STORI; ERICK EVARIST
Masistaduu wawili wa tasnia ya filamu Bongo ambao hivi karibuni waliunda Kundi la 2gether, Salma Jabu ‘Nisha’ na Flora Festo Mvungi, wanadaiwa kuibua timbwili zito baada ya kuzichapa kavukavu wakiwa ‘lokesheni’, Ijumaa linafunguka.
HABARI MEZANI
Kwa mujibu wa sosi makini wa habari hiyo, tukio hilo lilichukua nafasi katika nyumba moja waliyokuwa wakirekodia maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Chanzo hicho ambacho ni mmoja wa wasanii waliokuwa eneo la tukio (jina linahifadhiwa), kilimpigia simu paparazi wetu na kumweleza mkanda mzima ulivyokuwa hadi mastaa hao wa filamu kufikia hatua ya kutwangana.
CHANZO NI NINI?
“Sisi hatukujua chanzo ni nini, mwanzoni walianza kurushiana maneno ya kashfa, lakini ghafla hali ilibadilika baada ya Nisha kusikika akimtolea mwenzake (Flora) maneno makali.
“Nisha alisikika akimwambia Flora hamuwezi kwa chochote kuanzia mafanikio kimaisha na hata uigizaji.
“Kilichomfanya Flora akasirike zaidi ni kitendo cha Nisha kumwambia kuwa hata kama ni mwanaume basi yeye ana mwanaume mzuri kuliko H. Baba (Mwanamuziki Hamis Ramadhan) ambaye ni mchumba wa Flora,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Baada ya Flora kuambiwa hivyo huku Nisha akionesha dharau, ndipo alipojibu mapigo kwa kumwambia asitafute umaarufu kupitia kwake.”
NGUMI ZACHAPWA
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa, kitendo cha Nisha kuambiwa anasaka umaarufu kupitia kwa Flora ndicho kilichosababisha Nisha kupandwa hasira na kumtandika mwenzake kofi.
“Flora naye siyo mchezo, aligeuka mbogo akamtandika Nisha makofi ya kutosha kabla ya H. Baba kuitwa akaja kuamulia timbwili huku nguo zao za ndani zikiwa nje nje kwani mbali na makofi, pia walikunjana na kufunuana vigauni vyao, kila mmoja alikuwa na hasira vibaya na hata sasa hivi hawako vizuri,” kilisema chanzo chetu.
WENYEWE WANASEMAJE?
Baada ya kujiridhisha na maelezo ya chanzo chetu, Ijumaa liliwatafuta Flora na Nisha kwa nyakati tofauti ambapo mastaa hao waliofunika kwenye filamu yao ya Macho Yangu itakayoingia sokoni mwisho wa mwezi huu, walifunguka kila kitu huku kila mmoja akidai mwenzake ndiye chanzo.
NISHA:
“Ni kweli siku hiyo nilikuwa mimi, Flora na Shilole (msanii Zuwena Mohamed) wakati tunamalizia kushuti filamu yetu ya Macho Yangu maeneo ya Mbezi, siku zote nilikuwa nikimkanya Flora aache kujitapa kwangu kuwa yeye ni bora kuliko mimi, alikuwa hasikii lakini siku hiyo alipitiliza ndiyo maana nikamtembezea kichapo.”
FLORA:
“Wewe Nisha humjui? Anapokuwa sehemu anapenda sana kujishaua ili aonekane yupo juu, hawezi kunidharau mimi hadi mpenzi wangu, aliniudhi sana nikashindwa kuzuia hasira.”
HALI IKOJE SASA?
Wawili hao waliliambia Ijumaa kuwa wanajitahidi kusahau yaliyotokea ili kulinda heshima ya kundi lao kwa mashabiki wao.
Comment
Mwe! jamani haya makubwa eti uzuri wa mwanaume ni sausage.
Comment by mohamed saadan on March 29, 2012 at 2:35pm uzuri wa mwanaume ni pesa plus sausage sio sura(wengi wa mahandsome si ridhkiii).pumbavu weeeeeeeeeeeeeeeeeehhhhhhhh
Comment by Bill Semsela on March 27, 2012 at 9:21pm
Comment by Mwafongo M on March 27, 2012 at 12:32pm heshima haiji bila kuzichapa
Comment by hussein,m albeity on March 26, 2012 at 11:40am haya hongera mapema sana
Comment by meggie impostra on March 25, 2012 at 1:36pm hv hawa wasanii kupign kila siku kwa nn wao tuuu mabifu yasiyo na msingi upuudhi mtupu
Comment by Ukweli100 on March 25, 2012 at 2:06am lakini florah uko juu1! ila watu wengine wapotezee, ni mashetani wanaweza kuchoropoa hiyo mimba yako bureee...mwendawazimu huyo ulizidunda naye.
Comment by lumi mwandelile on March 24, 2012 at 3:14pm utoto unawasumbua
Comment by Juma Hilal Sleiman on March 24, 2012 at 3:04pm nyinyi nyote hamna kitu mnauza sura tu muonekane kama mpo basi mana hamna njia nyengine ya kutokea,pili mnatangaza iyo filam yenu tujue kama mnaekti. kama ni kweli uyo alopiga cm angeleta na ushahidi wa picha na nyie global hajamuhoji? kila cm ina kamera cku hizi au na nyie mmepewachenu?
Comment by Ukweli100 on March 24, 2012 at 1:45pm hahah! afadhali mmepigana, natumaini hasira zimekwisha, mko tayari kwa kazi now
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
NDAUKA the GREAT |
| 3 |
julius manning |
| 4 |
LJH_3 |
| 5 |
hope |
| 6 |
Tatu Majaliwa |
| 7 |
mayalilwa |
| 8 |
steven emmanuel |
| 9 |
Matilanga Lukingita |
| 10 |
Mishy chunga |
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies 0 Likes
JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies 8 Likes
Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies 3 Likes
Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…
Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE on Monday. 27 Replies 5 Likes
HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies 4 Likes
Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…
Tags: SOKA
Started by GLOBAL in Habari. Last reply by Billy Frank Irungu Apr 26. 118 Replies 21 Likes
Tags: NCHINI, HAPA, UNAFURAHIA, HUDUMA, ZAKE?
Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies 4 Likes
hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?
Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies 9 Likes
Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…
© 2013 Created by Global Publishers.




You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers