Queen of the Gorillas (Malkia wa Masokwe) - 125

SIRI aliyoificha Harrison kwa kipindi kirefu inafichuka. Inabainika kwamba kumbe hakufa bali alimkimbia Linda kabla hawajafunga ndoa, kisha akatengeneza ajali feki ambayo ilionesha kwamba amekufa.Akakimbilia kwenye Msitu wa Tongass kumsaka malkia wa masokwe.

Baada ya miaka mingi kupita, akiwa tayari ameshamuoa malkia wa masokwe, anaamua kurejea nyumbani kwao ambapo ujio wake unasababisha kizaazaa kikubwa.
Baadaye anaeleza ukweli na kuwaomba radhi watu wote kwa kilichotokea. Kikao cha kifamilia kinafanyika na kuombana msamaha.

Baadaye Harrison anaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kueleza ukweli lakini muda mfupi baada ya kumaliza kueleza kila kitu, anawekwa chini ya ulinzi na askari wenye silaha.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

Askari hao wenye silaha wakamfunga pingu na kuondoka naye mpaka kwenye Kituo cha Polisi cha Miami alikotakiwa kutoa maelezo ya kutosha juu ya mahali alikoipata maiti waliyoitumia kuandaa ajali feki, kama alivyoeleza mbele ya waandishi wa habari.
Alipomtaja rafiki yake waliyeshirikiana kwenye tukio hilo, Daktari Rogers ambaye ndiye aliyefanikisha mpango wa kupatikana kwa maiti, naye alienda kukamatwa siku hiyohiyo na kuunganishwa na Harrison, wakawekwa nyuma ya nondo.
Baada ya wote wawili kukamatwa na kupelekwa mpaka kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Miami, taratibu za kuwaburuza mahakamani zilianza kufanywa haraka iwezekanavyo. Shinikizo kutoka kwa viongozi wa jeshi la polisi nchini humo lilikuwa kubwa kwani walijua wakiwaachia bila kuwachukulia hatua yoyote, wananchi watawadharau na hadhi yao mbele ya jamii itashuka sana.
Hata hivyo, kwa kuwa mahojiano aliyokuwa akiyafanya Harrison na waandishi wa habari yalionekana na watu wengi, mawakili wengi kutoka pande mbalimbali za nchi hiyo walijitokeza kutaka kumsaidia. Kila mmoja alijua wakati anafanya kosa hilo, hakuwa sawa kiakili na ndiyo maana alifikia hatua ya kufanya tukio la ajabu kiasi hicho.
Gumzo nchini Marekani likawa ni habari ya Harrison ambapo kila mtu alikuwa akisema lake. Wanaharakati wa haki za wanawake, walikilaani mno kitendo cha Harrison kumkimbia Linda kanisani wakati kila kitu kilishakamilika. Wakasisitiza kwamba alikuwa na nafasi ya kumweleza ukweli kuliko mateso aliyomsababishia.
Hata hivyo, kwa sababu mwenyewe alikiri kufanya makosa na kuwaomba radhi wote aliowakosea akiwemo Linda, baadhi walimsamehe ingawa kuna kundi dogo bado liliendelea kumsakama kwa kitendo alichokifanya.
Harrison aliendelea kutawala kwenye vyombo vya habari, runinga, redio na magazeti vyote vikawa vinazungumzia kwa kina mazungumzo yake aliyoyafanya na waandishi wa habari na hatua ambazo jeshi la polisi lilimchukulia kutokana na alichokifanya. Wazazi na ndugu zake pamoja na ndugu wa Linda walikuwa pamoja na Harrison kwani walikubali kuupokea msamaha wake kwa dhati.
Angel ndiyo alikuwa na hali mbaya zaidi kutokana na kukamatwa kwa mumewe, akawa analia muda wote, hali iliyowapa kazi ya ziada mama yake Harrison, bibi na babu yake. Alikuwa na wasiwasi mkubwa kuwa huenda mumewe akahukumiwa kifungo kirefu gerezani, jambo ambalo hakuwa tayari kuona linatokea.
Wakawa wanambembeleza na kumweleza kuwa kila kitu kitapita, wote wakawa wanashinda nje ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Miami wakijaribu kutafuta njia ya kumuwekea dhamana. Hata hivyo, kutokana na uzito wa kesi iliyokuwa inamkabili, hakupata dhamana kwa urahisi. Siku ya kwanza ikapita wakiwa nyuma ya nondo.
Siku iliyofuata, kesi yao ilisomwa kwa mara ya kwanza mahakamani ambapo Harrison na mwenzake walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu; kumuua mtu kisha kutumia maiti yake kuudanganya ulimwengu kwamba ni Harrison, kupanga njama na kufanya udanganyifu.
Timu ya mawakili watano walijipanga kuwatetea Harrison na mwenzake na baada ya kesi hiyo kutajwa, mawakili hao ambao awali walifanya mazungumzo ya kina na Harrison pamoja na mwenzake, Dokta Rogers wakiwa mahabusu.
Kesi ilipoanza kunguruma, mawakili hao walianza kuwatetea wateja wao. Wakaieleza mahakama kwamba hawakumuua mtu yeyote kama mashtaka yao yalivyokuwa yanasema bali maiti waliyoitumia ilichukuliwa kutoka kwenye mochwari ya hospitali ambayo Rogers alikuwa akifanyia kazi.
“Mtukufu hakimu, maiti iliyotumika ilikuwa imekaa zaidi ya siku nne ndani ya mochwari na mipango ilishaanza kufanywa ili ikazikwe na manispaa. Hivi hapa ni vithibisho vyake,” alisema wakili mmoja huku akiweka mezani cheti cha kifo cha maiti iliyotumika.
Wakili mwingine alieleza kuwa wakati mteja wao anafanya yote hayo, hakuwa sawa kiakili kutokana na kushinikizwa kumuoa mwanamke ambaye hakuwa akimpenda kutoka ndani ya moyo wake. Kesi iliendelea kuunguruma kwa saa kadhaa huku pande mbili za mawakili wa upande wa serikali na wa upande wa Harrison na mwenzake wakivutana.
Mpaka muda wa mahakama unaisha, tayari Harrison na mwenzake walikuwa wameyapangua mashtaka ya mauaji na kubakiza mashtaka mawili ya kupanga njama na udanganyifu ambayo hata hivyo, kisheria yalikuwa na dhamana. Taratibu zikafanywa na ndugu zao kisha wote wawili wakaachiwa kwa dhamana.
Ilikuwa ni furaha iliyoje kwa Angel na familia nzima ya Harrison. Akakumbatiana na ndugu zake kwa furaha na kurudi hadi nyumbani kusubiri siku nyingine ya mashtaka yao kusomwa. Habari hiyo pia ilitangazwa sana na vyombo vya habari, jina la Harrison likazidi kuwa maarufu midomoni mwa watu huku mauzo ya kitabu chake cha Queen of Gorillas yakizidi kuongezeka.
Kila mtu alikuwa na hamu ya kukisoma kitabu hicho ambacho kilikuwa kinaelezea jinsi Harrison alivyokutana na malkia wa masokwe kwa mara ya kwanza. Mauzo hayo yalizidi kuitunisha akaunti yake na kumfanya apate fedha nyingi.
Siku zilizidi kusonga mbele, hatimaye tarehe ya kutajwa tena kwa kesi iliyokuwa ikimkabili Harrison iliwadia. Wakaenda tena mahakamani ambapo kesi ilianza kunguruma huku umati mkubwa wa watu wakiwa wamehudhuria mahakamani sambamba na waandishi wa vyombo vya habari.
Katika hali ambayo wengi hawakuitegemea, hakimu alipoisoma kesi hiyo, mwanasheria mkuu wa serikali aliwasilisha hati maalum kutoka kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ya Marekani (DPP), James Conrad na kuieleza mahakama kuwa baada ya kuupitia mwenendo mzima wa kesi hiyo na mazingira ambayo tukio hilo lilitokea, aliamua kuwafutia mashtaka Harrison na Rogers.
Hakimu akagonga nyundo mezani na shangwe za hapa na pale zikatawala mahakamani, Harrison akawa anakumbatiana na mawakili wake pamoja na ndugu zake na mashabiki wengi waliokuwa wamefurika mahakamani. Hoihoi, nderemo na vifijo vikatawala eneo lote la mahakama mpaka umati ulipoanza kuondoka kuelekea nyumbani kwa akina Harrison.
“Nakupenda sana mume wangu, narudia tena kukuhakikishia kwamba nitakupenda mpaka mwisho wa maisha yangu,” alisema Angel huku akitokwa na machozi ya furaha, akakumbatiana na Harrison kimahaba. Watu waliokuwa wamewazunguka wakawa wanashangilia kwa nguvu.
Huo ukawa mwanzo wa maisha mapya ya uhuru wa Harrison na familia yake. Waandishi mbalimbali waliendelea kumtembelea nyumbani kwa mama yake na kumhoji maswali mbalimbali kuhusu ugumu alioupata mpaka alipofanikiwa kumpata malkia wa masokwe. Ilikuwa ni simulizi ya mapenzi iliyomsisimua kila aliyeisikia.
Baada ya wiki moja, Harrison na mkewe walianza maandalizi ya safari ya kwenda Tanzania kumtafuta baba mzazi wa Angel na kuijua vyema asili ya msichana huyo ambaye sasa alikuwa ni mke wake halali, akiwa na baraka zote kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Harrison.
***
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
Kila siku jiulize: “Hivi nikifa leo nitakwenda jehanam au peponi?” Kila mmoja wetu analo  jibu lake, bila shaka sote tungependa kwenda peponi. Kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu. Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.

Je, nini kitafuatia? Usikose kufuatilia Jumatatu kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda.

Views: 4176

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by penina mwailunda on July 8, 2013 at 9:45am

Hii naona inakaribioa kwisha, Tunategemea ingine sweet kama hii  

Comment by JASIRI SETH LUVANDA on July 6, 2013 at 8:06pm

nice story jamani inaonekana wikifika tanzania watamkuta baba  wa angel akiwa hai nice job bro

Comment by Juma Kambuki on July 6, 2013 at 12:52pm
Kwanini wasomaji wengi wa liwaya hizi za shigongo wakimaliza kusoma hadithi hawasomi ukumbusho wa mtunzi?
Comment by hussein vuai ame on July 5, 2013 at 3:43pm

Harrison ns mkeo karibu kwenye mlima kilimanjaro pamoja na mavutio ya kitalii ya pale Jozani zanzibar utawaona kima punju mfano wa sokwe Karibuni Tanzania

Comment by robert ludger nyagali on July 5, 2013 at 3:04pm

Hii inavutia sana kwani hii ya Harrison ni Kali kwelikweli

Comment by Mishy chunga on July 5, 2013 at 2:53pm

amkute akiwa hai jamani, isije kuwa alishakufa!

Comment by DORAH FREDY on July 5, 2013 at 2:14pm

Nzuri sana

Comment by Zayda on July 5, 2013 at 2:01pm
You're warmly welcome in Tanzania,Harrison & Angel.
Comment by neema erasto on July 5, 2013 at 12:53pm

mmmmh!! nzuri sana

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

maxmizan posted a status
2 minutes ago
mdsohel173 posted a status
7 minutes ago
mdsohel173 posted a status
9 minutes ago
mdsohel173 posted a status
11 minutes ago
wakwaw posted a status
14 minutes ago
maxmizan posted a status
14 minutes ago
maxmizan posted a status
15 minutes ago
maxmizan posted a status
15 minutes ago
maxmizan posted a status
15 minutes ago
misu babu posted a status
16 minutes ago
maxmizan posted a status
16 minutes ago
maxmizan posted a status
16 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }