Na Mwandishi Wetu
MWACHENI Mungu aitwe Mungu! Wakati Visiwa vya Zanzibar vikiendelea kuomboleza msiba mkubwa wa kuwakosa ndugu zao waliokuwa wakisafiri kwa meli iliyopinduka na kuzama ya MV Spices Islander (pichani),  maajabu yanabaki kwa mtoto mchanga wa miezi minne aliyekutwa akielea bila boya la kuogelea.

Kwa mujibu wa waokoaji wa tukio hilo lisilosahahulika lililotokea eneo la Nungwi, ambapo meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kwenda Pemba, mtoto huyo ambaye jina lake halikupatikana alikuwa akielea kwa saa 5 tangu ilipozama meli hiyo.

Ilidadavuliwa kuwa, baada ya waokoaji kufika eneo hilo wakiwa na helkopta, walimuona mtoto huyo ambapo ilibidi wambebe peke yake na kumuwahisha katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.

ASHTUKA USINGIZINI, AANZA KULIA
Ilielezwa kuwa, katika harakati za kumuokoa, alipoguswa ndipo aliposhtuka kutoka usingizini na kuanza kulia huku mama yake akisadikiwa kuzama baharini na kufariki.
Kwa mujibu wa Runinga ya Channel Ten, mtoto huyo alikutwa akielea juu ya maji licha ya kutovalishwa kifaa chochote maalumu cha kuogolea.

AIBUA MJADALA MZITO
Hata hivyo, taarifa ya kutozama kwa mtoto huyo iliibua mjadala mzito ambapo kwa mujibu wa wanamaji, inawezekana alikuwa amevalishwa nepi na ‘pempasi’ yenye nailoni ndiyo maana hakuzama.

Kundi lingine lilidai kuwa, hata kama angekuwa amefungwa pempasi, angezama eneo la kichwa na kubakiza sehemu iliyofungwa pempasi ikiwa juu hivyo wao waliamini ni Mungu tu!

 Hata hivyo, habari za uhakika zilidai kuwa mtoto huyo anaendelea vizuri.
Hadi gazeti hili linatinga mitamboni, zaidi ya watu 240 waliripotiwa kupoteza maisha na zaidi ya 600 kuokolewa katika ajali hiyo mbaya.

KUTOKA RISASI MCHANGANYIKO
Timu ya gazeti hili inawapa pole ndugu, jamaa na marafiki waliwapoteza wapendwa wao katika ajali hiyo. Mungu awape moyo wa subira.

Views: 4473

Tags: mchanganyiko11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by MARIAM SHABANI on September 20, 2011 at 2:24pm
Nilivyosikia habari hii nilijiuliza maswali mengi, ikiwa pampers ndio imemsaidia kutokuzama je lile baridi ya yale maji ilikuwaje na ukizingatia ni mtoto mdogo? licha ya hivyo malaika wa watu alilala fofofo kana kwamba yupo kwenye kitanda. Hakika Mungu wetu ni mkubwa na pia anamakusudi yake kwa huyu mtoto. muacheni mungu aitwe mungu,,,!!
Comment by neema molleli on September 20, 2011 at 12:34pm
MUNGU ANAYOMAKUSUDI MAKUBWA SANA NA YULE MTOTO,, HAKIKA ATAKUA MTU WA BARAKA SANA MUNGU AWALAZE MAREHEMU MAHALI PEMA POPONI.
Comment by REBECA ZAMBI on September 19, 2011 at 8:23pm
YEYE NI ALFA NA OMEGA
Comment by sophy on September 19, 2011 at 4:44pm
Inshallah mwenyezi mungu atamkuza huyo mtoto.
Comment by magdalena cathbert on September 18, 2011 at 9:18pm
kweli kabisa tumwache mungu aitwe mungu
Comment by SOSPETER on September 18, 2011 at 1:51pm
jambo gani l kumshinda MUNGU
Comment by Jashirati Obwere on September 17, 2011 at 8:09am
Mwacheni Mungu aitwe Mungu maana kuelea kwa mtoto huyo ni miujiza yake tu. Mola amjalie nguvu na afya njema mtoto wetu mpendwa.
Comment by Tausi Raphael on September 15, 2011 at 3:54pm
malaika wa watu, Mungu amjalie maisha mema na marefu
Comment by jemadari mimi on September 15, 2011 at 1:48pm
mola amjalie huyo mtoto akue salama
Comment by samora rajab albert on September 14, 2011 at 9:34pm
bado ni mja wa duniani


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
6 minutes ago
GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
6 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website