Mtoto Cesilia Edward enzi za uhai wake.
Mtoto Cesilia Edward amefariki dunia juzi saa tano usiku wa tarehe 08 katika hospitali ya Regency ya hapa jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amelazwa kwa siku mbili kwaajili ya matibabu.
Marehemu Cesilia alikuwa na umri wa miaka 14 alikuwa na tatizo la moyo na figo kushindwa kufanya kazi na kusababisha tumbo kujaa maji na kuvimba. Aligundulika na tatizo hilo tangu alipozaliwa.
Kampuni ya Africa media Group wamiliki wa Channel ten Kupitia kipindi mimi na Tanzania ilifanikiwa kumpeleka mtoto Cesilia nchini India kwa matibabu mwaka 2011 mwezi Oktoba lakini hakufanikiwa kupata matibabu (operation) baada ya madaktari kuthibitisha kuwa alikuwa amechelewa kwa matibabu.
Cesilia alikuwa mtoto yatima na kulelewa na familia ya Bw. Peter Nyarugembe mkazi wa Mbagara kuu ambaye alikuwa akimlea baada ya kukuta akilelewa na dada yake wilayani Kisarawe na alimkuta na tatizo hilo ila kutokana na hali ya uchumi aliyo nayo hakuweza kumsaidia kupona ugonjwa alio nao na kuamua kuomba msaada kwa wasamalia wema kupitia Kipindi cha mimi na Tanzania.
Marehemu alifikishwa hospitali jumatatu ya tarehe 6 mwezi huu akiwa na hali mbaya iliopelekea kupoteza fahamu na kumbukumbu kila wakati hali iliendelea hivyo mpaka umauti ulipo mkuta.
Mungu ailaze roho ya marehemu Cesilia mahala pema peponi.
-Amen.
Comment
Comment by Santa Santiago on February 16, 2012 at 10:21am R.I.P CECY
Comment by mawnaisha bakary vuyaa on February 13, 2012 at 12:11pm mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu Cecilia
Comment by Neema Kibwana Shomary on February 13, 2012 at 10:25am
Comment by ANDERSON SOGOLE on February 13, 2012 at 8:28am
Comment by samora rajab albert on February 11, 2012 at 7:50pm innaa lillahi wainna ilayhi rajiun
Comment by Kakytee The Director on February 11, 2012 at 8:59am
Comment by kokusima on February 10, 2012 at 11:45pm Poleni sana familia. Pumzika kwa amani mtoto mwema usiye na hatia Cecy.
Comment by julius manning on February 10, 2012 at 4:57pm poleni sana wana familia. Mungu amweka mahali pema peopni, Amina.
Comment by Lillian j on February 10, 2012 at 4:48pm pumzika kwa amani mpendwa we2 umeteseka sana
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
julius manning |
| 3 |
Man KKK |
| 4 |
Sili Silali |
| 5 |
IL-YA |
| 6 |
chama baby |
| 7 |
msichoke mlugu |
| 8 |
kaka |
| 9 |
Maji Marefu |
| 10 |
Kelvin Luhala Eto'o |
othman Ochu posted a status
mrembo commented on Sili Silali's photo

You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers