Queen of the Gorillas (Malkia wa Masokwe) - 71

LINDA, mtoto kutoka familia ya kitajiri, yupo juu ya ghorofa refu la Hospitali ya Oklahoma Medics na anataka kujirusha hadi chini ili afe baada ya kipenzi cha moyo wake, Harrison kumkana kanisani siku ya ndoa yao. Linda anatoa sharti moja kuwa mpaka Harrison atakapokubali kumuoa ndiyo atabatilisha uamuzi wake wa kujiua.
Upande wa pili, vyombo mbalimbali vya habari vinaripoti tukio la ajali mbaya iliyotokea kwenye Daraja la Miami. Mtu anayesadikiwa kuwa ni Harrison, anapata ajali mbaya akiwa anaendesha pikipiki na mwili wake unaokotwa ukielea baharini.
Habari hizo zinawashtua watu wote waliokuwa wanamfahamu Harrison, wanakimbilia eneo la tukio ambapo ushahidi wa pikipiki aliyokimbia nayo Harrison pamoja na mavazi ya harusi aliyokuwa ameyavaa, unafanya kila mmoja aamini kuwa Harrison amekufa.
Hakuna anayejua kuwa kila kitu kimetengenezwa na Harrison kwa  kushirikiana na rafiki yake Rogers, ambao wanatumia mbinu za hali ya juu kucheza na akili za watu. Akili ya Harrison ipo kwa msichana mrembo anayeishi na masokwe ndani ya msitu mkubwa wa Tongass. Ndoto zake ni kumuoa msichana huyo.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

“LINDA, Linda! Kuna habari tumezipata muda si mrefu kumhusu Harrison.”
“Sitaki habari zozote, namtaka Harrison aje hapa.”
“Tusikilize kwanza, ni muhimu ukajua kinachoendelea kwani tunaamini ulikuwa unampenda sana Harrison.”
“Bado nampenda, nimesema hapa siondoki mpaka aletwe,” alisema Linda na kuwakata kauli maafisa usalama wa hospitali ile ambao walikuwa wanataka kumfikishia habari za ajali aliyoipata Harrison.
“Jamani tufanyeje? Inaonekana hataki kuelewa chochote.”
“Mi nashauri runinga moja iletwe huku juu haraka iwezekanavyo kabla habari za ajali aliyopata Harrison hazijaisha,” alisema mmoja kati yao, utekelezaji ukafanyika mara moja.
Runinga ndogo ikaenda kuchukuliwa kutoka kwenye chumba kimoja cha ghorofa ile na kupandishwa mpaka kule juu kabisa alikokuwepo Linda na watu wengine. Waya mrefu ukatumika kuiunganisha kwenye umeme kisha ikawashwa na kuwekwa Kituo cha CNN.
“Tunaomba uangalie mwenyewe kinachotangazwa,” alisema mmoja kati ya wale maafisa huku akimgeuzia Linda runinga. Kwa muda wote huo, wazazi wake walikuwa wameshapata taarifa za kifo cha Harrison na walikuwa njiani kuelekea eneo la tukio kwenda kuthibitisha kama kweli walichokisikia ni sahihi.
Baada ya kugeuziwa runinga ile, Linda alishtuka kuliko kawaida kwa alichokuwa anakiona. Ilibidi mwenyewe asogee kutoka kule kwenye ukingo wa ghorofa mpaka jirani na ile runinga, akawa anatazama kilichokuwa kinatangazwa kama asiyeamini macho yake.
“Whaaat? Harrison amefanya nini? Noooooo!” alisema Linda kwa sauti kubwa huku akianza kuangua kilio kama mtoto mdogo. Maafisa usalama waliitumia nafasi hiyo kikamilifu, wakamzunguka pale alipokuwa amesimama ili asipate tena upenyo wa kukimbilia kwenye ukingo wa lile ghorofa.
“Noooooo! Harrison hajafa, hap…a…a…a…n,” Linda alishindwa kumalizia kauli yake, akadondoka chini na kupoteza fahamu kwa mara nyingine. Wale maafisa usalama na manesi wakambeba juujuu mpaka kwenye ngazi na kuanza kuteremka naye, wakaingia kwenye lifti na kushuka hadi chini ya jengo lile ambapo alianza kupewa huduma ya kwanza haraka.
***
“Jamani hivi ni kweli Harrison amekufa? Mbona mi siamini?”
“Yaani inasikitisha sana jamani kwani ndiyo kwanza alikuwa ameanza kupata mafanikio, roho inauma sana.”
“Au kuna mkono wa mtu? Mbona mi sielewi jinsi haya matukio yanavyotokea?”
“Mi mwenyewe nahisi kuna mkono wa mtu, haiwezekani bwana harusi amkimbie bibi harusi kanisani halafu akapate ajali mbaya na kufa, lazima kuna jambo hapa,” watu waliokuwa wamekusanyika wakitazama taarifa ya habari kwenye runinga, walikuwa wakijadiliana, kila mmoja akizungumza la kwake.
Baada ya mwili kuopolewa baharini, ulipelekwa mpaka kwenye Hospitali ya Miami ambapo ulifanyiwa vipimo kadhaa kisha kwenda kuhifadhiwa kwenye chumba cha maiti kusubiri ndugu wa marehemu wawasili.
Kila aliyeisikia habari ile alipatwa na uchungu usioelezeka kwani ndiyo kwanza nyota ya mafanikio ya Harrison ilikuwa imeanza kung’ara baada ya kuchapisha kitabu cha Malkia wa Masokwe, kilichouza mamilioni ya nakala nchini Marekani na nje ya nchi.
Ndugu wa Harrison wakiongozwa na mama mzazi wa kijana huyo, Skyler, babu yake, Dk Lewis na mkewe, waliwasili kwenye Hospitali ya Miami wakiwa hawaamini kilichotokea. Skyler ndiyo alikuwa katika hali mbaya zaidi kwani hakuwa na mtoto mwingine yeyote zaidi ya Harrison na hakutaka kuolewa baada ya kipenzi cha moyo wake, Harvey kufariki dunia.
“Nina mkosi gani mimi mama? Furaha pekee ya maisha yangu nayo imetoweka, nitaishi maisha gani mimiiii?” alilia Skyler kwa huzuni wakati wakiwasili kwenye Hospitali ya Miami.
“Jikaze mwanangu, yote kazi ya Mungu! Tulimpenda Harrison lakini Mungu kampenda zaidi, ukilia sana utakufuru,” mama Skyler alikuwa akimbembeleza mwanaye. Wakati wakiendelea kuomboleza, wazazi wa Linda nao waliwasili hospitalini pale, mama yake akawa analia kama mwendawazimu. Huzuni kuu ilitanda kila mahali.
Baada ya Linda kurejewa na fahamu, alipelekwa mpaka msibani, akawa anaendelea kuomboleza kwa uchungu kuliko watu wote waliofika msibani.
 Baada ya taratibu za kuchukua maiti kukamilika hospitalini pale, mwili ulichukuliwa mpaka nyumbani kwa Dk Lewis ambapo ndipo ndugu walipokubaliana msiba uwekwe. Kampuni ya Oklahoma Funerals iliyopewa kazi ya kusimamia msiba ule, ikapeleka gari la kubebea maiti pamoja na mengine ya kuwabeba ndugu na jamaa wa marehemu.
Maelfu ya watu walifurika nyumbani kwa Dk Lewis kwenye msiba ule wa kihistoria, idadi ya waliokuwa wanapoteza fahamu kutokana na kumlilia Harrison ikawa inaongezeka kwa kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo runinga na redio, vikawa vinatangaza moja kwa moja kila kilichokuwa kinaendelea msibani.
***   
Baada ya kushirikiana na rafiki yake, Rogers kutengeneza ajali feki ya kuonesha kwamba amekufa, Harrison alisafiri kwa siri hadi kwenye Msitu wa Tongass akiwa na lengo moja tu, kumpata malkia wa masokwe.
Tofauti na zamani ambapo kila alipokuwa anawasili Tongass alikuwa akienda kuomba kibali cha kuingia kwenye msitu huo mkubwa, safari hii Harrison aliingia bila kutoa taarifa sehemu yoyote. Mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa malkia wa masokwe yalimchanganya kiasi cha kutoiona hatari iliyokuwa mbele yake iwapo ataingia kichwakichwa ndani ya msitu huo.
“Samahani sana Linda, najua ulinipenda kwa moyo wako wote lakini ukweli ni kwamba yupo ninayempenda zaidi yako. Najua kumbukumbu za kitendo cha kukukimbia kanisani hazitafutika maishani mwako lakini ilibidi iwe hivyo, samahani kwa yote! Nampenda malkia wa masokwe kuliko wewe,” alijisemea Harisson kimoyomoyo wakati akikatiza kwenye vichaka kuingia ndani ya msitu wa Tongass.
Kumbukumbu za tukio la ajali waliyoitengeneza na rafiki yake, Rogers bado zilikuwa zikijirudiarudia ndani ya kichwa chake kama filamu ya kutisha. Alikuwa akijiuliza maswali mengi ambayo hakuyapatia majibu lakini kwa kuwa alishaamua kumtafuta malkia wa masokwe kwa nguvu zote, alipiga moyo konde.
Akiwa anaendelea kujipenyeza kwenye vichaka, Harrison alishtuka kupita kiasi baada ya kusikia matawi ya miti yakitingishika kwa nguvu huku sauti za ajabu zikisikika. Akiwa bado ameduwaa, alishtukia kitu kizito kikimuangukia mgongoni na kumuangusha chini.

Je, nini kitafuatia? Usikose Ijumaa kwenye Gazeti la Ijumaa.

Views: 2076

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by GETRUDE SEVERIN NJAU on January 1, 2013 at 7:35am

nzuriiiiiiiiii

Comment by francisca nyoni on December 31, 2012 at 12:16pm
utamu unakuja utamu unakata..........
Comment by DORAH FREDY on December 31, 2012 at 11:13am

mmmh Mungu wangu ndiyo mwisho wake nini jamani Erick fanya ndefu basi kdigo imekuwa fupi sana duh tunasubiri Ijumaa kwa hamu sana duh haya bwana

Comment by FURAHA TAUSI on December 31, 2012 at 9:06am

mmh masokwe lazima yakutafune

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mayalilwa Mar 8. 26 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

Latest Activity

tina babi left a comment for venans
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
1 minute ago
tina babi left a comment for VALLENTINO Rossi
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
1 minute ago
tina babi left a comment for Hitboy
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
1 minute ago
tina babi left a comment for Godlove W Nkya
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
1 minute ago
tina babi left a comment for Isack Mlungwe
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
1 minute ago
Noreen Kowalski posted a status
"Tupe mpya yako ya leo....."
1 minute ago
Leonida Nash posted a status
2 minutes ago
Leonida Nash posted a status
""
2 minutes ago
Leonida Nash posted a status
"Tupe mpya yako ya leo....."
3 minutes ago
Leonida Nash posted a status
"Tupe mpya yako ya leo....."
3 minutes ago
tina babi left a comment for NELSON J.KUNAMBI
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
3 minutes ago
tina babi left a comment for mongita kora
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
3 minutes ago

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service