MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Subira Malefya (53), mkazi wa Kijiji cha Ipinda wilayani Kyela, mkoani hapa, amelazwa katika hospitali ya wilaya baada ya kumwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto na mumewe ambaye ni mwalimu mstaafu, Boniface Mwakinyuke (64).
Kaimu Katibu Tarafa wa Ntebela, Cathbert Mwalukama alisema kuwa mwanamke huyo alimwagiwa mafuta ya taa mwili mzima kisha kuchomwa moto saa nne usiku hivi karibuni akiwa amelala fofofo.
“Siku hiyo walikuwa wote kwenye kilabu cha pombe lakini mke aliwahi kurudi nyumbani na alilala,” alisema Mwalikama.
Hata hivyo, baadhi ya watu waliokuwa kilabuni walioogopa kutaja majina walisema mwalimu huyo mstaafu alipoona mkewe kaondoka alianza ‘kulia’ wivu kwamba amechukuliwa na mwanaume mwingine.
Walisema mwalimu huyo baadaye alikwenda dukani na kununua mafuta ya taa lita moja na nusu na kiberiti na kwenda nayo nyumbani kwake ambapo aliyatumia kumlipua mkewe.
Baada ya kitendo hicho, wasamaria walimkimbiza mama huyo katika Kituo cha Afya cha Ipinda na baadaye akahamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Kyela ambapo anaendelea na matibabu. Mwalimu huyo alikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Kyela ambako anashikiliwa.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Dk. Festo Ndungange amethibitisha kumpokea mgonjwa huyo na kusema amelazwa wadi namba tatu kwa matibabu zaidi.
Comment
jamani wivu hadi uzeeni
Comment by Berthaa Kobelo on October 25, 2012 at 1:24pm we babu huoni kuwa umri wako na mambo uliyoyafanya hayaendani!!!!!!!!!!!..sa km ulihisi wivu kwann usingeenda na mkeo nyumbani!!!!..yn elimu iliyonayo nadhani haikusaidia kitu..sasa km angekufa je..nae siungefia jela na huo umri wako jamani..mbona unambipu Isarael!!!!!!!!
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
NDAUKA the GREAT |
| 3 |
LJH_3 |
| 4 |
hope |
| 5 |
julius manning |
| 6 |
mayalilwa |
| 7 |
Tatu Majaliwa |
| 8 |
steven emmanuel |
| 9 |
Mishy chunga |
| 10 |
shabani abdallah nguluko |
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies 0 Likes
JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies 8 Likes
Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies 3 Likes
Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…
Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mayalilwa Mar 8. 26 Replies 5 Likes
HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies 4 Likes
Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…
Tags: SOKA
Started by GLOBAL in Habari. Last reply by Billy Frank Irungu Apr 26. 118 Replies 21 Likes
Tags: NCHINI, HAPA, UNAFURAHIA, HUDUMA, ZAKE?
Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies 4 Likes
hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?
Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies 9 Likes
Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…
Kimama Kinini commented on GLOBAL's blog post MADAI MAZITO NISHA AHONGWA NYUMBA
nellicy maluli commented on GLOBAL's blog post DR. FERDINAND MASAU WA TANZANIA HEART INSTITUE AFARIKI DUNIA© 2013 Created by Global Publishers.




You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers