Na Imelda Mtema
LILE sakata la staa wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya kutuhumu kumshika ugoni staa mwenzake aliyemtoa kwenye gemu, Lucy Francis Komba limeingia sura nyingine kuafutia picha za filamu inayodaiwa kuchezwa na wawili hao kunaswa na Ijumaa, twende hatua kwa hatua.

Katika baadhi ya matoleo ya Magazeti ya Global Publishers zilichapishwa habari za mastaa hao kuzua bifu zito kufuatia Lucy kumchukua mwanasoka wa Rwanda ambaye ni mume wa ndoa wa Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ na kucheza naye filamu jambo ambalo Uwoya alilipinga.

KWA NINI UWOYA ALIPINGA?
Uwoya alipinga mumewe kushiriki filamu hiyo kwa sababu aliambiwa washiriki ni wawili tu, mumewe Ndikumana na Lucy. Filamu inaitwa Kwa nini Nisimuoe?
Kwa mujibu wa Uwoya, hajawahi kuona filamu ya kawaida inachezwa na watu wawili tu, akasema Lucy alitumia nafasi hiyo kuwa na mumewe kimapenzi.
Hata hivyo, Uwoya alisema akiviona vipande vya picha za filamu hiyo atajua ukweli.
Wiki iliyopita aliviona vipande hivyo na kuweka msimamo wake kwamba hakuna filamu ni mapenzi tu.

IJUMAA LAFUKUNYUA, LAIBUKA NA PICHA
Kama kawaida ya Magazeti ya Global Publishers, liwe Ijumaa, Uwazi, Ijumaa Wikienda, Amani, Championi au Risasi ni kuchimba mambo kwa undani na kuupata ukweli wa jambo, hivyo timu ya wanahabari wetu ilizama mitaani na kuzisaka picha za filamu hiyo.
Julai 23, 2013, Ijumaa lilifanikiwa kuzipata picha hizo ambazo moja baada ya nyingine zinawaonesha Lucy na Ndikumana wakiwa katika mapozi mbalimbali ndani ya filamu (angalia picha).

MWANZO, MWISHO NI WAWILI TU!
Katika picha hizo ambazo ziko mikononi mwa dawati la Ijumaa, wasanii walioonekana ni Lucy na Ndikumana tu hivyo kushibisha yale maswali ya Uwoya kuwa ni kwa nini filamu nzima ichezwe na watu wawili tu?

HADITHI YA FILAMU YADAIWA NI KISA CHA KWELI CHA UWOYA NA NDIKU
Habari za hivi karibuni zilisema kuwa,   cha ajabu, kisa kinachosimuliwa katika filamu hiyo ni cha kweli.
Ilidaiwa kuwa kisa hicho kilimpata Ndiku baada ya kukutana na Uwoya kwa mara ya kwanza kabla ya kufunga ndoa.
Madai hayo yanaongeza chachu katika moyo wa Uwoya na kuzidi kuamini kuna kitu kinaendelea kati ya mumewe na Lucy.

UWOYA AKATISHA ZIARA SWAZILAND
Uwoya alipotafutwa na Ijumaa juzi ili kumsikia msimamo wake kuhusu hali tete katika ndoa yake baada ya hisia zake kuwa anaibiwa mumewe na Lucy, alisema atapasua jipu atakapotua Bongo akitokea nchini Swaziland ambako alikwenda kwa ziara binafsi.
Alisema kuwa amelazimika kukatisha ziara na kurudi Tanzania kwa vile suala la Lucy na mumewe linamnyima raha kuendelea kuwepo ugenini.
“Narudi Bongo Jumatano (juzi). Unajua hili suala limeninyima raha kabisa. Siwezi kuendelea kuwepo huku ugenini. Nikifika nitatoa la moyoni,” alisema Uwoya.

LUCY AZUNGUMZA KUTOKEA DENMARK
Wakati Uwoya akizungumza kutokea jijini Mbabane, Swaziland, Lucy yeye alitoa sauti yake akiwa nchini Denmark kwenye Jiji la Copenhagen.
Alipoulizwa kuhusu tambo za Uwoya baada ya yeye kucheza filamu na mumewe Ndikumana, alijibu:
“Mimi sina cha kusema, yeye anajua mimi ni nani katika filamu. Mumewe kaonesha mapenzi ye kucheza filamu yangu, sasa anaposema ningemtaarifu yeye kama nacheza filamu na mumewe ili iweje? Kwa nini asimlaumu mume wake ambaye ndiye alipaswa kumtaarifu?” alisema Lucy.
Lucy aliongeza: Kama Ndiku angekuwa mtoto chini ya miaka kumi na nane nataka kucheza naye filamu hapo kweli, ningepaswa kumtaarifu Uwoya kama mama mtu, lakini mume, si sahihi kunilaumu.

MADAI YA HADITHI YA FILAMU KUWA KISA CHA KWELI
Kuhusu madai kwamba hadithi ya kwenye filamu hiyo ni kisa cha kweli kati ya Uwoya na Ndiku, Lucy alijibu:
“Teh! Teh! Si kweli bwana. Kama Uwoya ndiyo kasema hivyo basi ana kisa kinachofanana na cha filamu yangu. Mimi filamu ni yangu na hadithi ni yangu.”

WAONGOZA FILAMU BONGO WANASEMAJE KUHUSU WATU WAWILI TU?
Ili kujifunza juu ya wasanii wawili kucheza filamu nzima, Ijumaa liliwatafuta baadhi ya waongoza filamu Bongo.
Jumanne Kihangala ‘Mr Chuz’: Kusema kweli ni vigumu sana. Labda kama zile filamu za porini, mtu anakimbizwa na wanyama (documentary).
“Lakini kucheza filamu za mjini halafu wawili tu, mnagombana wenyewe mnapatana wenyewe ni kazi sana,” alisema Chuz.
Jacob Steven ‘JB’: Du! Labda kama utakuwa umekusudia kupunguza bajeti, lakini pia haitakuwa filamu nzuri, wawili tu?! Kwanza ni filamu gani hiyo ya watu wawili tu?
Ijumaa lilimkatia simu.
Mahsin Awadh ‘Dk Cheni’: Mh! Zipo kama mtu mwenyewe atakuwa ameamua, lakini sidhani kama sokoni itakubalika. Ni nani huyo kwani?
Ijumaa likamkatia simu.
Wazoefu wengi wa filamu walisema documentary ndizo zinaweza kuwa na watu wawili lakini si filamu.

SOMA GAZETI ZIMA LA IJUMAA KWA KUBOFYA HAPA

Views: 17502

Tags: ijumaa11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Aisha Hussein Juma on August 2, 2013 at 11:48am

mhhhhhhhhh hapa hata ingekuwea mimi ningeomba maelezo ya kina

Comment by Jerry Jerry on July 28, 2013 at 9:45am

IT LOOKS GUD BANA ,KWANI  JB NANI ?? ,CHUZ NANI ?? WAKUDA TU HAO WOTEEE , PICHA POA LETE MTAANI TUTANUNUA , KWENDENI ZENU  KULEEEEE WAKUDA

Comment by James Buyoya on July 27, 2013 at 9:10am
Kwa maana hiyo walkkuwa wanashoot wenyewe na hizo picha wamezipiga wenyewe wakazisambaza mimi binafsi haingi akilini kama hao ni wapenzi wangekuwa na mpango huo hAta picha msinge zipata nini ijumaa mkitaka ukweli watafuteni walioshoot sio kina JB cheni hao wote wazushi na hawaitakii mema bongo movie kwa kusababisha mabifu yasio kuwa na maana ktk tamsinia yao
Comment by Jamal amor on July 27, 2013 at 8:58am
DADA UWOYA. MOLA ATAKULIPIA. INSHAALA. WE2 NI MWENYE MALI. KIHALALI. Na siyo KIMADA. Ngoja mwezi mtukufu wa RAMADHANI. Iwishe. Humpe CHAI YAKE UYO MWIZI WA WAUME ZAWATU
Comment by TZ on July 27, 2013 at 7:21am

Hizi picha ni za kumtia kizaazaa huyu UWOYA hazionyeshi kuwa kuna mapenzi hapo ikisha angalia wanavyobusiana kama watu ambao wana kifafa au kifua kikuu. Ni USANII tu huu

Comment by nellicy maluli on July 27, 2013 at 1:46am

TENA WAMEPENDEZANA SANA, LUCY NA NDIKUMANA NA KAMA NI KWELI MMH MDADA IRENE, POLE SANA. UMECHEZEA SHILINGI CHOONI, ULAUMU SANA MDOMO WAKO KWA KUTOA MANENO YA KEJELI JUU YA NDIKU, UNAONA SASA MAJUTO NI MJUKUU? ULIKUWA UNATINGISHA KIBIRITI KUONA KM NJITI ZIMEJAA. HILI NI FUNDISHO KWA WOTE WENYE MIDOMO MICHAFU JUU YA WAUME ZAO.

Comment by Jamal amor on July 26, 2013 at 10:23pm
DA2 UWOYA. Hapo hakuna FILM YA WATU 2. Ni mapenzi kwenda mpele. Mi2 nakuomba tena ufanye HARAKA BILA KUCHELEWA. Ni kumtwanga TALAKA UYO MRWANDA. Pamoja na huyo MALAYA WA WANAUME ZA WATU. LUCY.WAENDELE NA UMALAYA WAO. UWOYA CHUKUA MTOTO WAKO ULEE
Comment by steven emmanuel on July 26, 2013 at 8:29pm

ndiku umekuwa mwanaume wa ukweli!!mwanamke asikupelekepeleke kama zoba

Comment by Zee La Udaku on July 26, 2013 at 5:12pm

Lucy chukua Ndiku moja kwa moja umtulize moyo. Jamaa huyu anaonekana ni mtulivu sana ila basi tu alioa changudoa ambaye anampa presha kila siku. Mwanamke gani haishi kubadilisha wananume kila siku ilihali akijua kaolewa. Ningekuwa Ndiku ningetulia na Lucy moja kwa moja, na huenda kweli sasa hivi wako pamoja huko Denmark

Comment by steven emmanuel on July 26, 2013 at 4:00pm

sanaaaaa tu ndiku!!kobe akiinama ujue anatunga sheria!!uwoya alijua wew ni bwegee umefanya la maana sana kumtifuatifua sasa  tumekurudisha kundin kwenye kundi  la wanaume HALISI

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

jancikop posted a status
44 seconds ago
Alan Munk posted a status
1 minute ago
Alan Munk posted a status
2 minutes ago
Alan Munk posted a status
2 minutes ago
Alan Munk posted a status
3 minutes ago
Alan Munk posted a status
3 minutes ago
Alan Munk posted a status
4 minutes ago
Alan Munk posted a status
4 minutes ago
Alan Munk posted a status
5 minutes ago
Alan Munk posted a status
6 minutes ago
Alan Munk posted a status
6 minutes ago
Ruth D. Fay posted a status
7 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }