Queen of the Gorillas (Malkia wa Masokwe) - 59

MAISHA ya familia ya Dk Lewis yanarudi kwenye mstari na anafanikiwa kuiunganisha upya familia yake kufuatia kupatikana kwa mtoto wake wa kipekee, Skyler ambaye alitoweka kipindi kirefu kilichopita. Skyler anakuja  na mtoto wa kiume, Harrison ambaye amefanana vitu vingi na marehemu baba yake.
Siku zinasonga mbele kwa kasi na Harrison anazidi kuwa mkubwa. Anamaliza elimu ya msingi na kuanza shule ya sekondari anakohitimu kidato cha nne. Baadaye anajiunga na chuo cha Michigan State University anakosomea masomo ya tabia za wanyama, Ethology. Anahitimu masomo yake na kuwa mtaalamu wa tabia za wanyama.
Baada ya kuhitimu masomo, anaenda kufanya utafiti kwenye msitu wa Tongass, lengo lake likiwa ni kujua mambo mbalimbali yahusuyo wanyama, hususan sokwe wengi wanaopatikana kwenye msitu huo mkubwa.
Je, nini kitafuatia?
SONGA NAYO...
ILIBIDI akajibanze kwenye mti mkubwa na kuangalia ni wanyama gani, macho yake yakatua kwenye kundi kubwa la sokwe wakubwa waliokuwa wanaruka kutoka tawi moja kwenda jingine kwa kasi kubwa, wakawa wanaelekea pale alipokuwa amejibanza.
Kelele zilizidi kuongezeka, utulivu uliokuwepo ndani ya msitu ule ukatoweka, Harrison akazidi kujibanza pale kwenye mti huku bastola yake iliyokuwa inatumia risasi za mpira ikiwa mkononi, tayari kwa kujihami endapo lolote lingetokea.
“Mungu wangu, mbona wakubwa hivi? Halafu mbona wengi kiasi hiki?” alijiuliza Harrison huku akiichukua kamera yake kwenye begi kwa mkono mmoja, akakaa vizuri na kuanza kupiga picha kwa mbali. Alipiga picha kadhaa, akawa anaendelea kushangaa jinsi sokwe wale walivyokuwa wakubwa na wengi.
Kundi lile la masokwe lilipotoweka, alishusha pumzi ndefu na kuweka vifaa vyake vizuri. Ilibidi arudi kwenye hema lake, akaenda kuweka kumbukumbu za alichokiona. Akawa anaandika baadhi ya mambo kwenye kijitabu chake cha kumbukumbu.
Siku zilizidi kuyoyoma Harrison akiwa bado ndani ya msitu wa Tongass, kila siku akawa anaendelea na kazi ya utafiti juu ya tabia za masokwe na viumbe wengine katika msitu ule, pamoja na kuchunguza uoto wa asili. Taratibu alianza kuwazoea masokwe wale wakubwa na wa kutisha.
Tofauti na wanyama wengine, sokwe wa msitu wa Tongass walikuwa wakitembea kwa makundi makubwamakubwa, huku moja likionekana kuwa kubwa zaidi. Kila alipobahatika kuwaona, walikuwa kwenye makundi, wakiruka juu ya matawi ya miti kwa namna ambayo ilimshangaza sana Harrison.
Baada ya kukaa kwa muda wa wiki mbili ndani ya msitu ule, Harrison aliamua kuondoka na kurejea nyumbani kwao kwenda kufanyia kazi taarifa mbalimbali za kiuchunguzi juu ya tabia za wanyama hususan masokwe wa Msitu wa Tongass alizozipata.
Alijiandaa kwa kufungasha vitu vyake vyote, akalikunjua hema na kulibana kwa namna ambayo ilikuwa rahisi kubebeka, alipohakikisha amechukua kila kitu, aliianza safari ya kuelekea kwenye ofisi za msitu ule kwa ajili ya kukabidhi baadhi ya vifaa alivyokuwa amepewa.
“Umefanikiwa?”
“Nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa na namshukuru Mungu sijapata madhara yoyote.”
“Unawaonaje masokwe wa Msitu wa Tongass?”
“Mh! Sijawahi kuona sokwe wakubwa kama hawa, halafu wanatembea kwa makundi makubwa sana, lazima nitarudi tena kwani nadhani ndani ya msitu huu nitajifunza vitu vingi ambavyo awali sikuwa navifahamu.
“Ngoja nikafanyie kazi hizi data nilizozipata,” alisema Harrison wakati akizungumza na askari wa wanyama pori aliyemkuta kwenye ofisi za msitu ule.
Baada ya makabidhiano, Harrison alitembea kwa miguu kwa kilometa chache kabla ya kuifikia barabara kuu. Akasimamisha gari na safari ya kurejea nyumbani kwao, Miami ikaanza.
”Ooh! Karibu baba, umekuwa mweusi kweli, inaonesha kuna baridi sana huko ulikotoka.”
“Ahsante sana, kuna baridi kali kwenye Msitu wa Tongass lakini namshukuru Mungu nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema Harrison wakati akipokelewa na bibi yake.
“Mama yupo wapi?”
“Ameenda kazini lakini muda si mrefu atarudi. Mh! Habari za huko?”
“Nzuri kabisa mama, nimeifurahia sana safari yangu kwenye Msitu wa Tongass, nimewaona sokwe wakubwa haooo! Yaani hata wewe nikikuonesha picha utashangaa,” alisema Harrison.
Baada ya kuingia ndani na kupumzika kwa muda, Harrison alienda kuoga na kubadilisha nguo, akachukua kamera zake mbili alizokuwa anazitumia kupigia picha na kwenda kuziunganisha kwenye kompyuta kwa lengo la kuzitoa zile picha na kuzihifadhi vizuri.
Alichomeka waya maalum kutoka kwenye kamera na kuunganisha kwenye kompyuta, akaanza kutoa picha, zoezi lililomchukua zaidi ya nusu saa. Alipomaliza alianza kuzichunguza vizuri moja baada ya nyingine. Aliendelea na zoezi lile huku akizitenganisha katika mafaili mbalimbali, kuanzia zile za mazingira, za uoto wa asili mpaka zile za makundi ya sokwe.
Wakati akiendelea kuzifuatilia, aligundua jambo ambalo lilimshangaza. Kila alipokuwa akizichunguza kwa makini picha alizopiga makundi yale ya sokwe, aligundua kama kuna kitu katikati yao ambacho hakikuwa kikionekana vizuri.
Alibaini pia kuwa sokwe wale walikuwa wakitembea kwa mtindo wa kuweka duara, hata walipokuwa wanaruka kutoka mti mmoja kwenda mwingine, katikati kulikuwa na kitu ambacho walionekana kukilinda kwa nguvu kubwa.
“Hiki ni nini?” alisema Harrison huku akijaribu kuivuta picha karibu kwenye kompyuta, ‘akai-zoom’ mpaka mwisho, hali iliyomsaidia kuona vizuri, akagundua kuna kitu kilikuwa katikati ya sokwe wale ingawa hakuelewa mara moja ni kitu gani.
Aliendelea kufuatilia picha zile kwa muda, akajikuta akisisimka mwili mzima kutokana na kitu alichokuwa anakiona.
“Lazima nirudi Tongass, nitaenda kufuatilia kwa makini ili nijue ni kitu gani,” alijisemea Harrison huku akiendelea kuzitazama zile picha. Aliifanya kazi ile kwa muda mrefu mpaka muda wa kulala ulipowadia.
Kesho yake, alfajiri na mapema Harrison aliamka na kuaga kuwa anarudi tena kwenye msitu wa Tongass kuendelea na kazi.
“Wewe si ulisema utapumzika kidogo? Kinachokufanya uwahi kurudi bila kukaa nasi hata kidogo ni nini?”
“Mama kuna kazi ya muhimu nilikuwa sijaimalizia, ni muhimu sana,” alisema Harrison bila kutaka kufafanua ni kazi gani. Mama yake hakuwa na hiyana, alimruhusu lakini akawa anajiuliza maswali mengi ambayo hayakupata majibu.
Harrison akasafiri kwa mara nyingine kurudi kwenye msitu wa Tongass. Safari hii hakupanda treni bali alisafiri kwa mabasi, akaunganisha safari mpaka alipofika Tongass.
“Mbona umerudi tena? Kuna kitu umesahau?” askari wa wanyama pori aliyemuacha jana yake, alimuuliza Harrison, akamweleza kuwa kuna jambo la muhimu alisahau kulifanyia kazi. Hata hivyo, hakumueleza ni jambo gani, akapewa vifaa na kurudi msituni, akaenda kuweka kambi pembeni kidogo ya pale alipokuwa amesimamisha hema lake.
Kwa kuwa tayari muda ulikuwa umeenda huku uchovu wa kuunganisha safari ukimsumbua, Harrison aliamua kupumzika mpaka kesho yake. Kulipopambazuka tu, aliwahi kuamka na kwenda nje ya hema, akawa anaangaza macho huku na kule akitegemea kuliona tena lile kundi la sokwe.
Muda ulianza kwenda lakini masokwe hawakutokea, ikabidi aanze kuwatafuta sehemu mbalimbali za msitu ule. Kuna wakati alisikia kelele, akahisi watakuwa ni wenyewe lakini alipofuatilia, alikuta kundi la tai likiufaidi mzoga wa mnyama aliyekuwa amejifia.
Akaendelea kuzunguka huku na kule, akijipenyeza katikati ya miti iliyokuwa imefungamana  ndani ya msitu huo. Baada ya kuhangaika sana bila mafanikio, Harrison aliamua kurudi kwenye hema lake kupumzika. Akiwa mita chache kutoka kwenye hema, alianza kusikia kelele upya, alipoangaza macho yake juu ya miti, aliwaona sokwe wakiruka kwa kasi, akatafuta sehemu na kujibanza, akawa anaangalia kwa makini katikati ya lile kundi.
Kamera yake nayo ilikuwa mkononi, akiwa tayari kupiga picha endapo angekiona kile kitu alichokuwa anakisubiri. Hata hivyo, kazi haikuwa nyepesi, kila sokwe wale walipokuwa wanaruka, walikuwa wameweka duara huku wakiwa makini kuziba kitu kilichokuwa katikati yao.
Je, nini kitafuatia? Usikose kufuatilia Ijumaa kwenye Gazeti la Ijumaa.

Views: 2597

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by raphael Joram on November 20, 2012 at 4:09pm
mh!yule mtoto
Comment by DORAH FREDY on November 20, 2012 at 11:33am

Hicho kitu ni yule mtoto wa Doctor ha ha ah ha ah haaa

Comment by Nadra M. Issa on November 19, 2012 at 4:32pm
hahaha icho kitu ni yule mtoto quen of gorillas
Comment by FURAHA TAUSI on November 19, 2012 at 4:29pm
mmmmh makubwa sasa hayo mimi ningekimbia nivunjike naogopa sana hao wadudu
Comment by Richard Rugajo on November 19, 2012 at 1:30pm

Hadithi tamu sana hii, yaani mhh! asante kaka!!

Comment by SAIDI ABDUL SAID on November 19, 2012 at 11:34am

nimeipienda sana iyo big up sana

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

Shakil Hasan posted a status
24 seconds ago
Shakil Hasan posted a status
46 seconds ago
kmraju posted a status
1 minute ago
Shakil Hasan posted a status
1 minute ago
Shakil Hasan posted a status
1 minute ago
vitalia posted a status
1 minute ago
sushanta posted a status
"2015 Melbourne Cup Carnival 03 November Tuesday…"
1 minute ago
Shakil Hasan posted a status
1 minute ago
Shakil Hasan posted a status
2 minutes ago
jennyloffer posted a status
2 minutes ago
Shakil Hasan posted a status
2 minutes ago
sushanta posted a status
"The Melbourne Cup 2015 Carnival Live Stream Race Schedule 3rd November http://melbournecuplivestream.com.au/"
3 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }