Na Mwandishi Wetu
KWA mara nyingine tena, hali ya staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ (pichani) imewazidishia hofu Watanzania baada ya kuanguka jukwaani akiwa jijini Arusha, Amani linakujuza.

Sajuki baada ya kuanguka chini.

Tukio hilo lilitokea katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa hivi karibuni kulipokuwa na tamasha lililowahusisha wasanii wa sinema ambapo Sajuki alitakiwa kupanda jukwaani ili kusalimia kadamnasi.
Cha ajabu, baada ya kukabidhiwa kipaza sauti, Sajuki hakuweza kuongea, badala yake alipaza sauti na kupiga kelele kisha kuanguka chini, hali iliyozua hofu uwanjani hapo.
Baada ya tukio hilo, Sajuki ambaye ni mgonjwa kwa muda mrefu sasa, alichukuliwa na wasanii wenzake na kuwekwa pembeni kwa ajili ya huduma ya kwanza.
Miongoni mwa maneno yaliyomtoka kinywani kwa wakati huo ni haya: “Sijisikii vizuri, hali yangu ni mbaya.”
Baadhi ya watu waliohojiwa na Amani, walisema msanii huyo anapaswa kufanyiwa maombi maalum ili aweze kupata nguvu za kuendelea kufanya shughuli zake.

Wadau wakijaribu kumnyanyua Sajuki baada ya kudondoka jukwaani.

“Mungu amuongoze lakini anahitaji maombi kwa kweli. Si suala la daktari peke yake,” alisema Mary Shimo, mkazi wa Kijenge jijini hapa.
Hata hivyo, baadhi ya madaktari walioongea na mwandishi wetu walisema wanashangazwa na tabia ya  msanii huyo kuzunguka mikoani na wasanii wenzake huku afya yake  ikiwa mgogoro.
“Sajuki bado hajapona, muda mwingi anatakiwa apumzike kuliko kusafiri kama anavyofanya,” alisema mmoja wa madaktari hao.
Hivi karibuni, Sajuki na baadhi ya wasanii wa filamu walifanya ziara mjini Iringa na msanii huyo alianguka jukwaani kama ilivyomtokea jijini hapa.
Habari zilizopatikana wakati tunakwenda mitamboni zinasema, zinatakiwa shilingi milioni 18 ili msanii huyo arudi India kwa ajili ya kuendelea na matibabu.
Mei mwaka huu, Sajuki alikwenda nchini India kwa lengo la kutibiwa, lakini ikasemekana alirudishwa ili atimize baadhi ya mambo kabla ya kwenda kufanyiwa matibabu kamili.

Simon Mwakifwamba (kushoto) na wadau wakimpa kampani Sajuki kutoka jukwaani.

Views: 8482

Tags: amani11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by penina mwailunda on December 27, 2012 at 2:42pm

Labda ni vile maisha ya bongo ni magumu lakini kwa ule ukweli Sajuki unatakiwa upate muda mrefu wa kuupumzisha mwili wako, ili lishe ipate nafasi ya kufanya kazi ya kuupa mwili wako afya na nguvu. (pia uwe makini na vyakula)

Comment by Hashim Yahya Settembo on December 23, 2012 at 8:18pm

Pole Bro Mungu Akupe Maisha marefu na akuepushe na maradhi yanayokusumbua

Comment by pjoan audes on December 22, 2012 at 3:08pm

Hajawa katika hali ya kumuwezesha kufanya shuruba sema huu ukata nao noma, si inabidi ajitafutie vijisenti vya kumrudisha india kutibiwa akisema apumzike atapewa na nani ikiwa wasamalia wote siku hizi wanataka kupigwa picha za video kwenye tv uma uone walivyosaidia?!

Comment by Domino Bagambisa on December 21, 2012 at 8:22pm

ole sana pata mapumziko ya kutosha nyumbani ili urejeshe afya iliyotetereka kwa maradhi makubwa yaliyokusibu awali nahisi yanatoka taratibu.

Comment by lilliany on December 21, 2012 at 3:06pm

Pole sana, nningekushauri upumzike nyumbani mpaka utakapo pata nafuu.

Comment by Halima Kimoto on December 21, 2012 at 11:09am

Pole Mwenyezi Mungu atakuafu na Ishallah utapata nafuu vizuri.  Hata hivyo nakushauri upumzike angalau kwa muda wa mwaka mmoja uitizame afya yako.  Najua hali ya maisha ni ngumu lakini sali sana na umuomba Mwenyezi Mungu akujalie wepesi kwani hakuna lisowezekana kwa Mwenyezi Mungu

Comment by nellicy maluli on December 21, 2012 at 8:44am

BABA, RAIS WETU JAKAYA KIKWETE TUNAKUOMBA UMWANGALIE MWANAO SAJUKI ANAVYOTESEKA, TUNAOMBA KWA NIABA YA FAMILIA YAKE UGUSWE NA MAUMIVU YAMPATAYO KIJANA WAKO ILI UMSAIDIE KIMATIBABU. NI MUELIMISHAJI MZURI KATIKA JAMII NA PIA BADO ANAHITAJIKA KATIKA SANAA, TUNAOMBA BABA YETU.

Comment by DORAH FREDY on December 21, 2012 at 8:41am

Pole sana Sajuki ila pumzika na ule vinzuri acha kusafari safiri kila mara pumzika utapona utakuja tu kutembea

Comment by mayalilwa on December 21, 2012 at 8:20am

Watanzania tunapendana tangazeni kiasi cha pesa kinachotakiwa kufanikisha matibabu yake tutachanga.

Comment by philipo zabuli on December 21, 2012 at 8:09am

huyu bwana Sajuki analazimika kuzunguka mikoani katika matamasha ya wasanii sio kwamba anapenda kufanya hivyo. anayo majukumu ya kifamilia - mke na mtoto. pili anatafuta pesa kwa ajili ya matibabu yake. jamani wenye huruma - viongozi serikalini na wafanyabiashara na watanzania wenye huruma msaidieni.

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE yesterday. 27 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

Latest Activity

tina babi left a comment for Jeremiah John
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
11 seconds ago
tina babi left a comment for jkk
"tinalutunku@yahoo.com Hello, My name is Miss tina lutunku. i saw your profile today and become…"
50 seconds ago
tina babi left a comment for juma maulid
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
1 minute ago
tina babi left a comment for Aidan Charlie Seif
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
1 minute ago
Quentin Burchfield posted a status
5 minutes ago
tina babi left a comment for masakilija haruna yusuph
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
11 minutes ago
tina babi left a comment for peter kileo
"tinalutunku@yahoo.com Hello, My name is Miss tina lutunku. i saw your profile today and become…"
11 minutes ago
tina babi left a comment for jaymore
"tinalutunku@yahoo.com Hello, My name is Miss tina lutunku. i saw your profile today and become…"
11 minutes ago
tina babi left a comment for zecho
"tinalutunku@yahoo.com Hello, My name is Miss tina lutunku. i saw your profile today and become…"
11 minutes ago
tina babi left a comment for ferdinand geras
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
13 minutes ago
Olga Bliss posted a status
13 minutes ago
tina babi left a comment for Ank Ngassa
"tinalutunku@yahoo.com Hello, My name is Miss tina lutunku. i saw your profile today and become…"
13 minutes ago

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service