MWANAJESHI AUAWA KWA WIVU WA MAPENZI

Na  Mwandishi Wetu, Songea
MWANAJESHI mmoja wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya Mlale, wilaya ya Songea, Payi Milinga ameuawa kwa kuchomwa na chupa shingoni baada ya kufumaniwa na mke wa mtu katika Kijiji cha Masangu, wilayani humo, mkoa wa Ruvuma.
Habari kutoka kijijini hapo zinasema Peter Haule alimkuta mkewe akiwa Milinga na walikuwa wameketi pamoja wakinywa bia, huku mwanamke akichezea simu ya marehemu, ndipo valangati lilipoanza.
“Haule  alisema siku nyingi amekuwa akijuwa kwamba Milinga anatembea na mkewe na sasa amethibitisha, ndipo alipomshika mkewe na kuanza kumkung’uta.
“Hata hivyo, mwanajeshi huyo alishikana na mtuhumiwa na kuanza kupigana baada ya mwanamke kukimbia ndipo Haule  alipochukua chupa na kuivunja kisha kumshindilia mgoni wake shingoni na kufariki palepale,” kilisema chanzo chetu.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, George Chiposi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo amesema lilitokea Januari 14 mwaka huu.
“Mwenye mke baada ya kumchoma chupa shingoni mwanajeshi, alitokwa na damu nyingi zilizosababisha afariki dunia palepale,” alisema Kamanda Chiposi.
Akaongeza kuwa mtuhumiwa anasakwa na polisi kwani baada ya kufanya kitendo hicho alitoroka na hajulikani alipo.

Views: 558

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by richardngeze on January 28, 2013 at 6:50pm

Marehemu alitaka kutumia uafande wake kula vya watu ona sasa hatima yake!

Comment by Ibu on January 28, 2013 at 11:37am
Ukisikia mke wa mtu sumu si mpaka aue panya

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 22. 11 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by mark gibson on Monday. 29 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 22. 45 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 22. 74 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson on Saturday. 12 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson on Sunday. 36 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

UKIMYA WA VYOMBO VYA DOLA KUTOA TAARIFA ZA MATUKIO YA MAUAJI NA UTEKAJI NI ISHARA KUWA WANAHUSIKA?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson 11 hours ago. 22 Replies

Absalom Kibanda akiwa ICU.USIKU wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi…

Tags: UTEKAJI, NA, MAUAJI, NI, ISHARA

TOP NEWS WEEK HII

Latest Activity

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service