Kiongozi wa Kanisa la Efatha la jijini Dar es Salaam, Nabii Josephat Mwingira (pichani) amewashangaza waumini wake alipodai Jumapili iliyopita kuwa, kuna mabinti wawili wachawi waliomfuma na kumvamia kanisani humo na akadai wametoka Loliondo katika Kijiji cha Samunge, hivyo amewakamata.

Tukio hilo lililowashtua waumini wake lilioneshwa moja kwa moja na televisheni ya kanisa hilo. Kiongozi huyo akadai kuwa, kitendo cha kuwakamata wachawi hao ni ushujaa na ushindi kwake.

Kiongozi mmoja mwandamizi wa kanisa hilo aliliambia Uwazi kuwa, Mwingira ana maono ya aina yake na mabinti hao wamejitokeza wenyewe na kudai kuwa walikuja kumdhuru.

“Wakati nabii huyo alipokuwa akiendesha ibada kanisani hapo ndipo binti mmoja alipoibuka na kudai kuwa ameagizwa kuja kuwanga kanisani hapo,” alisema kiongozi huyo aliyeomba jina lake kutoandikwa gazetini kwa kuwa siyo msemaji.
Mwandishi wetu alishuhudia binti huyo akihojiwa na Mwingira na kukiri mbele ya hadhara kuwa, yeye anafanya ulozi pamoja na mwenzake ambaye yupo kanisani humo. Muda mfupi baadaye naye alijitokeza na kwamba alifundishwa na bibi yake ambaye hakumtaja jina.

Hata hivyo, uongozi wa kanisa hilo uliwawekea ulinzi mkali na ukakataza mtu yeyote kuwapiga picha, hali iliyosababisha minong’ono kwa watu.

“Kama kweli ni wachawi kwa nini wanakataza wasipigwe picha?” Alisikika mtu mmoja akihoji kwa sauti ya chini na akadakia mwingine aliyehoji kwa nini majina yao hakutajiwa mwandishi?

Mwandishi wetu alifuatilia kuona hatma ya mabinti hao lakini akashuhudia wakiingizwa katika gari na kutoweka eneo la kanisa na mmoja wa viongozi wa kanisa hilo na kuelekea kusikojulikana.

Views: 3191

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Luka Yoram Million on April 18, 2011 at 7:45pm
Mwingira usijiite nabii wewe.Maana ajikwezaye atashushwa na ajishushaye atakwezwa.
Comment by baraka ndesamburo on April 18, 2011 at 6:00pm
teh teh teh waumini kuweni makini akili kichwani mwenu haya makanisa mengine shauri lenuu
Comment by Gerald Mlyomi on April 17, 2011 at 1:45pm

mchawi ni lazima atajwe jina ili apate aibu mbele ya jamii.asipo tajwa inaleta picha tofauti

 

Comment by Beachman on April 17, 2011 at 9:00am
Wapendwa Biblia inasema kila roho humtambua roho mwenziwe,kuna shirika gani kati ya nuru na giza;Huyu Mwingira kawatambua vipi hawa wachawi na kusema wametumwa kutoka Loliondo?Tuache hilo,mimi siku zote najiuliza kama kweeli wana uwezo wa miujiza ya kuponya na wanania ya kweli kabisa yenye roho wa Mungu ndani,Dar'salaam pekee kuna walemavu ombaomba chungumzima,kwanini wasiwasaidie masikini hawa wakatembea ili kweli tuone huo upako.Lakini imekua kinyume,akiponywa mtu,huwezi kuuona mwisho wake,atapotea tu.Mungu atusaidie sana,lakini hebu tujitahidi kuyacunguza maandiko;Yesu anasema,watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Kwanza neno nimeokoka mie naona ni UZUSHI kabisa,maana utaokokaje wakati mwisho haujafika,wakati bado uko katika dunia ya dhambi,na shetani bado anatujaribu kila siku.Mie nadhani atakaevumilia mpaka mwisho katika kutenda mema ndie atakae okoka;Hivi sasa tunachuchumilia wokovu tu,bado tupo katika mbio,na vita dhidi ya shetani,Yesu atakapo kuja na kuwachukua watu wake;wakiisha kuuingi mji ule ndipo watakaposema sasa tumeokoka,maana hapo hakuna mashindano mengine tena.Unajua hata katika mashindano ya kawaida,huwezi kusema nimeshinda kabla ya mpambano kuisha,mpira ni dakika tisini.Tusidanganyike!Biblia inasema shetani ni kama simba angurumae akizunguka zunguka kumtafuta mtu ammeze.Tafakari chukua hatua.
Comment by Mpeni Kabaka on April 15, 2011 at 7:11pm

Huo ni uongo hakuna kitu kama hicho mbona mnakua hataki kutaja majina yenu au na nyinyi ni manabii wa uongo.

 

Comment by Majid Majid on April 13, 2011 at 10:25am
Dear Mwingira, sasa hivi jaribu kumrudia Mugu na kutubu, ulio watia changa la macho wanechoshwa,  Watazania wa jana sio wa leo sasa wanaelewa na wamechoshwa na saundi na si wavivu tena wa kutafakari mambo, Na inaonekana sasa umekosa mwelekeo kabisa baada ya kutafakari Bibilia unatakari Loliondo.
Comment by peter camil on April 13, 2011 at 9:34am
nasiwndwa kutowashangaa wale wote  "tunao hukumu kabla ya hukumu" hivi watania naomba niulize, ni nani mwenye majibu juu ya dawa ya babu? ikiwa hata wizara yenye dhamana haina majibu hayo! je ni nani aliyetumia dawa na kukutwa hana virusi au anavyo pia? nani mwenye mamlaka ya kujitangaza yeye ni nabii?nimkumbuke Ray alivyoigiza tamthilia ya THE FAKE PASTORS, ninyi mnaosema babu ni muongo au ni mkweli niwaite  WANAFKI maana hamna jibu sahii juu ya hili! kwani dawa ile inatibu UKIMWI tu na mbona magonjwa mengine hamyazungumzii! kama babu ni muongo wale wajinga wachache watakuwa wameliwa na kama ni mkweli aibu iwe kwa Mwingila na wale wote wanaomsapoti! tuache hilo basi tuje tujadili unabii wa ke nao tuone, anatumia biblia kutangaza huu ni mwisho wa dunia na dalili zote zinaonyesha at the same time anasema kutakuwa na manabii wa uwongo Je mwingila yeye haingii ndani ya hawa manabii kweli, mimi sijui lkn nani alitoa mamlaka ya kujitangazia unabii au ni matendo na maono yako? je mwingila kama ni nabii a predict some future ili tumwamini! unless otherwise na yeye ni mwongo na hafai katika jamii maana anatupotosha! hebu watanzania tuache kulopoka na tukumbuke hili """"""NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK""""""""" HIVI IKITOKEA DAWA INATIBU WATU WALIOIKATAA DAWA HIYO WATAZIWEKA WAPI SURA ZAO AU NDO HOFU YA KUWA WATU WATAKIMBIA NA KUWA waumini wa babu na kupata hofu ya sadaka katika makanisa yao!  ahhhhhhaaaaaaaaaaaaa natania tu makanisa yoooooooooooote yatapika na kauli zote zitapia lkn msimamo wa kanisa takatifu la mitume ni ule ule! kama mtakatifu  PETER (PETRO) aliyeachiwa mamlaka ya dunia akifufuka na kuyakuta haya  atfuga mamlaka yake ya dunia aliyoachiwa na yesu kristo.
Comment by Anselm on April 13, 2011 at 9:06am

Kwanza nilim'watch mwenyewe kwa macho yangu katika Tv yake akitukana Viongozi wa Serikali yetu kwamba eti ni Wazinzi na Washerati hawana akili na ndo maana wanafululiza kwenda kwa Babu....wapi mamlaka husika?

Mimi nimemtoa thamani sana,Jumapili ang'avu kama ya juzi badala ya kuanza kuhubiri neno la MUNGU yeye akaanza kumwaga fitina zake kwa Babu,almost a full hour...Babu...Babu...Kikombe...Kikombe,yeye kinamhusu nini? kwakweli nimekaa na kumtafakari nimefikia kuwaonea huruma Wafuasi wake,kwani ni dhahiri shahiri anawapoteza.

Mtu gn badala ya kusaidia wasiojiweza kama wanavyofanya wenzake to mention 1 T.B Joshua yeye ndo anazidi kuwakamua,eti wamnunulie Landcruiser GX sijui VX, haya waumini wake mmeshamnunulia embu tujuzeni hapa.

Comment by apple on April 13, 2011 at 7:20am
Mmmh! Hapa full sound.
Comment by allan on April 12, 2011 at 10:48pm
Nabii siku zote huwa akubaliki Nyumbani fanya kazi baba Mwingira pamoja sana tu.ukweli wa Loliondo upo karibu kujulikana tatizo watanzania tunaenda vichwa vichwa kwa kila kinachoibuka
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }