanzo ilikuwa vigumu sana kwani hakuwa anaelewa chochote lakini baada ya kukaa muda mrefu, taratibu alianza kuelewa herufi kadhaa. Akawa anaweza kutamka kama mwalimu Gallagher alivyokuwa anatamka, hali iliyomfanya Harrison afurahi kuliko kawaida.
Baada ya kumfundisha kwa zaidi ya saa tano mfululizo, mwalimu Gallagher aliaga na kuondoka, akaahidi kurudi kwa ajili ya masomo ya jioni. Huku nyuma Harrison akawa anacheza na malkia wa masokwe huku akiendelea kumfundisha ustaarabu, ikiwa ni pamoja na namna ya kutumia choo anapobanwa na haja.
Jioni ilipofika, mwalimu Gallagher alirudi tena na Harrison akamchukua malkia wa masokwe na kukaa naye kwa utulivu, tayari kwa awamu ya pili ya masomo. Taratibu malkia wa masokwe akaanza kuingiza neno mojamoja kwenye kichwa chake.
***
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
Kila siku jiulize: “Hivi nikifa leo nitakwenda jehanam au peponi?” Kila mmoja wetu analo jibu lake, bila shaka sote tungependa kwenda peponi. Kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu.
Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.

Je, nini kitafuatia? Usikose kufuatilia Jumatatu kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda. 

Views: 4014

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Rashid on March 4, 2013 at 8:59pm

kweli jitihada huwa inahitjika unapotaka kitu

 

Comment by penina mwailunda on March 3, 2013 at 10:51am

Mimi wasi wasi wangu upo kwa Linda, sasa itakuja kuwaje akija kukutana na Harrison tiyari akiwa na malikia wa masokwe?

Comment by Majoy on March 3, 2013 at 2:24am

mapenzi hayo mwee!! hongera Harrison kwa ushindi

Comment by makumazani on March 2, 2013 at 5:17pm

malikia wa masokwa anaonekana atakuja kuwa na kipaji sana na kunapurukushani kubwa sana mbele ya safari

Comment by sarah rolick on March 2, 2013 at 11:47am

ahhaaaa!nzuri sana

Comment by Charity Chikoleka on March 2, 2013 at 1:56am

mwacheni jamani kipendacho roho

Comment by Isabella Bakana on March 1, 2013 at 8:10pm

nice story

Comment by fredy kullaya on March 1, 2013 at 7:16pm

Nimeanza kuifurahia hadithi,n nzuri sana.

Comment by Henry timothy on March 1, 2013 at 6:28pm

nzuri lakini fupi!!!!!!!!!

Comment by omar sebbo on March 1, 2013 at 3:00pm
una bd harson n dat is how a man should be.
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }