Queen of the Gorillas (Malkia wa Masokwe) -4

KELELE nyingi zilitawala ndani ya jahazi, watu wakawa wanalia na kuomba msaada ili kunusuru maisha yao kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa, hatari kubwa ilikuwa mbele yao na ingewakumba ndani ya muda mfupi. Bahari ilikuwa imechafuka, upepo ulioandamana na mawimbi makubwa ulikuwa ukivuma kutoka pande kuu nne za dunia, hali ilikuwa imebadilika kabisa.

Abiria wote wakaanza kumwomba Mungu awasaidie kwani kama jahazi lingepinduka tu, basi asingesalia mtu hata mmoja. Watu wote mia moja na ishirini wangekufa maji na miili yao kuliwa na samaki wakubwa baharini.

“Mungu ninakuomba unisamehe kwa kila dhambi niliyoitenda na uipokee roho yangu na kuilaza mahali pema peponi, amina!” alisema Harvey huku akishuhudia dhoruba hiyo.
Kwa muda wa saa nzima watu wote walishaamka na walionekana kufanya jitihada kubwa ili kujiokoa lakini dhoruba ilikuwa imewashinda. Tayari ndani ya jahazi kulishaanza kuingia maji na taratibu lilianza kupoteza mawasiliano.

Wakati wakifikiria nini wafanye, sauti ya nahodha ikasikika ikiwatangazia kwamba jahazi lilikuwa katika hali ya hatari hivyo kungeweza kutokea kitu chochote, akawataka watu wavae makoti maalum (life jackets) ambayo yangewasaidia wasizame ili kuokoa maisha yao mara jahazi litakapozama.

Hali ya hewa ilishachafuka, hakukuwa na mawasiliano tena ndani ya jahazi, kila mtu alikuwa akifikiria kuokoa nafsi yake na si vinginevyo. Wengi walilia na kujilaumu kwa kuamua kuchukua uamuzi wa kuondoka nchini kwao kukimbia mauaji. Waligundua kuwa kumbe walikuwa wameruka majivu na kukanyaga moto na sasa walikuwa wakifa kwa maumivu.

Harvey alikuwa kimya kabisa, taswira za ndugu zake zilikuwa zikijirudia ndani ya akili zake, akaamini kwamba muda si mrefu angeungana nao huko walikokuwa.
“Ninakuja kuungana nanyi muda si mrefu…,” alisema maneno hayo na akashuhudia wimbi kubwa likilipiga jahazi huku watu wakipiga mayowe bila mafanikio. Akiwa hapo akashuhudia wimbi la pili nalo likija kwa nguvu na kulipiga jahazi lao, maji mengi yakaingia ndani. Watu wakaanza kutapatapa huku na kule, wengi wakionekana kuzimia.

Akashuhudia pia watu wakijirusha kutoka jahazini hadi baharini huku wakizidi kupiga mayowe ya kuomba msaada bila mafanikio. Harvey akauona mwisho wake, hakutaka kuamini kuwa atakufa kifo cha uchungu cha kuzama bahari na mwili wake kuliwa na samaki wakubwa. Machozi yakawa yanambubujika, pamoja na maumivu hayo alifurahi kwamba alikuwa anakwenda kuungana na baba, mama na dada yake, akajikuta akiachia kicheko.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...

WIMBI la tatu likapiga tena, safari hii kwa nguvu zaidi. Harvey akashuhudia jahazi likipinduka na hatimaye kuzama huku kelele za watu zikisikika. Ghafla ukimya wa ajabu ukatanda eneo lote. Ilikuwa ni ajali mbaya katika jahazi hilo lililokuwa na watu mia moja na ishirini. Hakika lilikuwa tukio la kuhuzunisha kupita maelezo.

Ni wakati wimbi la tatu linapiga na Harvey kulishuhudia kwa macho yake likija kwa kasi, akasogea karibu na kijana mmoja kati ya wale waliofanikiwa kukimbia vita pamoja na kumshika mkono huku akimweleza maneno ya uchungu.
“Sasa ni wakati wa sisi kufa lakini kabla hatujafa ni lazima tujaribu kufanya kitu, sogea karibu yangu na wote tushikane mikono kwa nguvu,” aliongea Harvey na kwa pamoja huku wakitetemeka wakaruka na kuliacha jahazi likizama.

Walizama na kuibuka mara kadhaa baharini na walipojaribu kutupa macho yao kuona kama wangepata msaada hawakufanikiwa kuona kitu zaidi ya giza nene lililokuwa limetanda kila upande, wakalia machozi ya uchungu kwamba nao pia wangekufa muda si mrefu.
“Harvey?”
“Mh!”
“Sidhani kama tutapona.

“Tutapona nishike mkono vizuri usiniachie.”
“Siwezi nimechoka naona nguvu zinaniishia.”
“Hapana usifanye hivyo kamata vizuri tutapata msaada muda si mrefu.”
Akaushika vyema mkono wa Harvey na kwa pamoja wakaanza kusonga kwenda mbele wakijaribu kuokoa maisha yao. Ni juhudi za Harvey akimfariji mwenzake ndizo ziliwafikisha juu ya mgongo wa jahazi wakapanda kwa pamoja na kumshukuru Mungu.

“Ahsante Mungu kwa ukombozi wako, hakika huu ni muujiza!” aliongea Harvey huku jahazi likisukumwa taratibu na upepo kwenda mbele.
“Tunayo kazi kubwa mpaka kufika tunakokwenda.”
“Kwa neema za Mungu tutafika tu.”

Harvey alizidi kumpa moyo mwenzake ambaye alionekana kukata tamaa waziwazi. Wakati jahazi likisukumwa na upepo taratibu walijaribu kuangaza huku na kule kuona kama wangefanikiwa kuona mtu mwingine lakini haikuwa hivyo, wakatoka eneo moja kwenda jingine bila mafanikio.

Wakiwa hawajui muelekeo wa maisha na hatima yao, njaa, kiu na baridi kali viliendelea kuwasumbua lakini hawakupoteza tumaini.
“Nasikia homa,” aliongea rafiki wa Harvey.
“Pole lakini huna budi kuvumilia rafiki yangu, tunachotaka sisi ni kufika Marekani basi,” Harvey alizidi kuongea akimpa moyo rafiki yake.

“Unachozungumza ni kweli tupu rafiki yangu lakini sijui…”
Waliongea wakiwa juu ya jahazi hatimaye mchana ukaisha na usiku ukaingia bila kupata msaada wowote ule huku bado wakiendelea kuteseka kwa njaa na baridi kali ambayo ilizidi kudhoofisha miili yao.

Wakiwa juu ya jahazi, bado waliendelea kuona machafuko ya bahari, upepo mkali ukivuma na kulisukuma jahazi. Wakiwa juu yake, waliendelea kumwomba Mungu anusuru maisha yao. Hakika kwao ilikuwa ni safari ndefu na yenye machungu mengi lakini hawakuwa na jinsi, ilibidi waikubali kwani huko walikokuwa wakitoka hakukuwa na amani, vita ndivyo vilivyotawala na kupoteza ndugu, jamaa na marafiki. Walitaka wafike Marekani, kuanza maisha upya na kutafuta ndugu wengine. Huko ndiko yangekuwa maisha yao yote kama wangefanikiwa kufika wakiwa hai.

Wiki ya kwanza ikakatika, ya pili, hatimaye ya tatu wakiwa bado wako juu ya jahazi bila msaada wowote na hatimaye nao wakaanza kuchoka na kukata tamaa ya kufika Marekani salama, wakakiona kifo mbele yao, afya zao zilikuwa mbaya, wakakonda kupita maelezo na nguvu nazo zikaisha, tumaini la kufika salama likapotea, wakati huo wakakitamani kifo zaidi kuliko uhai.
“Harvey!”

“Unasemaje?”
“Mimi ninakufa muda si mrefu, nimevumilia vya kutosha naona sasa niachie na kuzama baharini.”
“Usiniache peke yangu bado nakuhitaji ni wewe ndiye ndugu yangu tafadhali jitahidi.”
“Siwezi, hali ni mbaya, njaa inanisumbua.”
“Sikiliza! Piga moyo konde amini kwamba Marekani tutafika.”

“Lini? Wakati hakuna hata dalili ya kisiwa wala meli baharini ambayo itaweza kutuokoa?”
“Mungu ataleta muujiza,” Harvey aliongea.
Jahazi likazidi kusukumwa na upepo kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele ambapo hali ikazidi kuwa mbaya.
“Harvey acha mimi nitangulie, hakika siwezi kuendelea tena nimechoka, Mungu akipenda tutaonana.”

“Nasema hapana, huwezi kufa nitakulinda.”

“Najua unanipenda kweli lakini si mimi, ni moyo ndiyo umetamani kuwa hivyo, hakika siwezi kuendelea na safari hii ninakufa.”
Harvey akageuka na kumshika vyema rafiki yake huku akiongea maneno ya faraja lakini bado hayakuonekana kumwingia kichwani mwake kwani bado aliendelea kusisitiza kwamba ni bora afe. Akajitahidi kwa nguvu zake zote mwisho naye akachoka kubembeleza na kumwachia Mungu aamue.

Akiwa pembeni tu akashuhudia rafiki yake mpendwa, ndugu pekee aliyebaki naye akilegea taratibu na mikono yake kuachia sehemu aliyokuwa amejishikilia, mwisho akasikia kilio kikali kikiambatana na mlio.
“Dubwi!”
Harvey akalia huku akimwomba Mungu amnusuru rafiki yake na kifo, akiwa juu ya jahazi akashuhudia kwa macho yake akizama mara ya kwanza na kuibuka, mara ya pili ya tatu pamoja na kwamba giza lilishaanza kuingia hakumwona tena akiinuka juu akajua tayari ameshakufa maji.

Akaangua kilio kwani tayari alikuwa amebaki peke yake bila mtu yeyote, kwake tumaini la kufika alikokuwa akielekea lilishaanza kutoweka ndani ya moyo wake.
Nguvu zikiwa zimemwishia taratibu akajilaza juu ya jahazi akiendelea kumwomba Mungu amtendee muujiza. Mara kadhaa alikumbuka familia yake akaziona taswira za baba, mama na dada yake zikimwita awafuate, akashindwa kujizuia na kwikwi ya kulia ikamkaba.

Akaliona giza nene machoni mwake, mwili wake pia ulikuwa ukichemka kwa homa kali, mwisho wake naye ulikuwa umekaribia taratibu akashuka na kujilaza juu ya jahazi akayafumba macho yake na kumwomba Mungu amsamehe dhambi zake zote na ikiwezekana amkaribishe kwenye ufalme wake. Alipomaliza tu salama hiyo usingizi mzito ukamchukua.

Je, nini kitatokea? Harvey atanusurika kifo? Fuatilia siku ya Jumatatu katika Gazeti la Ijumaa Wikienda.

Views: 3965

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Dr Nyasika Edson on May 22, 2012 at 2:08am

erick hiz story za kuhuzunisha punguza coz znztia majonz

Comment by paul william masele on May 18, 2012 at 2:44am

very nice

Comment by Abuu The Prince on May 15, 2012 at 11:05pm

mhh!! kabaki peke yake!!

Comment by ESSERO MAFURU on May 14, 2012 at 7:24pm
He got da + thoughts Mungu atamsaidia!
Comment by Raphael Mitimingi on May 14, 2012 at 8:59am

Ah!  Hemed Mtana mbona unawahi sana kabla, si uache tufike huko wenyewe, unaondoa ohondo kwa kubashiri mambo yatakayotokea, Mwachieni mhadithiaji atupeleke hadi tufike kwa nafasi inayotakiwa.

Comment by Hemed Mtana on May 13, 2012 at 2:18pm
jahazi litasogezwa na maji hadi kwenye misitu ya amazoni na harvey ataokotwa na sokwe
Comment by saada Yussuf hussein on May 13, 2012 at 11:42am

pole sana kijana mungu yupo pamoja na wewe

 

Comment by Juma Kambuki on May 12, 2012 at 9:07pm
Nishaijua hii haithi harvay ataokotwa na magorila kisha atakutana na malkia wa magorila kama mov ya shala
Comment by Mija Mihayo on May 12, 2012 at 5:52pm

Starring huwa hafi so hadithi njoo utamu kolea. Big up Eric wa Shigongo

Comment by laurenciamsunga on May 12, 2012 at 3:10pm

pole sana kijana mungu yupo atakupigania utashinda

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }