Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’.
Judith Wambura ‘Jide’.
Na Musa Mateja
TUNAWEZA kusema mwaka 2012 ni wa mimba kwa mastaa wa Kibongo, kwani kwa jumla wanafika watano wenye vibendi, wengine ni wa leo au kesho kujifungua, Amani lina ripoti kamili.
Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, mastaa hao karibu wote wanahesabu siku kwa vile wamebakiza muda mchache, wengine wameanza kununua nepi na bebi shoo.
HAWA HAPA
Mastaa hao ni Shamsa Ford, Judith Wambura ‘Jide’, Maimartha Jesse, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na Zamaradi Mketema.
NANI KAWADUNGA?
Hata hivyo, swali linaloulizwa na mashabiki wao limebaki kuwa nani wahusika wa mimba hizo kwa kila mmoja.
Shamsa Ford; jamaa anayetajwa kwa jina la Dickson ndiye anadaiwa kumdunga ujauzito staa huyo wa muvi za Kibongo huku Jide ambaye ni mwanamuziki mkubwa Bongo akijulikana ni mke wa mtangazaji Gardner G. Habash.
Maimartha yeye alifunga ndoa ya siri hivi karibuni na Raymond Mushi ambaye hataki picha yake ionekane kwenye vyombo vya habari, ikidaiwa anafanya kazi sehemu nyeti katika nchi hii.
Mcheza sinema Thea ni mke wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’ kwa hiyo hakuna shaka kuwa, mimba inabaki kuwa ‘kitanda hakizai haramu’.
VIPI ZAMARADI?
Kazi iko kwa Mtangazaji wa Kipindi cha Take-One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema ambaye mpaka sasa, baba wa mtoto wake mtarajiwa, hataki kumwanika licha ya kwamba, jina lake linajulikana na wengi kwa sababu ni mtu mwenye cheo.
WAHOFIA KUJIFUNGUA KWA ‘KISU’
Aidha, habari za kusikitisha ni kwamba, baadhi ya mastaa hao wenye ‘vibendi’ wanahofia endapo watajifungua kwa njia ya upasuaji (kisu).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Amani, mastaa hao walisema wanamuomba Mungu kwa nguvu zote ili awaondelee shetani wa kisu siku ikifika.
Shamsa: “Namuomba Mungu anijalie nijifungue kawaida, siyo kwa upasuaji kwa sababu naogopa sana kupasuliwa na kutokana na maombi yangu naamini atanijalia.”
Zamaradi: “Mimba yangu ni kubwa sana na ninatarajia kujifungua siku si nyingi ila sitaki kuzungumzia chochote kwa sasa hadi nitakapojifungua.”
Thea: “Mimba hii ina miezi mingi ila haijafikia kujifungua na nitafurahi sana kama nitapata mtoto wa kike ingawa hayo yote ni mipango ya Mungu likiwemo la njia ya kujifungua.”
Kwa upande wao Maimartha na Jide hawakupatikana hewani kuzungumzia ishu hii.
Comment
Comment by isabella godfrey on February 21, 2012 at 10:40am inapendeza sana kwa maamudhi mliyochukua mtoto ni mzuri na anaraha yake hongereni sana.
Comment by Dongonyo Juniour on February 21, 2012 at 1:29am Hongereni
Comment by Geo M. Godfrey on February 15, 2012 at 3:27pm EH! ILA ZAMARADI KAKOMAA AISEE!! HE! UTADHANI AMELALA KWENYE PUMBA NA KUPAKA MAFUTA YA TAA!
Comment by Beatus Nchemwa. on February 15, 2012 at 3:16pm HATIMAYE JIDE NAE KAPATA UJAUZITO! Mungu mkubwa!
Comment by kokusima on February 11, 2012 at 12:26am
Comment by kaka on February 10, 2012 at 2:56pm Maimartha Jesse, HIYO MIMBA NI YA MBEGU FUPI?MAANA WEEK MOJA BADO MIMBA YA MIEZI SIPATI JIBU NDIO MAANA ULITAFUTA MUME BWEGE HATA KUTUONYESHA TAABU
Comment by thabit .. on February 10, 2012 at 12:13pm ZAMARADI KAKOMAAA UTAZANI ANAKULA CEMENT!!!!
Comment by Tumaini john on February 9, 2012 at 5:04pm
Comment by juma othman shaaban on February 9, 2012 at 4:50pm jamni kwani hawa ni watu kamw wengine , cha msingi ni kuwaombea dua tuu
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
julius manning |
| 3 |
Man KKK |
| 4 |
Sili Silali |
| 5 |
IL-YA |
| 6 |
chama baby |
| 7 |
msichoke mlugu |
| 8 |
kaka |
| 9 |
Maji Marefu |
| 10 |
Kelvin Luhala Eto'o |
othman Ochu posted a status
mrembo commented on Sili Silali's photo

You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers