MWANACHUO WA CHUO CHA UALIMU ST. AGREY JIJINI MBEYA AUAWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA BODABODA

Vedasto Pius baada ya kupigwa vibaya na wananchi.

Pikipiki inayodaiwa kuibiwa na Vedasto Pius.

Kitambuliso cha Chuo cha Vedasto Pius.

Mwananchuo mmoja kutoka Chuo cha Ualimu cha ST Aggrey kilichopo Uyole jijini Mbeya, anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma za kuiba pikipiki ya kusafirishia abiria maarufu kama bodaboda.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30.

Mgonja amesema tukio hilo lilitokea mnamo Julai 2 mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika daraja lililopo karibu na hotel ya Rift Valley barabara ya kuelekea Isanga, Jijini Mbeya.

Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada ya tuhuma za kuiba pikipiki yenye No T 438 BZU aina ya T-BETTER mali ya JOSEPH KAPASI (23) mkazi wa Ilomba jijini hapa.

Kwa upande wake mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema aliombwa kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae mtuhumiwa alipoanza kuendesha vizuri alitokomea na pikipiki hiyo. Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikutwa eneo la Isanga akielekea barabara ya Chunya akiwa na pikipiki hiyo ndipo alipoanza kupewa kipigo na wananchi wenye hasira kali mpka mauti kumfika.

PICHA KWA HISANI YA http://mbeyayetu.blogspot.com/

Views: 2785

Tags: MAUAJI

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by marsha maulid marsha on July 8, 2012 at 11:43am

JAMANI CHIZI HANA KIBALI.KUNA WATANZANIA WENGINE NI ZAIDI YA YULE ISRAEL MTOA ROHO ZA VIUMBE HAI.IKO SIKU TUTAKUJA UANA NDUGU KWA NDUGU KWA ROHO MBAYA ZETU.TUNAPEANA HUKUMU HAPA HAPA DUNIANI INGALI WOTE TUMEUMBWA,MMEJIVISHA CHEO AMBACHO HAMNA UWEZO NACHO,HAKIKA MUUMBA ATAKUADHIBUNI HAPA HAPA DUNIANI KWA MLICHO KITENDA.

WATANZANIA HEBU TUJIFUNZE KUHESHIMU UTU WA MTU JAMAAAAAAAAAAAAAAAAAA.

KIUKWELI HII INAUMA TENA KWA SANAAAAAAAA

Comment by Ng'wanashija on July 7, 2012 at 3:15pm

Mbona MAFISADI hamuwapondi mawe namna hii wakati wao ndiyo source ya matatizo mengi katika jamii. Juzi hapa imeripotiwa kuwa mafisadi wameficha mabilioni kule USWIZI, mbona wananchi wako kimya tu? Hasira yao iko wapi?

Natamani kweli siku moja FISADI mmoja naye auawe namna hii na wananchi wenye hasira...Siku hiyo nitaonja bia !!!!

Comment by Nigga S on July 7, 2012 at 2:15pm

dah hiyo nouma sasa jaman!

Comment by meggie impostra on July 7, 2012 at 10:49am

yani imeniuma kwa kweli masikini mbona mbeya kuna matukio ya ajabu sana mauaji ni mengi sijui kwa nn police wa huko hawayafanyii kzi ipasavyo haya mambo sasa suala kama hili masikini usikute alinogewa na piki piki kujua kuendesha akaona azunguke weeee atairejeshaaa kwa nn wasingesubilia mpk siku ipiteeee yani ujinga mtupu labda na siku zake zilifikaaa sheria ichukue mkondo wakee kwa hili iwe fundishio wa wananchi wanaopenda kuua ovyo bila kufanya uchunguzi wa kina

Comment by john bosco on July 7, 2012 at 8:15am

huu ni unyama  .ukatili angepelekwa polisi!!!!!!

Comment by julius manning on July 6, 2012 at 8:53pm
HAPA KUNA NAMNA
Comment by samora rajab albert on July 6, 2012 at 7:27pm

duh umejitafutia kifo cha bure tena cha ghazabu

Comment by lumi mwandelile on July 6, 2012 at 3:35pm

WIZI SIO MZURI JAMANI, WENYE MIKONO YA UDOKOZI JIFUNZENI

Comment by zepporah on July 6, 2012 at 2:17pm

sasa hao watu waliosimama pembeni na mwingine na kanzu ya kislam ..wameiacha maiti nje nje namna hiyo hata kuisitiri kwa mashati waliovaa kajani...ama kweli huko nyumbani mnakoenda sio pazuri hata kidogo jamani....

Comment by zubeda on July 6, 2012 at 12:54pm

so sad

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }