Nabii Josephat Mwingira.

Na Elvan Stambuli
ANAYEJIITA Mtume na Nabii, Josephat Elias Mwingira wa Kanisa la Efatha la jijini Dar es Salaam ambalo anadai ni la mwisho tayari kwa unyakuo,  amekiri kununua  changudoa ‘changu’ Mererani,  mkoani Arusha.
Mwingira amekiri hilo katika kitabu chake alichokiandika na kukisambaza sehemu mbalimbali  nchini kikiwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Wito Wangu na Kusudio Langu’ ambapo amesema alibobea kwa kufanya zinaa na machangudoa.
Katika kitabu hicho chenye kurasa 34, Mwingira amesema licha ya uzinzi alibobea pia katika ulevi na kwamba siku moja akiwa na kahaba (Changu) huko Mererani Arusha alitokewa na Bwana Yesu ambaye alimuambia aachane na mambo hayo na amfuate yeye ili amtumikie.
Hata hivyo, Mwingira amesema licha ya wito huo wa Yesu, wakati huo alikuwa kwenye mazingira ambayo hayakuwa mazuri kwa sababu  alikuwa katika hali ya ulevi na mshiriki wa mambo mengi ya kidunia.

CHANGU ALITIMUA
“Yule dada (Changu) alipoona hali hiyo, akakimbia nikabaki peke yangu. Bwana Yesu akasema, mimi ninakutaka wewe uache maovu yote na unitumikie,” amesema Mwingira.
 Ameongeza kuwa baadaye wakati Yesu alipotaka kuondoka ikabidi amshike miguu na kumng’ang’ania na akamuambia,  “Usiniache!”.
Alifafanua kuwa Yesu akamshika bega la mkono wa kulia akasema, “Nitakuwa na wewe”, halafu akatoweka na baada ya hapo ndipo alipoanza kuombea watu.
Mwingira amekiri kuwa hata baada ya ‘kumuona’ Yesu, aliendelea kunywa pombe lakini ikawa anaitapika na akawa anatokewa na Kristo ndotoni au anatuma Malaika na kumuelekeza watu ambao atakwenda kuwaombea uponyaji kutokana na matatizo yao.

MCHUNGAJI AMPINGA
Hata hivyo, mchungaji mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini alipokisoma kitabu hicho alipingana na Mwingira, akasema Yesu hawezi kumtokea mtu akiwa katika harakati za kufanya ukahaba.
“Mungu anachukia sana ukahaba na mifano ipo. Aliteketeza Sodoma na Gomora ikawa jivu kutokana na watu wa kule kuendekeza ukahaba, aliunguza mji wa Babeli kutokana na mambo hayohayo, sasa siyo rahisi mtu atokewe na Yesu wakati yupo katika harakati za uhakaba,” alisema mchungaji huyo.
Aliongeza: “Mtu anaweza kutokewa na shetani la ngono kama atakuwa anaendekeza mambo hayo na baadaye kuwa moto kwelikweli wa uzinzi, hivyo kila mtu achukue tahadhari.”

Views: 9781

Tags: mchanganyiko11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by hope chaula on November 20, 2012 at 10:23am

nimependa sana compnt zenu japo kua kunawengine wanatakiwa kufanyiwa ukombozi wa hari ya juu  sana wanasema tu but ukweli utabaki pale pale NABII HANA HESHIMA KWAO...usiangalie nyuma kulikuaje wala alikua anafanya nini IMANI NI KUTARAJIA UNACHO TAKA KUTARAJIA basi kwan wewe unaamini ukifa ama baada ya maisha ya hapa duniani unaenda wap kama unakujua basi fanya hivyo tunao amini manabii tuache tuamini namuombea sana JOSEPAHT ELIAS MWINGIRA huyo huyo alie baka kua MUNGU AMPE UPAKU wa hali ya juu sana aendelee kutuombea tulio waznzi na makahaba na walevi kama yeye alivyo tokewa na yesu bas nasi tukafunguliwe KWAKO BABA NAKUPENDA SANA NA SITOKUACHA DAIMA NITAKUSIKILIZA NA NITATII KILE UTAKACHO NIAMBIE NIFANYE ...je WAPENDWA NAPENDA MSIKILIZE WIMBO WA BAHAT BUKUKU....KWENYE ALBAM MPYA....

mungu awape macho ya rohoni mtambue wapi uwze kutulia na kuabudu jina la YESU LIBARIKIWE AMINA NAWAPENDA

Comment by hope chaula on November 20, 2012 at 10:08am

sikilizeni wapendwa je napenda kusema kitu 1..mnapenda watu wavae nguo za ajabu 2 mnapnda watu waaendelee na ulevi na madawa ya kulevya.3 je mnapenda watu waatende zambi mchana kutw...

basi kama tunapenda mungu aendelee kuwa hapa tanzania na makanisa mengine tujifunze iman ni nni ....unatarajia nini katika maisha yako baada ya kifo ...pia usiangalie ya jana wala yaliyo pita songa mbele na kumbuka biblia inasema waacheni atawashughulikia mwenyewe.. sasa maswali na mtu unadhubutu kabisa kusema eti nabii muongo embu tubu makosa yako wewe mkweli haya anzisha kanisa na sisi tukuletee sadaka fungula kumi na zaka ok

mwache kila mwenye imani aamini imani yake na wanao abudu na kutoa sandaka damu za watu hao mtasemaje....

jamani kila mtu aamini anacho amini kwani mimi na mwamini mungu kupitia manabii wake
alio watuma unaye sema manabii wa uongo haya tutajua pala panda itakapo lia

nawapenda wote jina la yesu kristo kupitia nabii wake mwingila libarikiwe saaaaaaaaaaaaaaana tena sana na na mwombea mungu azidi kua na nguvu za kufanya miujiza zaidi na zaidi kuponya tanzania haleluya alie na sikio asikie ....

Comment by Nicodemus Katembo on March 6, 2012 at 9:26am

Mambo ya kufikirika,  Kawalimishe Kibaha na huko Rukwa. Huo ndio ujanja wenyewe.

Comment by master samom on March 6, 2012 at 8:53am
Mwiringa Wizi mtupu, mtume gani ktk historia alikua kahaba? Hakuna k2 km hch
Comment by Charles Mandonky on March 5, 2012 at 10:56am

Huyu jamaa labda alitokewa na Yesu alie igiza filamu ya passion of christ yule jamaa anaitwa (Merygibson) lakini sio yesu huyu tunae msubiria, maana kama ukiwa na changu ndio yesu anakutokea basi inamaana huko Buguruni siingekua noma yesu angeonekana kila maali.

Comment by Frank Fungamenza on March 5, 2012 at 2:01am

naomba niseme na mimi kuhusu huyu Mwingira!!.mimi naamini kama Yesu anaweza kumtokea mtu akiwa katika tendo la ukahaba!...kwasababu yeye hataki watoto wake tupotee! unapokuwa unatenda kosa,roho na nafsi wakati mwingine huwa inasita,6!..ile ni kauli ya Mungu kukuonya!..kabisaaa mwana wani!....ila hapa anaposema alikamata miguu ya Yesu,sijui kwani sikuwepo,ila amini nakuambia mwana global publisher leo,Mungu na timu yake wapo!...kuna siku familia yetu na majirani tulimuona malaika akipita mida ya saa 2 jioni baada ya kusali rozali kwa imani kwa kipindi kisichopungua mwezi 1 hv.Naomba amini hili,tulimuona mtu alieonekana kapiga magoti hewani nakuweka mikono yake vinzuri kwa ishara ya imani katika kidevu chake! na baada ya dakika kadhaa,tukiendelea kushangaa,nyota iliwaka kichwani pake kwa muda wote akipita! na siku hizo mama yangu mzazi alikuwa anaumwa sanaa,hakuna alieamini kama atapona! tulipomuamsha kumuona malaika,mama alipona mpaka leo,na hv sasa ni mtumishi wa Mungu! mwene kuamini aamini,asie amini potelea mbali maana maandiko yenyewe bado kwetu ni shida kuamini!...ukitaka kupata full mkanda nitafute!....alafu pia nina tukio jingine ambalo lilitutokea mm na jamaa zangu mwaka jana ambalo sote tuligeuka kulitukuza jina la muumba baada ya tukio hilo! ww nitafute nitakupa full info na evidez!...kwahio labada Mwingira kweli alikamata miguu ya Yesu,mm sijui il IMANI NINAYO!!...HAYA WAPENDWA KTK BWANA

Comment by leonard de caprio on March 4, 2012 at 3:14pm

Wapendwa haina haja kuumiza kichwa juu ya Unabii wa huyu mwenzetu maana yote yalishatabiriwa na Yesu katika kitabu cha Mathayo 24 anzia mstari wa 1-5 na kisha malizia kusoma mstari wa 24...bila shaka utaufahamu unabii wa Mheshimiwa huyu, lakini kwa ndugu zangu waislamu nadhani wao hawashangai kwa hali hii, maana Mtume wao alikwisha tabiri pia kuhusu fitna za Masuhudajjal na jisnsi atakavyokuja na ishara nzito nzito kiasi cha kufufua wafu....Wapendwa wangu muda huu ni wakuzidisha imani sana na kuomba huruma za Muumba tu.

Comment by kaka on March 4, 2012 at 10:04am

NABII ZOA SADAKA ZA WAJINGA KAKA KWANI WASHAHILI TUNAMSEMO WAJINGA DIOO WALIWAOOOOO

PESA NA MALI ZAO

Comment by Ukweli100 on March 3, 2012 at 12:19am

mh mimi siamini mtu , biblia tu!

Comment by Samson Masija on March 2, 2012 at 9:25am

We Mchungaji unaepinga, ni mshamba wa Maandiko. SOma Biblia uone watu aliowahi kuwatokea walikuwa wanafanya nini. Soma habari za Paulo aliyeitwa Sauli, alitokewa akiwa njiani kwenda kuua na kuzuia Ukristo. Sasa unasemaje. Neema ya Mungu haichagui. Soma Luka, Yesu anasema hakuja kwa ajili ya wenye haki bali Waovu. Sasa unakataa nini.

Simtetei Nabii bali nakusahihisha unaposema Mungu hashughuliki na Wazinzi. Hata wewe kabla ya kuwa Mchungaji ulikuwa Mzinzi na hata Jambazi na Mlevi lakini leo, unabisha kwamba Mungu hawezi kumtokea Mtu Mwovu. Rudi chuoni Usome na kuielewa Biblia. La sivyo utaongoza vipofu wenzio. Zingatia ushauri huu.

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

Tipu Sultan posted a status
1 minute ago
GLOBAL's 10 blog posts were featured
5 minutes ago
GLOBAL posted blog posts
6 minutes ago
jennyloffer posted a status
8 minutes ago
jennyloffer posted a status
17 minutes ago
jennyloffer posted a status
23 minutes ago
vanhelsing posted a status
27 minutes ago
vanhelsing posted a status
27 minutes ago
vanhelsing posted a status
27 minutes ago
vanhelsing posted a status
27 minutes ago
jennyloffer posted a status
28 minutes ago
vanhelsing posted a status
30 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }